MISINGI YA IMANI: MAFUNDISHO YA KIBIBLIA KUHUSU IMANI YA KIKRISTO (THE WESTMINSTER CONFESSION OF FAITH AND LARGER CATECHISM) [1] 9789976572612

Tafsiri ya kitabu hiki imezingatia muktadha wa kanisa la Tanzania na Afrika kwa ujumla. Katika kuzingatia muktadha huu,

869 265 1MB

Kiswahili Pages 202 Year 2020

Report DMCA / Copyright

DOWNLOAD FILE

Polecaj historie

MISINGI YA IMANI: MAFUNDISHO YA KIBIBLIA KUHUSU IMANI YA KIKRISTO (THE WESTMINSTER CONFESSION OF FAITH AND LARGER CATECHISM) [1]
 9789976572612

Table of contents :
YALIYOMO
Tabaruku i
Dibaji ii
Maelezo ya Mfasiri iv
Maelekezo kwa Mtumiaji vii
Utangulizi xii
I. KIRI YA IMANI 1
SURA YA 1. KUHUSU MAANDIKO MATAKATIFU 2
SURA YA 2. KUHUSU MUNGU NA UTATU MTAKATIFU 8
SURA YA 3. KUHUSU AMRI ZA MUNGU ZA MILELE 10
SURA YA 4. KUHUSU UUMBAJI 14
SURA YA 5. KUHUSU MAONGOZI YA MUNGU 15
SURA YA 6. KUHUSU ANGUKO LA MWANADAMU, DHAMBI, NA ADHABU YA DHAMBI 18
SURA YA 7. KUHUSU AGANO LA MUNGU NA MWANADAMU 21
SURA YA 8. KUHUSU KRISTO MPATANISHI 24
SURA YA 9. KUHUSU UTASHI HURU 28
SURA YA 10. KUHUSU WITO WENYE UFANISI 30
SURA YA 11. KUHUSU KUHESABIWA HAKI 32
SURA YA 12. KUHUSU KUFANYWA WANA 35
SURA YA 13. KUHUSU UTAKASO 36
SURA YA 14. KUHUSU IMANI IOKOAYO 37
SURA YA 15. KUHUSU TOBA ILETAYO UZIMA 39
SURA YA 16. KUHUSU MATENDO MEMA 41
SURA YA 17. KUHUSU UVUMILIVU WA WATAKATIFU 45
SURA YA 18. KUHUSU UHAKIKISHO WA NEEMA NA WOKOVU 46
SURA YA 19. KUHUSU SHERIA YA MUNGU 49
SURA YA 20. KUHUSU UHURU WA KIKRISTO NA UHURU WA DHAMIRI 53
SURA YA 21. KUHUSU IBADA NA SIKU YA SABATO 55
SURA YA 22. KUHUSU VIAPO HALALI NA NADHIRI 59
SURA YA 23. KUHUSU MAMLAKA YA KIRAIA 62
SURA YA 24. KUHUSU NDOA NA TALAKA 65
SURA YA 25. KUHUSU KANISA 68
SURA YA 26. KUHUSU USHIRIKA WA WATAKATIFU 70
SURA YA 27. KUHUSU SAKRAMENTI 71
SURA YA 28. KUHUSU UBATIZO 73
SURA YA 29. KUHUSU MEZA YA BWANA 76
SURA YA 30. KUHUSU SERIKALI YA KANISA NA NIDHAMU 80
SURA YA 31. KUHUSU SINODI NA MABARAZA YA KANISA. 81
SURA YA 32. KUHUSU HALI YA MWANADAMU BAADA YA KIFO NA UFUFUO WA WAFU 83
SURA YA 33. KUHUSU HUKUMU YA MWISHO 84
II. KATEKISIMU KUBWA 86
SEHEMU I. KANUNI ZA MSINGI 87
SEHEMU II. KILE AMBACHO MWANADAMU ANAPASWA KUAMINI KUHUSU MUNGU 88
Sehemu ya IIA. Asili ya Mungu 88
Sehemu ya IIB. Amri za Mungu 90
Sehemu ya IIB.1. Agano la Neema 98
Sehemu ya IIB.2. Asili ya Kristo, Mpatanishi wa Agano la Neema 100
Sehemu ya IIB.3. Mchakato wa Ukombozi katika Agano la Neema 110
SEHEMU YA III. JUKUMU AMBALO MUNGU ANATAKA KWA MWANADAMU 125
Sehemu ya IIIA. Amri Kumi 128
Sehemu ya IIIA.1. Wajibu wetu kwa Mungu 131
Sehemu ya IIIA.2. Wajibu wetu kwa Wanadamu 142
Sehemu ya IIIB. Asili ya Dhambi 156
Sehemu ya IIIC. Njia za Neema 160
Sehemu ya IIIC.1. Neno 160
Sehemu ya IIIC.2. Sakramenti 164
Sehemu ya IIIC.2.1. Ubatizo 166
Sehemu ya IIIC.2.2. Meza ya Bwana 167
Sehemu ya IIIC.3. Maombi 173
viambatisho 185
1. Imani ya Mitume 185
2. Imani ya Nikea (AD 325) 185
3. Sala ya Bwana 186
4. Amri Kumi (Kut. 20:1-17) 186

Citation preview

MISINGI YA IMANI

MAFUNDISHO YA MSINGI YA KIBIBLIA KUHUSU IMANI YA KIKRISTO

THE WESTMINSTER CONFESSION OF FAITH AND LARGER CATECHISM

D.J. SENI 2

Hakimiliki © D.J. Seni 2020 Chapa ya kwanza, [email protected]

Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP) [+255-755-643-590] Mchapaji: Truth Printing [+255-764-425-704] hakuna sehemu ya chapisho hili la Kiswahili inayoweza kuzalishwa tena katika umbo kama hili kwa manufaa ya kibiashara bila idhini ya mfasiri. Hata hivyo, wasomaji wanaruhusiwa kutoa nakala kwa kadri wawezavyo isipokuwa isiwe kwa ajili ya biashara. _____________________________ Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV). Kitabu hiki kimetanguliwa na mambo muhimu katika Imani ya Kikristo; Imani ya Mitume, Imani ya Nikea (AD 325), Sala ya Bwana, na Amri Kumi za Mungu. ________________________ Kinapatikana Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam.

3

Tabaruku Kwa wachungaji, Wazee wa Kanisa, Mashemasi, Viongozi wa idara, na Wakristo wote watakatumia kitabu hiki.

i

Dibaji Ukichunguza historia utagundua kwamba Kanisa la Afrika kwa sasa ndilo tumaini la ulimwengu. Tumeona mataifa ya Magharibi yanapoteza nguvu ya injili, lakini mataifa ya Afrika yanamtafuta Mungu kwa shauku kubwa. Zamani, Ukristo huko Ulaya uliunda “Jumuiya ya Wakristo” ambayo iliongoza jamii, vivyo hivyo, leo, makanisa ya Afrika yanaunda “Jumuiya ya Wakristo” barani Afrika licha ya mizozo na migogoro ya kijamii. Hamu hii ya makanisa ya Afrika kwa Injili inaathiri makanisa ya Ulaya, Amerika Kaskazini na Kusini, na Asia; mataifa ambayo yalituma wamishonari Afrika. Afrika ni hazina ya maliasili na watu ambao wana hekima waliyopewa na Mungu na ubora wa kiroho. Hata hivyo, ili Kanisa la Afrika liunde “Jumuiya ya Wakristo” ya kweli kupitia injili, kipaumbele cha kwanza ni kuelewa na kutumia ukweli unaozungumzwa katika Biblia pamoja na shauku yao kwa injili. Katika mazingira haya, Mungu ameachilia baraka yake ya kushangaza, kwamba Mch. Daniel John Seni ametafsiri na kuchapisha tafsiri ya Kiswahili ya “Westminster Confession Faith and Shorter Lager Catechism.” Siku hizi Kiswahili kimekuwa kikitumika katika nchi za maziwa makuu; Tanzania, Kenya, DRC, Uganda, Rwanda na nyinginezo. Pia ni lugha rasmi ya matumizi kwa EAC na SADC. Kwa hiyo, ninaamini kuwa kuchapishwa kwa vitabu hivi katika lugha ya Kiswahili itakuwa fursa kwa wachungaji wanaohudumu katika nchi zinazozungumza Kiswahili, na vile vile walei ambao hawajui lugha za kigeni kama vile Kiingereza na Kifaransa, kwa urahisi wanaweza kusoma, kuelewa na kutumia ukweli wa injili kwa maisha yao kupitia kitabu hiki. Ikumbukwe kwamba, madhumuni ya vitabu hivi katika miaka ya 1600 ilikuwa siyo tu kurekebisha maisha ya mtu binafsi ii

bali pia familia, kanisa na serikali kupitia injili na theologia ya kibiblia. Katika historia ya Kanisa, Wapuriti walishika mafundisho haya, na waliposafiri kutoka Uingereza kwenda Amerika waliunda Amerika ya leo kama msingi wa jamii ya Kikristo, na Upresibiteri, ambapo kwa pamoja zikawa nguvu ya demokrasia ya Ulaya na maendeleo ya kiuchumi. Kwa hiyo, kupitia kitabu hiki natumaini kwamba itakuwa hatua nzuri kwa kanisa la Afrika kuibadilisha Afrika kuwa nchi ya baraka, na theologia thabiti, huku Tanzania ikiongoza vuguvugu la mabadiliko hayo. Rev. Joshua J. S. Lee Mwanzilishi wa Korea Church Mission Tanzania Mwanzilishi wa Chuo cha Calvin Theological College-Dar es salaam. Mwanzilishi wa Chuo cha United African University of Tanzania-Kigamboni, Dar es salaam Mmisionari Mwandamizi wa Tanzania.

iii

Maelezo ya Mfasiri Kama leo nikiulizwa ni kazi gani ngumu ambayo iliwahi kuniumiza, kunikera na kunisumbua; lakini pia ni kazi iliyowahi kunifurahisha na kunifundisha, basi itakuwa ni kazi ya kutafsiri vitabu vya Westminster Confession of Faith na Westminster Shorter and Larger Catechisms.” Ugumu wa kazi hii unatokana na sababu zifuatazo: Kwanza, Kiingereza ambacho kimetumika ni cha kizamani. Kama tunavyojua kwamba lugha hukua, kiingereza cha mwaka 1600 hakiwezi kufanana na kiingereza cha leo Pili, kutafsiri kitabu cha mafundisho ya Kikristo (Christian Doctrines) inahitaji ufahamu za ziada ya theologia; kwani si suala la kujua Kiswahili na Kiingereza tu. Kwa sababu hiyo, ilihitaji kuwa na mawanda mapana ya ufahamu na msimamo mzuri wa Kitheologia ili kuepuka ushawishi wa mawazo ya kizushi katika tafsiri. Ingawa ilikuwa ni kazi ngumu, bado nilisukumwa na sababu kuu mbili: Kwanza, ni ile nia yangu ya kutafsiri vitabu hivi na msukumo wa ndani wa muda mrefu wa kutamani kutafsiri vitabu ambavyo vina mafundisho sahihi ya Kikristo. Hata nilipokuwa mwanafunzi wa Calvin Theological College (CTC)nilijaribu kutafsiri Katiba ya Kanisa letu iliyokuwa katika lugha ya Kiingereza, kazi ambayo ilizaa matunda machache ukilinganisha na nguvu iliyotumika. Nilipomaliza CTC nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es saalam na kusoma shahada ya Kiswahili. Wakati ule sikujua kwa nini nilichukua somo la Kiswahili; kwa kweli, mwalimu na mlezi wangu alinishauri nisome tu Kiswahili. Nimekuja kujua kusudi la Mungu kwa nini alitaka nisome lugha iv

hii adhimu; ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba ninatafsiri na kuandika vitabu vya Kitheologia. Sababu ya pili, ni kutokana na kozi ya Uzamivu. Nilipojiunga na chuo cha “Calvin University Graduate School of Theology,” somo la kwanza lilikuwa ni Soteriologia na Neumatologia, (soteriology and Pneumatology) na kazi ambayo nilipewa ni kufanya uchambuzi wa “Westminster Confession of Faith” kwa kuzingatia vitabu vya Wanamarekebisho. Kwa kweli haikuwa kazi rahisi, hata hivyo, ni kazi ambayo ilinichochea sana kutafsiri kwa sababu nilijikuta naogelea kwenye vitabu hivi kwa zaidi ya miezi mitatu. Mwishoni mwa kozi nilimua kwa vyovyote vile lazima nitafsiri vitabu hivi ambavyo ni lulu kwa Kanisa. Ninaamini kwamba mamlaka ya mwisho kwetu Wakristo ni Biblia, hata hivyo, kitabu hiki ni ufafanuzi na uchambuzi bora wa mafundisho muhimu ya Kibiblia kwa Wakristo. Tafsiri ya kitabu hiki imezingatia muktadha wa kanisa la Tanzania na Afrika kwa ujumla. Katika kuzingatia muktadha huu, niliamu kuviunganisha vitabu vyote viwili ili kiwe kitabu kimoja. Baada ya kushauriana na Wachungaji kadhaa, niliamua kuviita kwa jina moja, “Misingi ya Imani: Mafundisho ya Msingi ya Kibiblia kuhusu Imani ya Kikristo.” Kwa jina hili, haimaanishi kwamba kuna mabadiliko yoyote ya ujumbe au muundo wa ndani, bali ni kitu kilekile isipokuwa nimeangalia muktadha wetu. Pamoja na kuzingatia muktadha, hata hivyo nimezingatia pia tahajia ya awali, bila kupoteza maana ya msingi. Mwishoni mwa kitabu hiki nimeambatisha imani ya mitume, imani ya Nikea, Sala ya Bwana na Amri Kumi za Mungu. viambatisho hivi havipo kwenye lugha chanzi ya vitabu hivi lakini nimeona ni vyema kuviweka kwa sababu ya ufupisho wake wa imani ya Kikristo. v

Nawashukuru wote ambao walinitia moyo na kuniombea katika kutafsiri vitabu hivi. Nawashukuru pia wale ambao wamesaidia uchapishaji wa kitabu hiki. Nawashukuru wamishenari wote wanaofanya kazi nchini Tanzania, bila kuwasahau kwa upekee wamisionari wa Korea Church Mission Tanzania (KCM) kwa umoja wao na ushirikiano na subira ya kutamani kitabu hiki kichapishwe ili kitumike katika makanisa ya Tanzania. Daniel John Seni Calvin Graduate School of Theology Seoul, Korea Kusini Desemba 2020

vi

Maelekezo kwa Mtumiaji 1. Maneno yaliyo katika mabano haya […..] ni ufafanuzi wangu binafsi kwa ajili ya kuelewesha zaidi 2. Mabano ( ) yakiwa juu yanamaanisha namba ya andiko linalohusiana na maelezo hayo. a) Mabano haya yanaonyesha maelezo yaliyo kushoto na wala si kulia. Kwa mfano “Kuna Mungu mmoja aliye hai, wa kweli (1) mkamilifu,(2)…” Hapa namba moja (1) inalejelea sentensi ya kwanza. Kwamba ukiangalia chini utakuta Maandiko yake kwa namba moja. b) Kwa maneno mengine, pale unapokutana na namba iko kwenye mabano ( ) unapaswa kuendelea kusoma bila kusimama, isipokuwa zingatia alama za uandishi. c) Namba za kwenye mabano siyo mbadala wa alama za uandishi, hivyo zisitumike kama alama za uandishi na badala yake zitumike kuongoza uthibitisho wa Maandiko. d) Msomaji unashauriwa kusoma mpaka mwisho wa “sehemu” ndipo urudi nyuma kuanza kuthibitisha kwenye Maandiko ikiwa utataka kufanya hivyo. 3. Vifupisho vya Biblia vilivyotumika siyo rasmi kwa sababu kuna aina mbalimbali za vifupisho; hata hivyo vifupisho vilivyotumika vinavyojulikana kwa walio wengi. 4. Unukuzi: Msomaji unapotaka kunukuu au kurejelea kitabu hiki tumia mfumo ufuatao: a) Kwa kitabu cha Imani anza na neno WCF ikifuatiwa na namba ya sura, na kisha namba ya sehemu; Kwa mfano WCF/1/1 b) Kwa Katekisimu, anza na neno WLC, likifuatiwa na namba ya swali; Kwa mfano WLC/1/ vii

YALIYOMO Tabaruku ............................................................................................ i Dibaji ................................................................................................ ii Maelezo ya Mfasiri .......................................................................... iv Maelekezo kwa Mtumiaji ............................................................... vii Utangulizi........................................................................................ xii I.

KIRI YA IMANI ....................................................................... 1

SURA YA 1. KUHUSU MAANDIKO MATAKATIFU ................. 2 SURA YA 2. KUHUSU MUNGU NA UTATU MTAKATIFU ..... 8 SURA YA 3. KUHUSU AMRI ZA MUNGU ZA MILELE ......... 10 SURA YA 4. KUHUSU UUMBAJI .............................................. 14 SURA YA 5. KUHUSU MAONGOZI YA MUNGU .................... 15 SURA YA 6. KUHUSU ANGUKO LA MWANADAMU, DHAMBI, NA ADHABU YA DHAMBI ...................................... 18 SURA

YA

7.

KUHUSU

AGANO

LA

MUNGU

NA

MWANADAMU ............................................................................ 21 SURA YA 8. KUHUSU KRISTO MPATANISHI ........................ 24 SURA YA 9. KUHUSU UTASHI HURU ..................................... 28 SURA YA 10. KUHUSU WITO WENYE UFANISI .................... 30 SURA YA 11. KUHUSU KUHESABIWA HAKI ........................ 32 SURA YA 12. KUHUSU KUFANYWA WANA ......................... 35 SURA YA 13. KUHUSU UTAKASO ........................................... 36 SURA YA 14. KUHUSU IMANI IOKOAYO ............................... 37 viii

SURA YA 15. KUHUSU TOBA ILETAYO UZIMA ................... 39 SURA YA 16. KUHUSU MATENDO MEMA ............................. 41 SURA YA 17. KUHUSU UVUMILIVU WA WATAKATIFU .... 45 SURA YA 18. KUHUSU UHAKIKISHO WA NEEMA NA WOKOVU ...................................................................................... 46 SURA YA 19. KUHUSU SHERIA YA MUNGU ......................... 49 SURA YA 20. KUHUSU UHURU WA KIKRISTO NA UHURU WA DHAMIRI ............................................................................... 53 SURA YA 21. KUHUSU IBADA NA SIKU YA SABATO ......... 55 SURA YA 22. KUHUSU VIAPO HALALI NA NADHIRI.......... 59 SURA YA 23. KUHUSU MAMLAKA YA KIRAIA ................... 62 SURA YA 24. KUHUSU NDOA NA TALAKA .......................... 65 SURA YA 25. KUHUSU KANISA ............................................... 68 SURA YA 26. KUHUSU USHIRIKA WA WATAKATIFU ........ 70 SURA YA 27. KUHUSU SAKRAMENTI .................................... 71 SURA YA 28. KUHUSU UBATIZO ............................................. 73 SURA YA 29. KUHUSU MEZA YA BWANA ............................ 76 SURA YA 30. KUHUSU SERIKALI YA KANISA NA NIDHAMU ........................................................................................................ 80 SURA YA 31. KUHUSU SINODI NA MABARAZA YA KANISA. ........................................................................................................ 81 SURA YA 32. KUHUSU HALI YA MWANADAMU BAADA YA KIFO NA UFUFUO WA WAFU ................................................... 83 SURA YA 33. KUHUSU HUKUMU YA MWISHO .................... 84 ix

II.

KATEKISIMU KUBWA .................................................... 86

SEHEMU I. KANUNI ZA MSINGI .............................................. 87 SEHEMU II. KILE AMBACHO MWANADAMU ANAPASWA KUAMINI KUHUSU MUNGU ..................................................... 88 Sehemu ya IIA. Asili ya Mungu .................................................. 88 Sehemu ya IIB. Amri za Mungu .................................................. 90 Sehemu ya IIB.1. Agano la Neema .......................................... 98 Sehemu ya IIB.2. Asili ya Kristo, Mpatanishi wa Agano la Neema ..................................................................................... 100 Sehemu ya IIB.3. Mchakato wa Ukombozi katika Agano la Neema ..................................................................................... 110 SEHEMU YA III. JUKUMU AMBALO MUNGU ANATAKA KWA MWANADAMU ................................................................ 125 Sehemu ya IIIA. Amri Kumi...................................................... 128 Sehemu ya IIIA.1. Wajibu wetu kwa Mungu ......................... 131 Sehemu ya IIIA.2. Wajibu wetu kwa Wanadamu .................. 142 Sehemu ya IIIB. Asili ya Dhambi .............................................. 156 Sehemu ya IIIC. Njia za Neema ................................................. 160 Sehemu ya IIIC.1. Neno ......................................................... 160 Sehemu ya IIIC.2. Sakramenti................................................ 164 Sehemu ya IIIC.2.1. Ubatizo .................................................. 166 Sehemu ya IIIC.2.2. Meza ya Bwana ..................................... 167 Sehemu ya IIIC.3. Maombi ........................................................ 173 x

viambatisho ................................................................................... 185 1.

Imani ya Mitume ................................................................... 185

2.

Imani ya Nikea (AD 325) ...................................................... 185

3.

Sala ya Bwana ....................................................................... 186

4.

Amri Kumi (Kut. 20:1-17) .................................................... 186

xi

Utangulizi Kitabu hiki ni tafsiri ya vitabu viwili; The Westminster Confession of Faith and Larger Catechisms, ambapo kwa Kiswahili tunatafsiri “Kiri ya Imani ya Westminster na Katekisimu Kubwa. Kiri ya Imani ya Westminster iliandaliwa kuanzia mwaka 1643 hadi 1647 na baraza kuu la Westminster. Inaitwa Kiri ya Imani ya Westminster kwa sababu mkutano ulifanyika katika mji wa Westminster huko London, Uingereza. Ama kuhusu Katekisimu, kuna katekisimu za Westminister za aina mbili; Katekisimu Kubwa na katekisimu Fupi. Katekisimu hizi ziliandaliwa na Baraza la Westminster kuanzia mwaka 1643 hadi 1649. Katekisimu iliyo katika kitabu hiki ni ile Kubwa. Kitabu hiki kimesheheni mambo ya msingi ya imani ya Kikristo. Kwa sababu hiyo, madhehebu mengi ya Kikristo hutumia vitabu hivi kwa sababu ya ufupisho wake. Mafundisho yote ya msingi kuhusu imani ya Kikristo yamefafanuliwa. Kitabu hiki kinaweza kutumika kwanza kuwafundishia wachungaji na wazee wa kanisa, halafu baadaye watumie katika kufundishia shule za Jumapili zijulikanazo kama ‘Sunday Schools kwa watu wazima” au “Bible Studies” makanisani. Kwa sababu hiyo kitabu hiki tumekiita “Misingi ya Imani: Mafundisho ya Kibiblia kuhusu Imani ya Kikristo.” Tunashauri watumiaji wa Kitabu hiki watumie pamoja na Maandiko Matakatifu.

Daniel John Seni Calvin Graduate School of Theology Seoul, Korea Kusini Desemba 2020

xii

I. KIRI YA IMANI

1

SURA YA 1. KUHUSU MAANDIKO MATAKATIFU Sehemu ya 1 Ingawa kazi ya uumbaji hudhihirisha wema, hekima, na nguvu za Mungu, kwa kutowaacha watu pasipo na udhuru;(1) Hata hivyo, kazi za uumbaji wa Mungu hazitoshi kutoa ujuzi wote juu ya Mungu, na mapenzi yake, ambayo ni muhimu kwa wokovu.(2) Kwa hiyo ilimpendeza BWANA, kwa nyakati tofauti, na kwa njia tofauti, kujifunua mwenyewe, na kutangaza mapenzi yake kwa Kanisa lake.(3) Baadaye ilimpendeza kuweka ufunuo huu mzima katika Maandiko [yaani Biblia] ili ukweli uweze kuhifadhiwa na kupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Na kwamba kanisa liweze kuwa imara, na kufarijika pindi linapokabiliwa na ufisadi wa kimwili na makusudi mabaya ya Shetani na ulimwengu. (4) Kwa kuwa Mungu hajifunui tena kwa watu wake kwa njia hizo za zamani, (5) basi, Maandiko Matakatifu ni ya muhimu sana. (6) (1) Rum. 2:14-15, 1:19-20, Zab. 19:1-4, Rum. 1:32, 2:1 (2) 1 Kor. 1:21, 2.13-14, 2:9-12, Mdo. 4:12, Rum. 10:13-14 (3) Ebr. 1:1-2, Gal. 1:11-12, Kumb. 4:12-14 (4) Mith. 22:19-21, Lk 1:3-4, Rum. 15:4, Mt. 4:4,7,10, Lk. 24:27, 2 Tim. 3:16, 2 Pet. 3:15-16). (5) Ebr. 1:1-2, (6) 1Tim 3:15-16, 2 Pet. 1:10, Lk. 16:29-31, Ebr. 2:1-3

Sehemu ya 2 Kile tunachokiita Maandiko Matakatifu au Neno la Mungu lililoandikwa ni pamoja na vitabu vyote vya Agano la Kale na Agano Jipya ambavyo ni hivi vifuatavyo: 2

VITABU VYA SHERIA Mwanzo Kutoka Mambo ya Walawi Hesabu Kumbukumbu la Torati VITABU VYA HISTORIA Yoshua Waamuzi Ruthu 1 Samwel 2 Samwel 1 Wafalme 2 Wafalme 1 Nyakati 1 Nyakati Ezra Nehemia Esta

AGANO LA KALE VITABU VYA MASHAIRI Ayubu Zaburi Mithali Mhubiri Wimbo Ulio Bora MANABII WAKUBWA Isaya Yeremia Maombolezo Ezekiel Daniel

3

VITABU VYA MANABII WADOGO Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki

AGANO JIPYA VITABU VYA INJILI NYARAKA Mathayo Warumi, Marko 1 Wakorintho, Luka 2 Wakorintho Yohana Wagalatia, KITABU CHA HISTORIA Waefeso Matendo ya Mitume Wafilipi Wakolosai 1 Wathesalonike 2 Wathesalonike 1 Timotheo 2 Timotheo Tito Filemoni, Waebrania Yakobo 1 Petro 2 Peter 1 Yohana 2 Yohana 3 Yohana Yuda KITABU CHA UNABII Ufunuo.

Maandiko haya yote yamevuviwa na Roho Mtakatifu kuwa mwongozo wa imani na maisha kwa ujumla (Lk 16:29,31, Efe 2:20, Ufu. 22:18-19, 2 Tim 3:16, Mt 11:27).

4

Sehemu ya 3 Vitabu vilivyo katika Apokrifa sio sehemu ya Biblia, kwa sababu havijavuviwa na Mungu. Hii inamaanisha kuwa havina mamlaka kwa Kanisa. Badala yake, tunapaswa kuvichukulia kama vile maandishi mengine ya kibinadamu tu.(1) Hakuna vifungu vya moja kwa moja vinavyozungumzia Kanoni ya Maandiko lakini kwa ushuhuda wa Yesu na mitume wake; na maandishi ya kale; Waandishi wa Kikristo wa zamani na mabaraza ya kanisa, na kwa ushahidi wa ndani ulioonyeshwa katika vitabu tofautitofauti huthihirisha uwepo wa kanoni. (1) Lk 24.27,44, Rum 3:2, 2 Pet 1:21. Sehemu ya 4 Biblia inazungumza kwa mamlaka na kwa hiyo watu wanapaswa kuiamini na kuitii. Mamlaka haya hayategemei ushuhuda wa mtu yeyote au kanisa, lakini inategemea Mungu mwenyewe, ambaye ndiye mwandishi wa Biblia, na yeye mwenyewe ni ukweli. Kwa hiyo, Biblia inapaswa kupokelewa kuwa ndiyo kweli, kwa sababu ni Neno la Mungu (2 Pet 1:19,21, 2 Tim 3:16, 1 Yoh 5:9, 1 Thes 2:13, Gal 1:11-12). Sehemu ya 5 Ushuhuda wa kanisa unatusukuma kuithamini sana Biblia na kuiheshimu, na Maandiko yenyewe yanaonyesha kwa njia nyingi sana kwamba ni Neno la Mungu; kwa mfano, katika mambo yake ya kiroho, katika ukamilifu wa mafundisho yake, ubora wa namna ilivyo, ukubalifu wa sehemu zake zote, kusudi lake tangu mwanzo mpaka mwisho [kumpa Mungu utukufu wote, na ufunuo wake kuhusu wokovu wa mwanadamu. Pia 5

Roho Mtakatifu anashuhudia ndani ya mioyo yetu kwa kutuhakikishia ukweli wa Biblia usiotakunguka na mamlaka ya Kimungu (1 Tim 3:15, 1Yoh 2:20,27, Yn 16:13-14, 1 Kor 2:1012, Isa 59:21, 1 Kor 2:6-9). Sehemu ya 6 Mungu ameweka katika Biblia kila kitu tunachohitaji kujua juu ya utukufu wake, wokovu, imani, na maisha yetu. Yeye ameandika vitu hivi katika Biblia moja kwa moja, na ameturuhusu kuvichunguza kwa kutumia hoja zetu.(1) Hakuna kitu kinachohitajika kuongezwa kwenye Biblia, iwe ni "ufunuo mpya kutoka kwa Roho" au iwe ni mila na tamaduni za mwanadamu.(2) Walakini, tunatambua kuwa mwangaza wa ndani wa Roho wa Mungu ni muhimu kwa ufahamu uokoao uliofunuliwa katika Neno.(3) Tunatambua pia kuwa vitu muhimu vya ibada ya Mungu na serikali ya kanisa vinapaswa kuelekezwa kulingana na uelewaji wetu wa asili na busara yetu ya Kikristo na tunapaswa kufuata sheria za jumla za Neno.(4) (1) (2) (3) (4)

Mk 7:5-7 2 Tim 3:15-17, Gal 1:8-9, 2 Thes 2:2 Yn 6:45, 1 Kor 2:9-10, 12 1 Kor 11:13-14, 14:26,40

Sehemu ya 7 Sio kila kitu kiko wazi kwenye Biblia, na sio mafundisho yote yafundishwayo yako wazi kwa kila mtu.(1) Walakini, kila kitu ambacho tunapaswa kujua, na kuamini kuhusu wokovu vimefunuliwa wazi katika Biblia; yaani kwamba wasio na elimu, na wenye elimu pia wanaweza kuelewa vya kutosha matumizi sahihi ya njia ya kawaida ya neema.(2) (1) 2 Pet 3:16, Yn 6:60, 16:17 (2) Zab.119:105, 130, Mdo 17:11-12

6

Sehemu ya 8 Agano la Kale kwa Kiebrania (lugha ya asili ya watu wa kale wa Mungu) na Agano Jipya kwa Kiyunani (lugha iliyojulikana sana kimataifa wakati Agano Jipya lilipoandikwa) yalivuviwa moja kwa moja na Mungu na Maagano haya mawili (Kale na Jipya) yametunzwa bila kuchafuliwa kwa vizazi na vizazi. Kwa hiyo ni Maandiko ya kweli na yanatumika pia kama marejeleo kwa kanisa katika mabishano (Mt 5:18, Isa 8:20, Mdo 15:1418, Yn 5:9,46). Hata hivyo lugha za asili za Biblia hazieleweki na watu wote wa Mungu. Lakini watu wote wa Mungu wana haki ya kusoma na kujua kilicho ndani ya Biblia na Mungu mwenyewe huwaamuru watu wasome Neno lake kwa hofu na kumheshimu Mungu (Yn 5:39, 2 Tim 3:14-15, 2 Pet 1:19, Mdo 17:11). Kwa hiyo, Biblia inapaswa kutafsiriwa kwa lugha ya asili ya kila kabila. Na hapo ndiposa Neno la Mungu litaishi kikamilifu kwa kila mtu; kila mtu ataweza kumwabudu Mungu kwa njia inayokubalika; na Waamini wote wanaweza kuwa na tumaini kupitia uvumilivu wao na faraja ya Biblia (1 Kor 14:6, 9, 1112, 24, 27-28, Kol 3:16, Rum 15:4, Mt 28:19-20). Sehemu ya 9 Kiwango kamili cha kutafsiri Biblia ni Biblia yenyewe. Na kwa hiyo swali lolote juu ya ukweli kuhusu kifungu katika Biblia kinaweza kujibiwa kwa kurejelea vifungu vingine ambavyo huzungumza waziwazi juu ya kitu kilekile, kwa sababu Biblia ina umoja na haipingani. (2 Pet 1:20-21, Mdo15:15, Yn 5:46, Mt 4:5-7, 12:1-7)

7

Sehemu ya 10 Roho Mtakatifu anayezungumza katika Biblia ndiye Mwamuzi mkuu wa mabishano yote ya kidini, maamuzi yote ya mabaraza ya kanisa, maoni yote ya waandishi wa zamani, mafundisho yote ya wanadamu, na kila maoni ya kibinafsi. Tunapaswa kuridhika na hukumu yake (Mt 22:29,31, Efe. 2:20, Mdo 28:25, Lk 10:26, Gal 1:10, 1 Yn 4:1-6).

