WESTMINSTER SHORTER CATECHISM IN SWAHILI (KATEKISIMU FUPI) [1, 1 ed.] 9789976884609

Katekisimu [κατηχέω] ni neno la Kigiriki lenye maana ya kufundisha kwa mdomo kwa mfumo wa maswali na majibu. Ni njia amb

872 114 695KB

Kiswahili Pages 30 Year 2020

Report DMCA / Copyright

DOWNLOAD FILE

Polecaj historie

WESTMINSTER SHORTER CATECHISM IN SWAHILI (KATEKISIMU FUPI) [1, 1 ed.]
 9789976884609

Table of contents :
Yaliyomo
1. Kusudi la Maisha na Maandiko Matakatifu (Swali 1-3)
2. Mungu Mmoja na Utatu (Swali 4-6)
3. Mpango wa Mungu wa Milele (Swali 7-8)
4. Uumbaji (Swali 9-10)
5. Maongozi ya Mungu (Swali 11- 12)
6. Dhambi katika Jamii ya Wanadamu (Swali 13-19)
7. Agano la Mungu la Neema (Swali 20)
8. Kristo Mpatanishi: Nafsi na asili ya Mpatanishi (Swali 21-22)
9. Kristo Mpatanishi: Ofisi tatu za Kristo (Swali 23- 26)
10. Kristo Mpatanishi: Hali ya Kristo ya kujishusha (Swali 27)
11. Kristo Mpatanishi: Hali ya kuinuliwa kwa Kristo (Swali 28)
12. Wito wa Mungu wenye ufanisi (Swali 29-31)
13. Faida katika maisha haya (Swali 32)
14. Faida katika maisha haya: Kuhesabiwa haki (Swali 33)
15. Faida katika maisha haya: Kufanywa Wana (Swali 34)
16. Faida katika maisha haya: Utakaso (Swali 35)
17. Faida nyinginezo:
a. Katika maisha haya (Swali la 36)
b. Wakati wa kifo (Swali la 37)
c. Wakati wa ufufuo (Swali la 38)
18. Sheria ya Maadili (Swali 39-40)
19. Sheria ya Maadili: Muhtasari Wake (Swali 41-42)
20. Sheria ya Maadili: Ufafanuzi wa amri kumi (Swali 43-81)
21. Sheria ya Maadili: Makosa na Adhabu (Swali 82-84)
22. Amri ya Mungu katika Injili (Swali 85)
23. Amri ya Mungu katika injili:
a) Imani (Swali la 86)
b) Toba iletayo Uzima (Swali 87)
24. Njia za Neema (Swali 88)
a) Neno la Mungu (Swali 89-90)
b) Sakramenti (Swali 91-93)
i. Ubatizo (Swali 94-95)
ii. Meza ya Bwana (Swali 96-97)
25. Maombi (Swali 98-99)
26. Ufafanuzi wa Sala ya Bwana (Swali 100-107)

Citation preview

Katekisimu Fupi Westminster Shorter Catechism

Muhtasari wa Kile Tunachoamini

PRESBYTERIANS

Hakimiliki © 2020 Daniel John Seni Chapa ya Kwanza, 2020 nakala 200 Chapa ya Pili, 2020 nakala 7000

Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP) [+255-755-643-590] Mchapaji: Moccony Printing Press [+255-718-908-631] ___________________________________________ Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya kitabu hiki inaweza kuzalishwa tena bila ruhusa ya Mfasiri isipokuwa kwa mhakiki ambaye anaweza kunukuu vifungu vifupi vifupi katika hakiki zake; Wala sehemu yoyote ya kitabu hiki hairuhusiwi kuwekwa katika umbo lingine bila kibali cha mfasiri. _______________________________________ Katekisimu Fupi (The Westminster Shorter Catechism) Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV)

Inasambazwa na:Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam _________________________ Kwa manufaa ya Kanisa la Mungu - Afrika Mashariki

i

Yaliyomo 1. Kusudi la Maisha na Maandiko Matakatifu (Swali 1-3) 2. Mungu Mmoja na Utatu (Swali 4-6) 3. Mpango wa Mungu wa Milele (Swali 7-8) 4. Uumbaji (Swali 9-10) 5. Maongozi ya Mungu (Swali 11- 12) 6. Dhambi katika Jamii ya Wanadamu (Swali 13-19) 7. Agano la Mungu la Neema (Swali 20) 8. Kristo Mpatanishi: Nafsi na asili ya Mpatanishi (Swali 21-22) 9. Kristo Mpatanishi: Ofisi tatu za Kristo (Swali 23- 26) 10. Kristo Mpatanishi: Hali ya Kristo ya kujishusha (Swali 27) 11. Kristo Mpatanishi: Hali ya kuinuliwa kwa Kristo (Swali 28) 12. Wito wa Mungu wenye ufanisi (Swali 29-31) 13. Faida katika maisha haya (Swali 32) 14. Faida katika maisha haya: Kuhesabiwa haki (Swali 33) 15. Faida katika maisha haya: Kufanywa Wana (Swali 34) 16. Faida katika maisha haya: Utakaso (Swali 35) 17. Faida nyinginezo: a. Katika maisha haya (Swali la 36) b. Wakati wa kifo (Swali la 37) c. Wakati wa ufufuo (Swali la 38) 18. Sheria ya Maadili (Swali 39-40) 19. Sheria ya Maadili: Muhtasari Wake (Swali 41-42) 20. Sheria ya Maadili: Ufafanuzi wa amri kumi (Swali 43-81) ii

21. Sheria ya Maadili: Makosa na Adhabu (Swali 82-84) 22. Amri ya Mungu katika Injili (Swali 85) 23. Amri ya Mungu katika injili: a) Imani (Swali la 86) b) Toba iletayo Uzima (Swali 87) 24. Njia za Neema (Swali 88) a) Neno la Mungu (Swali 89-90) b) Sakramenti (Swali 91-93) i.

Ubatizo (Swali 94-95)

ii.