SURA YA 2. KUHUSU MUNGU NA UTATU MTAKATIFU Sehemu 1 Kuna Mungu mmoja aliye hai, wa kweli (1) mkamilifu, (2) ni Roho,(3) asiyeonekana, (4) asiye na mwili, (5)asiyebadilika, (6) Mkuu sana(7) wa Milele, (8) asiye na Mwanzo wala Mwisho,(9) mwenye Nguvu,(10) mwenye Busara,(11) Mtakatifu, (12) mwenye uhuru wa kufanya lolote.(13) Yeye hufanya kazi kulingana na kusudi, mwenye Haki, mwenye Utukufu, (14) mwenye Upendo usokifani. (15) Mwenye Neema, mwenye Huruma, na Uvumilivu. Yeye hufurika kwa Wema na Ukweli. Yeye husamehe uovu, udhalimu, na dhambi (16) Hulipa malipo wale wanaomtafuta kwa bidii.(17) Hukumu zake ni za haki kabisa na za kushangaza, (18) Mwenye kuchukia dhambi. (19) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Kumb. 6:4, 1 Kor 8:4,6, 1 Thes 1:9, Yer 10:10 Ayu. 11:7-9, 26:14, Yer 23:24, Zab. 147:5, 1Fal 8:27, Zab. 139 Yn 4:24 1 Tim 1.17 Kumb. 4:15-16, Yn 4:24, Lk 24:39, Mdo 14:11,15 Yak. 1:17, Mal 3:6. 6 1 Fal 8:27, Yer 23:23-24

8

(8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17) (18) (19)

Zab. 90:2, 1Tim 1:17 Zab.145:3, Rum 11:33 Mwa. 17:1, Ufu. 4:8. Rum 16.27 Isa. 6.3, Ufu. 4:8 Zab. 115:3 Mith.16:4, Rum 11:36, Ufu 4:11 1 Yn 4:8-10, 16, Yn 3:16 Kut. 34:6-7 Ebr. 11:6 Neh 9.32-33, Hes. 10.28-31 Zab. 5:5-6, Ebr 1:13

Sehemu ya 2 Mungu anao uhai wote, utukufu, wema, na baraka. (1) Yeye pekee anajitosheleza, hahitaji uumbaji wake wowote au kupata utukufu wowote kutoka kwa viumbe vyake, na badala yake, anajidhihirishia utukufu wake mwenyewe.(2) Yeye ndiye chanzo pekee cha wenye uhai wote, kupitia yeye, na kwake kila kitu kinaishi. (3) Hutawala juu ya vitu vyote na hufanya kwa ajili yao chochote apendacho.(4) Kila kitu hufunuliwa wazi kwake.(5) Maarifa yake hayana mipaka, na hayafanyi kwa kutegemea kiumbe chochote alichokiumba.(6) Yeye ni Mtakatifu kabisa katika makusudi yake yote, kazi, na amri.(7) Ni wa kuabudiwa na viumbe vyote duniani. (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Yn 5:26, Mdo 7:2, Zab. 119:68, 1 Tim 6:15, Rum 9:5. Mdo 17:24-25, Ayu. 22:2,23, Zab. 50:12, Isa 4:12-17). Rum 11:36, Isa 40:12-17). Ufu. 4:11, 1 Tim 6:15, Dan 4:25, 35, Efe. 1:11). Ebr. 4:13). Rum 11:33-34, Zab. 147:5). Zab. 145:17, Rum 7:12

9

Sehemu ya 3 Katika umoja wa Uungu kuna nafsi tatu, zenye asili moja, nguvu, na umilele: Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu.(1) Mungu Baba hajazaliwa, na wala hatokani na chanzo chochote, Mungu Mwana ni wa milele kutoka kwa Baba. (2) na Mungu Roho Mtakatifu ni wa milele kutoka kwa Baba na Mwana. (3) (1) 1 Yn 5:7, Mt 3:16-17, 28:19, 2 Kor 13:14, Efe. 2:18 (2) Yn 1:14,18, 17:24, Ebr 1:2-6, Kol 1:15-17 (3) Yn 15:26, Gal 4:6

SURA YA 3. KUHUSU AMRI ZA MUNGU ZA MILELE Sehemu ya 1 Tangu asili, Mungu ameamua na kuweka kila kitu kinachotokea. Yeye hufanya maamuzi haya kwa uhuru na kwa mapenzi Yake ya busara na utakatifu.(1) Hakuna kitu ambacho ameamua tangu asili kinaweza kubadilika. Maamuzi haya haimaanishi kwamba Mungu ndiye mwanzilishi wa dhambi,(2)na kwamba Yeye hutulazimishi kufanya vitu kinyume cha mapenzi yetu. Yeye ndiye chanzo cha kila kitu, lakini hii haimaanishi kwamba vitu vingine havihusiki; hata hivyo, Mungu ndiye sababu ya vitu vingine kuwepo.(3) (1) Efe 1:11, Rum 11:33, Ebr 6:17, Rum 9:15,18, Mdo 4:27-28, Mt 10:29-30, Efe. 2:10, Isa 45:6-7). (2) Yak. 1:13-14, 17, 1 Yn 1:5, Mh. 7:29, Zab 5:4 (3) Mdo 2:23, Mt 17:12, Mdo 4:27-28, Yn 19:11, Mith 16:33, Mdo 27:23-24, 34, 44).

10

Sehemu ya 2 Ingawa Mungu anajua chochote kinachoweza kutokea katika hali zote zinazowezekana, (1) hata hivyo, hajaamuru kitu chochote kitokee kwa sababu aliona tangu asili kwamba kitatokea kwa namna yoyote ile. (2) (1) Mdo. 15:18, 1Sam. 23:11-12, Mt 11:21,23, Zab. 139:1-4, Mith. 16:33 (2) Rum. 9:11,13, 15-16, 18, 2 Tim 1:9, Efe. 1:4-5).

Sehemu ya 3 Ili kudhihirisha utukufu wake Mungu amewachagua watu wengine na malaika kwa uzima wa milele,(1) na kwamba wengine amewachagua kwa maangamizo ya milele. (2) (1) 1 Tim 5:21, Mt 25:31,41, Mdo 13:48, Rum 8:29-30, Yn 10:2729, Mk 8:38, Yud 6. (2) Rum 9:22-23, Efe. 1:5-6, Mith 16:4, Mt 25:41, Yud 4).

Sehemu ya 4 Mungu amechagua idadi fulani ya watu na malaika kwa umilele wake. Idadi hii haiwezi kuongezeka wala kupunguzwa (2 Tim 2:19, Yn 13:18, 10:14-16,27-29, 6:37-39, Mdo 13:48, Yn 17:2,6,9-12). Sehemu ya 5 Mungu, kabla hata ya kuumba ulimwengu, (1) kulingana na mpango wake wa milele, usiobadilika, (2) na kusudi lililofichika la mapenzi yake mema (3) amewachagua baadhi ya wanadamu katika Kristo, (4) ambao amewachagua kwa uzima na utukufu 11

wa milele, (5) Amefanya hili kwa rehema na upendo wake na kwa sifa ya neema yake ya ajabu, (6) alifanya uchaguzi huu kwa uhuru wake mwenyewe, kwa jinsi alivyotaka viumbe vyake viwe. Uchaguzi huu hautegemei imani yao au matendo yao mema au uvumilivu wao, bali inategemea Mungu mwenyewe katika uchaguzi wake. (7) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Efe. 1:4 Efe. 1:11 Efe. 1:9 2Tim 1:9 Rum 8:30, 1Thes 5:9, 1 Pet 5:10 Efe. 1:5-6, 12 Rum 9:11, 13, 15-16, Efe. 1:4,6,9, 2 Tim 1:9, Efe. 2:8-9

Sehemu ya 6 Kwa kuwa Mungu ameamuru Wateule watukuzwe katika yeye, vivyo hivyo, katika kusudi lake la milele na huru kabisa la mapenzi yake, amepanga namna ambavyo uchaguzi huo unatimizwa. (1) Na hivyo, wale waliochaguliwa, wakiwa wameanguka katika Adamu, wamekombolewa katika Kristo. (2) Wameitwa kwa Kristo kwa imani na Roho wake anafanya kazi ndani yao kwa wakati unaofaa, (3) na wamehesabiwa haki (4) wamefanywa wana, (5) wametakaswa, (6) na wamehifadhiwa na nguvu zake kupitia imani kwa ajili ya Wokovu. (7) Ni Wateule tu, na hakuna wengine, wanaokombolewa na Kristo, wanaoitwa, wanaohesabiwa haki, wanaofanywa wana, wanaotakaswa, na wanaookolewa. (8) (1) 1 Pet. 1:2, Efe. 1:4-5, 2:10, 2 Thes. 2:13 (2) 1 Thes. 5:9-10, Tim. 2:14, Rum. 5:19 (3) Rum. 9:11, 2 Thes. 2:13-14, 1Kor.1:9

12

(4) (5) (6) (7) (8)

Rum. 8:30 Efe. 1:5 2 Thes. 2:13, Efe. 1:4, 1 Thes. 4:3 1 Pet. 1:5, Yn. 10:28 Yn. 17:9, Rum. 8:28-39, Yn. 6:64-65, 8:47, 10:26, 1 Yoh 2:19, Mdo. 13:48

Sehemu ya 7 Mungu, kulingana na makusudi ya siri ya mapenzi yake mwenyewe, ambayo yeye hutoa au huzuia rehema kwa jinsi apendavyo yeye, na kwa utukufu wa uweza wake wa kutawala juu ya viumbe vyake, ilimpendeza kutowaita baadhi ya watu wengine (1) na kuwaweka kwa uharibifu kwa ajili ya dhambi zao, (2) kwa sifa ya haki yake tukufu. (3) (1) Mt 11:25-26, 1 Pet 2:8 (2) Rum 9:14-22, Yuda 4, Rum 2:8-9, 2 Thes 2:10-1 (3) 2 Tim 2:19-20, Ufu. 15:3-4

Sehemu ya 8 Fundisho hili muhimu na la kushangaza la Kuchaguliwa na Mungu lazima lishughulikiwe kwa busara sana, ili kutii mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa katika neno lake, watu wengine wanaweza kuwa na hakika kuwa wamechaguliwa milele kutokana na ukweli wa wito wao wenye ufanisi. Kwa njia hii, fundisho la uchaguzi wa Mungu litazidi kuwafanya watu wamsifu Mungu na kuendelea kuwa wanyenyevu na kutii Injili (Rum 9:20, 11:33, Kumb. 29:29, 2 Pet 1:10, Efe. 1:6, Rum 11:5-6, 20, 8:33, Lk 10:20).

13

SURA YA 4. KUHUSU UUMBAJI Sehemu ya 1 Hapo mwanzo ilimpendeza Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu (1) kuumba ulimwengu bila kutumia kitu chochote [exnihilo] ili kudhihirisha utukufu wa uweza wake wa milele, hekima, na wema.(2) Alifanya kila kitu ulimwenguni kinachoonekana na kisichoonekana, kwa muda wa siku sita, na Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.(3) (1) Ebr. 1:2, Yn 1:2-3, Mwa. 1:1-3, Ayu. 26:13, 33:4, Rum. 11:36, 1 Kor 8.6 (2) Rum. 1:20, Yer. 10:12, Zab. 104:24, 33:5-6 (3) Mwa. 1, Ebr 11.3, Kol 1:16, Mdo. 17:24, Kut. 20:11

Sehemu ya 2 Baada ya Mungu kuumba viumbe vingine vyote, alimwumba mwanadamu: mwanamume na mwanamke aliwaumba, (1) wakiwa na roho zisizokufa.(2) Akawapa maarifa, haki, na utakatifu wa kweli kwa mfano wake, (3) na aliandika sheria yake mioyoni mwao. (4) Mungu pia akawapa uwezo wa kutii sheria yake na uwezekano wa kutokutii; yaani, aliwapa uhuru wa hiari yao, ambao ungeweza kubadilika. (5) Aliwamuru pia wasile kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya.(6) Ikiwa wangetii sheria ya Mungu na amri hii, wangekuwa na furaha katika ushirika na Mungu (7) na wangekuwa na nguvu juu ya viumbe vingine.(8) (1) Mwa. 1:27

14

(2) Mw. 2:7, Mhu. 12:7, Lk 23:43, Mt 10:28, Zab. 8:5-6, Mwa. 2:19-20 (3) Mwa.1:26, Kol 3:10, Efe. 4:24 (4) Rum 2:14-15 (5) Mhu. 7:29, Mwa. 3:6,17, 2.16-17, Kol 3:10, Efe. 424 (6) Mwa. 2:16-17 (7) Mwa. 2:17, 3:8-11, 23 (8) Mwa. 1:26,28, Zab. 8:6-8, Mwa. 1:29-30

SURA YA 5. KUHUSU MAONGOZI YA MUNGU Sehemu ya 1 Mungu, aliyeumba vitu vyote, (si tu kwamba aliviumba) pia anavishikilia, anaviamuru, anavisimamia, anavitawala. (1) Kwa hekima yake takatifu, Mungu anatawala kulingana na ujuzi wake kamili kwa kila kitu, kila tendo litakalotokea baadaye, na kulingana na mapenzi Yake yasiyobadilika. (2) Ushuhuda wake unastahili sifa zetu. (3) (1) Ebr. 1:3, Dan. 4:34-35, Zab. 135:6, Mdo. 17:25-26,28, Ayu. 3841, Mt 10:29-31, 6:26,30, Neh 9:6, Zab. 114:14-16 (2) Efe. 1:11, Zab. 33:10-11). (3) Isa. 63:14, Efe 3:10, Rum. 9:17, Mwa. 45:7, Zab 145:7

Sehemu ya 2 Mungu hupanga na anajua kila kitu kabla hakijatokea. Yeye ndiye "sababu ya kwanza," kwa hiyo, kila kitu kinakwenda kulingana na mpango Wake, bila kushindikana au kubadilika (1) Walakini, kwa mpango huohuo, anaamuru mambo kutokea kwa kusababishwa na viumbe vyake. Kama matokeo ya matendo ya 15

viumbe vyake kuna mambo ambayo lazima yatokee.(2) Mambo mengine yanaweza kutokea au kutokutokea kulingana na dhamira ya hiari ya vitu vinavyohusika; na mambo mengine hayatakiwi kutokea lakini yanaweza kutokea kwa kutegemeana na hali zingine.(3) (1) Mdo. 2:23, Yer. 32:19 (2) Mwa. 8:22, Yer. 31:35 (3) Kut. 21:13, Kumb. 19:5, 1 Fal. 22:28,34, Isa. 10:6-7, Mwa. 50:19-20

Sehemu ya 3 Mungu hutumia njia za kawaida kutekeleza mipango yake kila siku.(1) Lakini hufanya kwa kadri apendavyo (2) anaweza kufanya kazi au kitu chochote bila kutegemea njia za kawaida [yaani bila kutegemea viumbe vyake].(3) (1) Mdo. 27:24, 31, 44, Isa. 55:10-11, Hos. 2:21-22 (2) 2 Fal. 6:6, Dan. 3:27, 1Fal. 18:17-39, Yn. 11:43-45, Rum. 1:4 (3) Hos. 1:7, Mt. 4:4, Ayu. 34:10, Rum. 4:19-21

Sehemu ya 4 Mpango wa Mungu hufunua nguvu zake, hekima isiyojulikana kibinadamu, na wema usio na kipimo. Mpango wake unaenda hadi kwenye anguko na kwa dhambi zingine zote za malaika na wanadamu. (1) Dhambi hizi si kwamba Mungu aliruhusu tu, lakini pia zimefungwa katika mpango wake, (2) zimeamuriwa na kutawaliwa naye katika utimilifu wa hekima na nguvu yake ili kutimiza kusudi lake takatifu. (3) Walakini dhambi inabaki kwa kiumbe chenyewe na haitokani na Mungu ambaye haki yake takatifu haina uhusiano wowote na dhambi.(4) 16

(1) Rum. 11:32-34, 2 Sam. 24:1, 1 Nyak. 21:1, 1 Fal. 22:22-23, 1 Nyak. 10:4, 13-14, 2 Sam. 16:10, Mdo. 2:23, 4:27-28 (2) Mdo. 14:16, Zab. 76:10, 2 Fal. 19:28, Isa. 10:5-7,12, 15 (3) Mwa. 50:20, Isa. 10:6-7, 12-15 (4) Yak. 1:13-14, 17, 1 Yoh. 2:16, Zab. 50:21 Sehemu ya 5

Mungu, katika utimilifu wa hekima yake, haki, na neema, mara nyingi huruhusu watoto wake kujaribiwa kwa njia tofauti na kwa muda fulani kufuata uovu wa mioyo yao. Mungu huruhusu haya ili kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao za zamani na kuwafunulia nguvu iliyofichika ya uovu na udanganyifu katika mioyo yao, ili wawe wanyenyekevu.(1) Mbali na matokeo mengine kadhaa ya haki, Waamini husogezwa kwa karibu zaidi kumtegemea Mungu na pia hufanywa wawe makini zaidi katika kujua na kupinga fursa za kutenda dhambi. (2) (1) 2 Nyak. 32:25,26,31, 2 Sam. 24:1,25, Kumb. 8:2, Lk 22:31-32 (2) 2 Kor. 12:7-9, Zab 73, 77:1-12, Mk. 14:66-72, Yn. 21:15-19

Sehemu ya 6 Mungu kama Mwamuzi mwadilifu, ili kuwaadhibu watenda dhambi, huwapofusha na kuwafanya wafuate dhambi zao. (1) Pia kutoka kwa hao waovu, Mungu haondoi tu neema yake, ambapo katika hiyo wangeweza kuangaziwa kiroho (2) bali wakati mwingine huondoa zawadi yoyote ya ufahamu wa kiroho ambao walikuwa nao hapo awali (3) na kwa makusudi, huwasukumia kwenye fursa za kutenda dhambi ambayo asili yao ya uovu moja kwa moja hutafuta.(4) Kwa hiyo anawapa matamanio yao wenyewe, kwa majaribu ya ulimwengu, na kwa nguvu za Shetani (5) hivyo, wanakuwa wagumu wenyewe, hata 17

katika mazingira ambayo Mungu huyatumia kuwarudisha kwake.(6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Rum. 1:24-26,28, 11:7-8, 2 Thes. 2:11-12 Kumb. 29:4, Mk. 4:11-12 Mt. 13:12, 25:29, Mdo. 13:10-11, 2 Kor. 11:13,15 Kumb. 2:30, 2 Fal. 8:12-13 Zab. 81:11-12, 2 Thes. 2:10-12, 2 Kor. 2.11, 11:3 Kut.7:3, 8:15,32, 2 Kor. 2:15-16, Isa. 8:14, 1 Pet 2:7-8, Isa. 6:9-10, Mdo. 28:26-27

Sehemu ya 7 Kama vile Maongozi ya Mungu kwa ujumla yanavyoenea kwa kila kiumbe, kwa hivyo, kwa njia ya kipekee, yanalitunza kanisa lake na kuagiza vitu vyote kwa faida yake (1 Tim 4:10, Amo 9:8-9, Rum 8:28, Isa 43:3-5,14, Efe 1:22, Mt 16:18).

SURA YA 6. KUHUSU ANGUKO LA MWANADAMU, DHAMBI, NA ADHABU YA DHAMBI Sehemu ya 1 Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza walidanganywa na kula matunda yaliyokatazwa na Mungu kwa ushawishi wa Shetani. (1) Mungu aliwaruhusu watende dhambi kama hii kwa ajili ya kujitukuza mwenyewe, kulingana na mpango wake wa busara na mtakatifu. (2) (1) Mwa. 3:13, 2 Kor. 11:3, Mwa. 3:1-14 (2) Rum. 11:32, 5:19-21

18

Sehemu ya 2 Adamu na Hawa hapo awali walikuwa kamili, na waliweza kuzungumza na Mungu moja kwa moja, (1) lakini kwa sababu ya dhambi walianguka. Baada ya anguko walikuwa wachafu kiroho, na walikuwa wamekufa katika dhambi. Kila sehemu ya miili yao na roho ilikuwa imechafuliwa kabisa. (2) (1) Mwa. 3:6-8, Mhu. 7:29, Rum. 3:23, Mwa. 2:17 (2) Mwa. 2:17, Efe. 2:1-3, Rum. 5:12, Tit 1:15, Mwa. 6:5, Yer. 17:9, Rum. 3:10-19, 8:6-8, Zab. 58:1-5

Sehemu ya 3 Kwa kuwa Adamu na Hawa ni shina la wanadamu wote, hatia ya dhambi hii ilipitishwa kwa wanadamu wote (1) ambao ni uzao wao kwa asili na wamerithi kifo katika dhambi na asili ileile ya uchafu. (2) (1) Mwa. 1:27-28, 2:16-17, Rum. 5:12,15-19, Mdo.17:26, 1 Kor. 15:21-22,45,49 (2) Zab 51:5, Mwa. 5:3, Ayu. 14:4, 15:14, Yn. 3 na 6, Rum. 3:1018

Sehemu ya 4 Dhambi zote za kutenda [au dhambi halisi] zinatokana na dhambi hii ya asili, uchafu ambao unatufanya tushindwe kabisa kufanya mema, na hatutaki kabisa kufanya mema. (1) Kwa kweli, tunapinga mema yote. (2) (1) Rum. 5:6, 7:18, 8:7, Kol. 1:21, Yn. 3:6, Mwa. 6:5, 8:21, Rum. 3:10-19 (2) Yak. 1:14-15, Efe. 2:2-3, Mt. 15:19

19

Sehemu ya 5 Asili yetu iliyochafuliwa inabaki ndani yetu wakati wa maisha haya, hata baada ya kuzaliwa mara ya pili [kuokoka]. (1) Hata ingawa tumesamehewa kupitia Kristo, uchafu wa dhambi na athari zake zote bado zipo. (2) (1) 1 Yoh. 1:8,10, Rum. 7:14, 17-18, 21-23, Yak. 3:2, Mith. 20:9, Mhu. 7:20 (2) Rum. 7:5, 7-8, 25, Mwa. 5:17

Sehemu ya 6 Kila dhambi ya asili na ile ya kutenda, inakiuka sheria ya haki ya Mungu na inaleta hatia kwa mwenye dhambi. (1) Kila mwenye dhambi anawajibika kwa hasira ya Mungu, (2) laana ya sheria, (3) na kifo, (4) na taabu zote zinazotokana na dhambi; za kiroho, za muda, na za milele.(5)

(1) 1 Yoh. 3:4, Rum. 2:15, 3:9,19 (2) Efe. 2:3, Rum. 5:12 (3) Mwa. 3:10 (4) Rum. 6:23, Mwa. 2:17 (5) Efe. 4:18, Rum 8:20, Omb. 3:39, Mt. 25:41, 2 Thes 1:9, Rum. 1:21-28, Law. 26:14

20

SURA YA 7. KUHUSU AGANO LA MUNGU NA MWANADAMU Sehemu ya 1 Mungu ndiye Muumbaji wetu; sisi ni viumbe vyake. Yeye yuko juu sana, yuko juu yetu, na ni jukumu letu kumtii. Lakini hatuzawadii malipo kwa sababu tumejitahidi sana kumtii. Badala yake, Yeye hushuka kwa hiari yake mwenyewe, kwa kiwango chetu na kutubariki na ahadi, au maagano. (Yer, 40:13-17, Ayu 9:32-33, 1 Sam 2:25 (Zab 100:2-3, 113:5-6, Ayu 22:2-3, 35:7-8, Lk 17:10, Mdo 17.24-25.) Sehemu ya 2 Agano la kwanza la Mungu lilikuwa ni kati Yake na Adamu. Mara nyingi huitwa "Agano la Matendo”(1) Mungu aliahidi uzima kwa Adamu na watoto wake,(2) maadamu wangemtii kikamilifu. (3) (1) Hos. 6:7, Mwa. 2:6-17, Gal. 3:10, Rum. 5:12,19, 1 Kor. 15:22,47, Gal. 3:12.) (2) Rum. 5:12-20, 10:5) (3) Mwa. 2:17, Gal. 3.10; Linganisha Mwa. 2:16-17 na Rum. 5:12-14, 10:5, Lk. 1:25-28, na maagano ya Nuhu na Ibrahimu. Sehemu ya 3 Kwa kuanguka kwake, mwanadamu alishindwa kuishi chini ya agano hilo, na kwa hiyo Bwana akafanya agano la pili, ambalo ni Agano la Neema. (1) Ndani ya Agano la Neema Mungu huwapatia watenda dhambi uzima na wokovu kupitia Yesu 21

Kristo. Na ili aokolewe, mwanadamu anahitaji imani kwa Yesu peke yake (2) na Yesu anaahidi kutoa Roho Wake Mtakatifu kwa wote ambao wamewekwa tayari kwa kuamini. (3) (1) Gal. 3:21, Rum. 3:20-21, 8:3, Mwa. 3.15, Isa. 42:6, Mt. 26:28, Ebr. 10:5-10 (2) Mk. 16:15-16, Yn. 3:16, Rum. 10,6,9, Gal. 3:11, Mdo. 16:3031, Mt. 28:18-20, Rum. 1:16-17 (3) Eze. 36:26-27, Yn. 6:37,44-45, 5:37, 3:5-8, Mdo. 13:48, Lk. 11:13, Gal. 3:14

Sehemu ya 4 Agano hili la neema hujulikana mara kwa mara katika Maandiko kama agano, kwa kurejelea kifo cha Yesu Kristo na kwa urithi wa milele na kila kitu kikijumuishwa kwake na ambaye anatuahidi urithi udumuo milele (Ebr 9:15-17, 7:22, Lk 22:20, 1 Kor 11:25.) Sehemu ya 5 Agano la Neema lilitekelezwa tofauti wakati wa sheria na wakati wa Injili. (1) Chini ya sheria lilitekelezwa kwa ahadi, unabii, sadaka, tohara, mwana-kondoo wa pasaka, na aina zinginezo na maagizo waliyopewa Wayahudi, yote yalikuwa ni kivuli cha Kristo. (2) Kwa wakati huo agano lililowekwa chini ya sheria kupitia utendaji kazi wa Roho na lilitosha katika kuwafundisha Wateule na kujenga imani yao kwa Masihi aliyeahidiwa (3) ambaye kwake walikuwa na ondoleo kamili la dhambi zao na wokovu wa milele. Utekelezaji huu wa Agano la Neema unaitwa Agano la Kale. (4) (1) 2 Kor. 3:6-9, Ebr. 1:1-2 22

(2) Ebr. 8-10, Rum. 4:11, Kol. 2:11-12, 1 Kor. 5:7, Kol. 2:17 (3) 1 Kor. 10:1-4, Ebr. 11:13, Yn. 8:56, Gal. 3:6-8 (4) Gal. 3:7-9, 14, Mdo. 15:11, Rum. 3:30 Sehemu ya 6 Chini ya Injili, Kristo, ambaye ndiye kiini cha neema ya Mungu amefunuliwa. (1) Njia za neema katika Agano Jipya ni pamoja na kuhubiriwa kwa Neno na usimamizi wa sakramenti za Ubatizo na Meza ya Bwana. (2) Ingawa njia hizi ni chache (1) kwa idadi na zimesimamiwa kwa unyenyekevu zaidi na utukufu wa nje, lakini zinapatikana kwa Wayahudi na watu wa Mataifa (3) na ndani yao nguvu ya kiroho ya Agano la Neema imeendelezwa zaidi. (4) Kimsingi, hakuna maagano mawili ya neema, lakini agano ni moja chini ya utekelezaji tofauti. (5) (1) (2) (3) (4) (5)

Gal. 2:17, Kol. 2:17 Mt. 28:19-20, 1 Kor. 11:23-25, 2 Kor. 3:7-11 Mt. 28:19, Efe. 2:15-19, Lk. 2:32, Mdo. 10:34-35 Ebr. 12:22-28, Yer. 31:33-34, Ebr. 8:6-13, 2 Kor. 3:9-11 Lk. 22:20, Ebr. 8:7-9, Gal. 3:14,16, Mdo. 15:11, Rum. 3:2123,30, Zab. 32:1, Rum. 4:3,6,16-17,23-24, Ebr. 13:8.

1

Kanisa Ekklesiolojia kuna wanatheolojia wanaona kwamba njia za neema ni nyingi na haziwezi kuwa mbili tu, kama WCF inavyosema. Wengine huongeza; maombi, ushirika (fellowship), kutoa nk

23

SURA YA 8. KUHUSU KRISTO MPATANISHI Sehemu ya 1 Mungu, katika kusudi lake la milele ilimpendeza kumchagua na kumteua Bwana Yesu, Mwana pekee, kuwa mpatanishi kati ya Mungu na Mwanadamu; (1) Yesu ndiye Nabii (2) Kuhani na Mfalme (3) kichwa na Mwokozi wa Kanisa lake, (4) mrithi wa vitu vyote, (5) na Mwamuzi wa ulimwengu. (6) Tangu milele yote Mungu alimpa watu kuwa uzao wake (7) na kwa wakati, uzao wake wakombolewe, waitwe, wahesabiwe haki, watakaswe na watukuzwe naye.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Isa. 42:1, 1Pet 1:19-20, Yn 3:16, 1Tim 2:5 Mdo.3:20-22, Kumb. 18:15 Ebr. 5:5-6 Zab. 2:6, Lk 1:33, Isa 9:6-7 Efe. 5:23 Ebr. 1:2 Mdo. 17:31, 2 Kor 5:10 Yn. 17:6, Zab 22:30, Isa 53:10, Efe 1:4, Yn 6:37,39

Sehemu ya 2 Mwana wa Mungu, nafsi ya pili ya Utatu, ni Mungu wa milele, ni sawa na Baba. Katika utimilifu wa wakati alichukua asili ya mwanadamu, (1) alichukua sifa muhimu na udhaifu wa kawaida wa mwanadamu-isipokuwa kwamba alikuwa hana dhambi, (2) Yesu alichukuliwa mimba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu tumboni mwa Bikira Mariamu, ambapo alichukua mwili. (3) Kwa maneno mengine, Yesu ana asili mbili tofauti ya Kimungu na ya kibinadamu. Asili zote ni kamili. Asili ya Kimungu na ya 24

kibinadamu zimeunganishwa pamoja katika mtu mmoja, lakini alibaki kuwa Mungu na mwanadamu. Kwa hiyo, Yesu sio mchanganyiko wa Mungu na mwanadamu (4) bali ni Mungu kweli na Mwanadamu kweli, lakini, bado ni Kristo mmoja, mpatanishi wa pekee kati ya Mungu na mwanadamu. (5) (1) (2) (3) (4) (5)

Yn 1:1,14, 1Yoh 5:20, Fili 2:6, Gal 4:4, Ebr 2:14 Ebr 2:14, 16-17, 4:15 Lk 1:27,31,35, Gal 4:4 Lk 1:35, Col 2:9, Rum 9:5, 1 Pet 3:18, 1Tm 3:16, Mt 16:16 Rum 1:3-4, 1 Tim 2:5

Sehemu ya 3 Yesu alipofanyika mwanadamu, alitakaswa na kutiwa Mafuta na Roho Mtakatifu zaidi ya kipimo.(1) Katika yeye mna hazina zote za hekima na maarifa,(2) na ndani yake ilimpendeza Baba kwamba utimilifu wote ukae.(3) Kusudi la Mungu lilikuwa kwamba Yesu, Mtakatifu, asiye na ila, wala uchafu wowote, na amejaa neema na ukweli, atekeleze jukumu lake la kuwa Mpatanishi na Mdhamini. (4) Yesu hakujifanya mwenyewe kuwa Mpatanishi, bali aliitwa na Baba yake (5) ambaye alimpa nguvu zote na uwezo kamili wa kuhukumu. (6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Zab 45:7, Yn 3:34, Lk 4:18-19, 21, Mdo. 10:38, Ebr 1:8-9 Kol 2:3 Kol 1:19 Ebr 7:26, Yn 1:14, Mdo 10:38, Ebr 12:24, 7:22, Lk 4:18-21 Ebr 5.4-5 Yn 5:22,27, Mt 28:18, Mdo 2:36

25

Sehemu ya 4 Bwana Yesu alichukua kazi ya Upatanishi kwa hiari yake mwenyewe.(1) Ili kuifanya kazi hiyo, alishushwa chini (2) na akaitimiza sheria kikamilifu.(3) Alivumilia mateso makali sana katika roho yake(4) na maumivu makali sana katika mwili wake;(5) Alisulubiwa na akafa (6) Akazikwa na akabaki chini ya nguvu ya mauti, lakini mwili wake haukuona uharibifu; (7) Siku ya tatu alifufuka kutoka kwa wafu(8) na mwili uleule ambao ulipata mateso(9)na akiwa na mwili huohuo alipaa mbinguni. Huko ameketi mkono wa kuume wa Baba yake(10)akiwaombea Waamini(11) Atarudi kuwahukumu wanadamu na malaika wakati wa mwisho wa ulimwengu.(12) (1) Zab 40:7-8, Ebr 10:5-10, Yn 10:18, Fil 2:8, Yn 4:34 (2) Gal 4:4 (3) Mt 3:15, 5:17, Yn 17:4 (4) Mt 26:37-38, Lk 22:44, Mt 27:46 (5) Mt 26 na 27 (6) Fil 2:8 (7) Mdo 2:23-24, 27, Mdo 13:37, Rum 6:9, Mt 27:60 (8) 1Kor 15:3-4 (9) Yn 20:25,27 (10) Mk 16:19, Lk. 24:50-51, Mdo 1:9, 2:33-36, 1Pet 3:22, Rum 8:34 (11) Rum 8:34, Ebr 9:24, 7:25 (12) Rum 14:9-10, Mdo 1:11, 10:42, Mt 13:40-42, Yud 6, 2Pet 2:4, Mt 16:27, 25:31-33, 2Tim 4:1, Yn 5:28-29

Sehemu ya 5 Yesu Kristo kwa utii wake mkamilifu alijitoa kama dhabihu kwa Mungu mara moja na milele kupitia yule Roho wa milele, alitimiza haki ya Baba yake.(1) Kwa dhabihu yake, alilipa deni 26

letu, lakini pia alitununulia urithi katika ufalme wa mbinguni ambao utadumu milele.(12) (1) Rum 5:19, Ebr 9:14,16, 10:14, Efe 5:2, Rum 3:25-26 (2) Dan 9:24,26, Kol 1:19-20, Efe 1:11,14, Yn 17:2, Ebr 9:12,15, Rum 5:10-11, 2 Kor 5:18,20

Sehemu ya 6 Ilikuwa tu baada ya Yesu Kristo kuwa mwanadamu ndipo kweli tumeokolewa, ndipo tunaweza kusema "malipo yamekamilika". Lakini hata kabla ya hapo, tangu mwanzo wa ulimwengu, watu wa Mungu wameweza kuona wema na nguvu ya kuokolewa. Hii ni kwa sababu Mungu alifunua wokovu wake kwa watu wake kupitia ahadi, alama, na dhabihu za Agano la Kale. Ishara hizi zilionyesha kuwa Yesu ni uzao wa Mwanamke ambaye "angeponda kichwa cha nyoka". Zilionyesha kuwa Yeye ndiye "Mwanakondoo aliyechinjwa" tangu mwanzo wa ulimwengu. Kwamba Yesu ni Yeye yule jana, leo, na hata milele (Gal 4:4-5, Mwa. 3:15, Ufu 13:8, Ebr 13:8) Sehemu ya 7 Katika kazi ya upatanisho, Kristo hufanya kulingana na asili zake zote, kila asili inafanya kile kinachopaswa kufanywa kwa wakati, (1) walakini, kwa sababu ya umoja wa nafsi yake, wakati mwingine katika Maandiko, vitu ambavyo Yesu hufanya kama mtu husemwa kuwa vimefanywa na Mungu, na wakati mwingine kama vimefanywa na asili yake ya Mwanadamu.(2) (1) Ebr 9:14, 1 Pet 3:18, Yn 10:17-18 (2) Mdo 20:28, Yn 3:13, 1 Yn 3:16 27

Sehemu ya 8 Kristo daima hutoa wokovu kwa kila mtu ambaye amemnunulia wokovu huo.(1) Yeye hupatanisha kati ya Mwanadamu na Mungu (2) na Yeye anaonyesha siri za wokovu kupitia Neno Lake; (3) Yeye hushawishi kwa Roho wake Mtakatifu kuamini na kutii, na anatawala mioyo ya waaminio kwa Neno lake na kwa Roho wake; (4) Yeye hushinda maadui wote kwa uweza wake na hekima Yake, kwa njia ambazo zinalingana sawa na mpango Wake wa kushangaza. (5) (1) (2) (3) (4)

Yn 6:37,39, 10:15-16,27-28 Yn 2:1-2, Rum 8:34 Yn 15:13,15, Efe 1:7-9, Yn 17:6, Gal 1:11-12 Yoh 14:16, Ebr 12:2, 2 Kor 4:13, Rum 8:9,14, 15:18-19, Yn 17:17, Tit 3:4-5 (5) Zab 110:1, 1Kor 15:25-26, Mal 4:2-3, Kol 2:15, Lk 10:19

SURA YA 9. KUHUSU UTASHI HURU Sehemu ya 1 Mungu amempa mwanadamu utashi, ambao kwa asili ni utashi huru, yaani sio wa kulazimishwa au lazima kuelekea mema au mabaya (Mt 17:12, Yak. 1:14, Kumb. 30:19, Yn 5:40, 7:17, Ufu 22:17, Mdo 7:51, Yak 4:7.) Sehemu ya 2 Katika hali yake ya kutokuwa na hatia mwanadamu alikuwa na uhuru kamili na uwezo wa asili wa kufanya yaliyo mema na ya kumpendeza Mungu.(1) Mungu pia alimfanya mwanadamu apoteze uhuru huo.(2) 28

(1) Mhu. 7:29, Mwa. 1:26, Kol 3:10 (2) Mwa. 2:16-17, 3:6 Sehemu ya 3 Mwanadamu alianguka katika hali ya dhambi kwa kutotii kwake na hivyo akapoteza kabisa uwezo wake wa kiroho.(1) Kwa hiyo mwanadamu aliyeanguka kwa asili anapingana kabisa na uzuri wa kiroho (2) amekufa katika dhambi (3) na hana uwezo wake mwenyewe, ama nguvu ya kujibadilisha mwenyewe au kujiandaa kwa wokovu.(4) (1) Rum 5:6, 8:7, Yn 15:5 (2) Rum 3:9-10, 12, 23, 8:7 (3) Efe 2:1,5, Kol 2:13 (4) Yn 6:44,65, 1Kor 2:14, Efe 2:2-5, Tim 3:3-5, Rum 8:8 Sehemu ya 4 Wakati Mungu anapombadilisha mtenda dhambi na kumleta katika hali ya neema, anamwachilia kutoka utumwa wake wa asili wa dhambi. Kwa neema ya Mungu pekee aliyopewa kwa hiari, mwanadamu mwenye dhambi amewezeshwa kufanya yaliyo mema kiroho.(1) Walakini, kwa kuwa asili ya zamani ya dhambi bado ipo, Mwamini hawezi kutenda kwa ukamilifu yaliyo mema kwa kuwa pia anataka kutenda mabaya.(2) (1) Kol 1:13, Yn 8:34,36, Fil 2:13, Rum 6:18,22 (2) Gal 5.17, Rum 7:15,18-19,21-23, 1Yn1:8,10

29

Sehemu ya 5 Utashi wa mwanadamu ni huru kabisa na una mwelekeo mzuri wa pekee katika hali ya utukufu (Efe 4:13, Ebr 12:23, 1Yoh 3:2, Yud 24, Ufu 22:3-4, 2Nyak. 6:36, 1Yoh 1:8-10, 2:1-6, Zab 17:15)

SURA YA 10. KUHUSU WITO WENYE UFANISI Sehemu ya 1 Mungu huwaita kwa wakati unaofaa wale tu ambao yeye amewaandaa kwa uzima wa milele. Anawaita kwa Neno lake na Roho wake kutoka kwenye hali yao ya asili ya dhambi na kifo ili kuingia katika neema na wokovu kupitia Yesu Kristo. (1) Anawaangazia katika akili zao za kiroho uelewa uokoao wa vitu vya Mungu.(2) Anaondoa mioyo yao ya mawe na huwapa mioyo ya nyama.(3) Yeye huboresha mapenzi yao kwa uweza wake uwezao kuwaongoza kwa yaliyo mema.(4) Na kwa hiyo anawavutia kwa Yesu Kristo.(5) Lakini wanakuja kwa Yesu kwa hiari yao wenyewe, wakiwezeshwa na neema ya Mungu.(6) (1) Rum 8:28,30, 11:7, Efe 1:5,10-11, 2 Thes 2:13-14, 2Kor 3:3,6, Rum 8:2, 2Tim 1:9-10, Yn 15:16, Mdo 13:48, 1Thes 5:9, Yak 1:18, 1Kor 2:12, Efe 2:1-10 (2) Mdo 26:18, 1Kor 2:10,12, Efe 1:17-18, 2Kor 4:6 (3) Eze 36:26 (4) Eze 11:19, Fil 2:13, Kumb. 30:6, Eze 36:27, Fil 4:13, Yn 3:5, Gal 6:15, Tim 3:5, 1Pet 1:23 (5) Efe 1:19, Yn 6:44-45 (6) Zab 110:3, Yn 6:37, Rum 6:16-18, Mt 11:28, Ufu 22:17

30

Sehemu ya 2 Wito huu ni tendo maalum la neema ya Mungu. Haitegemei chochote kile ambacho Mungu alikijua tangu asili juu ya mtu huyo.(1) Aliyeitwa ni mpokeaji tu wa neema hiyo. Mungu mwenyewe hutoa uhai na kufanya upya kwa Roho Mtakatifu. (2) Kwa hiyo humwezesha kila mtu kuitikia wito wake na kukubali neema anayoitoa.(3) (1) 2Tim 1:9, Tim 3:4-5, Efe 2:4-5, 8-9, Rum 9:11 (2) 1Kor 2:14, Rum 8:7-9, Efe 2:5 (3) Yn 6:37, Eze 36:27, Yn 5:25 Sehemu ya 3 Watoto wachanga waliochaguliwa, wanaokufa wakiwa wachanga, hubadilishwa na kuokolewa na Kristo, kupitia Roho wake (1) anayefanya kazi kwa wakati wake na kwa jinsi apendavyo. (3) Vivyo hivyo kwa Wateule wengine wote ambao hawawezi kupokea wito kwa njia ya huduma ya Neno.(3) (1) Lk 18:15-16, Mdo 2:38-39, Yn 3:3,5-6, 1 Yn 5:12, Rum 8:9, Mwa. 17:7, Zab 105:8-10, Eze 16:20-21, Gal 3:29, Mdo 16:15,31-33, 1 Kor 1:16 (2) Yn 3:8 (3) 1Yn 5:12, Mdo 4:12, Yn 3:8, 16:7-8

Sehemu ya 4 Wengine, wasio Wateule, wanaweza kuitwa na huduma ya Neno, na Roho anaweza kufanya kazi ndani yao kwa njia ambazo hufanya kwa Wateule. Walakini, kamwe hawatakuja kwa Kristo na kwa hiyo hawawezi kuokolewa.(1) Na kwa kweli, watu bila kumkiri Kristo hawawezi kuokolewa kwa njia 31

nyingine yoyote;(2) haijalishi wanajaribu sana kuishi maisha ya maadili kulingana na uelewa wao wenyewe au kujaribu kufuata sheria za dini nyingine. Kusema wanaweza kuokolewa ni hatari sana na wazo kama hilo halina ukweli. (3) (1) Mt 22:14, 7:22, 13-15, 20-21, Ebr 6:4-6, Yn 6:64-66, 8:24, 1 Yoh. 2:19, Mdo 28:24 (2) Mdo 4:12, Yn 14:6, Efe 2:12-13, Yn 4:22, 17:3 (3) 2 Yn 9-11, 1 Kor 16:22, Gal 1:6-8

SURA YA 11. KUHUSU KUHESABIWA HAKI Sehemu ya 1 Wale ambao Mungu amewaita, pia amewahesabia haki.(1) Yeye hajaweka haki ndani yao lakini anasamehe dhambi zao na kuwakubali kana kwamba ni waadilifu, sio kwa sababu ya kitu chochote kinachofanya kazi ndani yao au kinachofanywa na wao, lakini kwa ajili ya Kristo peke yake. Mungu hazingatii imani yao; yaani kile kitendo cha kuamini, kama ndiyo haki yao au mwitikio wowote mwingine wa utii kwa Injili kwa upande wao. Badala yake, ameweka utii wa Kristo kwao (2) ambapo wao wanapokea na kupumzika juu ya Kristo na haki yake kwa imani (na imani hii sio yao wenyewe lakini ni zawadi ya Mungu) (3) (1) Rum 8:30, 3:24 (2) Rum 4:5-8, 2 Kor 5:19,21, Rum 3:22,24-25,27-28, Tim 3:5,7, Efe 1:7, Yer 23:6, 1 Kor 1:30-31, Rum 5:17-19 (3) Mdo 10:43-44, Gal 2:16, Fil 3:9, Mdo 13:38-39, Efe 2:7-8, Yn 1:12, 6:44-45, Fil 1:29

32

Sehemu ya 2 Hivyo basi, imani ni kupokea na kupumzika juu ya Kristo na haki yake, na hii ndiyo njia pekee ya kuhesabiwa haki. (1) Walakini kwa mtu ambaye amehesabiwa haki, wakati wote kunaambatana na njia za neema zinginezo zifanyazo kazi kwa upendo.(2) (1) Yn 1:12, Rum 3:28, 5:1, Yn 3:16,18,36 (2) Yak 2:17,22,26, Gal 5:6 Sehemu ya 3 Kwa utii na kifo chake Kristo alilipa kabisa deni kwa wote ambao wamehesabiwa haki na aliridhisha haki ya Baba yake kwa niaba yao. (1) Kwa kuwa Kristo alitolewa kwa hiari na Baba kwa ajili yao (2) na kwa kuwa utii wake na kuridhika vilikubaliwa, (3) basi, kuhesabiwa haki kwao ni matokeo ya neema yake ya bure (4) ili haki kamili na neema ya Mungu iweze kutukuzwa kwa haki ya wenye dhambi.(5) (1) Rum 5:8-10,18-19, 1Tim 2:5-6, Ebr 10:10,14, Dan 9:24,26, Isa 53:4-6,10-12, 1Kor 15:3, 2Kor 5:21, 1 Pet 2:24, 3:18 (2) Rum 8:32, Yn 3:16 (3) 2 Kor 5:21, Mt 3:17, Efe 5:2, Isa 53:6 (4) Rum 3:24, Efe 1:7, Rum 6:23, Efe 2:6-9 (5) Rum 3:26, Efe 2:7

Sehemu ya 4 Tangu umilele wote, Mungu aliamuru kuhesabiwa haki kwa Wateule wote (1) na katika utimilifu wa wakati Kristo alikufa 33

kwa ajili ya dhambi zao na kufufuka kwa kuhesabiwa haki kwao.(2) Walakini, Wateule hawahesabiwi haki hadi Roho Mtakatifu, kwa wakati unaofaa, awavute kwa Kristo.(3) 1) Gal 3:8, 1Pet 1:2,19-20, Rum 8:30) 2) Gal 4:4, 1Tim 2:6, Rum 4:25, 1Pet 1:21 3) Kol 1:21-22, Gal 2:16, Tim 3:4-7, Yn 3:5,18,36 Sehemu ya 5 Mungu anaendelea kusamehe dhambi za wale ambao wamehesabiwa haki; (1) ingawa hawawezi kamwe kuanguka kutoka kwenye hali ya kuhesabiwa haki. (2) Hata hivyo, kwa sababu ya dhambi zao, Mungu kama baba yao huweza huwarudi kwa muda; ili wanyenyekee na kuomba msamaha kwa toba.(3) (1) Mt. 6:12, 1 Yn. 1:7,9, 2.1-2 (2) Lk 22:32, Yn 10,28, Ebr. 10,14, Fil. 1:6, 1Yon 2:19 (3) Zab 89:31-33, 51:7-12, 32.5, Mt 26:75, 1Kor 11:30,32, Lk 1:20 Sehemu ya 6 Kwa njia hizi zote, Waamini katika Agano la Kale walihesabiwa haki kwa njia sawa na ambao wanaamini katika nyakati za Agano Jipya (Gal. 3:6-9,13-14, Rum. 4:22-24, Ebr. 13:8, 11:13, Yn. 8:56, Mdo. 15:11, Rum. 3:30.)

34

SURA YA 12. KUHUSU KUFANYWA WANA Sehemu ya 1

Mungu anathibitisha kufanywa wana kwa wale wote ambao wamehesabiwa haki kwa ajili ya Mwana wake pekee, Yesu Kristo. (1) Wale waliofanywa wana wanafurahia uhuru na haki za watoto wa Mungu (2) jina la Mungu limewekwa juu yao, (3) wanapokea Roho wa kufanywa wana, (4) wanaweza kukikaribia kiti cha neema kwa ujasiri,(5)na wamewezeshwa kulia, Abba, Baba.(6) Wamehurumiwa, (7) wanalindwa, (8) wametengwa (9) wanarudiwa na Mungu kama baba yao. (10) Hawatupiliwi mbali (11) Wametiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi, (12) na kurithi ahadi (13) kama warithi wa wokovu wa milele. (14) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14)

Efe 1:5, Gal 4:4-5 Rum 8:17, Yn 1:12 Yer 14:9, 2Kor 6:18, Ufu 3:12 Rum 8:15 Efe 3:12, Rum 5:2, Ebr 4:16 Gal 4:6 Zab 103:13 Mith 14:26, Zab 27:1-3 Ebr 12:6 Omb 3:31-32, Ebr 13:5 Efe 4:30 Ebr 6:12 1Pet 1:3-4, Ebr 1:14

35

SURA YA 13. KUHUSU UTAKASO Sehemu ya 1 Wale ambao wameitwa na kuzaliwa upya wana moyo mpya na roho mpya iliyoundwa ndani yao. Kwa kweli wametakaswa kwa nguvu ya kifo cha Kristo na ufufuo na kwa Neno lake na Roho anayeishi ndani yao.(2) Nguvu ya dhambi inayotawala juu ya mwili wote imeharibiwa,(2) na tamaa za ubinafsi za kidunia zinazoofishwa. (3) Wakati huohuo uwezo wa kutenda utakatifu wa kweli, ambapo bila huo hakuna atakayemwona Bwana (4) unaimarishwa na neema zote ziokoazo.(5) (1) 1 Kor 6:11, Mdo 20:32, Fil 3:10, Rum 6:5-6,Yn 17:17,19, Efe 5:26, 2Thes 2:13, 1Kor 1:30 (2) Rum 6:6,14 (3) Gal 5:24, Rum 8:13, Kol 3:5 (4) 2Kor 7:1, Ebr 12:14, Kol 1:28, 4:12 (5) Kol 1:10-11, Efe 3:16-19, 2 Pet 3:13-14

Sehemu ya 2 Utakaso huu hufanya kazi ndani ya Wateule, (1) lakini hawawezi kuwa wakamilifu katika maisha haya. Asili ya zamani ya dhambi inajaribu kuthibiti mwili, akili, na roho. Na hivyo vita vya daima na visivyopatana vinaendelea kwa kila Mwamini. Asili ya zamani inajaribu kupingana na Roho, na Roho anapigana kudai mamlaka yake juu ya mwili.(2) (1) 1Thes 5:23 (2) 1 Yn 1:10, Rum 7:18,23, Fil 3:12, Gal 5:17, 1 Pet 2:11

36

Sehemu ya 3 Ingawa asili ya zamani inashinda kwa muda vita hivi,(1) utakaso wa Roho Mtakatifu wa Kristo huwawezesha Wateule kushinda zaidi.(2)Na hivyo Watakatifu wanakua katika neema.(3) Wakikamilishwa katika utakatifu kwa kumcha Mungu. (4) (1) Rum 7:23 (2) Rum 6:14, 1Yn 5:4, Efe 4:15-16 (3) 2 Pet 3:18, 2 Kor 3:18 (4) 2 Kor 7:1

SURA YA 14. KUHUSU IMANI IOKOAYO Sehemu ya 1 Zawadi ya imani inafanya uwezekano wa mioyo ya Wateule kuokolewa kwa kumwamini Yesu Kristo. Zawadi hii ni kazi ya Roho wa Kristo ndani ya mioyo ya Wateule (1) na inakamilishwa kwa kawaida na huduma ya Neno.(2) Pia inaongezwa na kuimarishwa kwa Neno, kwa maombi, na kwa utekelezaji wa sakramenti. (3) (1) Ebr 10:39, 2Kor 4:13, Efe 1:17-20, 2:8, 1Kor 12:3, Ebr 12:2 (2) Rum 10:14,17, Mt 28:19-20, 1Kor 1:21 (3) 1Pet 2:2, Mdo 20:32, Rum 4:11, Lk 17:5, Rum 1:16-17, Mt 28:19, 1Kor 11:23-29, 2Kor 12:8-10, Lk 22:19, Yn 6:54-56, Lk 22:32

37

Sehemu ya 2 Kwa imani hii, Mkristo anaamini kile kinachofunuliwa katika Neno kuwa ni ukweli kutoka kwa Mungu mwenyewe.(1) Kwa imani hii, muumini pia hutenda kulingana na Neno la Mungu. Kwa imani hii, Muumini hujitiisha kwa unyenyekevu na kumtii Mungu na maagizo yake anuwai.(2) Yeye hutetemeka mbele za Mungu(3) na anakubali ahadi zake juu ya maisha haya na maisha ya baadaye.(4)Lakini hatua kuu za imani iokoayo ni kukubali, kupokea, na kupumzika juu ya Kristo.(5) (1) Yn 4:42, 1Thes 2:13, 1Yn 5:10, Mdo 24:14). (2) Rum 16:26, Mt 22:37-40). (3) Isa 66:2), (4) Ebr 11:13, 1Tim 4:8). (5) Yn 1:12, Mdo 16:31, Gal 2:20, Mdo 15:11) Sehemu ya 3 Imani hii ina viwango tofauti vya nguvu na udhaifu.(1) Inaweza kushambuliwa na kudhoofishwa mara kwa mara na kwa njia nyingi, lakini inapata ushindi.(2) Waamini huimarika na kuwa na uhakika kabisa kupitia Kristo(3) ambaye hukamilisha imani yao.(4) (1) Ebr 5:13-14, Rum 4:19-20, Mt 6:30, 8:10 (2) Lk 22:31-32, Efe 6:16, 1Yn 5:4-5, 1Kor 10:13 (3) Ebr 6:11-12, 10:22, Kol 2:2, 2Tim 1:12 (4) Ebr 12:2

38

SURA YA 15. KUHUSU TOBA ILETAYO UZIMA Sehemu ya 1 Toba iletayo uzima ni zao la Injili inayofanya kazi katika maisha ya Waamini. (1) Huenda sambamba na mafundisho ya imani katika Kristo ambayo yanahubiriwa na kila Mhudumu ya Injili. (2) (1) Zek 12:10, Mdo 11:18 (2) Lk 24:47, Mk 1:15, Mdo 20:21 Sehemu ya 2 Katika toba, mtenda dhambi anaweza kuziona dhambi zake kama vile ambavyo Mungu anavyoziona; kama mchafu na mwenye kuchukiza, na kuiona dhambi hiyo kuwa hatari kubwa mbele yake, kwa sababu dhambi zake zinapingana kabisa na asili takatifu na sheria ya haki ya Mungu. Akifahamu kwamba Mungu katika Kristo ni mwenye rehema kwa wale wanaotubu; pale mtenda dhambi anapohuzunika kwa kuchukia dhambi zake, na kwa hiyo anaamua kuachana nazo zote na kumgeukia Mungu,(1)na kujaribu kutembea na Mungu kulingana na amri zake zote.(2) (1) Eze 18:30-31, 36:31, Isa 30:22, Zab 51:4, Yer 31:18-19, Amo 5:15, Zab 119:128, 2 Kor 7:11). (2) Zab 119:6,59,106, Lk 1:6, 2Fal 23:25, Yn 14:23, Mt 21:28-29.

39

Sehemu ya 3 Ingawa toba hairidhishi chochote kwa dhambi na wala haisababishi msamaha wa dhambi(1) (kwa kuwa msamaha ni tendo la neema ya Mungu katika Kristo)(2) lakini ni muhimu kwa wenye dhambi, na hakuna mtu anayeweza kutarajia kusamehewa bila toba.(3) (1) Eze 36:31-32, 16:61-63, Tit 3:5, Mdo 5:31 (2) Hos 14:2,4, Rum 3:24, Efe 1:7 (3) Lk 13:3,5, Mdo 17:30-31

Sehemu ya 4 Kama vile ambavyo hakuna dhambi ndogo sana ambayo haistahili hukumu, (1) vivyohivyo hakuna dhambi kubwa ambayo inaweza kuleta hukumu kwa wale wanaotubu kwa kweli kutoka mioyoni mwao.(2) [hii inatokana na ukweli kwamba hakuna dhambi isiyosamehewa kwa Wateule.] (1) Rum 6:23, 5:12, Mt 12:36, Yak 2:10 (2) Isa 55:7, Rum 8:1, Isa 1:16,18 Sehemu ya 5 Waamini hawapaswi kutosheka na toba ya jumla, badala yake, ni jukumu la kila mtu kujaribu kutubu kila dhambi yake kibinafsi mbele za Mungu (Zab 19:13, Lk 19:8, 1 Tim 1:13,15, Dan 9, Neh 9). Sehemu ya 6 Kila mtu anapaswa kukiri dhambi zake kibinafsi kwa Mungu na kumwomba msamaha.(1) Kwa njia ya kukiri na kuomba 40

msamaha mtu hupata rehema za Mungu.(2) Mtu yeyote anayetenda dhambi dhidi ya nduguye wa kiroho au kanisa anapaswa kuwa tayari kukiri, kwa faragha au hadharani, kuonesha huzuni kwa dhambi yake, na kusema waziwazi toba yake kwa wale ambao amewadhuru,(3) ambapo wale ambao wameathiriwa na dhambi ya huyo anayetubu wanapaswa kumpokea kwa upendo. (4) (1) (2) (3) (4)

Zab 51:4-5,7,9,14, 32:5-6 Mith 28:13, 1 Yn 1:9 Yak 5:16, Lk 17:3-4, Yosh. 7:19, Zab 51 2 Kor 2:7-8, Gal 6:1-2

SURA YA 16. KUHUSU MATENDO MEMA Sehemu ya 1 Matendo mema ni kazi ambazo zinatambuliwa kuwa nzuri na Mungu na kuamriwa na yeye katika Neno lake Takatifu.(1) Kwa hiyo, kazi zingine zote, ambazo hazijaamriwa na Mungu, hata kama wanadamu wakifanya hazifai.(2) (1) Mik 6:8, Rum 12:2, Ebr 13:21, Kumb. 12:32, Zab 119:9, Mt 28:20, Lk 10:25-26, 2 Pet 1:19 (2) Mt 15:9, Isa 29:13, 1Pet 1:18, Rum 10:2, Yn 16:2, 1 Sam 15:2123, Kol 2:16-17,20-23, Kumb. 10:12-13

Sehemu ya 2 Matendo mema yanayofanywa kwa utii wa amri za Mungu, ni matunda na uthibitisho wa imani ya kweli na hai.(1) Waamini hufanya matendo hayo mema kwa kuonyesha shukrani zao(2)wanaimarisha uhakikisho wao wa wokovu(3) Wanawaadibisha ndugu zao katika Bwana(4) na kuwa manukato 41

ya wale wote wanaokiri Injili. (5) Matendo Mema kwa Waamini hunyamazisha wakosoaji na maadui wa Injili. (6) Matendo mema yanamtukuza Mungu(7) kwa kuonyesha kuwa Waamini ni kazi ya uumbaji wa Yesu Kristo. (8) Kwa hiyo, kuishi maisha ya utakatifu kunaongoza kwenye uzima wa milele. (9) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9)

Yak 2:18,22 Zab 116:12-13, 1Pet 2:9, Kol 3:17, 1 Nyak 29:6-9 1Yoh 2:3,5, 2Pet 1:5-10 2Kor 9:2, Mt. 5:16, 1Tim 4:12 Tit 2:5,9-12, 1Tim 6:1 1Pet 2:15 1 Pet 2:12, Fil 1:11, Yn 15:8 Efe 2.10 Rum 6.22

Sehemu ya 3 Waamini hupata uwezo wa kufanya matendo mema kutoka kwa Roho wa Kristo. (1) Mbali na athari zingine za neema za Mungu zilizopokelewa tayari, Waamini lazima waelekezwe na Roho Mtakatifu ili kufanya kile kinachompendeza Mungu.(2) Hata hivyo, hawapaswi kuwa wavivu wa kiroho, wakingojea mwongozo fulani maalum kutoka kwa Roho kabla ya kufanya kitu chochote kilichoamriwa na Mungu. Badala yake, wanapaswa kujaribu kwa bidii kutambua ni matendo gani mema ambayo Mungu ameamuru katika Neno lake na kisha wajaribu kwa bidii kufanya matendo hayo; huku wakiomba kwa bidii kila siku kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, anayeishi ndani yao.(3) (1) Yn 15:4-6, Eze 36:26-27, Lk 11:13 (2) Fil 2:13, 4:13, 2 Kor 3:5, Efe 3:16

42

(3) Fil 2:12, Ebr 6:11-12, 2 Pet 1:3,5,10-11, Isa 64:7, 2 Tim 1:6, Mdo 26:6-7, Yud 20-21 Sehemu ya 4 Hata watu wanaomtii Mungu vizuri katika maisha haya kamwe hawawezi kwenda juu na zaidi ya wito wa Mungu katika kutenda mema. Kwa kweli, watu kama hao bado wanapungukiwa na mambo mengi ambayo Mungu anawataka wayafanye (Lk 17:10, Neh 13:22, Ayu 9:2-3, Gal 5:17). Sehemu ya 5 Kwa kweli hatuwezi kusamehewa dhambi zetu na kupokea uzima wa milele kutoka kwa Mungu kwa matendo yetu mema. Kuna utofauti mkubwa kati ya matendo yetu mema katika maisha haya na utukufu ambao utafunuliwa ndani yetu, na kuna umbali kati yetu na Mungu, ambaye hafaidiki na matendo yetu mema na hakuwahi kuridhika nayo kwa kulipa deni la dhambi zetu.(1) Pindi tufanyapo matendo mema tuwezayo kuyafanya, ni jukumu letu, ni watumishi wasio na faida (2) [yaani hatusubiri wala kutegemea malipo kwa sababu ya kufanya matendo mema, bali matendo mema ni sehemu ya maisha yetu ya wokovu.] Hatuna uwezo wa kufanya Matendo mema kwa nguvu zetu wenyewe bali wema wa matendo yetu mema kwa kweli unatoka kwa Roho wake. (3) Na kwa sababu matendo haya mema yamefanywa nasi; ni machafu, dhaifu na yasiyo kamili, kwa hiyo hayawezi kuhimili hukumu kali ya Mungu.(4) (1) Rum 3:20, 4:2,4,6, Efe 2:8-9, Tit 3:5-7, Rum 8:18:22-24, Zab 16:2, Ayu 22:2-3, 35:7-8). (2) Lk 17.10). (3) Gal 5:22-23).

43

(4) Isa 64:6, Gal 5:17, Rum 7:15,18, Zab 143:2, 130:3).