Meza ya Bwana (Swali 96-97)

25. Maombi (Swali 98-99) 26. Ufafanuzi wa Sala ya Bwana (Swali 100-107)

iii

Utangulizi Katekisimu [κατηχέω] ni neno la Kigiriki lenye maana ya kufundisha kwa mdomo kwa mfumo wa maswali na majibu. Ni njia ambayo tangu zamani ilitumiwa kwa ajili ya kufundisha kwa muhtasari imani ya Kikristo. Tumelazimika kutoa ufafanuzi mfupi ili kupinga majaribio ya wazushi ambao hulaghai washirika kwa madai kwamba Katekisimu iko kidini sana, na siyo kiroho, madai ambayo hayana ukweli wowote. Watumiaji wanapaswa kujua kwamba Katekisimu hii imesheheni mafundisho ya msingi ya Ukristo kwa kuzingatia Biblia Takatifu. Kuna aina kuu mbili za Katekisimu za Westminister; Katekisimu fupi na Katekisimu ndefu. Katekismu fupi ina maswali 107 na Katekisimu ndefu ina maswali 196. Hii ni Katekisimu fupi ambayo ilianza kuandikwa mwaka 1646 na kumalizika mwaka 1647. Iliandaliwa na sinodi ya wanatheolojia Warefomati wa Uingereza na Scotland. Makanisa mengi ya “Ki-Refomati” (Reformed Churches), yakiwemo makanisa ya Ki-Presibiteriani hutumia Katekisimu hii. Hivyo basi, dhima yetu ni kuhakikisha kwamba washirika wote wanafundishwa misingi ya imani ya Kikristo kwa kuzingatia Katekisimu hii. Na kwamba baada ya kumakinika katika Katekisimu fupi, pia wawe tayari kumakinika katika Katekisimu ndefu. Tafsiri hii imetokana na toleo la Kiingereza cha Kisasa, na hivyo tumejaribu kuzingatia maneno-msingi na tahajia yake, na pia tumejaribu kwa umakini kuzingatia maana ya awali. Wenu,

Daniel John Seni (Mfasiri) Shekinah Presbyterian Church in Tanzania Oktoba, 2020 _________________

iv

Swali la 1. Je! Nini kusudi kuu la mwanadamu? Jibu. Kusudi kuu la mwanadamu ni kumtukuza1) Mungu na kumfurahia Yeye milele.2) 1) 1 Kor. 10:31; Rum. 11:36. 2) Zab. 73: 25-28.

Swali la 2. Je! Mungu ametoa mwongozo gani kutuelekeza jinsi tunavyoweza kumtukuza na kumfurahia? Jibu. Neno la Mungu, ambalo limo katika Maandiko ya Agano la Kale na Jipya1) ndiyo mwongozo wa kutuelekeza jinsi tunavyoweza kumtukuza na kumfurahia Yeye. 2) 1) II Tim. 3:16; Efe. 2:20. 2) I Yoh.1: 3-4.

Swali la 3. Je! Kimsingi Maandiko Matakatifu yanafundisha nini hasa? Jibu. Kimsingi, Maandiko Matakatifu yanafundisha kile ambacho mwanadamu anapaswa kuamini kuhusu Mungu, na kile ambacho Mungu anahitaji kwa mwanadamu. (II Tim. 1:13; 3:16).

Swali la 4. Mungu ni nani? Jibu. Mungu ni Roho,1) asiye na mipaka,2) wa milele,3) na asiyebadilika,4) katika utu wake,5) hekima,6) nguvu,7) utakatifu,8) haki, wema na ukweli.9) 1) 2) 3) 4) 5) 6) 7) 8) 9)

Yn. 4:24. Ayu. 11: 7-9. Zab. 90: 2. Yak. 1:17. Kut. 3:14. Zab. 147: 5. Ufu. 4: 8. Ufu 15: 4. Kut. 34: 6-7.

1

Swali la 5. Je! Kuna Mungu zaidi ya mmoja? Jibu. Hapana. Kuna Mungu mmoja tu, aliye hai na wa kweli. (Kumbu. 6: 4; Yer. 10:10).

Swali la 6. Je, Kuna nafsi ngapi katika Uungu wa Mungu? Jibu. Kuna nafsi tatu katika Uungu; Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu; na hizi nafsi tatu ni Mungu mmoja katika umoja, usawa kwa nguvu na utukufu. (I Yoh. 5: 7; Mt. 28:19). Swali la 7. Je! Amri za Mungu ni nini? Jibu. Amri za Mungu ni kusudi lake la milele, kulingana na shauri la mapenzi yake, ambapo kwa utukufu wake, amepanga mambo yote yatakayotokea. (Efe. 1:4, 11; Rum. 9: 22-23). Swali la 8. Je! Mungu hutimizaje amri Zake? Jibu. Mungu hutimiza amri Zake kupitia kazi za uumbaji Wake na Maongozi yake. Swali la 9. Kazi za uumbaji ni nini? Jibu. Kazi za uumbaji ni kazi zote zinazoonekana na zisizoonekana, kwamba Mungu, kwa muda wa siku sita, alifanya vitu vyote kwa kutokutumia kitu chochote kilichokuwepo [kwa sababu hakuna kilichokuwepo] kwa neno na nguvu zake, na vyote vilikuwa vyema. (Mwa 1; Ebr. 11: 3). Swali la 10. Je! Mungu alimwumbaje mwanadamu? jibu. Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke, kwa mfano wake mwenyewe, katika maarifa, haki na utakatifu, na akampa uwezo wa kutawala viumbe vingine. (Mwa 1: 26-28; Kol. 3:10; Efe. 4:24).

Swali la 11. Je! Kazi za Maongozi ya Mungu ni nini? Jibu. Kazi za Maongozi ya Mungu ni kazi zake takatifu zaidi, 1) za hekima,2) na kutawala viumbe vyake vyote, na kuongoza matendo yao yote.3) 2

1) Zab. 145: 17. 2) Zab. 104: 24; Isa. 28:29. 3) Zab. 103: 19; Mt. 10: 29-31.

Swali la 12. Je! Ni tendo gani maalum la Maongozi ambalo Mungu alifanya kwa mwanadamu baada ya uumbaji? Jibu. Wakati Mungu alipomwumba mwanadamu, aliingia katika agano la maisha pamoja naye, kwa masharti ya utii kamili; akamkataza kula matunda katika mti wa ujuzi wa mema na mabaya, huku akimuonya kwamba siku akila hakika atakufa (Gal. 3:12; Mwa 2:17).

Swali la 13. Je! Wazazi wetu wa kwanza waliendelea kuwa na hali ile waliyoumbwa nayo? Jibu. Hapana. Wazazi wetu wa kwanza, wakiwa wameachiliwa katika hali ya uhuru wa hiari yao wenyewe, walianguka kutoka kwenye hali ambayo Mungu aliwaumba nayo kwa kuasi. (Mwa 3: 6-8, 13; Mh. 7:29)

Swali la 14. Dhambi ni nini? Jibu. Dhambi ni utashi wowote wa kutokufuata sheria ya Mungu, au ukiukaji wa sheria ya Mungu. (I Yoh. 3:4) Swali la 15. Je! Ni dhambi gani ambayo wazazi wetu wa kwanza walifanya na kuanguka kutoka kwenye hali ile ambayo Mungu aliwaumba nayo? Jibu. Dhambi ambayo wazazi wetu wa kwanza walifanya na kuanguka kutoka kwenye hali ile ambayo waliumbwa nayo ilikuwa ni tendo la kula tunda walilokatazwa na Mungu. (Mwa 3: 6, 12).

3

Swali 16. Je! Wanadamu wote walianguka katika dhambi ya kwanza ya Adamu? Jibu. Ndiyo. Kwa sababu Agano ambalo Mungu alifanya na Adamu halikuwa kwa ajili yake peke yake, bali kwa kizazi chake; yaani kwa wanadamu wote; kuanzia kwake na kwa kizazi cha chake, wote walitenda dhambi, na wakaanguka pamoja naye, katika kosa lake la kwanza. (Mwa 2:16-17; Rum. 5:12; 1 Kor. 15: 21-22).

Swali la 17. Je! Anguko lilimleta mwanadamu kwenye hali gani? Jibu. Anguko lilimleta mwanadamu katika hali ya dhambi na majonzi. (Rom. 5:12). Swali la 18. Je! Dhambi ambayo mwanadamu alianguka inajumuisha nini? Jibu. Dhambi ambayo mwanadamu alianguka, inajumuisha hatia ya dhambi ya kwanza ya Adamu; yaani kupotea kwa utashi wa haki ya asili, na ufisadi wa asili yake yote, ambayo kwa kawaida huitwa Dhambi ya Asili; pamoja na makosa yote halisi yanayotokana na dhambi hiyo. (Rum. 5:12, 19; 5: 10-20; Efe. 2: 1-3; Yak. 1: 14-15; Mt. 15:19)

Swali la 19. Je! Wanadamu walipata shida gani katika anguko hilo? Jibu. Wanadamu wote kwa sababu ya anguko walipoteza ushirika na Mungu,1) wako chini ya ghadhabu yake na laana,2) na kwa hiyo wanawajibika kwa shida zote katika maisha haya; kwa kuanza na kifo chenyewe, na uchungu wa kuzimu milele. 3) 1) Mwa 3: 8, 10, 24. 2) Efe. 2: 2-3, Gal. 3:10. 3) Omb. 3:39; Rum. 6: 23, Mt. 25:41, 46.

4

Swali la 20. Je! Mungu aliwaacha wanadamu wote waangamie katika hali ya dhambi na shida? Jibu. Hapana. Mungu, katika uzuri wake, kwa mapenzi yake, tangu milele yote, amewachagua wengine kwenda uzima wa milele.1) Aliingia katika Agano la Neema, ili kuwaokoa katika hali ya dhambi na shida, na kuwaleta katika hali ya wokovu kupitia Mkombozi.2) 1) Efe. 1: 4. 2) Rum. 3: 20-22; Gal. 3: 21-22.

Swali la 21. Je! Mkombozi wa Wateule wa Mungu ni nani? Jibu. Mkombozi wa pekee wa wateule wa Mungu ni Bwana Yesu Kristo,1)ambaye, akiwa Mwana wa Mungu milele alifanyika mtu,2)na anaendelea kuwa mtu; Mungu na mtu katika asili mbili tofauti, na Mtu mmoja milele.3) 1) I Tim. 2: 5-6. 2) Yn. 1:14; Gal. 4: 4. 3) Rum. 9: 5; Luka 1: 35; Kol. 2: 9; Ebr. 7: 24-25.

Swali la 22. Ni jinsi gani Kristo, akiwa Mwana wa Mungu, alifanyika mtu? Jibu. Kristo, Mwana wa Mungu, alifanyika mtu kwa kuchukua mwili wa kweli,1) na roho safi,2) akachukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ndani ya tumbo la Bikira Mariamu na akazaliwa naye3) bila dhambi.4) 1) 2) 3) 4)

Ebr. 2:14, 16; 10: 5. Mt. 26:38. Lk 1:27, 31, 35, 42; Gal. 4: 4. Ebr. 4:15; 7:26.

Swali la 23. Je! Ni ofisi gani ambazo Kristo hufanya kazi kama Mkombozi wetu? Jibu. Kristo, kama Mkombozi wetu, anashikilia ofisi kuu tatu: ya nabii, ya kuhani, na ya mfalme, zote ziliwekwa kwa kipindi katika hali ya kujishusha, lakini baadaye kuinuliwa. 5

(Mdo. 3:21-22; Ebr. 12:25. linganisha II Kor. 13: 3; Ebr. 5: 5-7; 7:25; Zab. 2: 6; Isa. 9: 6-7; Mt. 21: 5; Zab. 2: 8-11.)

Swali la 24. Je! Kristo anatekelezaje ofisi ya nabii? Jibu. Kristo anatekeleza ofisi ya nabii katika kutufunulia mapenzi ya Mungu kwa ajili ya wokovu wetu. Hufanya hivyo kwa kutumia Neno na Roho Wake. (Yn. 1:18; 1Pet.1:10-12; Yn 15: 15; 20:31.)

Swali la 25. Je! Kristo anatekelezaje ofisi ya ukuhani? Jibu. Kristo anatekeleza ofisi ya ukuhani katika kujitoa kwake mwenyewe kuwa dhabihu ili kutosheleza haki ya Mungu,1) na kutupatanisha naye,2) na pia kutuombea kila wakati mbele za Mungu baba yake 3) 1) Ebr. 9:14, 28 2) Ebr. 2:17. 3) Ebr. 7: 24-25.

Swali la 26 Je! Kristo hutekelezaje ofisi ya mfalme? Jibu. Kristo anatekeleza ofisi wa mfalme kwa kutuvuta sisi kwake mwenyewe,1) katika kututawala na kututetea,2) na katika kuwashinda maadui zetu wote.3) 1) Mdo. 15:14-16. 2) Isa. 33:22. 3) I Kor. 15:25, Zab. 110.

Swali la 27. Je! Hali ya Kristo ya kujinyenyekesha ilijumuisha nini? Jibu. Unyenyekevu wa Kristo ulijumuisha kuzaliwa kwake katika hali ya chini,1) kufanywa chini ya sheria,2) kupitia masikitiko ya maisha haya,3) ghadhabu ya Mungu,4) na kifo cha laana msalabani;5) kwa kuzikwa,6) na kubakia chini ya nguvu ya kifo kwa muda.7) 1) Lk 2: 7. 2) Gal. 4: 4. 3) Ebr. 12: 2-3; Isa. 53: 2-3.

6

4) 5) 6) 7)

Lk 22:44; Mt. 27:46. Fil. 2: 8. I Kor. 15: 3-4. Mdo. 2: 24-27, 31.