Sehemu ya 6 Walakini, kwa kuwa Waamini wanakubaliwa kupitia Kristo, matendo yao mema katika maisha haya pia yanakubaliwa. (1) Sio kwamba yanawafanya wawe kamili machoni pa Mungu,(2) bali kwamba Mungu akiwaangalia katika Mwana wake, anafurahia na kubariki kile kinachofanywa na wao kwa dhati, ingawa yanaambatana na udhaifu mwingi na kutokamilika. (3) (1) Efe 1:6, 1 Pet 2:5, Kut. 28:38, Mwa. 4:4, Ebr 11:4 (2) Ayu 9:20, Zab 143:2, 1 Kor 4:3-4 (3) Ebr 13:20-21, 2Kor 8:12, Ebr 6:10, Mt 25:21,23 Sehemu ya 7 Matendo mema yanayofanywa na watu ambao hawajazaliwa upya kiroho yanaweza kuwa sawa na yale yaliyoamriwa na Mungu na yanaweza kuwa msaada kwa wengine.(1) Walakini, kwa kuwa hayatoki kwenye moyo uliosafishwa kwa imani,(2)na pia hayajafanywa kwa njia sahihi, yaani, kutoka kwenye mwitikio wa Neno la Mungu,(3) na hayajafanywa kwa kusudi sahihi, yaani kwa ajili ya utukufu wa Mungu,(4) basi, matendo haya mema yana dhambi, na kamwe hayawezi kumpendeza Mungu au kumfanya mtu kuwa sawa ili kupokea neema kutoka kwa Mungu.(5) Walakini, ni dhambi zaidi na isiyompendeza Mungu kutofanya matendo mema kuliko kufanya.(6) (1) (2) (3) (4)

2Fal 10:30-31, 1Fal 21:27,29, Fil 1:15-16,18 Mwa. 4:3-5, Ebr 11:4,6 1Kor 13:3, Isa 1:12, Mk 10:20-21), Mt 6:2,5,16, Rum 14:23),

44

(5) Hag 2:14, Tit 1:15, Amo 5:21-22, Hos 1:4, Rum 9:16, Tit 3:5, Mith 15:8, 28:9, Mk 7:6-7 (6) Zab 14:4, 36:3, Ayu. 21:14-15, Mt 25:41-45, 23:23, 25:24-28

SURA YA 17. KUHUSU UVUMILIVU WA WATAKATIFU Sehemu ya 1 Wale ambao Mungu amewakubali katika Mwana wake Yesu Kristo, na kwa kweli amewaita na kuwatakasa na Roho wake Mtakatifu, kamwe hawawezi kutoka katika hali yao ya neema. Badala yake, hakika wataendelea katika hali hiyo hadi mwisho na wameokolewa milele (Fil 1:6, 2 Pet 1:10, Yn 10:28-29, 1 Yn 3:9, 1 Pet 1:5,9, Ayu 17:9, Yer 32:40). Sehemu ya 2 Uvumilivu huu wa Watakatifu hautegemei hiari yao lakini kwa amri ya Mungu ya uchaguzi isiyobadilika, inayotokana na upendo wake wa hiari, usiobadilika.(1) Inategemea pia ufanisi wa huduma na maombezi ya Yesu Kristo.(2) Maombezi ya Yesu juu ya ujazo wa Roho Mtakatifu na uwepo wa mbegu ya Mungu inayokaa ndani ya Watakatifu.(3)Inategemea pia asili ya Agano la Neema(4)ambalo halitanguki. Hizi zote zinathibitisha ukweli wa kutokubadilika kwa uhifadhi wao.(5) (1) 2Tim. 2:18-19, Yer 31:3, Efe 1:4-5, Yn 13:1, Rum. 8:35-39 (2) Ebr 10:10,14, 13:20-21, 9:12-15, Rum 8:32-39, Yn. 17:11,24, Lk 22:32, Ebr 7:25 (3) Yn. 14:16-17, 1Yn 2:27, 3:9 (4) Yer. 32:40, Ebr 8:10-12 (5) Yn. 10:28, 2 Thes 3:3, 1 Yn 2:19, 1 Thes. 5:23-24, Ebr. 6:17-20

45

Sehemu ya 3 Walakini, majaribu ya Shetani, ulimwengu, na tabia zao [Watakatifu] za asili za kimwili, pamoja na kupuuza njia ya kuhifadhiwa kwao, inaweza kusababisha Waamini kufanya dhambi kubwa na kuendelea na dhambi hiyo kwa muda.(1)Matokeo yake ni kutokumpendeza Mungu(2) na kumhuzunisha Roho Mtakatifu.(3)Katika hili, baadhi ya matokeo ya neema ya Mungu na faida zake huondolewa kwao, (4) na hivyo wanafanya mioyo yao kuwa migumu,(5)na dhamiri zao zinajeruhi,(6) zinaumiza na kuwachukiza wengine,(7) na hivyo kujiletea hukumu ya muda juu yao wenyewe.(8) [Hii haimaanishi kwamba Wateule wanaweza kuondoka katika hali yao ya neema, bali Mungu huwarudi kwa njia mbalimbali, kwa sababu ya maovu yao.] (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mt. 26:70,72,74, Zab. 51, 2 Sm 12:9,13 Isa 64:5,7,9, 2 Sam 11:27 Efe. 4:30 Zab. 51:8,10,12, Ufu. 2:4 Isa. 36:17, Mk 6:52, 16:14, Zab. 95:8 Zab. 32:3-4, 51:8 2 Sam. 12:14, Eze. 16:54 Zab. 89:31-32, 1 Kor. 11:32, 2 Sam. 12:10

SURA YA 18. KUHUSU UHAKIKISHO WA NEEMA NA WOKOVU Sehemu ya 1 Wanafiki na wasiozaliwa mara ya pili wanaweza kujidanganya na tumaini la uongo na hisia za mwili kwamba wanampendeza 46

Mungu na kwamba wameokolewa.(1) Walakini hisia zao zitakufa pamoja nao.(2) Wale wanaomwamini kwa kweli Bwana Yesu, wanaompenda kwa dhati na wanajaribu kutembea kwa dhamiri njema mbele yake, wanaweza kuwa na hakika katika maisha haya, kwamba wapo katika hali ya neema.(3) Wanaweza pia kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu, na hawataona aibu kwa tumaini hilo.(4) (1) (2) (3) (4)

Ayu. 8:13-14, Mik 3:11, Kumb. 29:19, Yn 8:41 Mt. 7:22-23, Ayu. 8:13 1 Yoh. 2:3, 3;14, 18-19,21,24, 5:13, 2 Tim. 1;12 Rum. 5:2, 5; 2 Tim. 4:7-8

Sehemu ya 2 Uhakikisho huu haujaegemea katika tumaini la kubahatisha au kukisiakisia tu. Na badala yake, ni uhakikisho usiotanguka wa imani(1) iliyowekwa juu ya ukweli wa ahadi za Kimungu za wokovu.(2) Pia, kuna uthibitisho wa ndani wa ufahamu wa kiroho, ambao tumepewa na Mungu, ambapo ahadi hizi zinatimilizwa.(3) Na kuna ushuhuda wa Roho wa kufanywa watoto, akishuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu.(4) Roho huyu ndiye kiapo cha urithi wetu. Kwa yeye tumetiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Ebr. 6:11-12,19 Ebr. 6:17-18, 2 Pet. 1:4-5 2 Pet. 1:4-5,10-11, 1 Yn. 2:3, 3:14, 2 Kor. 1:12 Rum. 8:15-16 Efe. 1:13-14, 4:30, 2 Kor. 1:21-22

47

Sehemu ya 3 Uhakikisho huu usiotanguka sio muhimu sana kwa imani, kwani Mwamini wa kweli hawezi kuwa na mashaka na migongano juu uhakikisho huu, wakati mwingine hungoja kwa wakati mpaka uhakikisho huo utakapokua ndani yake (1) [Hoja hapa ni kwamba kama binadamu, haimaanishi kwamba uhakikisho ni sehemu ya imani. Mtu anaweza kuwa na mashaka na migongano ya kiimani ndani yake. Wakati mwingine anaweza kujiona kama hayuko salama, lakini kitu cha muhimu ni kwamba anakua katika uhakikisho huo mpaka kurudi kwa Kristo]. Lakini kwa kuwa Roho huwawezesha Waamini kujua vitu walivyopewa na Mungu kwa bure, kila Mwamini anaweza kujawa na uhakikisho kamili wa wokovu na kazi ya kawaida ya Roho pasi na ufunuo usio wa kawaida.(2) Kwa hiyo ni jukumu la kila Mwamini kujua ukweli wa wito wake na uchaguzi,(3) ili moyo wake ujazwe na amani, furaha katika Roho Mtakatifu, upendo, kumshukuru Mungu, na furaha ya utii, ambayo ndiyo matokeo ya uhakikisho.(4) Uhakikisho hautufanyi tuishi maisha ya dhambi bali kuepuka kuishi maisha ya dhambi ya aina yoyote ile.(5) [Kwa hiyo, wale wanaofanya dhambi kwa kisingizio cha uhakikisho wa wokovu wao ni dhahiri kwamba bado wapo gizani, wanahitaji mwangaza wa kuona mambo ya kiroho; au labda pengine si Wateule, bali ni waovu walioitikia wito kwa huduma ya Neno, na kamwe hawataokolewa]. (1) 1 Yn. 5:13, Isa 50:10, Mk. 9:24, Zab. 88, 77:1-20, 73 (2) 1 Kor. 2:12, 1 Yn. 4:13, Ebr. 6:11-12, Efe. 3:17-19, Zab. 77:1020, 73 (3) 2 Pet. 1:10 (4) Rum. 5:1-2, 5, 14:17, 15:13, Efe. 1:3-4, Zab 4:6-7, 119:32)

48

(5) 1 Yoh. 2:1-2, Rum. 6:1-2, Tim. 2:11-12,14, 2 Kor. 7:1, Rum. 8:1,12, 1 Yn. 3:2-3, Zab. 130:4, 1 Yn. 1:6-7, 2 Pet. 1:10

Sehemu ya 4 Hata Waamini ambao wana uhakika kuwa wameokolewa wanaweza kuyumbishwa [kutikiswa]. Wakati mwingine wanaweza kuwa na uhakika kidogo au kupoteza kwa muda uhakika huu. Hii inaweza kutokea kwa sababu kadhaa: kwanza, ikiwa hawajali kuwa wanaweza kuanguka katika dhambi fulani ambazo huumiza dhamiri zao na kumhuzunisha Roho Mtakatifu, pili ikiwa watajaribiwa ghafla, na tatu, ikiwa Mungu ataondoa mwangaza wa uwepo wake kwao, na matokeo yake hata yule anayemwogopa Mungu, kwa muda anaweza kutembea gizani.(1) Walakini, kamwe mbegu ya Mungu ndani yao haitoki; yaani maisha ya imani, upendo wa Kristo na upendo wa Waamini wengine, moyo wa dhati na dhamiri ya utii, ambayo kwa hiyo Roho anaweza kufufua tena uhakikisho huu kwa wakati (2) ili wasipotee gizani kabisa(3) (1) Zab. 51:8,12,14, Efe. 4:30-31, Zab. 77:1-10, Mt. 26:69-72, Zab. 31:22, Zab. 88, Isa. 50:10 (2) 1 Yn. 3:9, Lk. 22:32, Ayu 13:15, Zab. 73:15, Zab. 51:8,12, Isa. 50:10 (3) Mik. 7:7-9, Yer. 52:40, Isa. 54:7-10, Zab 22:1, 88, 2 Kor. 4:810

SURA YA 19. KUHUSU SHERIA YA MUNGU Sehemu ya 1 Mungu alimpa Adamu "Agano la Matendo," sheria ambayo yeye na uzao wake wote walipaswa kufuata. Walipaswa kuitii milele kabisa. Mungu aliahidi uzima kwa kuitunza na akatishia 49

kifo kwa kutotii, na alimpa mwanadamu nguvu na uwezo wa kuitunza (Mwa. 1:26-27, 2:17, Rum. 2:14-15, 10:5, 5.12,19, Gal. 3:10,12, Mhu. 7:29, Ayu 28:28, Efe. 4:24). Sehemu ya 2 Baada ya anguko, sheria hii iliendelea kuwa sheria kamilifu ya haki, na ilitolewa na Mungu katika Mlima Sinai kama Amri Kumi, iliyoandikwa kwenye mbao mbili;(1) Amri nne za kwanza huonyesha wajibu na majukumu yetu kwa Mungu. Na zile amri sita zinazobaki zinaonyesha uhusiano wetu kwa wanadamu.(2) (1) Yak. 1:25, 2:8,10-12, Rum. 13:8-9, Kumb. 5:32, 10:4, Kut. 34:1, Rum 3:19, Gal. 3:12, Hos. 6:7, Mwa. 2:16-17 (2) Mt. 22:37-40, Kut. 20,3-18

Sehemu ya 3 Kwa kuongezea, katika sheria hii, ambayo kwa kawaida huitwa sheria ya maadili, ilimpendeza Mungu kuwapa Waisraeli, kama Mkutano wa Waamini wa Kabla ya Ukristo “sheria za ibada” zilizokuwa na kanuni nyingi za kawaida. Baadhi ya maagizo haya ni matendo ya ibada kama kivuli cha Yesu Kristo, neema yake, mateso, na faida zinazopatikana kutokana na kumwamini.(1) Maagizo mengine yote yalikuwa na maelekezo kadhaa juu ya majukumu ya maadili.(2)Sheria hizi zote za ibada sasa zimefanywa kuwa chini ya Agano Jipya.(3) (1) Ebr. 9, 10:1, Gal. 4:1-3, Kol. 2:17 (2) 1Kor. 5:7, 2 Kor. 6:17, Yud. 23; tazama Law. 5:1-6, 6:1-7 (3) Kol. 2:14,16-17, Dan. 9:27, Efe. 2:15-16, Mk. 7:18-19, Gal. 2:4

50

Sehemu ya 4 Mungu pia aliwapa Waisraeli sheria anuwai za kimahakama. Hizi zilimaliza muda pindi hali ya Israeli ilipomalizika na hazitoi wajibu wowote kwa watu wa Mungu isipokuwa kwa masuala ya haki ya jumla yaliyo kwenye jamii ya sasa ambayo yamo kwenye sheria hizo (Kut. 21, 22:1-29, Mwa. 49:10, 1 Pet 2:13-14, Mt. 5:17,38-39, 1 Kor. 9:8-10) Sehemu ya 5 Sheria za maadili ni kwa kila mtu; aliyeokolewa na asiyeokolewa, ni ya milele, sio tu kwa heshima ya yaliyomo katika sheria hiyo, lakini pia katika uhusiano na mamlaka ya Mungu, Muumba, aliyeitoa.(1) Katika Injili, kwa namna yoyote ile Yesu Kristo haondoi wajibu huu, bali anauimarisha.(2) (1) Rum. 13:8-10, Efe. 6:2, 1 Yoh. 2:3-4,7-8, Rum. 3:31, 6:15, Yak. 2:8,10-11 (2) Mt. 5:17-19, Yak. 2:8, Rum. 3:31 Sehemu ya 6 Ingawa Waamini wa kweli hawahesabiwa haki au kulaaniwa na sheria kama vile ilivyo katika za Agano la Matendo (kazi)(1) Lakini, bado sheria hii ni muhimu sana kwao na kwa wengine. Kama sheria ya maisha, inawafahamisha mapenzi ya Mungu na wajibu wao kuitii. (2) Pia inafunua uchafu wa dhambi zao za asili (3) ili, wajichunguze wenyewe wapate kuwa na uhakika zaidi juu ya uwepo wa dhambi ndani yao, ili wadhalilishwe kupitia dhambi hizo na wazichukie zaidi na zaidi (4) kwa hiyo wanapata ufahamu bora wa hitaji lao kwa Kristo na kwa ukamilifu wa utii wake. (5) Makatazo dhidi ya dhambi (6) katika sheria pia yanafaa katika 51

kuwazuia Waamini kufuata matamanio yao ya asili, na adhabu ya kutotii katika sheria huwaonyesha ni nini dhambi zao zinastahili na matokeo yanayoweza kujitokeza kwa ajili yao katika maisha haya, ingawa wameachiliwa kutoka katika laana ya sheria.(7) Ahadi ya sheria vilevile huwaonyesha kuwa Mungu anakubali utii wao na kwamba baraka zinaweza kutarajiwa kwa utii huo,(8) ingawa siyo kama ilivyokusudiwa katika Agano la Matendo.(9) Ukweli kwamba sheria inahimiza kutenda mema na inakataa kufanya maovu haimaanishi kuwa mtu anayefanya mema na kujiepusha na uovu yuko chini ya sheria na sio chini ya neema.(10) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Rum 6:14, Gal 2:16, 3:13, 4:4-5, Mdo 13:39, Rum 8:1 Rum 7:12,22,25, Zab 119:4-6, 1 Kor 7:19, Gal 5:14,16,18-23 Rum 7:7, 3:20 Yak 1:23-25, Rum 7:9,14,24 Gal 3:24, Rum 7:24-25, 8:3-4 Yak 2:11, Zab 119:101,104,128 Ezr 9:13-14, Zab 89:30-34 Law. 26:1-14, 2 Kor 6:16, Efe 6:2-3, Zab 37:11, Mt 5:5, Zab 19:11 (9) Gal 2:16, Lk 17:10 (10) Rum 6:12,14, 1Pet 3:8-12, Zab 34:12-16, Ebr 12:28-29

Sehemu ya 7 Matumizi ya sheria hizi hayapo kinyume na neema ya Injili. Badala yake hukubaliana na Injili.(1) kwa sababu Roho wa Kristo kuwezesha mapenzi ya mwanadamu kufanya kwa hiari na kwa furaha mapenzi ya Mungu, yaliyofunuliwa katika sheria. (2) (1) Gal. 3:21, Tit. 2:11-14 (2) Ezr. 36.27, Heb. 8.10, Yer 31.33, Gal 3.13

52

SURA YA 20. KUHUSU UHURU WA KIKRISTO NA UHURU WA DHAMIRI Sehemu ya 1 Katika Injili, Kristo alinunua uhuru wa Waamini. Aliwaokoa kutoka kwenye hatia ya dhambi, na ghadhabu ya Mungu, pia kutoka kwenye laana ya sheria ya maadili.(1) Pia, amewaokoa na ulimwengu mbaya wanamoishi; kutoka utumwa wa Shetani, na kutoka kwenye utawala wa dhambi.(2) Kutoka kwenye mateso ya uovu, uchungu wa kifo, na kutoka kwenye adhabu ya milele. (3) Katika Kristo Waamini wanamfikia Mungu bure na wanaweza kumtii, sio kwa sababu ya woga wa utumwa, bali kwa upendo kama wa mtoto na nia ya kujitolea (4) Waamini walikuwa na uhuru huu hata walipokuwa chini ya sheria. (5) Lakini sasa katika Agano Jipya, uhuru wa Wakristo umepanuka zaidi, Wakristo wako huru kutoka kwenye “sheria za ibada” ambazo Wayahudi walipaswa kuzitunza.(6) Wakristo pia wana ujasiri zaidi wa kukikaribia kiti cha neema, (7) na wanaweza kuwasiliana kwa uhuru zaidi na Roho Mtakatifu. (8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Tit. 2:14, 1 Thes. 1:10, Gal. 3:13, Rum. 8:1 Gal. 1:4, Kol. 1:13, Mdo. 26:18, Rum. 6:14, 1 Yn. 1:7 Rum. 8:28, Zab. 119:71, 1 Kor. 15:54-57, Rum. 8:1 Rum. 8:14-15, 1Yoh. 4:18, Efe. 2:18, Gal 4:6, Ebr. 10:19 Gal. 3:9,14 Gal. 4:1-3, 6-7, 5:1, Mdo .15:10-11 Ebr. 4:14,16, 10:19-22 Yn. 7:38-39, 2 Kor. 3:13, 17-18, Rum. 5:5

53

Sehemu ya 2 Mungu pekee ndiye anayetawala dhamiri ya Mwamini na dhamiri haina mafundisho na maagizo ya wanadamu ambayo kwa njia yoyote ile yanapingana au yako tofauti na Neno Mungu katika maswala ya imani au ibada. (1) Na hivyo, kuamini aina yoyote ya mafundisho au kutii amri kama hizo za wanadamu kwa ajili ya dhamiri, kwa kweli tunasaliti uhuru wa dhamiri. (2) Ikiwa Waamini watakuwa vipofu katika imani na kuamini kitu chochote bila utambuzi, wanaangamiza dhamira zao.(3) (1) Yak. 4:12, Rum. 14:4,10, Mdo. 4:19, 5:29, 1Kor. 7:23, Mt 23:810, 2Kor. 1:24, Mt. 15:9 (2) Kol. 2:20-23, Gal. 1:10, 5:1, 2:3-5, Zab. 5:1, Gal 4:9-10 (3) Rum. 10:17, 14:23, Isa. 8:20, Mdo. 17:11, Yn. 4:22, Hos. 5:11, Ufu. 13:12,16-17, Yer. 8:9, 1Pet. 3:15

Sehemu ya 3 Wale ambao hufanya dhambi au kushadidia dhambi kwa kisingizio cha uhuru wa Kikristo, hawa wanaharibu kusudi lote la uhuru wa Kikristo ambao ni kwamba, tukiwa tumeokolewa kutoka kwenye mikono ya adui zetu, tunaweza kumtumikia Bwana bila woga na katika hali ya utakatifu na haki mbele zake siku zote za maisha yetu (Gal. 5:13, 1Pet. 2:16, 2 Pet. 2:19, Yn. 8:34, Lk. 1:74-75, Rum. 6:15,2 Pet. 3:15). Sehemu ya 4 Mungu hakukusudia mamlaka ambayo aliiweka ili kupinga uhuru ambao Kristo aliununulia kwa Waamini. Lakini vyote, Mamlaka na uhuru wa Kikristo vinapaswa kushirikiana. Na kwa hiyo, wale wanaopinga nguvu yoyote halali au utumiaji 54

halali wa nguvu, iwe ni ya kiraia au ya kikanisa, kwa kisingizio cha uhuru wa Kikristo, kwa kweli wanapingana na Mungu. (1) Ikiwa watu wanaeneza maoni au kufanya mambo ambayo yanapingana na mafundisho au kinyume na kanuni za Ukristo; kanisa lina kila haki ya kuwasimamisha na kuwaweka chini ya nidhamu (2) (1) Mt. 12:25, 1 Pet. 2:13-14,16, Rum. 13:1-8, Ebr. 13:17). (2) Rum. 1:32, 1Kor. 5:1,5,11-13, 2 Yoh. 5:10-11, 2Thes. 3:14, 1Tim. 6:3-5, Tim. 1:10-11,13, 3:10, Mt. 18:15-18, 1Tim. 1:1920, Ufu. 2:14-15,20, 3:9, Rum. 16:17, 2Thes. 3:6, Kumb. 13:612, Rum. 13:3-4, 2 Yoh. 5:10-11, Ezr. 7:23-28, Ufu. 17:12,1617.

SURA YA 21. KUHUSU IBADA NA SIKU YA SABATO Sehemu ya 1 Ufahamu wa asili unaonesha kuwa kuna Mungu, ambaye ni Bwana na Mfalme juu ya vitu vyote, ambaye ni Mwema na anayefanya mema kwa kila mtu, na kwa hiyo anapaswa kutukuzwa, kupendwa, kusifiwa, kuaminiwa na wote kwa mioyo yetu yote, na kwa nguvu zetu zote.(1) Njia inayokubalika ya kumwabudu Mungu wa kweli imeanzishwa na Mungu mwenyewe. Mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa hufafanua na kuelezea ibada sahihi ili mawazo ya wanadamu na Shetani yasifuatwe. Mungu haabudiwi chini ya uwakilishi wowote unaoonekana au kwa njia nyingine yoyote ile isipokuwa ile iliyoainishwa katika Maandiko Matakatifu. (2)

55

(1) Rum. 1:19-20, Mdo 17:24, Zab. 119:68, Yer 10:7, Zab 31:23, 18:3, Rum. 10:12, Zab. 62:8, Yosh. 24:14, Mk. 12:33, Zab. 19:1-6, Mdo. 14:17). (2) Kumb. 12:32, Mt 15:9, Mdo. 17:24-25, Mt 4:9-10, Kumb. 4:1520, Kut. 20:4-6, Kol. 2:20-23, Yn. 4:23-24).

Sehemu ya 2 Ibada zote zinapaswa kutolewa kwa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ni kwake peke yake tu (1) na sio kwa malaika, au kwa watakatifu fulani, au kwa kiumbe chochote kingine. (2) Tangu anguko, ibada imekuwa ikihusisha mpatanishi, na hakuna mpatanishi mwingine zaidi ya Kristo Yesu pekee. (3) (1) Mt. 4:10, Yn. 5:23, 2 Kor. 13:14, Ufu. 5:11-14, Mt. 28:19 (2) Kol. 2:18, Ufu. 19:10, Rum. 1:25 (3) Yn. 14:6, 1 Tim. 2:5, Efe. 2:18, Kol. 3:17

Sehemu ya 3 Maombi pamoja na shukrani ni sehemu ya ibada(1)na Mungu anamtaka kila mtu aombe.(2)Ili maombi yakubaliwe, lazima yafanywe kwa jina la Yesu(3)kwa msaada wa Roho wake Mtakatifu,(4)kulingana na mapenzi ya Mungu,(5)pamoja na ufahamu kamili, unyenyekevu, bidii, imani, na uvumilivu(6)na ikiwa mwombaji anaomba kwa sauti, basi ile lugha anayotumia ni lazima ijulikane. (7) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Fil. 4:6, 1Tim. 2:1, Kol. 4:2 Zab. 65:2, Lk. 18:1, 1Tim. 2:8, Zab. 67:3, 1Thes. 5:17-18 Yn 14:13-14, 1Pet. 2:5 Rum. 8:26, Efe. 6:18 1Yn. 5:14 Zab. 47:7, Mhu. 5:1-2, Ebr. 12:28, Mwa. 18:27, Yak 5:16, 1:6-7, Mk. 11:24, Mt. 6:12,14-15, Kol. 4:2, Efe. 6:18 (7) 1Kor. 14:14

56

Sehemu ya 4 Tunapaswa kuomba tu kile kinachoruhusiwa. (1) kuomba kwa ajili ya watu walio hai au wale wanaotarajia kuzaliwa [yaani watoto walio ndani ya matumbo ya mama zao] (2) lakini hatupaswi kuomba kwa ajili ya wafu. (3) Wala hatupaswi kuomba kwa watu wanaojulikana kuwa wamefanya dhambi ya mauti. (4) (1) (2) (3) (4)

Yoh. 5:14, Mt. 26:42 1Tim. 2:1-2, Yoh. 17:20, 2 Sam. 7:29, Rut 4:12 2 Sam. 12:21-23, Lk. 16:25-26, Ufu. 14:13 1 Yoh. 5:16

Sehemu ya 5 Ibada ya kawaida mbele za Mungu ni pamoja na; kusoma kwa uangalifu Neno la Mungu,(1)Kuhubiri mahubiri sahihi,(2)na kusikia kwa makini Neno la Mungu na kutii kwa imani;(3)kuimba kwa zaburi na neema mioyoni;(4)na kupokea Sakramenti zilizoanzishwa na Kristo.(5) Pia kuna utoaji wa ahadi(6) na viapo (7)kufunga(8)na kushukuru katika sherehe maalum.(9)Ibada inapaswa kufanywa kwa njia takatifu sana.(10) (1) Mdo. 15:21, Ufu. 1:3, Mdo. 17:11 (2) 2 Tim. 4:2 (3) Yak. 1:22, Mdo. 10:33, Mt. 13:19, Ebr. 4:2, Isa. 66:2 (4) Kol. 3:16, Efe. 5:19, Yak. 5:13, Mdo. 16:25 (5) Mt. 28:19, 1 Kor. 11:23-29, Mdo. 2:42 (6) Kumb. 6:13, Neh. 10:29 (7) Isa. 19:21, Mhu. 5:4-5, Mdo. 18:18, Zab. 116:14, Neh. 10:29 (8) Est. 4:16, Mt. 9:15, 1 Kor. 7:5, Mt. 6:17-18 (9) Zab. 107, Est. 9:22, Neh. 12:31-43 (10) Ebr. 12:28, Yn. 4:24, Ebr. 10:22

57

Sehemu ya 6 Katika nyakati za Injili, ibada haifungwi kwamba inapaswa kufanyika mahali fulani maalum au katika eneo fulani (1) Mungu anapaswa kuabudiwa kila mahali.(2) Pia anapaswa kuabudiwa katika roho na kweli; (3) katika familia,(4) kila siku, (5) faraghani, (6) na katika mikusanyiko ya hadhara, ambayo ni lazima watu wakusanyike kwa pamoja kwa ajili ya kumwomba na kumwabudu Mungu. (7) (1) (2) (3) (4)

Yn. 4:21 Mal. 1:11, 1Tim. 2:8 Yn. 4:23-24 Yer. 10:25, Kumb. 6:6-7, Ayu. 1:5, 2 Sam. 6:8-18, 20, 1 Pet. 3:7, Mdo. 10:2 (5) Mt. 6:11, Yosh. 24:15, Dan. 6:10 (6) Mt. 6:6, Efe. 6:18, Neh. 1:4-11 (7) Isa. 56:7, Ebr. 10:25, Mith. 1:20-21, 24, 8:34, Mdo. 13:42, Lk. 4:16, Mdo. 2:42

Sehemu ya 7 Ni sheria ya maisha yetu ya asili na ya kidunia kutenga muda fulani kwa ajili ya ibada kwa Mungu. Hata hivyo, Mungu, katika Neno lake, ameamuru watu wote katika kila kizazi kuweka siku moja katika siku saba na kuiweka takatifu kwake kama Sabato. (1) Tangu mwanzo wa ulimwengu hadi ufufuo wa Kristo, Sabato hii ilikuwa siku ya Mwisho ya Juma. Tangu ufufuo wa Kristo, imebadilishwa kuwa siku ya Kwanza ya Juma, katika Maandiko Matakatifu inaitwa “Siku ya Bwana” na inapaswa kuendelea hadi mwisho wa ulimwengu kama Sabato ya Kikristo; (2) Maandiko yanayohusu Sabato ya Kikristo mara

58

nyingi yamehusishwa na mfano wa mitume na kanisa la kwanza. (1) Kut. 20:8-11, Isa. 56:2,4,6-7 (2) Mwa. 2:2-3, 1 Kor. 16:1-2, Mdo. 20:7, Ufu. 1:10, Kut. 20:8,10, Mt. 5:17-18 Sehemu ya 8 Siku ya Sabato ni takatifu kwa Bwana. Watu wanapaswa kutayarisha mioyo yao kwa ajili ya ibada hiyo. Wanapaswa kuandaa mambo yao ya kila siku ili katika siku hiyo wanaweza kupumzika kwa njia takatifu. Wanapaswa kupumzika siku nzima na kuacha matendo, maneno, na hata mawazo juu ya kazi na burudani zao za kila siku.(1) Wanapaswa kutumia wakati wao wote katika ibada ya pamoja na ya kibinafsi kwa Mungu, na pia kufanya majukumu ambayo ni muhimu au kufanya matendo ya huruma. (2) (1) Kut. 20:8, 16:23, 25-26,29-30, 31:15-17, Isa. 58:13, Neh. 13:1522, Lk. 23:56 (2) Isa. 58:13, Mt. 12:1-13

SURA YA 22. KUHUSU VIAPO HALALI NA NADHIRI Sehemu ya 1 Viapo halali na nadhiri ni sehemu ya ibada. (1) Katika matukio sahihi Waamini wanaweza kuapa kiapo na kumwita Mungu kushuhudia kwamba kile wanachokidai ni kweli au kuahidi ni

59

kweli, na wanaweza kumwomba Mungu kuwahukumu kulingana na ukweli au uongo wa kile walichoapa.(2) (1) Kumb. 10:20. (2) Kut. 20:7, Law. 19:12, 2Kor. 1:23, 2Nyak. 6:22-23 Sehemu ya 2 Jina la Mungu ndilo jina pekee ambalo wanadamu wanapaswa kutumia katika kiapo, na jina hilo linapaswa kutumiwa kwa hofu takatifu na heshima. (1) Kwa hiyo, kuapa bure au kwa ujinga kwa jina hilo tukufu na lenye nguvu au kuapa kwa jina jingine lolote ni dhambi na aibu kubwa. (2) Kama ilivyo katika mambo muhimu, kiapo kinadhibitishwa na neno la Mungu, chini ya Agano Jipya na Agano la Kale, hivyo pindi mamlaka halali zinapotutaka kufanya kiapo cha aina hii kwa mambo muhimu, tunapaswa kuchukua kiapo hicho. (3) [kwa mfano ikiwa Mkristo utapaswa kuapa mbele ya Hakimu kwamba unayoenda kuzungumza yatakuwa ni kweli; Kiapo kama hiki ni halali na unapaswa kusimama katika ukweli na kinyume chake ni dhambi]. (1) Kumb. 6:13 (2) Kut. 20:7, Yer 5:7, Mt. 5:34,37, Yak 5:12 (3) Ebr. 6:16, 2 Kor 1:23, Isa 65:16, 1Fal. 8:31, Neh. 13:25, Ezr. 10:5, Mt. 26:63-64

Sehemu ya 3 Yeyote anayekula kiapo anapaswa kuzingatia kabisa umuhimu wa kitendo hicho, na kwa hiyo hapaswi kuapa kwa chochote kile isipokuwa kile anachoamini kabisa kuwa ni kweli. Hakuna mtu anayeweza kujifunga kwa kiapo kwa kitu chochote 60

isipokuwa kile kilicho kizuri na cha haki, na kwa kile anachoamini kuwa ni kweli, na pia kile anachoweza au amedhamiria kukitekeleza. Ni dhambi kukataa kuapa kiapo juu ya jambo lolote jema na la haki, pale inahitajika na mamlaka halali (Kut. 20:7, Yer. 4:2, Mwa. 24:2-3,5-6,8-9, Hes. 5:19,21, Neh. 5:12, Kut. 22:7-11) Sehemu ya 4 Kiapo kinapaswa kuchukuliwa kwa uwazi, maneno yanayotumika yawe na maana ya wazi. (1) Kiapo hakiwezi kumlazimisha mtu kutenda dhambi; lakini mara baada kuchukuliwa ni lazima kitekelezwe, hata kama ni kwa madhara ya mtu mwenyewe, (2) na hakipaswi kuvunjwa, hata ikiwa kimefanywa kwa wazushi au wasiomwamini Mungu.(3) (1) Yer. 4:2, Zab. 244, Kut. 20:7 (2) 1 Sam. 25:22, 32-34, Zab. 154 (3) Eze. 17:16,1 8-19, Yosh. 9:18-19, 2 Sam. 21:1 Sehemu ya 5 Nadhiri ni sawa na kiapo kinachoahidi kitu na kinapaswa kufanywa na kutekelezwa kwa uaminifu. (Isa 1:21, Mhu. 5:4-6, Zab 61:8, 66:13-14, Kumb. 23:21,23). Sehemu ya 6 Nadhiri haipaswi kufanywa kwa mtu yeyote isipokuwa kwa Mungu. (1) Ili kukubaliwa inapaswa kufanywa kwa hiari kama njia ya uaminifu na dhamiri kama shukrani kwa rehema tulizopokea. Nadhiri inatufunga zaidi kwa majukumu muhimu na hutusaidia kuyatekeleza majukumu hayo kikamilifu.(2) [kwa 61

mfano wachungaji katika viapo vyao hufanya nadhiri ya uaminifu katika huduma.] (1) Zab. 76:11, Yer. 44:25-26 (2) Kumb. 23:21,23, Zab 50:14, Mwa. 28:20-22, 1 Sam. 1:11, Zab. 66:13-14, 132:2-5 Sehemu ya 7 Hakuna mtu yeyote anayeweza kutoa nadhiri kufanya kitu chochote kilichozuiwa na Neno la Mungu, au kitu chochote kinachozuia jukumu lililoamriwa na Neno la Mungu, au kitu chochote nje ya uwezo wake mwenyewe, au hana kibali kutoka kwa Mungu katika kukitekeleza. (1) Kwa kuzingatia hili, nadhiri za monastiki ya useja wa kudumu, au kuishi maisha ya kimasikini, na kutii; hizi si njia zinazotuongoza kuishi maisha makamilifu bali ni mitego ya dhambi, ambayo hakuna Mkristo anayepaswa kujiingiza mwenyewe kwenye nadhiri hizo. (2) (1) Mdo. 23:12,14, Mk. 6:26, Hes. 30:5, 8, 12-13 (2) Mt. 19:11-12, 1 Kor. 7:2,9, Efe. 4:28, 1 Pet 4:2, 1Kor. 7:23, 1Thes. 4:11-12

SURA YA 23. KUHUSU MAMLAKA YA KIRAIA Sehemu ya 1 Mungu, Bwana aliye juu na Mfalme wa ulimwengu wote, ameteua wakuu wa serikali kuwa juu ya watu kwa niaba yake, kwa utukufu wake na uzuri wa umma. Hivyo, amezipa silaha na nguvu serikali za kiraia kuwatetea na kuwatia moyo wale

62

ambao wanatenda mazuri na kuwaadhibu watenda mabaya. (Rum. 13:1-4, 1 Pet. 2:13-14). Sehemu ya 2 Ni halali kwa Wakristo kukubali na kutekeleza kazi za kiserikali ikiwa huo ndio wito wao. (1) Katika usimamizi wa ofisi kama hizi wanapaswa kuchukua tahadhari ili kuunga mkono mambo ya haki, na amani kwa mujibu wa sheria nzuri za kila serikali.(2) Kwa kuzingatia hilo, ni halali, na ni muhimu kwa Wakristo kwenda vitani ikiwa sababu ya vita hivyo ni ya haki.(Mith 8:15-16, Rum 13:1-4) (1) Zab. 2:10-12, 1 Tim. 2:2, Zab. 82:3-4, 2 Sam. 23:3, 1 Pet. 2:13, Zab. 101 (2) Lk. 3:14, Rum. 13:1-4, Mt 8:9-10, Mdo. 10:1-2, Ufu. 17:14,16 Sehemu ya 3 Japokuwa mamlaka ya kiraia haiwezi kutoa huduma ya Neno la Mungu na Sakramenti, au usimamizi wa nidhamu ya kanisa au kuingilia chochote katika maswala ya imani,(1) lakini, bado ni jukumu la viongozi wa serikali kulinda kanisa la Bwana wetu, bila kutoa upendeleo kwa dhehebu lolote, ili kila mtu aliye na ushirika au majukumu ya kanisa aweze kufanya kazi kwa uhuru kamili. Tangu Yesu Kristo alipoelekeza uanzishwaji wa serikali za kanisa na nidhamu, hakuna sheria inayoruhusu kuingilia kati, au kuzuia zoezi sahihi la serikali ya kanisa miongoni mwa washirika wa madhehebu ya Kikristo. Ni jukumu la viongozi wa serikali kumlinda kila mtu ili kwamba hakuna mtu anayedhulumiwa, anayejeruhiwa, au anayedharauliwa kwa sababu ya imani yake.(2) Pia ni jukumu serikali kuhakikisha 63

kwamba makusanyiko yote ya kanisa yanafanyika bila usumbufu na upendeleo. (1) 2 Nyak. 26:18, Mt. 18:17, 16:19, 1Kor. 12:28- 29, Efe. 4:11-12, 1Kor. 4:1-2, Rum. 10:15, Ebr 5:4, Yn 18:36, Mdo. 5:29 (2) Isa. 49:23, Zab. 122:9, Ezr. 7:23-28, Law. 24:16, Kumb. 13:56,12, 2 Fal. 18:4, 1Nyak. 13:1-9, 2 Fal. 23:1-26, 2 Nyak. 34:33, 15:12-13, Rum. 13:1-6, Zab 105:15, Mdo. 18:14-16 (3) 2 Nyak. 19:8-11, 29, 30 Mt. 2:4-5, 2 Sam. 23:3, Rum. 13.4

Sehemu ya 4 Ni jukumu la watu kuwaombea wale walio katika mamlaka (1) kuwaheshimu, (2) kulipa kodi na chochote kinachodaiwa na serikali (3) kutii amri zao halali, na kuwa chini yao (4) Kutokuamini au kuwa na maoni tofauti ya kikanisa kwa upande wa viongozi wa serikali haimaanishi kwamba Waamini wasiwatii,(5)pale wanapotekeleza majukumu yao halali.(6) Kwa kweli, Papa, hana nguvu wala mamlaka juu ya viongozi wa serikali au watu walio chini yao katika maswala ya kidunia. Papa kamwe hana haki ya kuchukua mamlaka ya kidunia. Kwa hakika yeye hana nguvu ya kuchukua mamlaka kwa niaba ya serikali, au hata kutekeleza adhabu ya kifo kwa wale ambao anafikiria ni wazushi au kwa sababu nyingine yoyote ile.(7) [Katika historia, Papa alikuwa na uwezo wa kutoa hata hukumu ya kifo pindi mtu anapokuwa ameasi kanisa katoliki, hivyo basi hoja hii imejengwa kulingana na historia]. (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

1 Tim. 2:1-3 1 Pet. 2:17 Rum. 13:6-7, Mt. 22:2 Rum. 13:5, Tit. 3:1 Rum. 13:1, 1 Fal. 2:35, Mdo. 25:9-11, 2 Pet. 2:1, 10-11, Yud. 8-11 1 Pet 2:13-14, 16). 2 Thes. 2:4, Ufu. 13:15-17, 2 Tim. 2:24, 1 Pet. 5:3

64

SURA YA 24. KUHUSU NDOA NA TALAKA Sehemu ya 1 Ndoa ni umoja kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja iliyoanzishwa na Mungu kuwa ya kudumu muda mrefu maadamu wanandoa wote wako hai (Mwa. 2:23-24, 1 Kor. 7:2,39, Mt. 19:4-6, Efe. 5:28,31,33, 1 Kor. 13:8,13, Mt 5:31-32, Mk. 10:5-9, Rum. 7:2-3). Sehemu ya 2 Ndoa ilianzishwa kwa usaidizi wa pande zote; kwa mume na mke;(1) kwa ajili ya usalama, na kukuza tabia yao ya maadili na ya kiroho;(2) kwa kuishi katika nidhamu na maagizo ya Bwana (3)

(1) Mwa. 2:18,24 (2) Mwa. 1:27-28, Efe. 5:22-23, Kol. 3:18-19, Mwa. 2:1825, 1 Kor. 7:3-5, 9,36 (3) Mwa. 1:27-28, 9:1, Mal. 2:15, Mt. 18:5-6,10,14, 19:14, Efe 6:1-4, Kol 3:20-21, Mk. 10:13-16, Lk. 18:15-17 Sehemu ya 3 Watu wote ambao wanaweza kuwa na uamuzi kwa idhini yao wenyewe wanaweza kuoa au kuolewa (1) isipokuwa ndani ya mipaka ya uhusiano wa damu uliokatazwa na Maandiko, [mtu hawezi kuoa ndugu yake wa damu] (2) na ndoa ni halali mbele za Mungu na machoni pa kanisa ikiwa imezingatia mipaka. (3) Lakini hakuna ndoa inayoweza kuwa kamili na salama 65

isipokuwa wenzi wote wawili wawe katika imani ya Kikristo na wakusudie kwa pamoja kujenga familia ya Kikristo. Wakristo kutoka katika makanisa ya Kiinjili wanapaswa kutafuta wenzi kutoka kwenye makanisa ya Kiinjili wenye imani sawa.(4) (1) Mwa. 1:27-28 (2) Mk 6:18, 1 Kor 5:1, Law. 18:6-18 (3) Mk 1:30, Yn 2:1-2, 1Tim 5:14, Ebr 13:4, 1 Kor 7:7,36, 9:5, 1 Tim 4:3 (4) 1 Kor 7, hasa mstari wa 39, 2 Kor 6:14-15

Sehemu ya 4 Ndoa kwa Mkristo ina umuhimu wa kikanisa na wa kiserikali (1) Mchango wa kanisa katika kutekeleza ibada ya ndoa ni kuthibitisha Uungu katika taasisi ya ndoa;(2) kuomba baraka za Mungu juu ya wale wanaoingia kwenye uhusiano wa ndoa kwa mujibu wa Neno la Mungu, (3) kusikia viapo na nadhiri vya wale wanaooana; na kuwahakikishia wanandoa hawa neema ya Mungu ndani ya uhusiano wao mpya. (4) [Kwa upande wa serikali, ndiyo inayotoa vyeti vya ndoa na hivyo ndoa inakuwa halali katika sheria za kiraia] (1) (2) (3) (4)

Mith 18:22, Mt 19:6, Efe 5:29-30, 32, Mk 10:9, 11-12 Mwa. 1:27-28) Mk 10:9 Efe 5:22-23

Sehemu ya 5 Ni kusudi la Kimungu kwamba watu wanaoingia katika agano la ndoa wawe na umoja, hivyo utengano wa aina yoyote hauruhusiwi isipokuwa ule uliosababishwa na kifo cha mume 66

au mke.(1) Na ikiwa mume au mke anafanya uzinzi baada ya ndoa,[hasa inapotokea kwamba upande mmoja hautaki kutubu, ama kwa sababu ya dhambi ya uzinzi kuzoeleka kwa mmoja wa wanandoa] basi ni sababu tosha kwa mtu asiye na hatia kupata talaka. Ikiwa talaka itatolewa, mtu asiye na hatia anaweza kuoa au kuolewa na mtu mwingine, ikiwa yule mwenzi wake wa zamani atakuwa amefariki. (2) (1) Mwa. 2:23-24, Mt. 5:31-32, Mk. 10:5-9, Rum. 7:2-3, 1 Kor. 7:2, 10-11,39, Efe 5:28,31,33, Mt. 19:4-9, 1 Kor. 13:4-13 (2) Mk. 10:4-9, 1 Kor. 7:12-13, 15, Mt. 19:7-9

Sehemu ya 6 Watu ni wenye dhambi, na watajaribu kupata hoja zinazothibitisha kuvunja ndoa ambayo Mungu ameiunganisha. Walakini, talaka ni chaguo tu ikiwa mwanamume au mwanamke ametenda uzinzi, au ameachana na ndoa kwa ukaidi ili isiweze kurekebishwa na Kanisa au viongozi wa kiserikali. Katika hali hiyo, hoja za talaka lazima ziwe hadharani na kwa utaratibu, na mwanamume na mwanamke hawapaswi kuachwa kuwa na maamuzi wenyewe katika jambo hilo (1) [hoja kwamba wanandoa wanaotalikiana wasiachiwe kwa hiari yao wenyewe ni kwamba kila juhudi zinapaswa kufanyika kwa ajili ya kusuluhisha ndoa hiyo; hakuna sababu ya kuwaacha watu watengane ikiwa kuna uwezekano wa kusuluhisha; lakini pia kama ndoa imekuwa ni hatarishi, basi hekima itumie katika kutatua masuala haya, au hata kama ni talaka inaweza kutolewa. Hekima za Kimungu zitaongoza] Math. 19:8, 9; I Kor. 7:15; Math. 19:6. Kumb. 24:1, 2, 3, 4

67

SURA YA 25. KUHUSU KANISA Sehemu ya 1 "Kanisa lisiloonekana" linaundwa na watu wote ambao Mungu amewachagua ulimwenguni kote. Wamekusanywa katika kundi moja chini ya Kristo, ambaye ni kichwa cha kanisa. Kanisa ni mwili wake, bibi harusi wake, pia ni utimilifu wa Mungu, ambaye huwajaza watu wote (Efe 1:10, 22-23, 5:23,27,32, Kol 1:18). Sehemu ya 2 “Kanisa linaloonekana", kwa upande mwingine, limetengenezwa na sisi sote ambao tunasema ni Wakristo, pamoja na watoto wetu. Katika kipindi hiki cha Injili tofauti na wakati wa sheria ya Musa, wakati lilipokuwa taifa la Israeli tu. Kanisa linaloonekana ni ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni nyumba ya Mungu, familia yake. Wale walio nje ya kanisa hili linaloonekana kwa kawaida hawaokolewi. 1 Kor 1:2, 12:12-13, Zab 2:8, Ufu 7:9, Rum 15:9-12, I Kor. 7:14; Mdo 2:39; Eze. 16: 20, 21; Rum 11:16; Mwa. 3:15; Mwa. 17: 7. Mt. 13:47; Isa. 9: 7, Efe. 2:19; Efe. 3:15 Mdo 2:47 Sehemu ya 3 Kwa kanisa hili linaloonekana, Kristo ametoa huduma, mafundisho, na maagizo ya Mungu, kwa kukusanyika na kuwakamilisha watakatifu, katika maisha haya, hadi mwisho wa ulimwengu: na hufanya hivyo kwa uwepo wake mwenyewe na Roho, kulingana na ahadi. (I Kor. 12:28; Efe. 4: 11, 12, 13; Mt. 28:19, 20; Isa. 59:21). 68

Sehemu ya 4 Kanisa hili wakati mwingine linaonekana zaidi, wakati mwingine linaonekana kidogo.(1)Na Makanisa fulani, ambayo ni wanachama wake, ni safi au dhaifu, kwa kutegemea mafundisho ya Injili yanafundishwa na amri zinazosimamiwa, na ibada ya umma inayofanywa ni zaidi au kidogo ndani yao.(2) (1) Rum. 11: 3, 4; Ufu 12: 6, 14 (2) Ufu. 2 na 3; 1 Kor. 5: 6, 7 Sehemu ya 5 Makanisa safi kabisa chini ya mbingu yanachanganyikana na makosa:(1) na mengine yameharibika, kana kwamba sio Makanisa ya Kristo, lakini masinagogi ya Shetani. (2) Walakini, kutakuwa na Kanisa kila wakati duniani, ambalo linamwabudu Mungu kulingana na mapenzi yake.(3) (1) I Kor. 13:12; Ufu 2 na 3; Mt. 13:24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 47 (2) Ufu 18: 2; Rum 11:18, 19, 20, 21, 22 (3) Mt. 16:18; Zab. 72:17; Zab. 102: 28; Mt. 28:19, 20 Sehemu ya 6 Hakuna mkuu mwingine wa Kanisa, isipokuwa Bwana Yesu Kristo, (1) wala Papa wa Roma si mkuu wa kanisa kwa maana yoyote ile, lakini yule ni mpinga-Kristo, yule mtu wa uasi, na mwana wa uharibifu, anayejiinua, katika Kanisa, dhidi ya Kristo na yote ambayo huitwa Mungu.(2) (1) Kol 1:18; Efe. 1:22 (2) Mt. 23: 8, 9, 10; II Thes. 2: 3, 4, 8, 9; Ufu 13: 6 69

SURA YA 26. KUHUSU USHIRIKA WA WATAKATIFU Sehemu ya 1 Watakatifu wote, ambao wameunganika katika Yesu Kristo kama kichwa chao kwa Roho wake na kwa imani, wana ushirika naye katika neema yake, mateso, kifo, ufufuo, na utukufu:(1) na wameunganishwa pia kwa upendo kwa kila mmoja. wanashirikiana kwa karibu karama na baraka za kila mmoja (2) na wanawajibika kutekeleza majukumu haya, kwa umma na faragha, kwa njia ambayo ni nzuri kwa mwili na roho.(3) (1) Yn 1: 3; Efe. 3:16, 17, 18, 19; Yn 1:16; Efe. 2: 5, 6; Fil. 3: 10; Rum 6: 5, 6; 2 Tim. 2:12 (2) Efe. 4:15, 16; 1 Kor. 12: 7; 1 Kor. 3:21, 22, 23; Kol 2: 19 (3) I Thes. 5:11, 14; Rum 1:11, 12, 14; 1 Yoh 3:16, 17, 18; Gal. 6:10

Sehemu ya 2 Watakatifu wanapaswa kutudumisha ushirika katika ibada ya Mungu. Na katika kufanya masuala mengine ya kiroho ambayo yamekusudiwa kwa ajili ya kujengana.(1)Kama washirika wengine wana mahitaji na tunao uwezo wa kuwasaidia, basi ni lazima tusaidiane. Kwa kadri Mungu anavyotupatia fursa tunahitaji kushiriki ushirika huu na kila mtu anayeliitia jina la Bwana Yesu, haijalishi anaishi wapi.(2) (1) Ebr. 10:24, 25; Mdo 2:42, 46; Isa. 2: 3; 1 Kor. 11:20 (2) Mdo 2: 44, 45; 1 Yn 3:17; II Kor. Sura 8 na 9; Mdo 11:29, 30

70

Sehemu ya 3 Ushirika ambao Waamini wanao pamoja na Kristo haimaanishi kuwa wanashiriki sehemu ya Uungu wake au kwamba wao ni sawa na Yesu Kristo kwa njia yoyote ile. Imani kama hiyo haifai na ni kufuru mbele za Mungu.(1) Pia ushirikiano wa Waamini kwa pamoja hauondoi ukweli kwamba kila mmoja anamiliki mali zake binafsi. (2) (1) Kol 1:18, 19; 1 Kor. 8: 6; Isa. 42: 8; 1Tim. 6: 15, 16; Zab. 45: 7, na Ebr. 1: 8, 9 (2) Kut. 20:15; Efe. 4:28; Mdo 5: 4

SURA YA 27. KUHUSU SAKRAMENTI Sehemu ya 1 Sakramenti ni ishara takatifu na mihuri ya Agano la Neema;(1) iliyoanzishwa na Mungu mwenyewe;(2) kwa ajili kuwakilisha Kristo na faida zake; na kuthibitisha utashi wetu kwake, (3) Vile vile sakramenti hufanya kazi ya kutofautisha kati ya wale walio wa Kanisa na wale wa ulimwenguni(4) na kuwashirikisha huduma ya Mungu katika Kristo, kulingana na Neno lake.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Rum. 4:11; Mwa. 17: 7, 10 Mt. 28:19; 1 Kor. 11:23 Rum. 15: 8; Kut. 12:48; Mwa. 34:14 I Kor. 10:16; 1 Kor. 11:25, 26; Gal. 3:17 Rum. 6: 3, 4; 1 Kor. 10:16, 21

Sehemu ya 2 71

Katika kila Sakramenti kuna uhusiano wa kiroho, au umoja wa Sakramenti, kati ya ishara na kitu kinachowakilishwa: Hii ndio sababu maneno na vitendo vilivyotumika kuelezea ishara pia vinaweza kuelezea kile ambacho ile ishara inasimama kwacho (Mwa. 17:10; Mt. 26:27, 28; Tit. 3:5). Sehemu ya 3 Wakati Sakramenti zinapotumiwa ipasavyo, zinatupatia neema ambayo haitoki kwenye Sakramenti zenyewe. Wala hazifai tu pindi yule mtu anayeongoza ana nia takatifu.(1) bali ni kwamba neema ambazo Sakramenti hutupatia inategemea kazi ya Roho Mtakatifu(2)na Neno ambalo linathibitisha kuanzishwa kwake. Neno hili huidhinisha matumizi yake, kuahidi faida nyingi kwa wale wanaopokea inavyostahili.(3) (1) Rum. 2:28, 29; 1 Pet. 3:21 (2) Mt. 3:11; 1 Kor. 12:13 (3) Mt. 26:27, 28; Mt. 28:19, 20

Sehemu ya 4 Kuna Sakramenti mbili tu ambazo zilizowekwa na Bwana wetu Yesu Kristo katika Injili; yaani, Ubatizo na Ekaristi [Meza ya Bwana au Ushirika Mtakatifu] Sakramenti hizi zote haziwezi kutolewa na mtu yeyote yule isipokuwa Mhudumu wa Neno aliyewekwa kihalali [Mhudumu wa Neno maana yake ni mchungaji aliyesimikwa rasmi na kukubaliwa na dhehebu lake kufanya kazi hiyo] (Mt. 28:19; 1 Kor. 11:20, 23, 1 Kor. 4: 1; Ebr. 5: 4)

72

Sehemu ya 5 Kuhusu mambo ya kiroho ambayo yalionyeshwa katika Sakramenti zilizo katika Agano la Kale kimsingi ni sawa na yale yaliyooneshwa katika Sakramenti za Agano Jipya (I Kor. 10:1, 2, 3, 4).

SURA YA 28. KUHUSU UBATIZO Sehemu ya 1 Ubatizo ni Sakramenti ya Agano Jipya iliyowekwa na Yesu Kristo.(1) Ubatizo unaonyesha uaminifu kamili kwa yule anayebatizwa katika kanisa linaloonekana.(2)Pia, ubatizo ni ishara na muhuri wa Agano la Neema,(3) kwamba tumepandikizwa kwa Kristo,(4) tumezaliwa upya,(5) tumesamehewa dhambi,(6)Yesu Kristo alijitoa mwenyewe kwa Mungu ili kupitia yeye tuweze kutembea katika hali mpya ya maisha.(7)Ubatizo kwa maelekezo ya Kristo mwenyewe unapaswa kuwepo katika Kanisa lake hadi mwisho wa ulimwengu. (8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mt. 28:19 I Kor. 12:13) Rum. 4:11 na Kol. 2:11, 12 Gal. 3:27; Rum 6:5 Tit. 3: 5 Mk. 1: 4 Rum. 6: 3, 4 Mt. 28:19, 20

73

Sehemu ya 2 Vifaa vya nje vinavyotumika katika Sakramenti hii ni maji, hata hivyo yule anayebatizwa hubatizwa katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, na anayembatiza ni Mhudumu wa Injili, aliyeitwa kihalali (1) [Siyo mtu yeyote anaweza kubatiza kama ilivyo katika Kanisa Katoliki katika mazingira ya dharura]. (Mt. 3:11; Yohana 1: 33; Mt. 28:19, 20) Sehemu ya 3 Ubatizo sio lazima ufanyike kwa kumzamisha mtu ndani ya maji ingawa hata kule kuzamishwa siyo kosa. Hata kwa kumimina au kunyunyiza maji juu ya mtu huyo ni sawasawa tu [na ni ubatizo halali kwa sababu kitu cha muhimu ni maji na jina la UTATU] (Ebr. 9:10, 19, 20, 21, 22; Mdo 2:41; Mdo 16:33; Marko 7:4). Sehemu ya 4 Ubatizo siyo tu kwa wale ambao wanakiri imani na kumtii Kristo (1) lakini pia watoto wachanga wa Waamini (ama wazazi wote wawili wawe waamini au hata mmoja) wanaweza kubatizwa kwa mujibu wa Maandiko. (2) (1) Marko 16: 15, 16; Mdo 8:37, 38 (2) Mwa. 17: 7, 9, 10 na Gal. 3: 9, 14 na Kor. 2:11, 12 na Mdo 2:38, 39 na Rum. 4: 11, 12;1 Kor. 7:14; Mt. 28:19; Marko 10:13, 14, 15, 16; Lk 18:15

74

Sehemu ya 5 Ingawa ni dhambi kubwa kudharau au kupuuza agizo la kubatizwa,(1)hata hivyo, ubatizo haujafungwa sana kwenye neema ya Mungu na wokovu wake kiasi kwamba mtu hawezi kuzaliwa mara ya pili pasipo ubatizo;(2)au, kwamba wale wote ambao wamebatizwa wamezaliwa mara ya pili.(3) (1) LK 7:30 na Kut. 4:24, 25, 26 (2) Rum. 4:11; Mdo 10: 2, 4, 22, 31, 45, 47 (3) Mdo 8:13, 23 Sehemu ya 6 Ubatizo haufanyi kazi tu pindi unapofanyika. (1) Hata hivyo, katika matumizi sahihi ya ubatizo, Roho Mtakatifu anatupatia neema yake kweli, [iwe ni watu wazima au watoto]. Yeye humpa neema yake yeyote kulingana na kusudi la mapenzi ya Mungu mwenyewe na kwa wakati wake aliouweka.(2) (1) Yohana 3:5, 8 (2) Gal. 3:27; Tit. 3: 5; Efe. 5:25, 26; Mdo 2:38, 41 Sehemu ya 7 Sakramenti ya Ubatizo hutolewa mara moja tu kwa mtu anayepokea Sakramenti hiyo,(1) hata hivyo tunapaswa kujua kwamba ubatizo hufanywa kwa jina la UTATU, na ikiwa mtu alibatizwa bila jina la UTATU basi huyo hakubatizwa, na ikiwa alibatizwa kwa UTATU, bila kujali madhehebu gani, basi hahitaji kubatizwa tena. (Tit 3:5)

75

SURA YA 29. KUHUSU MEZA YA BWANA Sehemu ya 1 Bwana wetu Yesu Kristo katika usiku ule ambao alisalitiwa, alianzisha Sakramenti ya mwili wake na damu, iitwayo Meza ya Bwana ambayo inapaswa kuzingatiwa katika Kanisa lake hadi mwisho wa ulimwengu, kwa ukumbusho wa milele wa kujitolea kwake mwenyewe katika kifo chake; Meza ya Bwana inawakumbusha Waamini chakula cha kiroho na ukuaji katika Kristo. Huwasaidia pia katika kufanya majukumu wanayopaswa kufanya mbele za Mungu, vilevile inaonyesha uhusiano wao wa karibu na Yesu na Waamini wengine [ambao ni sehemu ya mwili wake Kristo]. (1 Kor. 11: 23, 24, 25, 26; 1 Kor. 10:16, 17, 21; 1 Kor. 12:13). Sehemu ya 2 Katika sakramenti hii, Kristo hajatolewa kwa Baba yake; wala hakuna dhabihu yoyote halisi inayotolewa kabisa kwa ondoleo la dhambi; (1)bali ni ukumbusho tu wa yule aliyejitolea mwenyewe, peke yake, juu ya msalaba, mara moja kwa wote: na toleo la kiroho la sifa zote zinazowezekana kwa Mungu;(2) Dhabihu ya Kanisa Katoliki ya misa (kama wanavyoiita) ni tusi kubwa kwa sadaka moja ya Kristo na ya pekee. Sadaka yake ndio kitu pekee kinachoweza kulipia dhambi za Wateule (3) [Hoja ya Wakatoliki ni kwamba Kristo wakati wa meza ya Bwana huwa anasulubiwa kwelikweli. Kwa mtazamo wao, Kristo husulubiwa kila mara kwa kadri wanavyoshiriki Meza ya Bwana.] (1) Ebr. 9:22, 25, 26, 28 (2) I Kor. 11:24, 25, 26; Mt. 26:26, 27 (3) Ebr. 7: 23, 24, 27; Ebr. 10:11, 12, 14, 18

76

Sehemu ya 3 Bwana Yesu, katika agizo hili, ameteua Wahudumu wake kutangaza Neno lake la kuanzishwa kwa Sakramenti hii kwa kuwakumbusha watu; kwa kuomba, na kwa kubariki mkate na divai; hapo Mhudumu kupitia maombi hayo huvitenga (mkate na divai) kutoka kwenye matumizi ya kawaida na kwenda kwenye matumizi ya utakatifu; na kisha kumega mkate, na kuchukua kikombe, na kuwagawia Washiriki (1) waliopo katika ibada hiyo ya meza ya Bwana, na wala haihusishi wale wasiokuwepo. (2) (1) Mt. 26: 26, 27, 28 na Marko 14: 22, 23, 24 na Luka 22: 19,20 na 1 Kor. 11: 23, 24, 25, 26 (2) Mdo. 20: 7; 1 Kor. 11:20

Sehemu ya 4 Kuna vitu kadhaa ambavyo vikifanyika katika kushiriki Meza ya Bwana huenda kinyume na asili ya kuanzishwa kwake; kwa mfano “kupokea sakramenti kutoka kwa kuhani peke yake(1) kuzuia watu wengine kunywa divai (2) kuviabudu vifaa (mkate na divai) kwa kuviinua zaidi katika ibada hiyo.(3)[Hoja hii inatokana na wazo la Wakatoliki kwamba Kuhani peke yake ndiye anatakiwa kukupatia mkate, na pia watu wa kawaida hawawezi kunywa divai; kwa sababu mtu wa kawaida anaweza kumwaga damu halisi ya Yesu]. (1) I Kor. 10:16 (2) Marko 14:23; 1 Kor. 11:25, 26, 27, 28, 29 (3) Mt. 15: 9

77

Sehemu ya 5 Mkate na divai katika Meza ya Bwana vinatengwa na kuwa vitakatifu, na hii inahusiana sana na Kristo aliyesulubiwa. Wakati mwingine huitwa kwa majina ya kile yanachowakilisha, kwa mfano; "mwili na damu ya Kristo". Kwa kweli ni "mwili na damu ya Kristo", kwenye Sakramenti.(1) Lakini katika hali ya kawaida vinabaki mkate na divai.(2) [kwa maana ya kwamba katika ulimwengu wa kimwili, mkate na divai havibadiliki, na kwamba mabadiliko yanayofanyika ni kule kutengwa tu kwa ajili ya matumizi maalum kwa wakati huo ili kuwakilisha mwili na damu ya Yesu.] (1) Mt. 26:26, 27, 28

(2) 1 Kor. 11:26, 27, 28; Mt. 26:29

Sehemu ya 6 Fundisho ambalo hudai mabadiliko ya mkate na divai kuwa mwili na damu ya Kristo halisi [linalojulikana kama "transubstantiation" ni mtazamo wa Kanisa Katoliki] wakati kuhani anapoitakasa au anapofanya maombi fulani, ni nidharau kubwa; ambayo sio kwa Maandiko peke yake, lakini hata kwa akili ya kawaida tu; kwani hupindua asili ya Sakramenti, na fundisho hili limekuwa, sababu ya ushirikina mwingi, na ni ibada ya sanamu (Mdo. 3:21 na 1 Kor. 11:24, 25, 26; Lk. 24: 6, 39). Sehemu ya 7 Waamini wanaopokea kwa nje mkate na divai katika Sakramenti hii (1) pia wanapokea kwa ndani kwa imani; lakini sio kwa kimwili, lakini ni kiroho, kupokea na kujilisha juu ya Kristo aliyesulubiwa, na faida zote za kifo chake: hata hivyo 78

mwili na damu ya Kristo havipo kimwili, wala havipo“ndani, au chini ya” mkate na divai [fundisho hili linajulikana kama “Consubstantiation” na ni mtazamo uliochukuliwa na Martin Luther]. Walakini, mwili wake na damu yake ni kweli katika akili zetu za kiroho kwa imani, kana kwamba mkate na divai vipo katika akili zetu za kimwili. (2) [kwa Wana Refomati, Kristo anakuwepo kiroho]. (1) I Kor. 11:28 (2) I Kor. 10:16 Sehemu ya 8 Ingawa watu wasio na ufahamu na waovu hupokea kwa nje mkate na divai katika Sakramenti hii: bado hawapokei kile ambacho kimekusudiwa kiroho, bali kwa kutokufaa kwao wanakuwa na hatia kwa mwili na damu ya Bwana kwa hukumu yao wenyewe. Hii inamaanisha kwamba wale wasio na ufahamu [Mfano watoto] na waovu hawaruhusiwi kushiriki Meza ya Bwana au kushiriki katika siri hii takatifu. (1) Watu kama hawa hawawezi kufurahia ushirika na Kristo na hawafai kuja kwenye meza yake. Ni dhambi mbaya dhidi ya Kristo kwa watu kuja wakati hawana ufahamu (wajinga) na wasiomcha Mungu.(2) (1) I Kor. 11:27, 28, 29; II Kor. 6:14, 15, 16 (2) I Kor. 5: 6, 7, 13; II Thes. 3: 6, 14, 15; Mt. 7: 6

79

SURA YA 30. KUHUSU SERIKALI YA KANISA NA NIDHAMU Sehemu ya 1 Bwana Yesu, ambaye ndiye Mfalme na kichwa cha kanisa lake, ameweka maafisa kusimamia kanisa. Serikali ya kanisa inapaswa kutengwa (kuwa tofauti) na serikali ya kiraia (Isa. 9: 6, 7; I Tim. 5:17; 1 Thes. 5:12; Mdo 20:17, 28; Ebr. 13: 7, 17, 24; 1 Kor. 12:28; Mt. 28:18, 19, 20). Sehemu ya 2 Yesu anawapa maafisa wa kanisa "funguo za ufalme wa mbinguni." Na funguo hizi, maafisa wa kanisa wana mamlaka ya: Kusamehe dhambi na kuzuia msamaha. Kufunga ufalme dhidi ya wale ambao hawatubu - hii inafanywa kwa kutumia Neno au kuwaweka chini ya nidhamu ya kanisa. Wana mamlaka ya kufungua ufalme kwa wale wanaotubu, kwa huduma ya Injili au kutumia nidhamu ya kanisa pale inapohitajika (Mt. 16:19; Mt. 18:17, 18; Yn 20:21, 22, 23; 2Kor. 2: 6, 7, 8). Sehemu ya 3 Nidhamu ya kanisa ni muhimu kwa sababu kadhaa: kwanza, kuwarejesha Wakristo wenye dhambi. Pili, kuwaondoa wengine kutoka kwenye dhambi kama hizo. Tatu, Kuondoa chachu ya dhambi ambayo inaweza kuchachusha mkate mzima. Nne, Kulikuza jina la Kristo na kazi ya Injili. Tano, kuzuia hasira ya Mungu, ambapo Yeye ana kila haki ya kuleta ghadhabu yake kwa kanisa ikiwa watavunja agano lake na kuruhusu kuchafuliwa na wenye dhambi (1 Kor. 5; Tim. 5:20; 80

Mt. 7: 6; 1Tim. 1:20; 1 Kor. 11:27 na kuendelea, Yud mst wa 23). Sehemu ya 4 Ili kutekeleza nidhamu ya kanisa, maafisa wa kanisa wanapaswa kumwonya mtu huyo, kisha wamzuie kushiriki Meza ya Bwana, na mwishowe wamtenge; kwa kumtoa kuwa mshiriki wa kanisa. Hili linapaswa kufanywa kwa uangalifu sana; kwa kuzingatia asili ya dhambi na hatia ya mtu huyo (1Thes. 5:12; 2Thes. 3:6, 14, 15; 1Kor. 5:4, 5, 13; Mt. 18:17; Tit. 3:10).