Swali la 28. Je! Nini kinajumuisha kuinuliwa kwa Kristo? Jibu. Kuinuliwa kwa Kristo ni pamoja na kufufuka kwake siku ya tatu kutoka kwa wafu,1) kupaa mbinguni,2) kuketi mkono wa kuume wa Mungu Baba,3) na kurudi tena kuhukumu ulimwengu katika siku ya mwisho.4) 1) 2) 3) 4)

1 Kor. 15: 4. Mk. 16:19. Efe. 1:20. Mdo. 1: 11; 17:31.

Swali la 29. Je! Tunafanywaje washiriki wa ukombozi ulionunuliwa na Kristo? Jibu. Tunafanywa washiriki wa ukombozi ulionunuliwa na Kristo, kwa Kristo kuuleta ukombozi huo kwetu1) kupitia Roho wake Mtakatifu.2) 1) Yn. 1: 11-12. 2) Tit. 3: 5-6.

Swali la 30. Je! Roho hutumiaje kwetu ukombozi ulionunuliwa na Kristo? Jibu. Roho Mtakatifu hutumia ukombozi ulionunuliwa na Kristo kwa kufanyia kazi imani iliyo ndani yetu,1) na kwa hiyo hutuunganisha na Kristo katika wito wetu wenye ufanisi. 2) 1) Efe. 1:13-14; Yn. 6:37, 39; Efe. 2:8.

2) Efe. 3:17, 1 Kor. 1:9.

Swali la 31. Wito wenye ufanisi ni nini? Jibu. Wito wenye ufanisi ni kazi ya Roho wa Mungu,1) ambapo, hututhibitishia juu ya dhambi zetu2) na kutia nuru ufahamu wetu katika kumjua Kristo,3) na kufanya mapenzi yetu upya.4) Pia hutushawishi na kutuwezesha kumkumbatia Yesu Kristo, aliyetolewa kwetu bure katika Injili.5) 7

1) 2) 3) 4) 5)

II Tim. 1: 9; II Thes. 2: 13-14. Mdo. 2:37. Mdo. 26:18. Ezek. 36: 26-27. Yn. 6: 44-45; Fil. 2:13.

Swali la 32. Je! Ni faida gani wale walioitwa kwa wito wenye ufanisi wanashiriki katika maisha haya? Jibu. Wale waliotiwa kwa “wito wenye ufanisi” katika maisha haya wanashiriki kuhesabiwa haki,1) kufanywa wana,2) na kutakaswa, pamoja na faida kadhaa ambazo katika maisha haya zinaambatana.3) 1) Rum. 8:30. 2) Efe. 1: 5. 3) I Kor. 1:26, 30.

Swali la 33. Kuhesabiwa haki ni nini? Jibu. Kuhesabiwa haki ni tendo la neema ya Mungu, ambapo ndani yake husamehe dhambi zetu zote,1) na hutukubali sisi kuwa waadilifu machoni pake,2) kupitia haki ya Kristo iliyohesabiwa kwetu,3) na kupokelewa kwa imani tu.4) 1) 2) 3) 4)

Rum. 3: 24-25; 4: 6-8. II Kor. 5:19, 21. Rum. 5: 17-19. Gal. 2:16; Fil. 3: 9.

Swali la 34. Kufanywa Wana ni nini? Jibu. Kufanywa Wana ni tendo la Neema ya Mungu,1) ambapo Wateule wanapokelewa kwenye familia ya Mungu, na kwamba wana haki zote za wana wa Mungu.2) 1) I Yoh. 3: 1. 2) Yn. 1:12; Rum. 8:17.

Swali la 35. Utakaso ni nini? Jibu. Utakaso ni kazi ya neema ya bure ya Mungu,1) ambapo kwa hiyo tunafanywa upya kwa mfano wa Mungu, 2) na 8

kuwezeshwa zaidi kufa kwa dhambi, na kuishi kwa haki.3) 1) II Thes. 2:13. 2) Efe. 4: 23-24. 3) Rum. 6: 4, 6.

Swali la 36. Je! Ni faida gani ambazo zinaambatana na kuhesabiwa haki, kufanywa wana na kutakaswa katika maisha haya? Jibu. Faida ambazo zinaambatana na kuhesabiwa haki, kufanywa wana, na kutakaswa katika maisha haya ni pamoja na uhakikisho wa upendo wa Mungu, amani ya dhamiri, 1) furaha katika Roho Mtakatifu,2) kuongezeka kwa neema,3)na uvumilivu.4) 1) 2) 3) 4)

Rum. 5: 1-2, 5. Rum. 14:17. Mith. 4:18. I Yoh. 5:13; I Pet. 1: 5.

Swali la 37. Waumini hupokea faida gani kutoka kwa Kristo wakati wa kufa kwao? Jibu. Roho za waumini katika kufa kwao hufanywa kamili katika utakatifu,1) na kuingia moja kwa moja kwenye utukufu.2) Miili yao, wakiwa wameshikamana na Kristo, 3) wanapumzika kwenye makaburi 4) hadi ufufuo.5) 1) 2) 3) 4) 5)

Ebr. 12:23. II Kor. 5: 1, 6, 8; Fil. 1: 23; Lk. 23:43. I Thes. 4:14. Isa. 57: 2. Ayu. 19: 26-27.

Swali la 38. Waumini watapokea faida gani kutoka kwa Kristo wakati wa ufufuo? Jibu. Katika ufufuo, waumini watainuliwa katika utukufu, 1) watakubaliwa waziwazi na kuachiliwa katika siku ya hukumu,2) na kubarikiwa kikamilifu katika starehe kamili ya Mungu 3) milele.4) 9

1) 2) 3) 4)

1 Kor. 15:43. Mt. 25:23; 10:32. I Yoh. 3: 2; I Kor. 13:12. I Thes. 4: 17-18.

Swali la 39. Je! Ni jukumu gani ambalo Mungu anamtaka mwanadamu kufanya? Jibu. Jukumu ambalo Mungu anamtaka mwanadamu kufanya ni kutii mapenzi yake yaliyofunuliwa. (Mik. 6:8; I Sam. 15:22) Swali la 40. Je! Ni nini ambacho Mungu hapo mwanzo alimfunulia mwanadamu kuwa mwongozo kwa utii wake? Jibu. Mwongozo ambao Mungu hapo mwanzo alimfunulia mwanadamu kwa utii wake ilikuwa ni sheria ya maadili. (Rum. 2: 14-15; 10: 5.)

Swali la 41. Je! Sheria ya maadili imeelezwa wapi kwa kifupi? Jibu. Sheria ya maadili imeelezwa kwa kifupi katika Amri Kumi za Mungu (Kumbu. 10: 4.) Swali la 42. Je! Jumla ya Amri Kumi ni ipi? Jibu. Jumla ya Amri Kumi ni kumpenda Bwana Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, kwa roho zetu zote, kwa nguvu zetu zote, na kwa akili zetu zote; na jirani zetu kama sisi wenyewe. (Mt. 22: 37-40.)