SURA YA 31. KUHUSU SINODI NA MABARAZA YA KANISA. Sehemu ya 1 Viongozi wa kanisa wanapaswa kupanga mikutano kati ya makanisa ili kusaidia kutawala na kujenga kanisa. Mikutano hii mara nyingi huitwa "sinodi" au "mabaraza." Wazee wa kanisa na viongozi wengine wa kanisa wamepewa mamlaka ya kupanga mabaraza haya; mamlaka hii wamepewa na Kristo ili kujenga, na sio kuharibu. Viongozi wa makanisa mbalimbali wanapaswa kukusanyika pamoja kwa njia hii mara kwa mara kwa kadiri inavyohitajika kwa faida ya kanisa. (Mdo 15:1 41, Ufu 2:1-6, Mdo 20:17,28, Isa. 49:23, 1Tim 2:1-2, 2 Nyak. 19:811, 29-30, Mt 2:4-5, Mith 11:14, Mdo 15, 20:17) Sehemu ya 2 Mabaraza ya kanisa yanapaswa kutumiwa kusaidia: Kuamua ya masuala ya ubishani. Kutengeneza sheria na maelekezo ya 81

kumwabudu Mungu kwa njia iliyo nzuri. Kushughulikia malalamiko juu ya uongozi mbaya kanisani, kuweka sheria na maelekezo ya usimamizi bora wa ibada ya umma ya Mungu na serikali ya kanisa, na kusikia malalamiko katika kesi za udhaifu na kuzitatua kimamlaka. Ikiwa maamuzi haya yanaambatana na Neno la Mungu, yanapaswa kukubaliwa sio tu kwa sababu yanakubaliana na neno, lakini pia kwa sababu mamlaka ya mabaraza ya kanisa huwekwa na Mungu katika Neno lake. (Mdo 15:15,19,24,27-31, 16:4, Mt 18:17-20,29). Sehemu ya 3 Mabaraza yote ya kanisa tangu wakati wa mitume yanaweza kufanya makosa, na wengi wamefanya makosa. Kwa hiyo maamuzi yao hayafai kufanywa kama sheria kwa imani yetu, lakini yanapaswa kutumiwa kusaidia imani yetu. (Efe. 2:20; Mdo 17:11; 1Kor. 2:5; 2Kor. 1:24). Sehemu ya 4 Mabaraza ya kanisa yanapaswa kushughulikia tu maswala ya kanisa. Kamwe hawapaswi kujiingiza katika maswala ya serikali ya kirai au katika siasa kiraia, isipokuwa kwa maombi ya heshima kwa maswala maalum, au ikiwa tu serikali italihitaji kanisa kutoa ushauri (Lk 12:13, 14; Yn 18:36, Mt 22:21).

82

SURA YA 32. KUHUSU HALI YA MWANADAMU BAADA YA KIFO NA UFUFUO WA WAFU Sehemu 1 Miili ya wanadamu, baada ya kifo, inarudi kwenye mavumbi na kupata uharibifu; (1) lakini roho zao zikiwa katika hali ya kutokufa, hurudi kwa Mungu ambaye alizitoa,(2) roho za waadilifu, zikiwa zimekamilishwa kwa utakatifu, hupokelewa katika mbingu za juu, mahali wanapouona uso wa Mungu, kwa nuru na utukufu, wakingojea ukombozi kamili wa miili yao.(3)Na roho za waovu hutupwa kuzimu, ambako hukaa kwenye mateso na giza nene, na kuhifadhiwa kwa ajili ya hukumu ya siku kuu.(4)Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu, roho ambazo zimetenganishwa na miili yao zinaweza kwenda moja kwa moja kati ya mojawapo ya maeneo mawili mbinguni au kuzimu. (1) (2) (3) (4)

Mwa. 3:19; Mdo 13:36 Lk. 23:43; Mhu. 12:7 Ebr. 12:23; 2 Kor. 5: 1, 6, 8; Fil. 1: 23, Mdo 3: 21 4:10 Lk 16: 23, 24; Mdo 1:25; Yud mst. 6, 7; 2Pet. 3:19

Sehemu ya 2 Siku ya mwisho, watakaokutwa wako hai hawatakufa, lakini watabadilishwa:(1) Watu ambao wamekufa watafufuliwa na miili ileile (ingawa itakuwa na sifa tofauti), na miili yao itaunganishwa tena na roho zao, milele.(2) (1) 1Thes. 4:17; 1 Kor. 15:51, 52 (2) Ayu 19:26, 27; 1 Kor. 15:42, 43, 44

83

Sehemu ya 3 Miili ya waovu itafufuliwa na Kristo kwa ajili ya aibu yao. Lakini miili ya wenye haki itafufuliwa na Roho Mtakatifu kwa heshima, na itafanywa kuwa kama mwili wa Kristo uliotukuzwa (Mdo. 24:15; Yn. 5: 28, 29; 1 Kor. 15:43; Fil. 3:21).

SURA YA 33. KUHUSU HUKUMU YA MWISHO Sehemu ya 1 Mungu ameweka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki, kupitia Yesu Kristo (1)ambaye amempa nguvu na hukumu zote .(2) Katika siku hiyo, sio malaika waasi tu watakaohukumiwa, (3) bali na watu wote ambao wameishi duniani watasimama mbele ya mahakama ya Kristo, ili kutoa hesabu ya mawazo, maneno, na matendo yao; na kupokea malipo kulingana na kile ambacho wamefanya katika mwili, ikiwa ni mazuri au mabaya. (4) (1) (2) (3) (4)

Mdo. 17:31 Yn. 5:22, 27 1 Kor. 6: 3; Yud. mst. 6; 2 Pet. 2: 4 2 Kor. 5:10; Mh. 12: 14; Rum. 2:16; Rum. 14:10, 12; Mt. 12:36, 37

Sehemu ya 2 Sababu ya Mungu kuiweka siku hii ni kwa ajili ya udhihirisho wa utukufu wa huruma yake, katika wokovu wa milele wa Wateule; na wa haki yake, katika hukumu ya waovu na 84

wasiotii. Lakini, wenye haki wataingia kwenye uzima wa milele, na kupokea utimilifu huo wa furaha na utulivu mbele ya uwepo wa Bwana. Lakini waovu ambao hawamjui Mungu, na wasiotii Injili ya Yesu Kristo, watatupwa katika mateso ya milele, na wataadhibiwa kwa uharibifu wa milele kutoka kwenye uwepo wa Bwana, na utukufu wa nguvu zake. (Mt. 25:31 nk; Rum 2:5, 6; Rum 9:22, 23; Mt. 25:21; Mdo 3:19; 2Thes. 1:7, 8, 9, 10). Sehemu ya 3 Kristo anataka tuwe na hakika kuwa kutakuwa na siku ya hukumu; hii ni kwa ajili ya kuwakataza kutenda dhambi na kuwafariji wenye haki katika nyakati ngumu. (1) Walakini, Yeye hatuambii siku hiyo itakuwa lini, hataki sisi tujihakikishie wenyewe, lakini tuwe macho siku zote. Hatujui ni siku gani au saa gani Bwana atarudi, lakini tunapaswa kuwa tayari kila wakati kusema, “Njoo, Bwana Yesu, njoo upesi! Amina. (2) (1) 2Pet. 3:11, 14; 2Kor. 5:10, 11; 2Thes. 1: 5, 6, 7; Lk. 21:27, 28; Rum. 8:23, 24, 25 (2) Mt. 24:36, 42, 43, 44; Mk. 13:35, 36, 37; Lk. 12:35, 36; Ufu. 22:20.

85

II. KATEKISIMU KUBWA

86

SEHEMU I. KANUNI ZA MSINGI

Swali la 1: Nini hatima ya msingi na ya juu ya mwanadamu? Jibu: Hatima ya msingi na ya juu ya mwanadamu ni kumtukuza Mungu na kumfurahia yeye milele (Rum. 11:36, I Kor 10,31:2. Zab 73:24-28, Yn 17:21-24).

Swali la 2: Tunajuaje kuwa kuna Mungu? Jibu: Uelewa wetu wa ndani na wa asili pamoja na ushuhuda wa nje wa kazi za Mungu unaonyesha wazi kuwa kuna Mungu. Lakini neno na Roho humfunua Mungu kwa usahihi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu (Rum 1:19-20, Zab 19:1-4, Mdo 17:28, 1 Kor 1:21, 2:9-10, 2 Tim 3:15-17, Yer, 59:21).

Swali la 3. Je! Neno la Mungu ni nini? Jibu: Biblia Takatifu, inayojumuisha Agano la Kale na Agano Jipya, ndilo neno la Mungu. Ni mamlaka pekee ya imani na utii (II Tim 3:15-17, II Pet 1:19-21, Efe 2:20, Ufu 22:18-19, Isa, 8:20, Lk 16:29,31, Gal 1:8-9, II Tim 3:15-16).

Swali la 4. Je! Tunajuaje kuwa Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu? Jibu: Maandiko Matakatifu yanajidhihirisha yenyewe kuwa ni Neno la Mungu kwa ukuu (1) na ubora wake (2)na ushikamani wa sehemu zake zote (3) na ujumbe thabiti ambao ni kumpa Mwenyezi Mungu utukufu wote (4)na kwa nuru na nguvu yake ya kuwashawishi na kuwabadilisha watenda dhambi, kuwafariji na kuwajengea waumini wokovu.(5) Lakini ni Roho wa Mungu 87

pekee, akishuhudia pamoja na Maandiko ndani ya mioyo yetu, anao uwezo wa kutushawishi kabisa kuamini kwamba Maandiko [Biblia] ni Neno la kweli la Mungu (6) (1) (2) (3) (4) (5)

Hos. 8:12, I Kor 2:6-7,13, Zab 119:18,129 Zab. 12:6, 119:40 Mdo. 10:43, 26:22 Rum. 3:19,27 Mdo. 18:28, Ebr 4:12, Yak 1:18, Zab 19:7-9, Rum 15:4, Mdo 20:32. (6) Yn. 16:13-14, 1 Kor 2:6-9, 1 Yn 2:20,27, Yn 20:31

Swali la 5. Je! Biblia inafundisha nini hasa? Jibu: Kimsingi, Biblia inafundisha kile tunachopaswa kuamini kuhusu Mungu na jukumu ambalo Mungu anahitaji sisi tufanye (2 Tim 1:13). SEHEMU II. KILE AMBACHO MWANADAMU ANAPASWA KUAMINI KUHUSU MUNGU

Swali la 6. Je! Biblia inadhihirisha nini kuhusu Mungu? Jibu. Biblia inatudhihirishia jinsi Mungu alivyo;(1)nafsi katika Uungu,(2)amri Zake (3)na jinsi amri Zake zinavyotekelezwa.(4) (1) (2) (3) (4)

Mt. 2:19, I Kor 13:14, I Yn 5:17 Efe. 1:11, Mdo 15:14-15,18 Mdo. 4: 27-27, Isa 42:9 Yn. 4:24, Kut 34:6-7, Ebr 11:6

Sehemu ya IIA. Asili ya Mungu

Swali 7. Mungu ni nani? 88

Jibu. Mungu ni roho,(1) ambaye hana ukomo katika kuwepo kwake,(2) mwenye baraka,(3)mkamilifu na,(5) anayejitosheleza,(6) wa milele,(7) asiyebadilika,(8) ni zaidi ya uelewa wetu,(9) yupo kila mahali,(10) Mwenyezi,(11) anajua kila kitu,(12) mwenye busara kabisa,(13) Mtakatifu kabisa,(14) mwenye haki kabisa,(15) mwenye rehema na neema, mvumilivu, na mwingi wa wema na ukweli.(16) (1) Yn. 4:24 (2) 1 Fal 8:27, Isa 40:20, Kut. 3:14, Ayu. 11:7-9 (3) Mdo 7:2 (4) I Tim 6:15 (5) Mt. 5:48 (6) Mdo 17:24-25, Mwa. 17:1 (7) Zab 90:2 (8) Mal 3:6, Yak 1:17 (9) I Fal. 8:27, Rum 11:33 (10) Yer 23:24, Zab 139 (11) Ufu. 4:8 (12) Ebr 4:13, Zab. 147:5 (13) Rum 16:27 (14) Isa. 6:3, Ufu. 15:4 (15) Kumb. 32:4 (16) Kut. 34:6

Swali la 8. Je! Kuna zaidi ya Mungu mmoja? Jibu. Hapana. Kuna Mungu mmoja tu, aliye hai na wa kweli (Kumb 6:4, 1 Kor 8:4,6, Yer 10:10).

Swali la 9. Kuna nafsi ngapi katika Uungu? Jibu. Kuna nafsi tatu katika Uungu: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. (1) Hizi Nafsi tatu ni Mungu mmoja wa kweli, wa milele, sawa katika ubora, sawa katika nguvu na katika utukufu, ingawa nafsi tatu huweza kutofautishwa. (2) 89

(1) I Yn 5:7, Mt 3:16-17 (2) Math. 28:19, II Kor 13:14, Yn 10:30

Swali la 10. Je! Kuna uhusiano upi wa kibinafsi katika nafsi tatu za Uungu? Jibu. Tangu milele yote, Mungu Baba alimtoa Mwana; (1) kwa hiyo Mwana ametoka kwa Mungu Baba (2) na Roho Mtakatifu hutoka kwa Mungu Baba na Mwana tangu milele.(3) (1) Ebr 1.5-6 (2) Yn 1:14,18 (3) Yn 15:26, Gal 4:6

Swali la 11: Kuna ushahidi gani kwamba Mwana, na Roho Mtakatifu ni Mungu sawa na Baba? Jibu: Maandiko yanaonyesha kuwa Mwana na Roho Mtakatifu ni Mungu sawa na Baba. Maandiko pia huwapa majina yanayoonesha(1) sifa,(2) kazi,(3) na kuabudiwa,(4) sawa na Mungu Baba. (1) (2) (3) (4)

Isa. 6: 3, 5, 8; Yn. 12:41; Mdo 5: 3-4; 28:25; I Yn. 5:20 Yn 1: 1; 2: 24-25; Isa. 9: 6; I Kor. 2: 10-11 Kol 1:16; Mwa 1: 2 Mt. 28:19; II Kor. 13:14

Sehemu ya IIB. Amri za Mungu Swali la 12: Je! Amri2 za Mungu ni zipi? 2

“amri” hapa kwa kiingereza ni “decree” lakini katika lugha ya Kiswahili imefasiriwa kama “amri” tu jambo ambalo kwa namna fulani linaleta mkanganyiko na zile amri kumi za Mungu. Hata hivyo, hapa haimaanishi amri kumi bali ni namna Mungu anavyofanya mambo yake.

90

Jibu: Amri za Mungu ni matendo yake yaliyo ya hekima na matakatifu ya shauri la mapenzi yake(1) ambapo tangu milele yote, kwa utukufu wake, tangu zamani ameshapanga bila kubadilisha kila kitu kinachotokea kwa wakati,(2) hasa juu ya malaika na wanadamu. (1) Efe. 1:11; Rum 9: 14-15, 18; 11:33 (2) Efe. 1: 4, 11; Rum 9: 22-23; Zab. 33:11

Swali 13: Je! Mungu ameamuru nini juu ya malaika na wanadamu? Jibu: Mungu, kwa amri ya milele na isiyoweza kubadilishwa, kutokana na upendo wake, kwa sifa ya neema yake tukufu, ili kudhihirishwa kwa wakati unaofaa, amewachagua malaika wengine kwa utukufu.(1) Katika Kristo, Mungu amewachagua watu wengine kwa ajili uzima wa milele,(2) na pia, kulingana na uweza wake, na shauri lisilochunguzika la mapenzi yake (ambapo yeye huongeza au hupunguza fadhila kama apendavyo), amewachagua wengine kuanguka kwenye aibu na hasira yake kwa ajili ya dhambi zao; na jambo hili linafanyika kwa sifa ya utukufu wa haki yake.(3) (1) I Tim. 5:21 (2) Efe. 1: 4-6; II Thes. 2: 13-14 (3) Rum. 9: 17-18, 21-22; Mt. 11: 25-26; II Tim. 2:20; Yud 1: 4; I Pet. 2: 8

Swali la 14: Je! Mungu hutimizaje amri Zake? Jibu: Mungu hutimiza amri Zake katika kazi za uumbaji wake, kulingana na mapenzi yake yasiyotanguka, na shauri lake lisilobadilika la mapenzi yake mwenyewe (Efe. 1:11) 91

Swali la 15: Kazi ya uumbaji ni nini? Jibu: Kazi ya uumbaji ni ile ambayo Mungu aliifanya hapo mwanzo, kwa Neno la uweza wake, aliumba ulimwengu si kutokana na kitu chochote kilichokuwepo (exnihilo); alifanya ulimwengu kwa ajili yake mwenyewe; alifanya kwa muda wa siku sita, na yote yalikuwa mema (Mwa.1; Ebr. 11:3; Mith. 16:4)

Swali la 16: Je! Mungu aliwaumbaje malaika? jibu: Mungu aliwaumba malaika wote,(1) aliumba roho zote,(2) malaika wasiokufa,(3) watakatifu,(4) walio bora katika maarifa,(5) hodari kwa nguvu.(6) Aliwaumba kwa ajili ya kutekeleza amri Zake, na kusifu jina lake(7) lakini malaika hawa wangeweza kubadilika.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Kol 1:16 Zab. 104: 4 Mt. 22:30 Mt. 25:31 II Sam. 14:17; Mt. 24:36 II Thes. 1:7 Zab. 103: 20-21 II Pet. 2:4

Swali la 17: Je! Mungu alimwumbaje mwanadamu? Jibu: Baada ya Mungu kuumba viumbe vingine vyote, aliwaumba mwanamume na mwanamke;(1) akaumba mwili wa mwanamume kwa mavumbi ya ardhi,(2) na mwili wa mwanamke kutoka kwenye ubavu wa mwanamume; (3) aliwapa roho hai, zenye busara, na zisizokufa;(4) aliwaumba kwa mfano wake mwenyewe, (5) katika maarifa, (6) haki, na utakatifu; (7) huku sheria Yake ikiwa imeandikwa mioyoni mwao, (8) na akawapa uwezo wa 92

kuitimiza, (9) na kutawala viumbe vyote; kulikuwepo na uwezekano wa kuanguka.(11) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11)

(10)

hata hivyo bado

Mwa 1:27 Mwa 2: 7 Mwa 2:22 Mwa 2: 7; Ayu. 35:11; Mw. 12: 7; Mt. 10:28; Lk 23:43 Mwa 1:27 I Kor 3: 10 Efe. 4:24 Rum. 2: 14-15 Mwa. 7:29 Mwa 1:28 Mwa 3: 6; Mwa. 7:29

Swali la 18: Je! Ni kazi gani za Maongozi ya Mungu?3 jibu: Kazi za Maongozi ya Mungu ni matendo yake matakatifu,(1) ya busara,(2) na nguvu ya kuhifadhi (3) na kutawala(4) viumbe vyake vyote; akiamuru matendo yao yote, (5) kwa utukufu wake mwenyewe. (6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Zab. 145: 17 Zab. 104: 24; Isa. 28:29 Ebr. 1: 8 Zab. 103: 19 Mt. 10: 29-31; Mwa 45: 7 Rum. 11:36; Isa. 43:14

Swali la 19. Nini Maongozi ya Mungu kwa malaika?

3

Maongozi ya Mungu-Providence of God.

93

jibu: Kwa kweli Mungu aliwaruhusu malaika wengine waanguke katika dhambi na hukumu kwa uchaguzi wao wenyewe na bila uwezekano wowote wa kurudi kwenye nafasi zao za awali;(1) huku akiamuru anguko lao kwa utukufu wake; na furaha yake; (3) akiwatumia apendavyo,(4) kulingana na mapenzi yake, kama mawakala wa utawala wa nguvu Zake, rehema, na haki.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Yud.1: 6; II Pet. 2: 4; Ebr. 2:16; Yn 8:44 Ayu. 1:12; Mt. 8:31 I Tim. 5:21; Mk 8:38; Ebr. 12:22 Zab. 104: 4 II Fal 19:35; Ebr. 1:14

Swali la 20: Maongozi ya Mungu yalikuwa yapi wakati alipomwumba Mwanadamu? jibu: Maongozi ya Mungu kwa mwanadamu alipoumbwa yalikuwa hivi: Mungu alimweka katika bustani ya Edeni, akamwagiza kuitunza, na kumpa uhuru wa kula matunda ya bustanini;(1)huku akiweka viumbe chini ya utawala wake, (2) na kuanzisha ndoa kwa msaada wake; (3) akaanzisha uhusiano pamoja naye (4) akaanzisha Sabato (5) akaingia katika agano la uhai pamoja naye kwa vigezo vya kibinafsi, haki na utii (6) ambapo mti wa uzima ulikuwa ndiyo amana. (7) na kumkataza kula mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwamba siku akila ataingia kwenye uchungu wa kifo. (8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Mwa 2:8, 15-16 Mwa 1:28 Mwa 2:18 Mwa 1:26-29; 3: 8 Mwa 2:3 Gal. 3:12; Rum 10:5 Mwa 2:9

94

(8) Mwa 2:17

Swali la 21: Je! Mwanadamu aliendelea katika hali hiyo ambayo Mungu alimuumba nayo mwanzoni? Jibu: Wazazi wetu wa kwanza wakiwa wameachwa katika uhuru kwa hiari yao wenyewe, kupitia jaribu la Shetani, walikiuka amri ya Mungu kwa kula tunda lililokatazwa; na kwa hivyo wakaanguka kutoka katika hali yao ya mwanzo (Mwa 3: 6-8, 13; 7:29; II Kor. 11: 3)

Swali la 22: Je! Wanadamu wote walianguka katika dhambi hiyo ya kwanza? Jibu: Ndiyo. Wanadamu wote walianguka katika dhambi hiyo ya kwanza kwa sababu agano lililofanywa na Adamu kama mtu wa kwanza, halikuwa kwa ajili yake tu, bali kwa kizazi chake pia, hivyo, wanadamu wote kwa kuwa wanatoka kwa wazazi wa kwanza, (1) wote walitenda dhambi ndani yake, na wakaanguka pamoja naye katika hilo kosa la kwanza.(2) (1) Mdo 17:26 (2) Mwa 2:16-17; Rum 5:12-20; I Kor. 15:21-22

Swali la 23: je! Anguko la Adamu liliwaleta wanadamu wote katika hali gani? Jibu: Anguko la Adamu liliwaleta wanadamu katika hali ya dhambi na shida (Rum. 3:23; 5:12)

Swali la 24: Dhambi ni nini?

95

Jibu: Dhambi ni uasi wa sheria yoyote ya Mungu, iliyotolewa kama maelekezo kwa kiumbe mwenye busara, yaani mwanadamu (I Yn 3: 4; Gal. 3: 10,12)

Swali la 25: Je! Hali ya dhambi ya mwanadamu alipoanguka inajumuisha mambo gani? Jibu: Hali ya dhambi ya mwanadamu alipoanguka inajumuisha; hatia ya dhambi ya kwanza ya Adamu; (1) alipoteza lile takwa la utakatifu ambao aliumbwa nao, kuingia katika hali ya uharibifu; tangu hapo mwanadamu alishindwa kufanya jema lolote na matendo yake yote yameelekea kwenye uovu na anaendelea kufanya uovu huo, (2) dhambi hii kwa kawaida huitwa “dhambi ya asili” ambapo kuanzia hapo mwanadamu anaendelea kutenda uovu.(3) (1) Rum. 5:12, 19 (2) Rum. 3: 10-19; 5: 6; 8: 7-8; Efe. 2: 1-3; Mwa 6: 5 (3) Yak. 1: 14-15; Mt. 15:19

Swali la 26. Dhambi ya asili hurithishwa kivipi kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza hadi kwa kizazi kingine? Jibu: Dhambi ya asili huridhishwa kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza hadi kwa kizazi kingine katika hali ya kawaida ya kuzaliwa. Kwamba wanadamu wote huchukuliwa mimba katika hali ya uovu na kuzaliwa katika dhambi (Zab. 51:5; Ayu. 14:4; 15:14; Yn 3:6)

Swali la 27: Anguko lilileta madhara gani kwa mwanadamu? Jibu: Anguko lilisababisha kupotea kwa ushirika kati ya Mungu na mwanadamu, (1) lilileta hali ya laana; kwa hivyo, sisi kwa asili 96

tu watoto wa ghadhabu,(2) watumwa wa Shetani, (3) na wenye kustahili adhabu ya haki katika ulimwengu huu na ule ujao(4) (1) Mwa 3: 8, 10, 24 (2) Efe. 2: 2-3 (3) I Tim. 2:26 (4) Mwa 2:17; Omb. 3:39; Rum 6: 23; Mt. 25:41, 46, Yud.1: 7

Swali la 28: Je! Nini adhabu ya dhambi katika ulimwengu huu? Jibu: Adhabu ya dhambi katika ulimwengu huu inaweza kuwa katika maeneo mawili (ndani na nje); kwa ndani ni pamoja na upofu wa akili,(1) upotofu,(2) ugumu wa moyo,(3) dhamiri chafu,(4) na kwa nje ni pamoja na laana ya Mungu kwa viumbe vyote kwa ajili yetu,(5) na maovu mengine yote ambayo yanatupata katika miili yetu;(6) pamoja na kifo chenyewe.(7) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Efe. 4:18 II Thes. 2:11 Rum. 2: 5 Rum. 1:26 Mwa. 3:17 Kumb. 28: 15-18 Rum. 6:21, 23

Swali la 29: Je! Ni nini adhabu ya dhambi katika ulimwengu ujao? Jibu: Adhabu ya dhambi katika ulimwengu ujao, ni kutengwa milele kutoka kwenye uwepo wa Mungu, na mateso makali katika roho na mwili, bila ukomo, kwenye moto wa Jehanam milele (II Thes. 1:9; Mk 9: 43-44, 46, 48; Lk 16:24) 97

Swali la 30: Je! Mungu amewaacha wanadamu wote waangamie katika hali ya dhambi na shida? Jibu: Hapana. Mungu hawaachi wanadamu wote waangamie katika hali ya dhambi na shida(1)pale walipoanguka kwa kuvunja agano la kwanza, linalojulikana kama Agano la Matendo;(2) bali kwa upendo wake na rehema Zake tu huwaokoa wateule wake, na kuwaleta katika milki ya wokovu na agano la pili, ambalo kwa kawaida huitwa Agano la Neema.(3) (1) I Thes. 5: 9 (2) Gal. 3: 10,12 (3) Tito 3: 4-7; Gal. 3:21; Rum 3: 20-22 Sehemu ya IIB.1. Agano la Neema

Swali la 31: Je, Agano la Neema lilifanywa na nani? Jibu: Agano la neema lilifanywa na Kristo kama Adamu wa pili, ambapo wateule wote wapo ndani yake kama uzao wake (Gal. 3:16; Rum 5:15-21; Isa. 53:10-11)

Swali la 32: Je, neema ya Mungu imeonyeshwaje katika agano la pili? Jibu: Neema ya Mungu imeonyeshwa katika agano la pili, kwa Mungu mwenyewe kuwapa wenye dhambi Mpatanishi, (1) Uzima, na wokovu katika Kristo;(2) na kuhitaji imani kama sharti.(3). Ndani yake, ameahidi kuwapa Roho wake Mtakatifu (4) wateule wake wote, na imani hiyo kufanya kazi ndani yao (5) na kuwawezesha kutii (6)kama uthibitisho wa kweli wa imani yao(7) na shukrani kwa Mungu,(8) na kama njia ambayo ameiteua kwa ajili ya wokovu.(9) 98

(1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9)

Mwa 3:15; Isa. 42: 6; Yn 6:27 I Yn 5: 11-12 Yn 1:12; 3:16 Mith. 1:23 II Kor. 4:13 Ezek. 36:27 Yak 2:18, 22 2 Kor. 5: 14-15 Efe. 2:18

Swali la 33: Je! Agano la neema lilitekelezwa kwa njia moja? Jibu: Hapana! Agano la neema halikutekelezwa kwa njia moja kila wakati, bali utekelezaji wake chini ya Agano la Kale ulikuwa tofauti na ule wa Agano Jipya (II Kor. 3:6-9)

Swali la 34: Je! Agano la neema lilitekelezwaje chini ya Agano la Kale? Jibu: Agano la neema lilitekelezwa chini ya Agano la Kale kwa ahadi,(1)kwa unabii,(2)kwa dhabihu(3)kwa tohara,(4)kwa pasaka,(5)na kwa aina nyingine za maagizo, ambayo yote yalikuwa kivuli cha Kristo. Na kwa wakati huo vilikuwa vinatosha kuwajenga wateule katika imani kwa Masihi aliyeahidiwa,(6)ambapo kwake walikuwa na ondoleo kamili la dhambi, na wokovu wa milele.(7) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Rum. 15:8 Mdo 3:20, 24 Ebr. 10:1 Rum. 4:11 I Kor. 5:7 Ebr. 8-10; 11:13 Gal. 3: 7-9, 14 99

Swali la 35: Je! Agano la neema linatekelezwaje chini ya Agano Jipya? Jibu: Chini ya Agano Jipya, Kristo hufunuliwa kama chombo cha agano lile lile la neema, ambalo sasa linasimamiwa katika kuhubiriwa kwa Neno,(1)na usimamizi wa Sakramenti za Ubatizo(2) na Meza ya Bwana(3)ambamo neema na wokovu zinafanywa kwa ukamilifu na ufanisi, kwa mataifa yote.(4) (1) (2) (3) (4)

Mk 16:15 Mt. 28:19-20 I Kor. 11:23-25 II Kor. 3: 6-9; Ebr. 8: 6, 10-11; Mt. 28:19

Swali la 36: Ni nani Mpatanishi wa agano la neema? Jibu: Mpatanishi wa pekee wa agano la neema ni Bwana Yesu Kristo,(1)ambaye, akiwa Mwana wa milele wa Mungu, aliye sawa na Baba,(2)kwa utimilifu wa wakati alifanyika mwanadamu,(3) huku akiendelea kuwa Mungu na mwanadamu; kwa asili mbili tofauti, katika mtu mmoja, milele.(4) (1) I Tim. 2:5 (2) Yn 1: 1,14; 10:30; Fil. 2: 6 (3) Gal. 4:4 (4) Lk 1:35; Rum 9:5; Kol 2:9; Ebr. 7: 24-25

Sehemu ya IIB.2. Asili ya Kristo, Mpatanishi wa Agano la Neema

Swali la 37: Ni kivipi Kristo Mwana wa Mungu alifanyika mwanadamu? 100

Jibu: Kristo Mwana wa Mungu alifanyika mwanadamu kwa kuchukua mwili, na roho;(1) akachukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu tumboni mwa bikira Mariamu,(2) lakini alizaliwa pasipo kuwa na dhambi.(3) (1) Yn 1:14; Mt. 26:38 (2) Lk 1:27, 31, 35, 42; Gal. 4: 4 (3) Ebr. 4:15; 7:26

Swali la 38: Je! Kwa nini ilikuwa lazima Mpatanishi awe Mungu? Jibu: Ilikuwa ni lazima Mpatanishi awe Mungu, ili apate kuzuia asili ya mwanadamu isiangamie chini ya ghadhabu ya Mungu, na nguvu ya kifo;(1) kwa dhamana na utoshelevu wa mateso yake, utii, na maombezi;(2) aweze kukidhi haki ya Mungu,(3) na kupata neema yake;(4) akawanunua wateule,(5) akawapa Roho wake,(6) akawashindia na maadui zao wote,(7) na akawaleta kwenye wokovu wa milele.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mdo. 2: 24-25; Rum 1:4; 4:25; Ebr. 9:14 Mdo 20:28; Ebr. 7: 25-28; 9:14 Rum. 3: 24-26 Efe. 1: 6; Mt. 3:17 Tit. 2: 13-14 Gal. 4: 6 Lk 1: 68-69, 71, 74 Ebr. 5: 8-9; 9: 11-15

Swali la 39: Je! Ni kwa nini ilikuwa muhimu kuwa Mpatanishi awe mwanadamu? Jibu: Mpatanishi ilibidi awe mwanadamu ili aweze kuboresha asili ya kibinadamu,(1)atii sheria,(2) ateseke na atuombee kwa hali 101

ya asili yetu,(3) na ajue kwanza udhaifu wa mwanadamu jinsi ulivyo;(4) na ili tuweze kufanywa wana,(5) na tuwe na faraja kwa ujasiri kukikaribia kiti cha neema.(6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Ebr. 2:16 Gal. 4:4 Ebr. 2:14; 7: 24-25 Ebr. 4:15 Gal. 4: 5 Ebr. 4:16

Swali la 40: Je! Ni kwa nini ilikuwa lazima Mpatanishi awe Mungu na mwanadamu katika “mtu mmoja”? Jibu: Ilikuwa ni lazima Mpatanishi awe Mungu mwenyewe na mwanadamu, kwa “mtu mmoja” ili kwamba kazi za kila asili (Mungu na Mwanadamu) ziweze kukubaliwa na Mungu kwa ajili yetu, na kutumainiwa na sisi,(1) kama kazi za mtu mmoja.(2) (1) Mt. 1:21, 23; 3:17; Ebr. 9:14 (2) I Pet 2: 6

Swali la 41: Kwa nini Mpatanishi wetu aliitwa Yesu? Jibu: Mpatanishi wetu aliitwa Yesu, kwa sababu alikuwa na kazi ya kutuokoa kutoka kwenye dhambi zetu (Mt. 1:21)

Swali la 42: Je! Kwa nini Mpatanishi wetu aliitwa Kristo? Jibu: Mpatanishi wetu aliitwa Kristo, kwa sababu alikuwa ametiwa mafuta na Roho Mtakatifu zaidi ya kipimo;(1) na kwa hivyo aliwekwa wakfu, na alipewa mamlaka kamili na uwezo, (2) kwa ajili ya kutekeleza ofisi ya nabii,(3) ofisi ya ukuhani,(4) na ofisi

102

ya kifalme kwa kanisa lake,(5) katika hali zote; kudhalilishwa na kuinuliwa (5) (1) (2) (3) (4) (5)

Yn 3:34; Zab. 45: 7 Yn 6:27; Mt. 28: 18-20 Mdo 3: 21-22; Lk 4:18, 21 Ebr. 4: 14-15; 5: 5-7 Zab. 2: 6; Mt. 21: 5; Isa. 9: 6-7; Fil. 2: 8-11

Swali la 43: Je! Kristo alitekelezaje ofisi ya nabii? Jibu: Kama nabii, Kristo alifunua mapenzi kamili ya Mungu (1) kwa kanisa lake (2) juu ya kila kitu kwa muundo wa kanisa na wokovu.(3) Yeye hufanya hivyo kwa vizazi vyote kwa njia tofauti tofauti (4) kupitia Roho wake na Neno.(5) (1) Yn 1:18 (2) I Petro 1: 10-12 (3) Ebr. 1: 1-2 (4) Yn. 15:15 (5) Mdo 20:32; Efe. 4: 11-13; Yn 20: 31

Swali la 44: Je! Kristo alitekelezaje kazi ya ukuhani? Jibu: Kristo alitekeleza kazi ya ukuhani pale alipojitoa mwenyewe kama dhabihu isiyo na doa kwa Mungu,(1) kuwa upatanisho kwa dhambi za watu wake;(2) na katika mwendelezo wa maombezi yasiyokoma kwa ajili yao.(3) (1) Ebr. 9:14, 28 (2) Ebr. 2:17 (3) Ebr. 7:25

Swali la 45: Je! Kristo anatekelezaje ofisi ya mfalme? 103

Jibu: Kristo anatekeleza ofisi ya mfalme, kwa kuwaita watu wa ulimwenguni kwake mwenyewe,(1)na huwapa maafsa(2) sheria,(3)na nidhamu, ambapo katika hizo kwa wazi anawatawala;(4) katika kuwapa wateule wake neema iokoayo,(5) akiwazawadia kwa utii wao, (6) na kuwarudi kwa dhambi zao,(7) huku akiwahifadhi na kuwasaidia katika majaribu na mateso yote, (8)akiwashindia na maadui zao wote,(9)na kwa nguvu akiviamuru vitu vyote kwa ajili ya utukufu wake,(10) na kwa faida yao;(11) na pia kwa kujilipiza kisasi kwa wale wengine wasiomjua Mungu, na wasiotii Injili.(12) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12)

Mdo 15: 14-16; Isa. 4: 4-5; Mwa 49:10; Zab. 110: 3 Efe. 4: 11-12; 1 Kor. 12:28 Isa. 33:22 Mt. 18: 17-18; 1 Kor. 5: 4-5 Mdo 5:31 Ufu. 2:10; 22:12 Ufu. 3:19 Isa. 63: 9 1 Kor. 15:25; Zab. 110: 1-2 Rum. 14: 10-11 Rum. 8:28 II Thes. 1: 8-9; Zab. 2: 8-9

Swali la 46: Je! Hali ya kudhalilishwa kwa Kristo ilikuwa nini? Jibu: Hali ya kudhalilishwa kwa Kristo ilikuwa ni ile hali ya kushushwa chini, ambapo kwa ajili yetu, alijitenga na utukufu wake, akachukua namna ya mtumwa; katika kuchukuliwa mimba hadi kuzaliwa, maisha yake hadi kifo chake na baada ya kifo kufufuka kutoka kwa wafu (Fil. 2: 6-8; Lk 1:31; II Kor. 8:9; Mdo 2:24)

104

Swali la 47: Je! Kristo alijinyenyekezaje katika kuchukuliwa mimba kwake na kuzaliwa? Jibu: Kristo, tangu milele akiwa Mwana wa Mungu, kifuani mwa Baba yake, ilimpendeza katika ukamilifu wa wakati kuwa Mwana wa mtu, akizaliwa na mwanamke kwa hali ya chini, na aibu (Yn 1:14, 18; Gal. 4: 4; Lk 2:7)

Swali la 48: Kristo alijinyenyekezaje katika maisha yake duniani? jibu: Kristo alijinyenyekeza katika maisha yake, kwa kujitiisha chini ya sheria, (1)ambayo aliitimiza kikamilifu;(2)na kwa kupingana na udhalimu wa ulimwengu,(3)majaribu ya Shetani, (4) na udhaifu katika mwili wake, ama yaliyo ya kawaida kwa asili ya mwanadamu au kwa kufuatana na hali yake ya chini.(5) (1) Gal. 4: 4 (2) Mt. 5:17; Rum 5:19 (3) Zab. 22: 6; Ebr. 12: 2-3 (4) Mt. 4: 1-12; Lk 4:13 (5) Ebr. 2: 17-18; 4:15; Isa. 52: 13-14

Swali la 49: Je! Kristo alijinyenyekezaje katika kifo chake? Jibu: Kristo, akiwa amesalitiwa na Yuda,(1)aliachwa na wanafunzi wake,(2)alidharauliwa na kukataliwa na ulimwengu,(3) alihukumiwa na Pilato, na kuteswa na watesaji;(4) alipokuwa akipingana na vitisho vya mauti, na nguvu za giza, akabeba uzito wa ghadhabu ya Mungu,(5)akatoa uhai wake kuwa toleo la dhambi,(6)akavumilia kifo cha uchungu, na cha aibu na cha laana ya msalaba.(7) (1) Mt. 27: 4 105

(2) (3) (4) (5) (6) (7)

Mt. 26:56 Isa. 53: 2-3 Mt. 27: 26-50; Yn 19:34 Lk 22:44; Mt. 27:46 Isa. 53:10 Fil. 2: 8; Ebr. 12: 2; Gal. 3:13

Swali 50: Je! Aibu ya Kristo baada ya kifo chake ilihusisha mambo gani? Jibu: Aibu ya Kristo baada ya kifo chake ilikuwa katika kuzikwa kwake,(1)na kushuka kwa wafu, chini ya nguvu ya kifo hadi siku ya tatu;(2) ambayo imeelezwa kwa maneno haya, “alishuka kuzimu.” (1) 1 Kor. 15: 3-4 (2) Zab. 16:10; Mdo 2: 24-27, 31; Rum 6: 9; Mt. 12:40

Swali la 51: Je! Hali ya kuinuliwa kwa Kristo ilikuwa nini? Jibu: Hali ya kuinuliwa kwa Kristo ilikuwa ni ule ufufuo wake,(1) kupaa kwake,(2) na kuketi mkono wa kuume wa Mungu Baba,(3) na baadaye kuja tena kuhukumu ulimwengu.(4) (1) (2) (3) (4)

1 Kor. 15: 4 Mk 16:19 Efe. 1:20 Mdo 1:11; 17:31

Swali la 52: Je! Kristo aliinuliwaje katika ufufuo Wake? Jibu: Kristo aliinuliwa katika ufufuo wake, kwa kuwa, hakuona uharibifu katika kifo (kwa kuwa ilikuwa haiwezekani kwake kushikiliwa na kifo) (1) na akiwa na mwili uleule ambao alipata 106

nao mateso,(2) (lakini ni mwili usiokufa, au kupatikanana na magonjwa mengine ya kawaida katika maisha haya), ukiungana na roho yake,(3) alifufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu kwa nguvu Zake mwenyewe;(4)ambapo alijidhihirisha kuwa Mwana wa Mungu, (5) ameridhisha haki ya Kimungu,(6)alishinda kifo, na yeye aliyekuwa na nguvu za kifo (yaani Shetani),(7) na kuwa Bwana wa walio hai na wafu: (8) Kichwa cha kanisa lake,(9)kwa kuhesabiwa haki kwao,(10) akiwasaidia dhidi ya maadui,(11)na kuwahakikishia ufufuo wao kutoka kwa wafu katika siku ya mwisho. (12) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12)

Mdo 2:24, 27 Lk 24:39 Rum. 6: 9; Ufu. 1:18 Yn 10:18 Rum. 1: 4 Rum. 8:34 Ebr. 2:14 Rum. 14: 9 Efe. 1:20, 22-23; Kol 1:18 Rum. 4:25 1 Kor. 15: 25-27 1 Kor. 15:20

Swali la 53: Je! Kristo aliinuliwaje katika kupaa kwake? Jibu: Kristo aliinuliwa katika kupaa kwake; kwamba, baada ya kufufuka kwake alionekana na kuzungumza na mitume wake juu ya mambo ya ufalme wa Mungu,(1)na kuwapa utume wa kuhubiri Injili kwa mataifa yote,(2)siku arobaini baada ya kufufuka kwake.(3)Kristo aliwashinda maadui,(4)kwa wazi alipaa kwenda mbinguni, kwa ajili ya kutoa karama kwa wanadamu,(5) na kututayarishia makao,(6)na atakuja mara ya pili mwishoni katika siku ya mwisho.(7) 107

(1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Mdo 1:2-3 Mt. 28: 19-20 Ebr. 6:20 Efe. 4: 8 Mdo 1: 9-11; Efe. 4:10; Zab. 68:18 Yn 14:3 Mdo 3:21

Swali la 54: Ni kivipi Kristo aliinuliwa katika kukaa kwake mkono wa kuume wa Mungu Baba? Jibu: Kristo aliinuliwa katika kukaa kwake mkono wa kuume wa Mungu Baba, kwa kuwa kama “Mungu-Mtu” ameinuliwa juu zaidi na Mungu Baba,(1)kwa utimilifu wote,(2)kwa utukufu,(3)na uweza juu ya vitu vyote mbinguni na duniani,(4) hulikusanya na kulitetea kanisa lake, na kuwashinda maadui wa kanisa; na kuwapatia watumishi wake na wateule wengine karama na neema,(5) na kuwaombea.(6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Fil. 2: 9 Mdo 2:28; Zab. 16:11 Yn. 17: 5 Efe. 1:22; 1 Petro 3:22 Efe. 4: 10-12; Zab. 110: 1 Rum. 8:34

Swali la 55: Je! Kristo hutuombeaje? Jibu: Kristo hutuombea kwa kuonekana kwake katika asili yetu kila wakati mbele ya Baba mbinguni,(1)katika sifa ya utii wake na dhabihu yake duniani,(2)kutangaza matakwa yake ya kutumika kwa waumini wote;(3)kujibu tuhuma zote dhidi yao, (4)na kuwapatia utulivu wa dhamiri, bila kujali mapungufu yao ya kila 108

siku,(5)kukifikia kwa ujasiri kiti cha neema,(6)na kukubalika kwa utu wao(7)na huduma.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Ebr. 9:12, 24 Ebr. 1: 3 Yn 3:16; 17: 9, 20, 24 Rum. 8: 33-34 Rum. 5: 1-2; 1 Yn 2: 1-2 Ebr. 4:16 Efe. 1: 6 I Pet 2: 5

Swali 56: Je! Kristo atainuliwaje katika kuja kwake kuhukumu ulimwengu? Jibu: Kwa kuwa Kristo alihukumiwa bila haki na watu waovu,(1) atakuja tena siku ya mwisho kwa nguvu kubwa,(2) na katika udhihirisho kamili wa utukufu wake mwenyewe, na wa Baba yake, na malaika wake wote watakatifu,(3) kwa kelele, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu,(4) atakuja kuhukumu ulimwengu kwa haki.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Mdo 3: 14-15 Mt. 24:30 Lk 9:26; Mt. 25:31 I Thes. 4:16 Mdo 17:31

Swali la 57: Je Kristo amepata faida gani kwa kazi yake upatanishi? Jibu: Kristo, kwa upatanishi wake, ametununulia ukombozi,(1) pamoja na faida zingine zote za agano la neema.(2) (1) Ebr. 9:12

109

(2) II Kor. 1:20

Sehemu ya IIB.3. Mchakato wa Ukombozi katika Agano la Neema

Swali 58: Je! Tunawezaje kuwa washiriki wa faida ambazo Kristo amepata? Jibu: Tumeumbwa kuwa washiriki wa faida ambazo Kristo amepata,(1) kwa matumizi yake kwetu, ambayo ni kazi hasa ya Mungu Roho Mtakatifu.(2) (1) Yn. 1: 11-12 (2) Tit. 3: 5-6

Swali la 59. Ni nani wanaofanywa kuwa washiriki wa ukombozi kupitia Kristo? Jibu: Wanaofanywa kuwa washiriki wa ukombozi kupitia Kristo ni wateule peke yake, kwa sababu ukombozi kwao ni hakika, hivyo ukombozi una ufanisi kwa wale wote ambao kwa ajili yao Kristo ameununua, (1) ambao wanawezeshwa na Roho Mtakatifu kwa wakati kumwamini Kristo kupitia Injili. (2) (1) Efe. 1: 13-14; Yn. 6:37, 39; 10: 15-16 (2) Efe. 2: 8; II Kor. 4:13

Swali la 60: Watu ambao hawajawahi kusikia Injili, na hawamjui Yesu Kristo au hawajawahi kumwamini, Je, wanaweza kuokolewa kwa mujibu wa nuru ya asili? Jibu: Wale ambao hawajawahi kusikia Injili,(1) wala hawamjui Yesu Kristo,(2)wala hawajamwamini, hawawezi kamwe kuokolewa,(3)ama kwa bidii yoyote ile ya namna wanavyoishi 110

kwa mujibu wa nuru ya asili(4) au kwa kufuata sheria za dini wanayoifuata;(5) wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, lakini ni katika Kristo peke yake,(6) ambaye ni Mwokozi wa mwili wake, yaani kanisa.(7) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Rum. 10:14 2 Thes. 1: 8-9; Efe. 2:12; Yn 1: 10-12 Yn. 8:24; Marko 16:16 I Kor. 1: 20-24 Yn. 4: 22; Rum 9: 31-32; Fil 3: 4-9 Mdo 4:12 Efe. 5:23

Swali la 61. Je! Kila mtu anayesikia Injili na kuwa mshirika wa kanisani linaloonekana ameokoka? Jibu: Hapana. Sio kila mtu anayesikia Injili na kuwa mshirika katika kanisa linaloonekana ameokoka, bali ni wale tu ambao ni washirika wa kweli wa kanisa lisiloonekana. (Yn. 12: 38-40; Rum 9: 6; 11: 7; Mt. 7:21; 22:14)

Swali la 62: Je! Kanisa linaloonekana ni nini? Jibu: Kanisa linaloonekana ni jamii iliyoundwa na watu wote katika kila kizazi na sehemu za ulimwengu ambao wanakiri Ukristo kuwa dini ya kweli,(1) pamoja na watoto wao.(2) (1) 1 Kor. 1: 2; 12:13; Rum 15: 9-12; Ufu 7: 9; Zab. 2: 8; 22: 27-31; 45:17; Mt. 28: 19-20; Isa. 59:21 (2) I Kor. 7:14; Mdo 2:39; Rum 11:16; Mwa 17: 7

Swali la 63: Je! Kanisa linaloonekana lina haki gani maalum?

111

Jibu: Kanisa linaloonekana lina upendeleo wa kuwa chini ya uangalizi maalum wa serikali ya Mungu;(1)upendeleo wa kulindwa na kuhifadhiwa katika vizazi vyote, licha ya upinzani wa maadui;(2)Na kufurahia ushirika wa watakatifu, njia za kawaida za wokovu,(3)na neema itolewayo na Kristo kwa washiriki wa kanisa katika huduma ya injili, ikishuhudia kwamba kila mtu amwaminiye ataokolewa;,(4) bila kuwakataa ambao wako tayari kuja kwake.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Isa. 4: 5-6; I Tim. 4:10 Zab. 115: 1-2, 9; Isa. 31: 4-5; Zek. 12: 2-4, 8-9 Mdo 2:39, 42 Zab. 147: 19-20; Rum 9: 4; Efe. 4: 11-12; Mk 16: 15-16 Yn 6:37.

Swali la 64: Je! Kanisa lisiloonekana ni nini? Jibu: Kanisa lisiloonekana ni idadi yote ya wateule ambao wamekuwa, au watakusanywa katika “mmoja” yaani chini ya Kristo kama kichwa chake (Efe. 1:20, 22-23; Yn 10:16, 11:52)

Swali la 65: Je! Ni faida gani maalum ambazo washiriki wa kanisa lisiloonekana wanafurahia pamoja na Kristo? Jibu: Washiriki wa kanisa lisiloonekana wanafurahia umoja na ushirika pamoja na Kristo katika neema na utukufu (Yn 17:21, 24; Efe. 2: 5-6).

Swali la 66: Je! Ni umoja gani ambao wateule wanao pamoja na Kristo? Jibu: Umoja ambao wateule wanao pamoja na Kristo ni kazi ya neema ya Mungu,(1)ambapo kwa njia ya kiroho na ya fumbo, 112

wameungana naye kama kichwa na mume;(2) hili linafanyika wakati wa wito wao “wenye ufanisi.”4 (3) (1) Efe. 1:22; 2: 6-8 (2) I Kor. 6:17; YN. 10: 28; Efe. 5: 23, 30 (3) I Petro 5:10; I Kor. 1: 9

Swali la 67: Wito wenye ufanisi ni nini? Jibu: Wito wenye ufanisi ni kazi ya uweza wa nguvu na neema ya Mungu,(1) ambapo (kutokana na upendo wake wa bure na maalum kwa wateule wake, na si kutokana msukumo wowote wa kufanya tendo hilo ndani yake(2)) kwa wakati wake uliokubaliwa, huwaalika na kuwavuta wateule kwa Yesu Kristo, kwa Neno lake na Roho wake; (3) na kuwaangazia akili zao kwa nguvu, (4) akiwafanya upya (5) ili kwamba wao (ingawa ndani yao wamekufa katika dhambi) wawezeshwe kuitikia wito wake kwa uhuru wao wenyewe, na kukubali na kukumbatia neema inayotolewa.(6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Yn 5:25; Efe. 1: 18-20; 2 Tim. 1: 8-9 Tit. 3: 4-5; Efe. 2: 4-5, 7-9; Rum 9:11 2 Kor. 5:20; 6: 1-2; Yn 6:44; II Thes. 2: 13-14 Mdo 26:18; 1 Kor. 2:10, 12 Eze. 11:19; 36: 26-27; Yn. 6:45 Efe. 2: 5; Fil. 2:13; Kumb. 30: 6

Swali la 68: Je! Ni wateule pekee ambao wanaitwa katika wito wenye ufanisi? Jibu: Ndiyo. Ni wateule pekee ambao wameitwa katika wito wenye ufanisi;(1) Ingawa wengine wanaweza, na mara nyingi huitwa kwa huduma ya Neno, (2) na wanaonyesha matokeo fulani 4

Wito wenye ufanisi- effectual calling

113

ya kiroho;(3)hata hivyo, kwa sababu ya kupuuza kwao kwa makusudi neema hiyo, wameachwa katika kutokuamini kwao, na kamwe hawatakuja kwa Yesu Kristo.(4) (1) (2) (3) (4)

Mdo 13:48 Mt. 22:14 Mt. 7:22; 13: 20-21; Ebr. 6: 4-6 Yn 6: 64-65; 12: 38-40; Mdo 18: 25-27; Zab. 81: 11-12

Swali la 69: Je, Washirika wa kanisa lisioloonekana wana uhusiano gani na Kristo? Jibu: Washirika wa kanisa lisiloonekana wanashiriki sifa ya upatanisho wa Kristo, katika kuhesabiwa haki,(1)kufanywa wana,(2)kutakaswa, na chochote kingine, katika maisha haya umoja wao na yeye hujidhihirisha.(3) (1) Rum. 8:30 (2) Efe. 1:5 (3) I Kor. 1:30

Swali la 70: Je! Kuhesabiwa haki ni nini? Jibu: Kuhesabiwa haki ni tendo la neema ya bure ya Mungu kwa wenye dhambi,(1)ambapo katika hiyo husamehe dhambi zao zote, huwapokea na kuwahesabia haki machoni pake;(2) siyo kwa kitu walichofanya kwa ajili ya kupokea haki hiyo(3) bali ni kwa utii na utoshelevu kamili wa Kristo(4)na wao hupokelewa kwa imani tu.(5) (1) Rum. 3:22, 24-25; 4: 5 (2) II Kor. 5:19, 21; Rum 3: 22-25, 27-28 (3) Tit. 3: 5, 7; Efe. 1: 7 (4) Rum. 4: 6-8; 5: 17-19 (5) Mdo 10:43; Gal. 2:16; Fil. 3: 9 114

Swali la 71: Je! Ni kivipi kuhesabiwa haki ni tendo la neema ya Mungu ya bure? Jibu: Ingawa Kristo, kwa utii wake na kifo, alifanya kitendo kilichoridhisha haki ya Mungu kwa niaba ya wale ambao wamehesabiwa haki;(1)hata hivyo, kwa sababu Mungu, anakubali kuridhika kwa malipo ambayo yalitolewa na Kristo yaliyopaswa kulipwa na waliohesabiwa haki, Yeye mwenyewe alijitolea malipo haya kupitia kwa Mwana wake pekee,(2) akaweka haki yake kwao;(3)na hahitaji kitu chochote kutoka kwao ili kuhesabiwa haki isipokuwa imani pekee,(4) ambayo pia ni zawadi kutoka kwake;(5) kwa hivyo kuhesabiwa haki kwao ni kwa neema ya bure.(6) (1) Rum. 5: 8-10, 19 (2) II Tim. 2: 5-6; Ebr. 7:22; 10:10; Mt. 20:28; Dan. 9:24, 26; Isa. 53: 4-6, 10-12; Rum 8:32; 1 Pet 1: 18-19 (3) II Kor. 5:21 (4) Rum. 3: 24-25 (5) Efe. 2: 8 (6) Efe. 1: 7

Swali la 72: Je! imani ya kuhesabiwa haki ni nini? Jibu: Imani ya kuhesabiwa haki ni neema iokoayo(1)ambayo inafanya kazi mioyoni mwa wenye dhambi kwa njia ya Roho Mtakatifu,(2)na Neno la Mungu.(3)Kwa hiyo wenye dhambi wanahakikishwa juu ya dhambi zao na hali mbaya na hugundua kuwa wao au mtu yeyote au kitu kingine chochote hakiwezi kuwaondoa katika hali hiyo ya upotevu (4) na kwa hiyo wanatoa uthibitisho kamili kwa ukweli wa ahadi ya Injili;(5)na wanapokea pumziko juu ya Kristo na haki yake kwa kusamehewa dhambi,(6)kama Injili inavyotuambia, na kwa kukubalika na 115

kuhesabiwa kuwa wenye haki mbele ya Mungu kwa ajili ya wokovu.(7) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Ebr 10:39. II Kor 4:13, Efe 1:17-19. Rum. 10:14:17, II Thes 2:13. Mdo 2:37, 16:30, Yn 16:8-9, Rum 6:6, 7:9, Efe 2.1, Mdo 4:12. Efe 1:13, Rum 10:8-10. Yn 1.12, Mdo 16:31, 10:43, Gal 2:15-16. Fil. 3.9, Mdo 15.11.

Swali la 73: Je! Imani inahusikaje katika kumhesabia haki mwenye dhambi mbele za Mungu? Jibu: Imani humstahilisha mwenye dhambi machoni pa Mungu,(1)sio kwa sababu ya neema zingine ambazo huongozana na imani kila wakati, au kwa sababu ya kazi nzuri ambazo ni matunda yake, au kana kwamba neema ya imani, au tendo lolote linalojitokeza kutoka kwake, kwamba Mungu aliamuru kwa ajili kuhesabiwa haki kwake,(2) bali imani inakuwa chombo ambacho hupokea na kutumia5 Kristo na haki yake. (1) Gal. 3:11; Rum 3:28 (2) Rum. 4: 5; 10:10 (3) Yn. 1:12; Fil. 3: 9; Gal. 2:16

Swali la 74: kufanywa wana ni nini? Jibu: Kufanywa wana ni tendo Mwana wake wa pekee Yesu waliohesabiwa haki hupokelewa wake,(3)jina Lake linawekwa 5

To apply- kutumia

116

la neema ya Mungu,(1)katika Kristo,(2)ambapo wale wote kuwa mojawapo ya watoto juu yao,(4)wanapewa Roho

Mtakatifu,(5)wako chini ya uangalizi wa Baba,(6)wanakubaliwa kwa uhuru na kupewa haki zote za wana wa Mungu, wanafanywa warithi wa ahadi zote, na warithi pamoja na Kristo katika utukufu. (7)

(1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

I Yoh. 3: 1 Efe. 1: 5; Gal. 4: 4-5 Yn 1:12 II Kor. 4:18; Ufu 3:12 Gal. 4: 6 Zab. 103: 13; Mith. 14:26; Mt. 6:32 Ebr. 6:12; Rum 8:17

Swali 75: Utakaso ni nini? Jibu: Utakaso ni kazi ya neema ya Mungu, ambapo Wateule wa Mungu, waliochaguliwa kuwa watakatifu kabla ya msingi wa ulimwengu, kwa wakati, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu(1) hutumia kifo na ufufuko wa Kristo kwa ajili yao, (2) huwafanya upya katika miili yao wote kwa mfano wa Mungu.(3)hupewa mbegu za toba iletayo uzima,(4)na neema ziokoazo zinaongezeka na kuwa na nguvu,(5) kwamba wanazidi kufa kwa dhambi, na kuwa hai katika maisha mapya. (6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Efe. 1: 4; 1 Kor. 6:11; II Thes. 2:13 Rum. 6: 4-6 Efe. 4: 23-24 Mdo 11:18; 1 Yoh. 3: 9 Yuda 1:20; Ebr. 6: 11-12; Efe. 3: 16-19; Kol 1: 10-11 Rum. 6: 4; 6:14; Gal. 5:24

Swali 76: Toba iletayo uzima ni nini?