Swali la 43. Je! Nini utangulizi wa Amri Kumi? Jibu. Utangulizi wa Amri Kumi uko katika maneno haya, mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. (Kut. 20: 2.) Swali la 44. Utangulizi wa Amri Kumi unatufundisha nini? Jibu. Utangulizi wa Amri Kumi unatufundisha kwamba kwa 10

sababu Mungu ni BWANA, na Mungu wetu, na Mkombozi, tunalazimika kuzishika amri zake zote. (Lk 1:74-75; I Pet. 1:15-19.) Swali la 45. Je! Amri ya kwanza ni ipi? Jibu. Amri ya kwanza ni hii“Usiwe na miungu mingine ila Mimi (mbele Yangu.)” 1(Kut. 20: 3) Swali la 46. Ni nini kinachohitajika katika amri ya kwanza? Jibu. Amri ya kwanza inatutaka tumjue na kumkubali Mungu kuwa ndiye Mungu wa pekee, na Mungu wetu;1) na tunapaswa tumwabudu na kumtukuza Yeye ipasavyo.2) 1) I Nyak. 28: 9; Kumb. 26:17. 2) Mt. 4:10; Zab. 29: 2.

Swali la 47. Je! Ni nini marufuku katika amri ya kwanza? Jibu. Amri ya kwanza inakataza kutomwabudu na kumtukuza Mungu wa kweli kama ndiye Mungu,1) na Mungu wetu;2) na inakataza kutoa ibada na utukufu kwa mtu mwingine yeyote, zaidi Yake pekee. 3) 1) Rum. 1:21. 2) Zab. 81: 10-11. 3) Rum. 1: 25-26.

Swali la 48. Je! Tunafundishwa nini hasa na maneno haya, “ila Mimi” (mbele Yangu) katika amri ya kwanza? Jibu. Maneno haya “ila Mimi” (mbele Yangu) katika amri ya kwanza yanatufundisha kuwa Mungu, anayeona yote, huyazingatia, na hapendezwi na dhambi ya kuwa na mungu mwingine yeyote. (Ezek. 8:5-18)

1

Maneno “Mbele Yangu” yanapatikana katika tafsiri ya moja kwa moja ya Kiingereza; “before Me.” Katika Lugha ya Kiswahili imetafsiriwa “Ila Mimi.” Nitatumia kwa kubadilishana maneno haya kwa kuzingatia muktadha wa swali.

11

Swali la 49, Je! Amri ya pili ni ipi? Jibu. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu (Kut. 20:4-6) Swali la 50. Je! Ni nini kinahitajika katika amri ya pili? Jibu. Amri ya pili inahitaji kupokea, kuzingatia, na kutunza kwa ukamilifu ibada zote za kidini na maagizo kama ambavyo Mungu ameagiza katika neno lake. (Kumb. 32:46; Mt. 28:20; Mdo. 2:42)

Swali la 51. Je! Ni nini marufuku katika amri ya pili? Jibu. Amri ya pili inakataza ibada ya Mungu kwa sanamu,1) au njia nyingine yoyote ambayo haijateuliwa katika neno lake. 2) 1) Kumb. 4:15-19; Kut. 32:5,8

2) Kumb. 12:31-32.

Swali la 52. Je! Ni ni sababu zipi zilizoambatishwa katika amri ya pili ili kuonesha utekelezaji wake? Jibu. Sababu zilizoambatishwa katika amri ya pili ili kuonesha utekelezaji wake ni ile enzi kuu ya Mungu juu yetu, 1) ubora wake ndani yetu,2) na bidii aliyo nayo kwa ibada yake mwenyewe.3) 1) Zab. 95: 2-3, 6. 2) Zab. 45:11. 3) Kut. 34: 13-14.

Swali la 53. Je! Amri ya tatu ni ipi? Jibu: Amri ya tatu ni hii “Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. (Kut. 20:7) 12

Swali la 54. Je! Ni nini kinahitajika katika amri ya tatu? Jibu. Amri ya tatu inahitaji utumiaji wa majina ya Mungu1) vyeo vyake,2) sifa zake3) maagizo yake,4) Neno lake,5) na kazi zake6) katika hali ya utakatifu na heshima. 1) 2) 3) 4) 5) 6)

Mt. 6: 9; Kumb. 28:58. Zab. 68: 4. Ufu 15: 3-4. Mal. 1:11, 14. Zab. 138: 1-2. Ayu. 36:24.

Swali la 55. Je! Ni nini kinakatazwa katika amri ya tatu? Jibu. Amri ya tatu inakataza unajisi wa aina yoyote au kuharibu kitu chochote pale ambapo Mungu amejifunua (Mal. 1: 6-7, 12; 2: 2; 3:14)

Swali la 56. Ni sababu ipi iliyoambatishwa katika amri ya tatu? Jibu. Sababu iliyoambatishwa katika amri ya tatu ni kwamba watu wataovunja amri hii wanaweza kuepuka adhabu kutoka kwa wanadamu, lakini kamwe hawataweza kuepuka hukumu ya haki ya Mungu. (I Sam. 2:12, 17, 22, 29; 3:13; Kumb. 28:58-59) Swali la 57. Je amri ya nne ni ipi? Jibu. Amri ya nne ni hii “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. (Kut. 20:8-11)

13

Swali la 58. Ni nini kinahitajika katika amri ya nne? Jibu. Amri ya nne inahitaji kuitakasa kwa Mungu siku moja katika siku saba kuwa Sabato kwake, kama ambavyo ameagizo katika neno lake (Kumb. 5:12-14) Swali la 59. Je! Ni siku gani ya saba ambayo Mungu ameiteua kuwa Sabato ya kila Juma? Jibu. Kuanzia mwanzo wa ulimwengu hadi ufufuo wa Kristo, Mungu aliteua siku ya saba ya Juma kuwa Sabato ya kila wiki; na tangu ufufuo mpaka mwisho wa ulimwengu ameteua siku ya kwanza ya Juma [yaani Jumapili] kuwa ndiyo Sabato ya Kikristo. (Mwa 2: 2-3; 1 Kor. 16:1-2; Mdo 20:7) Swali la 60. Je! Sabato inapaswa kutakaswa kivipi? Jibu. Sabato inapaswa kutakaswa kwa kufanya pumziko takatifu siku nzima,1) kupumzika kutoka kwenye kazi za ulimwengu na starehe ambazo tunazifanya katika siku zingine;2) na tunapaswa kutumia wakati wote katika kumwabudu Mungu kwa pamoja kanisani na kibinafsi, 3) tunaruhusiwa kufanya matendo mengine ambayo yanachukuliwa kuwa ni ya lazima. Matendo haya tunayaita matendo ya huruma na rehema.4) 1) 2) 3) 4)

Kut. 20: 8, 10; 16: 25-28. Neh. 13: 15-19, 21-22. Lk 4:16; Mdo 20: 7; Zab. 92; Isa. 66:23. Mt. 12: 1-31.

Swali. 61. Ni nini kinakatazwa katika amri ya nne? Jibu. Amri ya nne inakataza kutokuwa waangalifu kwa majukumu yanayotakiwa katika siku hiyo,1)inakataza kuichafua siku hiyo kwa uvivu,2) au kufanya mambo yasiyotakiwa,3) au mawazo yasiyostahili, maneno, au kazi za ulimwengu ambazo hazipaswi kufanywa katika siku hiyo.4) 1) Ezek. 22:26; Amo. 8: 5; Mal. 1:13. 2) Mdo. 20: 7, 9. 3)Ezek. 23:38. 4) Yer. 17: 24-26; Isa. 58:13.

14

Swali la 62. Je! Ni sababu gani zilizoambatishwa katika amri ya nne? Jibu. Sababu zilizoambatishwa katika amri ya nne ni; kwamba Mungu ameturuhusu kufanya kazi siku sita,1) akionesha mfano wake mwenyewe katika kufanya kazi siku sita na kuibariki siku ya Sabato. 2) 1) Kut. 20: 9.

2) Kut. 20:11.

Swali la 63. Amri ya tano ni ipi? Jibu. Amri ya tano ni hii “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.” (Kut. 20:12) Swali la 64. Je! Ni nini kinahitajika katika amri ya tano? Jibu. Amri ya tano inahitaji kuhifadhi heshima na kutekeleza majukumu ya kila mtu katika maeneo yao na mahusiano yao kadhaa, kama kwa wakubwa,1) wadogo,2) au walio sawa.3) 1) Efe. 5:21. 2) I Pet. 2:17. 3) Rom. 12:10.

Swali 65. Je! Ni nini kinakatazwa katika amri ya tano? Jibu. Amri ya tano inakataza kupuuza au kufanya jambo lo lote dhidi ya heshima na jukumu ambalo ni la kila mtu katika maeneo yao na mahusiano yao kadhaa. (Mt.15:4-6; Ezek. 34:2-4; Rum. 13:8)

Swali la 66. Je! Ni sababu gani imeambatishwa katika amri ya tano? Jibu. Sababu iliyoambatishwa katika amri ya tano ni ahadi ya maisha marefu na kufanikiwa kwa wote watakaotii amri hii. (Kut. 5:16; Efe. 6:2-3)

Swali la 67. Amri ya sita ni ipi? Jibu. Amri ya sita ni hii, “Usiue.” (Kut. 20:13) 15

Swali la 68. Ni nini kinachohitajika katika amri ya sita? Jibu. Amri ya sita inahitaji juhudi zote halali za kuhifadhi uhai wetu,1) na wa wengine.2) 1) Efe. 5: 28-29. 2) I Fal. 18: 4.

Swali la 69. Ni nini kinakatazwa katika amri ya sita? Jibu. Amri ya sita inakataza kutoa uhai wetu wenyewe, au uhai wa jirani zetu bila haki (Mdo. 16:28; Mwa 9: 6) Swali la 70. Amri ya saba ni ipi? Jibu. Amri ya saba ni hii “Usizini.” (Kut. 20:14) Swali la 71. Ni nini kinahitajika katika amri ya saba? Jibu. Amri ya saba inahitaji utunzaji wa hali zetu wenyewe na za majirani zetu katika usafi, na tabia nzuri. (I Kor. 7:2-3, 5, 34, 36; Kol. 4:6; I Pet. 3:2)

Swali la 72. Ni nini kinakatazwa katika amri ya saba? Jibu. Amri ya saba inakataza mawazo yote yasiyofaa, maneno, na matendo. (Mt. 15:19; 5:28; Efe. 5: 3-4) Swali la 73. Je! Amri ya nane ni ipi? Jibu. Amri ya nane ni hii, “Usiibe.” (Kut. 20:15) Swali la 74. Ni nini kinahitajika katika amri ya nane? Jibu. Amri ya nane inahitaji kumiliki mali halali na kuendeleza utajiri wetu wenyewe na wa wengine (Mwa 30:30; I Tim. 5: 8; Lawi. 25:35; Kumb. 22: 1-5; Kut. 23: 4-5; Mwa 47:14, 20).

Swali la 75. Je! Ni nini kinakatazwa katika amri ya nane? Jibu. Amri ya nane inakataza kila kitu kinachoweza kupoteza mali zetu wenyewe au za majirani zetu (Mith. 21:17; 23: 20-21; 28:19; Efe. 4:28).

16

Swali la 76. Amri ya tisa ni ipi? Jibu. Amri ya tisa ni hii “Usimshuhudie jirani yako uongo.” (Kut. 20:16)

Swali la 77. Je! Ni nini kinahitajika katika amri ya tisa? Jibu. Amri ya tisa inahitaji kudumisha na kukuza ukweli kati ya mtu na mtu1) na ukweli kati yetu wenyewe na wengine2) hasa katika kutoa ushahidi.3) 1) Zek. 8:16. 2) III Yoh 12. 3) Mith. 14: 5, 25.

Swali la 78. Je! Nini kinakatazwa katika amri ya tisa? Jibu. Amri ya tisa inakataza kila kitu ambacho kinapotosha ukweli, au kinachoweza kudhuru majina yetu au la majina ya majirani zetu. (I Sam. 17:28; Lawi 19:16; Zab. 15: 3) Swali la 79. Je amri ya kumi ni ipi? Jibu. Amri ya kumi ni hii, “Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.” (Kut. 20:17) Swali la 80. Ni nini kinahitajika katika amri ya kumi? Jibu. Amri ya kumi inahitaji kuridhika na hali zetu, 1) na moyo wa huruma kwa majirani zetu na wengineo.2) 1) Ebr. 13: 5; I Tim. 6: 6. 2) Ayu. 31:29; Rum. 12:15; I Tim. 1: 5; 1 Kor. 13: 4-7.

Swali la 81. Ni nini kinakatazwa katika amri ya kumi? Jibu. Amri ya kumi inakataza kutoridhika na hali zetu wenyewe,1) wivu au kuhuzunika kwa ajili ya maendeleo ya majirani zetu,2) na nia zote mbaya na hisia kuhusu majirani zetu.3) 17

1) I Fal. 21: 4; Est. 5:13; I Kor. 10:10. 2) Gal. 5:26; Yak. 3:14, 16. 3) Rum. 7: 7-8; 13: 9; Kumb. 5:21.

Swali la 82. Je! Kuna mtu anayeweza kutimiza amri za Mungu kikamilifu? Jibu. Hakuna mtu yeyote tangu anguko anayeweza kuzishika amri hizi kikamilifu katika maisha haya1) lakini kila siku tunavunja kwa mawazo, maneno, na matendo. 2) 1) Mhu. 7:20; I Yoh. 1: 8, 10; Gal. 5:17. 2) Mwa 6: 5; 8:21; Rum. 3: 9-21; Yak. 3: 2-13.

Swali la 83. Je! Makosa yote ya sheria yana uzito sawa? Jibu. Dhambi zingine kwa undani, na kwa jinsi zilivyo, ni mbaya sana mbele za Mungu kuliko zingine. (Ezek. 8: 6, 13, 15; I Yoh. 5:16; Zab. 78:17, 32, 56)

Swali la 84. Je! Kila dhambi inastahili nini? Jibu. Kila dhambi inastahili ghadhabu na laana ya Mungu, katika maisha haya, na yale yajayo. (Efe. 5: 6; Gal. 3: 10; Kumb. 3:39; Mt. 25:41)

Swali la 85. Je! Mungu anataka nini kwetu ili tuepuke ghadhabu na laana Yake kwa sababu ya dhambi? Jibu. Ili kuepuka ghadhabu na laana ya Mungu kwa sababu ya dhambi, Mungu anahitaji kutoka kwetu imani kwa Yesu Kristo, na toba iletayo uzima,1) na kutumia kwa bidii njia za neema ambazo Kristo hutumia kuleta kwetu kazi za ukombozi.2) 1) Mdo. 20:21. 2) Mith. 2: 1-5; 8: 33-36; Isa. 55:3.

Swali la 86. Je! Imani katika Yesu Kristo ni nini? Jibu. Imani katika Yesu Kristo ni neema iokoayo1) ambayo tunapokea na kupumzika juu yake kwa wokovu, kama yeye alivyotolewa kwetu katika Injili.2) 1) Ebr. 10:39.

2) Yn. 1:12; Isa. 26: 3-4; Fil. 3: 9; Gal. 2:16.

18

Swali la 87. Je! Toba iletayo Uzima ni nini? Jibu. Toba iletayo uzima ni neema ikoayo,1) ambayo mwenye dhambi, kutokana na ukweli wa dhambi yake, 2) na huruma ya Mungu katika Kristo,3) anachukia dhambi zake,4) na kwa hiyo, yeye hubadilika na kumgeukia Mungu, akikusudia na kujaribu kila wakati kutembea naye katika njia zote za utii mpya. 5) 1) 2) 3) 4)

Mdo. 11:18. Mdo. 2: 37-38. Yoel. 2:12; Jer. 3:22. Yer. 31: 18-19; Eze. 36:31. 5) II Kor. 7:11; Isa. 1: 16-17.

Swali la 88. Je! Ni njia gani za nje ambazo Kristo anatumia kuleta faida za Ukombozi kwetu? Jibu. Njia za nje na za kawaida ambazo Kristo anatumia kuleta faida za ukombozi kwetu ni maagizo yake, hasa Neno, Sakramenti, na Sala (Maombi); na haya yote yanatekelezwa kwa Wateule. (Mt. 28: 19-20; Mdo 2:42, 46-47) Swali la 89. Je! Neno hufanywaje kuwa lenye ufanisi kwa ajili ya wokovu? Jibu. Roho wa Mungu pengine huweza kutumia usomaji wa Neno kwa ajili ya kuwaleta watu katika wokovu, lakini hasa mahubiri ya Neno la Mungu ndiyo njia ya kuijua kweli. Neno huwashawishi wenye dhambi na huwavuta kwa Kristo. Kuwajenga katika utakatifu na faraja kupitia imani hadi wokovu. (Neh. 8: 8; I Kor. 14: 24-25; Mdo 26:18; Zab. 19: 8; Mdo 20:32; Rum. 15: 4; II Tim. 3: 15-17; Rum. 10: 13-17; 1:16.)

Swali la 90. Je! Ni jinsi gani neno linapaswa kusomwa na kusikilizwa ili liweze kufaa kwa wokovu? Jibu. Ni lazima tulisome neno la Mungu kwa bidii, 1) kwa kujiandaa 2) na kwa sala.3) Tunapaswa kulipokea kwa imani na upendo,4) na kuliweka mioyoni mwetu,5) na kulifanyia kazi katika maisha yetu.6) 19

1) 2) 3) 4) 5) 6)

Mith. 8:34. I Pet. 2: 1-2. Zab. 119: 18. Ebr. 4: 2; II Thes. 2:10. Zab. 119: 11. Lk. 8:15; Yak. 1:25.

Swali la 91. Je! Ni jinsi gani Sakramenti zinakuwa njia bora za wokovu? Jibu. Sakramenti zinakuwa njia bora za wokovu sio kutokana na kitu chochote kilicho ndani yake, au nguvu yoyote kutoka kwa yule anayesimamia; bali ni kwa baraka za Kristo tu, 1) na kazi ya Roho wake ndani ya Sakramenti ambapo wale wanaopokea, wanapaswa kupokea kwa imani pekee.2) 1) I Pet. 3:21; Mt. 3:11; 1 Kor. 3: 6-7. 2) I Kor. 12:13.

Swali la 92. Sakramenti ni nini? Jibu. Sakramenti ni agizo takatifu lililowekwa na Kristo ambapo Kristo na faida za Agano Jipya zinawakilishwa na kutiwa muhuri na kutumika kwa waumini. (Mwa 17: 7, 10; Kut. 12; 1 Kor. 11: 23, 26)

Swali la 93. Je! Sakramenti za Agano Jipya ni zipi? Jibu. Sakramenti za Agano Jipya ni Ubatizo,1) na Meza ya Bwana.2) 1) Mt. 28:19. 2) Mt. 26: 26-28.

Swali la 94. Ubatizo ni nini? Jibu: Ubatizo ni Sakramenti ya Agano Jipya, ambapo Kristo ameamuru kwa kuosha kwa maji, kwa jina la Baba, na Mwana, na la Roho Mtakatifu,1) kuwa ishara na muhuri ndani yake Kristo na kushiriki faida za Agano la Neema, na ushirikiano na Bwana.2) 20

1) Mat. 28:19. 2) Rom. 6:4; Gal. 3:27.

Swali la 95. Ubatizo unapaswa kutolewa kwa nani? Jibu. Ubatizo unapaswa kutolewa kwa mtu yeyote anayekiri imani ya Kristo na kumtii, na lazima awe mshirika wa kanisa linaloonekana;1) lakini watoto wachanga wa wale washirika wa kanisa linaloonekana hubatizwa.2) 1) Mdo 8: 36-37; 2:38. 2) Mdo 2: 38-39; Mwa 17:10. Linganisha. Kol. 2: 11-12; 1 Kor. 7:14.

Swali la 96. Meza ya Bwana ni nini? Jibu. Meza ya Bwana ni Sakramenti ambayo kwa kutoa na kupokea mkate na divai, kifo cha Kristo kinaonyeshwa; na wapokeaji wenye kustahili wanapokea kwa imani, wanafanywa washiriki wa mwili wake na damu. Katika kujilisha kiroho wanafanywa washiriki wa mwili wake na damu, pamoja na faida zake zote na katika ukuaji wao katika neema. (I Kor. 11:2326; 10:16)

Swali la 97. Ni nini kinahitajika kwa ajili ya kustahili kushiriki Meza ya Bwana? Jibu. Wale wanaoshiriki Meza ya Bwana wanapaswa kujichunguza wenyewe, na kwa ujuzi wao kutambua mwili wa Bwana, 1) imani yao ya kupokea2) toba yao,3) upendo wao kwa Bwana,4) na utii wao mpya kwa Bwana;5) wasije wakakaribia na kula na kunywa hukumu yao wenyewe.6) 1) 2) 3) 4) 5) 6)

1 Kor. 11: 28-29. II Kor. 13: 5. I Kor. 11:31. I Kor. 10: 16-17. I Kor. 5: 7-8. I Kor. 11: 28-29.

21

Swali 98. Maombi ni nini? Jibu. Maombi ni kutoa matakwa yetu kwa Mungu,1) kwa kuomba vitu ambavyo vinavyokubaliwa na mapenzi yake,2) kwa jina la Kristo,3) na kukiri dhambi zetu,4) kwa huruma na rehema zake.5) 1) 2) 3) 4) 5)

Zab. 62: 8. I Yoh. 5:14. Yn.16:23. Zab. 32: 5-6; Dan. 9: 4. Fil. 4: 6.

Swali la 99. Je, Ni kanuni gani ambayo Mungu ametupatia kama maelekezo katika maombi? Jibu. Neno la Mungu lote linatumika katika kutuelekeza katika maombi;1) lakini kanuni maalum ya mwongozo ni yale maombi ambayo Kristo aliwafundisha wanafunzi wake yajulikanayo kama "Sala ya Bwana.” 2) 1) I Yoh. 5:14. 2) Mt. 6:9-13. Linganisha na Lk. 11:2-4.

Swali la 100. Utangulizi wa Sala ya Bwana unatufundisha nini? Jibu. Utangulizi wa Sala ya Bwana ambao ni, “Baba yetu aliye mbinguni”1) unatufundisha kumkaribia Mungu kwa heshima na utakatifu wote, kama watoto kwa Baba, mwenye uwezo na utayari wa kutusaidia;2) na kwamba tunapaswa kuomba pamoja na wengine na kwa ajili ya wengine.3) 1) Mt. 6: 9. 2) Rum. 8:15; Luka 11:13. 3) Mdo. 12: 5; I Tim. 2: 1-2.

Swali la 101. Je tunaomba nini katika ombi la kwanza? Jibu. Katika ombi la kwanza ambalo ni, “jina lako litukuzwe”1) tunaomba kwamba Mungu atuwezeshe sisi, na wengine kumtukuza katika mambo yote ambayo yeye amejijulisha;2) na 22

kwamba aweze kuweka vitu vyote kwa utukufu wake mwenyewe.3) 1) Mt. 6: 9. 2) Zab. 67: 2-3. 3) Zab. 83.

Swali. 102. Tunaomba nini katika ombi la pili? Jibu. Katika ombi la pili ambalo ni, "Ufalme wako uje"1) tunaomba kwamba ufalme wa Shetani uharibiwe;2) na ufalme wa neema uendelezwe.3) Na sisi wenyewe na wengine tuletwe na tuweze kutunzwa katika ufalme huo.4) na kwamba ufalme wa utukufu wake uje. 1) 2) 3) 4) 5)

Mt. 6: 10. Zab. 68: 1, 18. Ufu. 12: 10-11. II Thes. 3: 1; Rum. 10: 1; Yn. 17: 9, 20. Ufu. 22:20.

Swali la 103. Tunaomba nini katika ombi la tatu? Jibu. Katika ombi la tatu ambalo ni, “Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani, kama huko mbinguni.”1) Hapa tunapaswa kuomba kwamba Mungu, kwa neema yake, atuwezeshe kujua, kutii na kujitiisha chini ya mapenzi yake, katika mambo yote, 2) kama vile malaika wanavyofanya huko mbinguni.3) 1) Mt. 6: 10. 2) Zab. 67; 119: 36; Mt. 26:39; II Sam. 15:25; Ayu. 1:21. 3) Zab. 103: 20-21.

Swali la 104. Tunaomba nini katika ombi la nne? Jibu. Katika ombi la nne ambalo ni, “Utupe leo liziki yetu.”1) Katika ombi hili tunapaswa kuomba kwamba; kwa neema ya Mungu ya bure tuweze kupokea sehemu bora ya vitu vizuri katika maisha haya, na kufurahia baraka zake kupitia vitu anavyotupatia.2) 1) Mt. 6:11. 2) Mith. 30: 8-9; Mwa 28: 20; I Tim. 4: 4-5.

23

Swali la 105. Tunaomba nini katika ombi la tano? Jibu. Katika ombi la tano ambalo ni, “Na utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.”1) Tunapaswa kuomba kwamba Mungu, kwa ajili ya Kristo, asamehe dhambi zetu zote.2) Tunatiwa moyo sana kuomba ombi hili kwa sababu tunawezeshwa na neema yake kusamehe wengine kutoka mioyoni.3) 1) Mt. 6:12. 2) Zab. 51: 1-2, 7, 9; Dan. 9: 17-19. 3) Lk. 11: 4, Mt. 18: 35.

Swali la 106. Tunaomba nini katika ombi la sita? Jibu. Katika ombi la sita ambalo ni, “Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule Mwovu”1) tunaomba kwamba Mungu ama atuzuie kujaribiwa kutenda dhambi,2) au atusaidie na kutuokoa pale tunapojaribiwa.3) 1) Mt. 6:13. 2) Mt. 26:41. 3) II Kor. 12: 7-8.

Swali la 107. Je! Hitimisho la Sala ya Bwana linatufundisha nini? Jibu. Hitimisho la Sala ya Bwana ambao ni, “Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele, “Amina” 1) linatufundisha kupata faraja yetu katika sala kutoka kwa Mungu peke yake,2) na kwamba katika maombi yetu tunapaswa kumtukuza Yeye, tukirudisha ufalme, nguvu na utukufu kwake.3) Na kwa ushuhuda wa nia yetu ya kupokea, na uhakika wa kusikiwa tunasema, “Amina.” 4) 1) 2) 3) 4)

Mt. 6:13. Dan. 9: 4, 7-9, 16-19. I Nyak. 29: 10-13. I Kor. 14:16; Ufu. 22: 20-21.

24