117

Jibu: Toba iletayo uzima ni neema iokoayo,(1)ambayo inafanywa na Roho Mtakatifu na Neno la Mungu moyoni mwa mwenye dhambi(2)ambapo mwenye dhambi anahuzunika sana, (3) na anachukia dhambi zake,(4)na kwa hiyo, yeye hubadilika na kumgeukia Mungu,(5)akikusudia na kujaribu kila wakati kutembea naye katika njia zote za utii mpya.(6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

2 Tim. 2:25 Zek. 12:10, Mdo 11:18, 20-21 Yer. 31: 18-19 2 Kor. 7:11 Mdo 26:18; Eze. 14: 6; 1 Fal 8: 47-48 Zab. 119: 6, 59, 128; Lk 1: 6; II Fal 23:25

Swali la 77: Je! Kuhesabiwa haki na utakaso hutofautiana kivipi? Jibu: Ingawa si rahisi kutenganisha kuhesabiwa haki na utakaso(1)lakini kuna tofauti kwamba; katika kuhesabiwa haki, Mungu anaonyesha haki ya Kristo;(2)lakini katika utakaso; Roho wa Mungu husababisha neema, na huwezesha kuitumia;(3) katika kuhesabiwa haki, dhambi imesamehewa;(4) lakini katika utakaso, dhambi imeshindwa:(5)vilevile, kuhesabiwa haki huwaachilia huru waumini wote kutoka kwenye hasira ya Mungu, na kwamba kuhesabiwa haki kumekamilika katika maisha haya,(6)lakini katika utakaso si sawa nyakati zote,(7)wala katika maisha haya haiwezekani kukamilika,(8)lakini unaendelea kukua kuelekea kwenye ukamilifu.(9) (1) (2) (3) (4) (5)

1 Kor. 1:30; 6:11 Rum. 4:6, 8 Eze. 36:27 Rum. 3:24-25 Rum. 6:6, 14

118

(6) (7) (8) (9)

Rum. 8:33-34 I Yoh. 2:12-14; Ebr. 5: 12-14 I Yoh. 1: 8,10 2 Kor. 7:1; Fil 3: 12-14

Swali la 78: Je! Kwa nini utakaso hauwezi kukamilika mara moja tu katika maisha haya? Jibu: Kutokukamilika kwa utakaso kwa waumini katika maisha haya hutokana na mabaki ya dhambi iliyo ndani ya kila sehemu yao, na tamaa za “mwili dhidi ya roho;” ambamo mara nyingi hushawishiwa na majaribu, na huanguka katika dhambi nyingi,(1)kwa hiyo wanazuiliwa katika huduma zao zote za kiroho,(2)na kazi zao nzuri hazina ukamilifu na zimetiwa unajisi machoni pa Mungu.(3) (1) Rum. 7:18, 23; Mk 14: 66-72; Gal. 2: 11-12 (2) Ebr. 12: 1 (3) Isa. 64: 6; Kut. 28:38

Swali la 79: Waamini wa kweli, kwa sababu ya kutokuwa wakamilifu katika maisha haya; na kwa sababu ya majaribu na dhambi nyingi ambazo mara kadhaa huwaangusha; je wanaweza kuanguka katika hali ya neema? Jibu: Waumini wa kweli, kwa sababu ya upendo wa Mungu usiobadilika,(1)na agano lake kuwa watavumilia,(2)na kwamba hawawezi kutengana na Kristo,(3)na kwa maombezi yake ya kudumu kwa ajili yao,(4) na kwamba Roho na mbegu ya Mungu ikikaa ndani yao,(5)kamwe hawawezi kuanguka katika hali ya neema,(6)lakini huhifadhiwa na nguvu ya Mungu kupitia imani hadi wokovu.(7) (1) Yer. 31: 3 119

(2) II Tim. 2: 19-21; II Sam. 23: 5 (3) 1 Kor. 1: 8-9 (4) Ebr. 7:25; Lk 22:32 (5) I Yoh. 2:27; 3: 9 (6) Yer. 32:40; Yoh. 10:28 (7) 1 Pet. 1: 5

Swali la 80: Je! Waumini wa kweli wanaweza kuhakikishwa kuwa wako katika hali ya neema na kwamba watavumilia mpaka mwisho? Jibu: Kwa kuwa waumini wamemwamini Kristo kwa ukweli, na wanajitahidi kutembea katika dhamiri njema mbele zake,(1) kwa imani yenye msingi wa kweli wa ahadi za Mungu, na kwamba Roho huwawezesha kutambua neema ambapo ahadi za uzima zimewekwa,(2)na kushuhudia pamoja na roho zao kuwa wao ni watoto wa Mungu,(3)wamehakikishwa kwamba wako katika hali ya neema, na watavumilia mpaka mwisho.(4) (1) (2) (3) (4)

1 Yoh. 2: 3 I Kor. 2:12; 1 Yoh. 3:14, 18-19, 21, 24; 4: 13, 16; Ebr. 6: 11-12 Rum. 8:16 I Yoh. 5:13

Swali la 81: Je! Waumini wote wa kweli wakati wote wanahakikishwa juu ya hali yao ya sasa ya neema, na kwamba wataokolewa? Jibu: Waumini wa kweli wakati wote wanahakikishwa juu ya hali yao ya sasa ya neema na kwamba wataokolewa, ijapokuwa wanaweza kupitia majaribu na kukata tamaa, lakini kamwe hawawezi kukosa msaada wa Roho wa Mungu ambaye hatawaacha wazame katika upotevu (Efe. 1:13, Isa. 50:10; Zab. 120

88 Zab. 22: 1; 31:22; 51: 8, 12; 77: 1-12; Wimb. 5: 2-3, 6, I Yoh. 3: 9; Ayu. 13: 15; Zab. 73:15, 23; Isa. 54: 7-10)

Swali la 82: Ni ushirika gani katika utukufu ambao washiriki wa kanisa lisiloonekana wanao pamoja na Kristo? Jibu: Ushirika katika utukufu ambao washiriki wa kanisa lisiloonekana wanao pamoja na Kristo; kwanza uko katika maisha haya,(1)pili, hata mara tu baada ya kifo unaendelea kuwepo,(2)na mwishowe utakamilishwa katika ufufuo siku ya hukumu.(3) (1) II Kor. 3:18 (2) Lk 23:43 (3) I Thes. 4:17

Swali la 83: Ni ushirika gani katika utukufu pamoja Kristo ambao washiriki wa kanisa lisiloonekana wanafurahia katika maisha haya? Jibu: Washiriki wa kanisa lisiloonekana, katika maisha haya ni malimbuko ya utukufu pamoja na Kristo, kwa kuwa wao ni washirika wake, naye ni kichwa chao, na kwa hivyo ndani yake wanavutiwa na utukufu huo ambapo Kristo anawamiliki kikamilifu; (1) na, wanafurahia upendo wa Mungu,(2) wanakuwa na amani ya dhamiri, furaha katika Roho Mtakatifu, na tumaini la utukufu, (3) lakini kinyume chake, hali ya hasira ya Mungu na matarajio ya kuogofya ya hukumu, na mateso yataendelea kwa waovu wote baada ya kufa,.(4) (1) Efe. 2: 5 (2) Rum. 5: 5; II Kor. 1:22 (3) Rum. 5: 1-2; 14:17 (4) Mwa 4:13; Mt. 27: 4; Ebr. 10:27; Rum 2: 9; Mk 9:44 121

Swali la 84: Je! Watu wote watakufa? Jibu: Ndiyo, watu wote watakufa kwa sababu kifo kilitolewa kama mshahara wa dhambi kwa watu wote.(1) Watu wote watakufa mara moja;(2)kwa kuwa wote wamefanya dhambi.(3) (1) Rum. 6:23 (2) Ebr. 9:27 (3) Rum. 5:12

Swali la 85: Kama kifo ni mshahara wa dhambi, kwa nini wateule hawaokolewi kutoka kwenye kifo, kwa kuwa dhambi zao zote zimesamehewa katika Kristo? Jibu: Wateule wataokolewa kutoka kwenye kifo katika siku ya mwisho, na hata sasa katika kifo huokolewa kutoka kwenye maumivu na laana yake;(1)Walakini, ingawa wanakufa, hata kifo ni kwa upendo wa Mungu,(2)kwa ajili ya kuwaweka huru kabisa kutoka kwenye dhambi na taabu,(3) na kuwafanya wawe na uwezo wa ushirika zaidi na Kristo katika utukufu, ambao baadaye wataingia.(4) (1) 1 Kor. 15:26, 55-57; Ebr. 2:15 (2) Isa. 57: 1-2; II Fal 22:20 (3) Ufu 14:13; Efe. 5:27 (4) Lk. 23:43; Fil 1:23

Swali la 86: Ni ushirika gani katika utukufu pamoja na Kristo washiriki wa kanisa lisiloonekana hufurahia mara baada ya kifo? Jibu: Ushirika katika utukufu pamoja na Kristo ambao washiriki wa kanisa lisiloonekana hufurahia mara tu baada ya kifo ni 122

kwamba roho zao zinakamilishwa katika utakatifu,(1) na kupokelewa mbinguni,(2)ambapo wanaona uso wa Mungu katika nuru na utukufu,(3) wakingojea ukombozi kamili wa miili yao,(4)ambayo hata baada ya kifo huendelea kuungana na Kristo,(5) na kupumzika kwenye makaburi yao kama katika vitanda vyao,(6) hadi siku ya mwisho wataunganishwa tena na roho zao.(7) Ambapo roho za waovu hutupwa kuzimu, ambapo hukaa kwenye mateso na giza nene kabisa, na miili yao huhifadhiwa kwenye makaburi yao, ambayo ni magereza yao, hadi ufufuo na hukumu ya siku kuu.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Ebr. 12:23 II Kor. 5: 1, 6, 8; Flp 1:23; Mdo 3:21; Efe. 4:10 I Yoh. 3: 2; 1 Kor. 13:12 Rum. 8:23; Zab. 16: 9 I Thes. 4:14 Isa. 57: 2 Ayu. 19: 26-27 Lk. 16: 23-24; Mdo 1:25; Yud 1:6-7

Swali 87: Je! Tunapaswa kuamini nini juu ya ufufuo? Jibu: Tunapaswa kuamini kwamba katika siku ya mwisho kutakuwa na ufufuo wa jumla wa wafu wote walio waadilifu na wasio waadilifu:(1)wakati wale watakaopatikana wakiwa hai watabadilishwa kwa muda mfupi. Na wale wafu, kwa miili ileile iliyokuwa imelazwa makaburini, wakiwa wameunganishwa tena na roho zao milele, watafufuliwa kwa nguvu ya Kristo.(2) Wenye haki, kwa Roho wa Kristo, na kwa sababu ya ufufuo wake kama kichwa chao, watainuliwa kwa nguvu, wakipewa miili ya utukufu isiyoweza kuharibika;(3) na miili ya waovu itafufuliwa kwa ajili ya aibu.(4) (1) Mdo 24:15 123

(2) I Kor. 15: 51-53; 1 Thes. 4: 15-17; Yn 5: 28-29 (3) 1 Kor. 15: 21-23, 42-44; Fil. 3:21 (4) Yn. 5:27-29; Mt. 25:33

Swali la 88: Je! Nini kitafuata mara tu baada ya ufufuo? Jibu: Mara tu baada ya ufufuo kitakachofuata ni hukumu ya jumla na ya mwisho ya malaika na wanadamu;(1) hata hivyo, hakuna ajuaye siku wala saa ambayo Bwana atarudi; lakini tunapaswa kukesha na kuomba na kuwa tayari kwa ujio wa Bwana wakati wowote.(2) (1) II Petro 2: 4; Yud. 1: 6-7, 14-15; Mt. 25:46 (2) Mt. 24:36, 42, 44; Lk 21: 35-36

Swali 89: Ni nini kitafanyika kwa waovu siku ya hukumu? Jibu: Katika siku ya hukumu, waovu watawekwa mkono wa kushoto wa Kristo,(1)na, kwa ushahidi ulio wazi, na dhamiri zao,(2) kutakuwepo na hukumu ya kutisha dhidi yao(3)ambapo wataondolewa kwenye uwepo wa Mungu, na watatupwa kwenye Jehanam, ili kuadhibiwa kwa mateso yasiyotamkika. Humo watateseka pamoja na Shetani na malaika zake milele.(4) (1) Mt. 25:33 (2) Rum. 2: 15-16 (3) Mt. 25: 41-43 (4) Luka 16:26; II Thes. 1: 8-9

Swali la 90: Je! Ni nini kitafanyika kwa wenye haki siku ya hukumu?

124

Jibu: katika siku ya hukumu, wenye haki watachukuliwa na Kristo katika mawingu;(1) watawekwa mkono wake wa kuume, na hapo watakubaliwa waziwazi;(2) watajiunga na Kristo katika kuwahukumu malaika na wanadamu,(3) na watapokelewa mbinguni,(4)mahali ambapo watakombolewa kikamilifu na milele kutoka kwenye dhambi zote na mikasa,(5)watajazwa na furaha isiyokuwa na kifani,(6)watafanywa watakatifu kabisa na wenye furaha katika mwili na roho, pamoja na watakatifu wasiohesabika na malaika watakatifu,(7)lakini hasa watakuwa mbele za Mungu Baba, Bwana Yesu Kristo, na ya Roho Mtakatifu milele yote.(8) Na huu ndio ushirika kamili ambao washiriki wa kanisa lisiloonekana watafurahia pamoja na Kristo katika utukufu wakati wa ufufuo na siku ya hukumu. (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

I Thes. 4:17 Mt. 10: 32, 25: 33 I Kor. 6: 2-3 Mt. 25:34, 46 Efe. 5:27; Ufu. 14:13 Zab. 16:11 Ebr. 12: 22-23 I Yn 3: 2; I Kor. 13:12; I Thes. 4: 17-18

SEHEMU YA III. JUKUMU AMBALO MUNGU ANATAKA KWA MWANADAMU

Swali la 91: Je! Ni jukumu gani ambalo Mungu anahitaji kwa mwanadamu? Jibu: Jukumu ambalo Mungu anataka kwa mwanadamu, ni utii kwa mapenzi yake yaliyofunuliwa. (Rum. 12: 1-2; Mik. 6: 8; I Sam. 15:22)

125

Swali la 92: Ni kitu gani ambacho Mungu alimfunulia mwanadamu kama sheria ya utii wake? Jibu: Sheria ya utii ilifunuliwa kwa Adamu katika hali ya kutokuwa na hatia, na kwa wanadamu wote ndani yake. Mbali na amri maalum ya kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ilikuwa “sheria ya maadili.” (Mwa 1: 26-27; 2:17; Rum 2:14-15; 10:5)

Swali la 93: Je! Sheria ya maadili ni nini? Jibu: Sheria ya maadili ni tamko la mapenzi ya Mungu kwa wanadamu, likimuelekeza na kumfunga kila mtu kufuata daima na kutii sheria hiyo;(1)na kutekeleza majukumu yote ya utakatifu na haki ambayo ni ya Mungu na mwanadamu:(2) ikiahidi uzima kwa wale wanaotii, na kifo kwa wale wanaovunja.(3) (1) Kumb. 5:1-3, 31, 33; Luka 10: 26-27; Gal. 3: 10; I Thes. 5:23 (2) Lk. 1:75; Mdo 14:16 (3) Rum. 10: 5; Gal. 3: 10,12

Swali la 94: Je, kuna matumizi yoyote ya sheria ya maadili baada ya anguko? Jibu: Ingawa hakuna mtu, tangu anguko, aliyeweza kupata haki na uzima kwa sheria ya maadili;(1) bado kuna matumizi makubwa ya sheria hii, pia yanajulikana kwa watu wote; waumini na wasio waumini.(2) (1) Rum. 8:3; Gal. 2:16 (2) I Tim. 1:8

126

Swali la 95: Je! Sheria ya maadili ina matumizi gani kwa watu wote? Jibu: Sheria ya maadili inatumika kwa watu wote kwa kuwajulisha juu ya asili takatifu ya Mungu na mapenzi ya Yake,(1) na wajibu wao na kwamba inawafunga watembee ipasavyo;(2) ikiwashuhudia namna wasivyoweza kuitekeleza kwa sababu ya ufisadi wa dhambi ya asili, uchafu wa mioyo na maisha yao;(3) pia huwafanya wanyenyekee kwa ajili ya dhambi na shida zao,(4) na hivyo kuwasaidia kuona wazi hitaji lao la Kristo,(5) na ukamilifu wa utii wake.(6) (1) Law. 11:44-45; 20: 7-8; Rum 7:12 (2) Mik. 6: 8; Yak. 2: 10-11 (3) Zab. 19: 11-12; Rum. 3:20; 7:7 (4) Rum. 3: 9, 23 (5) Gal. 3: 21-22 (6) Rum. 10:4

Swali la 96: Je! Kuna matumizi gani ya sheria ya maadili kwa wasioamini? Jibu: Sheria ya maadili inatumika kwa wasioamini kwa kuamsha dhamiri zao kukimbia ghadhabu inayokuja,(1) na kuwaelekeza kwa Kristo; (2) ama, wakiendelea katika hali yao ya dhambi, sheria ya maadili huwafanya wasiwe na udhuru,(3) na kuwa chini ya laana yake.(4) (1) I Tim. 1: 9-10 (2) Gal. 3:24 (3) Rum. 1:20; 2: 15 (4) Gal. 3:10 127

Swali la 97: Je! Kuna matumizi gani ya sheria ya maadili kwa waumini? Jibu: Ijapokuwa wale ambao wamezaliwa mara ya pili na kumwamini Kristo, wameokolewa kutoka kwenye sheria ya maadili kama “Agano la Matendo,”(1) na hivyo, wamehesabiwa haki(2) na wala hawahukumiwi;(3) lakini, mbali na matumizi ya jumla yanayojulikana kwa watu wote, sheria ya maadili ina matumizi ya pekee kwa waumini kwa kuwaonyesha ni kiasi gani wamefungwa katika Kristo;(4) na kwa hivyo kuwafanya waumini kushukuru zaidi(5) (1) Rum. 6:14; 7: 4, 6; Gal. 4:4-5 (2) Rum. 3:20 (3) Gal. 5:23; Rum 8:1 (4) Rum. 7:24-25; 8: 3-4; Gal. 3:13-14 (5) Lk. 1:68-69, 74-75; Kol 1:12-14 Sehemu ya IIIA. Amri Kumi

Swali la 98: Je! Sheria ya maadili inaelezwa wapi kwa kifupi? Jibu: Sheria ya maadili inaelezwa kwa kifupi katika “Amri Kumi,” ambazo zilitolewa na Mungu juu ya mlima Sinai, na kuandikwa naye katika mbao mbili za mawe;(1) na zimeandikwa katika kitabu cha Kutoka sura ya Ishirini. Amri nne za kwanza zinaelezea jukumu letu kwa Mungu, na zingine sita zinaelezea jukumu letu kwa mwanadamu.(2) (1) Kumb. 10: 4; Kut. 34:1-4 (2) Mt. 22: 37-38, 40

128

Swali la 99: Je! Ni miongozo gani inayopaswa kuzingatiwa kwa ufahamu sahihi wa zile amri kumi? Jibu: Kwa ufahamu sahihi wa zile amri kumi, mwongozo ufuatao lazima uzingatiwe: 1. Kwamba sheria ni kamilifu, na inamfunga kila mtu kwa unyofu kamili, ikidai utii wa milele, ikihitaji ukamilifu wa kila tendo linalotendwa. (1) 2. Kwamba sheria ni ya kiroho, na hivyo hufikia ufahamu, mapenzi, upendo, na nguvu zingine zote za kiroho; kwa maneno na matendo(2) 3. Kwamba jambo moja au lilelile, kwa njia tofauti, linahitajika kufanywa au limepigwa marufuku katika amri kadhaa. (3) 4. Kwamba kama jukumu limeamriwa, dhambi iliyo kinyume imepigwa marufuku;(4) na, ambapo dhambi imekatazwa, jukumu la kinyume linaamriwa: (5) 5. Kwamba kile ambacho Mungu anakataza, hakipaswi kufanywa;(6)kile anachoamuru kutenda, ni jukumu letu kutenda; (7) 7. Kwamba kile kilichozuiwa au kuamriwa kwa ajili yetu tumefungwa katika hicho, kwa hiyo tunawajibika kufanya kwa vyovyote vile. (8) 8. Kwamba tunapaswa kuwasaidia wengine katika kutekeleza sheria, hasa katika yale makatazo. (9) (1) Zab. 19: 7; Yak. 2:10; Mt. 5: 21-22 (2) Rum. 7:14; Kumb. 6: 5; Mt. 5: 21-22, 27- 28, 33- 34, 37- 39, 4344; 22: 37-39 (3) Kol 3: 5; Amo. 8: 5; Mith. 1:19; 2Tim. 6: 10

129

(4) (5) (6) (7) (8)

Isa. 58:13; Kumb. 6:13; Mt. 4: 9-10; 15: 4-6 Mt. 5: 21-25; Efe. 4:28 Ayu. 13: 7; 36:21; Rum 3: 8; Ebr. 11:25 Kumb. 4: 8-9 Mt. 5: 21-22, 27-28; 15: 4-6; Ebr. 10: 24-25; 1 Thes. 5: 22-23; Gal. 5:26; Kol. 3:21 (9) Kut. 20:10; Law. 19:17; Mwa 18:19; Yosh. 24:15; Kumb. 6: 6-7

Swali 100: Je! Ni mambo gani ya pekee ambayo tunapaswa kuzingatia katika Amri Kumi? Jibu: Tunachopaswa kuzingatia katika Amri Kumi ni utangulizi wake, uhalisia wa maagizo yenyewe, na sababu kadhaa zilizowekwa kwenye baadhi ya maagizo hayo.

Swali la 101: Utangulizi wa amri kumi unaelezwa kwa maneno gani? Jibu: Utangulizi wa amri hizo kumi umewekwa katika maneno haya, “mimi ndimi Bwana, Mungu wako, ambaye nimekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.”(1) Ambapo Mungu anaonyesha enzi yake, kuwa yeye ni YEHOVA, Mungu wa milele, mwenye nguvu zote;(2)na kwamba yeye ni Mungu katika Agano, kama ilivyo katika Israeli ya zamani, ndivyo ilivyo kwa watu wake wote;(4)kama alivyowatoa katika utumwa huko Misri, nasi anatuokoa kutoka katika utumwa wa kiroho; (5) na kwamba tunalazimika kumchukulia Mungu wetu kuwa ni Mungu wa pekee, na tunapaswa kuzishika amri Zake zote. (6) (1) Kut. 20: 2 (2) Isa. 44: 6 (3) Mwa 17: 7; Rum 3:29 (4) Lk 1: 74-75 (5) IPet. 1: 15-18; Law. 18:30, 19:37 130

Sehemu ya IIIA.1. Wajibu wetu kwa Mungu

Swali la 102: Je! Ni nini jumla ya amri nne ambazo zina jukumu letu kwa Mungu? Jibu: Jumla ya amri nne zilizo na jukumu letu kwa Mungu ni kumpenda Bwana Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, na kwa roho zetu zote, na kwa nguvu zetu zote, na kwa akili zetu zote. (Lk. 10:27)

Swali la 103: Je! Amri ya kwanza ni ipi? Jibu: Amri ya kwanza ni hii, “Usiwe na miungu mingine mbele yangu (au ila Mimi6). (Kut. 20:3)

Swali 104: Je! Ni majukumu gani yanahitajika katika amri ya kwanza? Jibu: Majukumu yanayohitajika katika amri ya kwanza ni kumjua na kumkiri Mungu kuwa ndiye Mungu wa pekee, na Mungu wetu;(1)na kumwabudu na kumtukuza ipasavyo,(2) kwa kufikiria,(3)kutafakari,(4)kukumbuka,(5)kumthamini,(6) umheshimu,(7)kumwabudu,(8)kumchagua,(9)kumpenda,(10)kumtama ni,(11)kumuogopa;13)kumwamini,(14)kumtumaini,(15)kumfurahia,(16) kufurahi kwake;(17) kuwa na bidii kwa ajili yake;(18) huku tukitoa sifa zote na shukrani kwake,(19) na kutii yote na kuzidi kujitiisha kwake;(20) kuwa waangalifu katika mambo yote ili kumpendeza,(21) na kuhuzunika pale tunapomkasirisha; (22)na kutembea pamoja naye kwa unyenyekevu.(23)

6

“Ila Mimi” ni tafsiri ya Kiswahili ambapo kwa Kiingereza ni “Before Me.” Tunatafsiri “Mbele Yangu” kwa kuzingatia muktadha wa swali.

131

(1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17) (18) (19) (20) (21) (22) (23)

2Nyak. 28: 9; Kumb. 26:17; Isa. 43:10; Yer. 14:22 Zab. 29: 2; 95: 6-7; Mt. 4:10 Mal. 3:16 Zab. 63: 6 Mhu. 12: 1 Zab. 71:19 Mal. 1: 6 Isa. 45:23 Yosh. 24:15, 22 Kumb. 6: 5 Zab. 73:25 Isa. 8:13 Kut. 14:31 Isa. 26: 4 Zab. 130: 7 Zab. 37: 4 Zab. 32:11 Rum. 12:11; Hes. 25:11 Fil. 4: 6 Yer. 7:28; Yak. 4: 7 I Yoh. 3:22 Yer. 31:18; Zab. 119: 136 Mik. 6: 8

Swali la 105: Je! Ni dhambi gani zilizokatazwa katika amri ya kwanza? Jibu: Dhambi zilizokatazwa katika amri ya kwanza ni, kutokumwamini Mungu, kwa kumkataa;(1) au kwa kuabudu sanamu au kuabudu miungu mingine badala ya Mungu wa kweli;(2) kutokujali chochote kilichoamriwa naye;(3) kuacha au kudharau chochote kile kilichoamriwa katika amri hii(4)ujinga,(5) usahaulifu,(6)kutokumwelewa,(6)maoni ya uongo,(8)mawazo yasiyostahili na mabaya juu yake;(9) kutafiti siri zake za ndani kwa 132

ujasiri,(10)kumtukana Mungu matusi,(11)chuki kwa (12) (13) Mungu; ubinafsi, kujipenda wenyewe badala ya (14) Mungu, kupenda mambo mengine kuliko kumpenda yeye;(15)kutokumjali Mungu,(16)kutoamini, au kuwa (17) (19) wazushi, kupinga mambo ya Mungu, kutokuwa na imani, (20) kukata tamaa,(21)kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi,(22) na kutojali hukumu,(23) ugumu wa moyo,(24) kiburi, (25) matendo ya kiburi,(26) kumjaribu Mungu; (27) kutumia njia zisizo halali, (28) kumpinga na kumhuzunisha Roho wake,(29) (na mambo mengine mengi ambayo hayawezi kuorodheshwa yote katika ukurasa mmoja) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17) (18) (19)

Zab. 14:1; Efe. 2:12 Yer. 2: 27-28; I Thes. 1: 9 Zab. 81:11 Isa. 43: 22-24 Yer. 4:22; Hos. 4: 1, 6 Yer. 2:32 Mdo 17:23, 29 Isa. 40:18 Zab. 50:21 Kumb. 29:29 Tit. 1:16; Ebr. 12:16 Rum. 1:30 2 Tim. 3: 2 Fil. 2:21 I Yoh. 2: 15-16; I Sam. 2:29; Kol. 3: 2, 5 I Yoh. 4: 1 Ebr. 3:12 Gal. 5:20; Tit. 3: 10 Mdo 26: 9

(20) (21) (22) (23) (24)

Zab. 78:22 Mwa 4:13 Yer. 5: 3 Isa. 42:25 Rum. 2: 5

133

(25) (26) (27) (28) (29)

Yer. 13:15 Zab. 19:13 Mt. 4: 7 Rum. 3: 8 II Kor. 1:24; Mt. 23:9

Swali la 106: Je! Tunafundishwa nini hasa na maneno haya “Mbele yangu (Ila Mimi) katika amri ya kwanza? Jibu: Maneno haya “mbele yangu,” au “mbele ya uso wangu,” katika amri ya kwanza yanatufundisha kwamba Mungu anaona vitu vyote, na kwamba anachukizwa na kuwepo kwa miungu mingine zaidi Yake;(1) na vile vile hutufundisha kufanya mambo yote machoni pake, yaani lolote tunalofanya katika huduma yake. (2)

(1) Eze. 8: 5-18; Zab. 44: 20-21 (2) I Nyak. 28: 9

Swali la 107: Amri ya pili ni ipi? Jibu: Amri ya pili ndiyo hii “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.” (Kut. 20:4-6)

Swali la 108: Je! Ni majukumu gani yanahitajika katika amri ya pili?

134

Jibu: Majukumu yanayohitajika katika amri ya pili ni kupokea na kufuata ibada zote za kidini na maagizo kama ambavyo Mungu ameanzisha katika Neno lake;(1)kufanya sala na shukrani kwa jina la Kristo;(2)kusoma, kuhubiri, na kusikia Neno lake;(3) Usimamizi na upokeaji wa Sakramenti; (4) serikali ya kanisa na nidhamu;(5)huduma na matengenezo yake;(6) kufunga; kuapa kwa jina la Mungu,(8) na kuapa kwake:(9) vile vile kukataa, na kupinga ibada zote za uongo; na ibada zote za sanamu.(11) (1) Kumb. 32: 46-47; Mt. 28:20; Mdo 2:42; II Tim. 6:13-14 (2) Fil. 4: 6; Efe. 5:20 (3) Kumb. 17:18-19; Mdo 15:21; 2 Tim. 4: 2; Yak. 1: 21-22 (4) Mt. 28:19; 1 Kor. 11: 23-30 (5) Mt. 16:19; 18: 15-17; 1 Kor. Sura ya 5; na 12:28 (6) Efe. 4:11-12; 2Tim. 5: 17-18; 1 Kor. 9: 1-15 (7) Yoel. 2: 12-13; 1 Kor. 7: 5 (8) Kumb. 6:13 (9) Isa. 19:21; Zab. 76:11 (10) Mdo 17: 16-17; Zab. 16: 4 (11) Kumb. 7: 5; Isa. 30:22

Swali 109: Je! Ni dhambi gani zilizokatazwa katika amri ya pili? Jibu: Dhambi zilizokatazwa katika amri ya pili ni pamoja na kuunda,(1)kushauri,(2)kuamuru,(3)kutumia,(4)na kukubaliana na ibada yoyote ya kidini isiyoanzishwa na Mungu mwenyewe; yaani(5) dini ya uongo;(6)kutengeneza uwakilishi wowote wa Mungu,(7) au kutengeneza aina yoyote ya picha au mfano wa kiumbe chochote kama kiwakilishi cha Mungu;(8)uundaji wowote wa miungu iliyotengwa,(9)na ibada zote, au huduma kwa miungu;(10)vifaa vyote vya ushirikina,(11)kuharibu ibada ya Mungu,(12)kuongeza, au kupunguza chochote kutoka kwa Mungu,(13)(na mambo mengine mengi ambayo hatujayataja hapa) 135

(1) (2) (3) (4) (5) (6)

Hes. 15:39 Kumb. 13: 6-8 Hos. 5:11; Mik. 6:16 I Falme 11:33; 12:33 Kumb. 12: 30-32 Kumb. 13: 6-12; Zek. 13: 2-3; Ufu 2: 2, 14-15, 20, Ufu 17:12, 16-17 (7) Kumb. 4: 15-19; Mdo 17:29; Rum 1: 21-23, 25 (8) Dan. 3:18; Gal. 4: 8 (9) Kut. 32: 8 (10) I Fal 18:26, 28; Isa. 65:11 (11) Mdo 17:22; Kol. 2: 21-23 (12) Mal. 1: 7-8, 14 (13) Kumb. 4: 2

Swali la 110: Je! Ni sababu gani zilizoambatishwa kwenye amri ya pili, zinazoharakisha utekelezaji wake? Jibu: Sababu zilizoambatishwa katika amri ya pili na kuharakisha utekelezaji wake ni maneno yafuatayo yaliyomo ndani yake, "BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.” (1) maneno haya ni zaidi ya enzi kuu ya Mungu juu yetu, na uzuri ndani yetu, (2) wivu kwa ibada yake mwenyewe, (3) na hasira yake ya kulipiza kisasi dhidi ya ibada zote za uongo, kama uzinzi wa kiroho; (4) anamwesabia yule anayevunja amri hii kwamba "anamchukia" na anamtishia kumwadhibu mpaka vizazi vijavyo(5) akiwazawadia wale wanaotunza amri hii na kuahidi rehema kwao na kwa vizazi vyao vya baadaye.(6) (1) Kut. 20: 5-6 136

(2) Zab. 45:11; Ufu 20: 3-4 (3) Kut. 34: 13-14 (4) 1 Kor. 10: 20-22; Yer. 7: 18-20; Eze. 16: 26-27; Kumb. 32: 16-20 (5) Hos. 2: 2-4 (6) Kumb. 5:29

Swali la 111: Je! Amri ya tatu ni ipi? Jibu: Amri ya tatu ni hii, “Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.” (Kut. 20:7)

Swali la 112: Ni nini kinachohitajika katika amri ya tatu? Jibu: Amri ya tatu inahitaji kwamba jina la Mungu, na vyeo vyake, sifa,(1)maagizo,(2)Neno,(3)Sakramenti,(4)sala,(5)viapo, (6) nadhiri(7)kazi zake, na kila kitu kingine ambacho kwa hicho Mungu hujijulisha vinapaswa kuchukuliwa kuwa vitakatifu. (8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mt. 6: 9; Kumb. 28:58; Zab. 29: 2; 68: 4; Ufu. 15: 3-4 Mal. 1:14; Mhu. 5: 1 Zab. 138: 2 1 Kor. 11: 24-25, 28-29 I Tim. 2: 8 Yer. 4: 2 Mhu. 5: 2, 4-6 Ayu. 36:24

Swali la 113: Je! Ni dhambi gani zilizokatazwa katika amri ya tatu? Jibu: Dhambi zilizokatazwa katika amri ya tatu ni kutotumia jina la Mungu kama isivyotakiwa;(1) na kutumia vibaya kwa 137

ujinga(2)ubatili,(3)kutokuwa na heshima, na (4) (5) (6) unajisi, ushirikina, kutumia majina yake, sifa zake, maagizo, (7) au kazi,(8) kwa kukufuru,(9)udanganyifu; (10) laana zote za dhambi, (11)viapo,(12) nadhiri,(13)kukiuka viapo;(14)na kuvitimiza kwa vitu visivyo halali;(15)kunung'unika na kugombana, (16) na matumizi mabaya ya amri za Mungu.(18) (1) Mal. 2: 2 (2) Mdo 17:23 (3) Mith. 30: 9 (4) Mal. 1: 6-7, 12; 3:14 (5) II Sam. 4: 3-5; Yer. 7: 4, 9-10, 14, 31; Kol. 2: 20-22 (6) II Fal.18:30, 35; Kut. 5: 2; Zab. 139: 20 (7) Zab. 50: 16-17 (8) Zab. 50: 16-17 (9) Isa. 5:12 (10) II Fal 19:22; Law. 24:11 (11) Zek. 5: 4; 8:17 (12) II Sam. 17:43; II Sam. 16: 5 (13) Yer. 5: 7; 23:10 (14) Est. 3: 7; 9:24; Zab. 22:18 (15) Zab. 24: 4, Eze. 17:16, 18-19 (16) Mk 6:26; II Sam. 25:22, 32-34 (17) Rum. 9:14, 19-20

Swali la 114: Je! Ni sababu gani zilizoambatishwa katika amri ya tatu? Jibu: Sababu zilizoambatishwa katika amri ya tatu zinaonekana kwa maneno haya, “maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.”(1) kwamba, kwa sababu yeye ndiye Bwana na Mungu wetu, jina lake halipaswi kuchafuliwa, au kudharauliwa kwa njia yoyote ile;(2) kwa sababu atamhesabia ana hatia mtu yule anayelitaja bure jina lake.(3) 138

(1) Kut. 20: 7 (2) Law. 19:12 (3) Eze. 36: 21-23; Kumb. 28: 58-59; Zek. 5: 2-4

Swali la 115: Je! Amri ya nne ni ipi? Jibu: Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. (Kut. 20:8-11)

Swali la 116: Amri ya nne inatutaka tufanye nini? Jibu: Amri ya nne inatutaka kuitakasa au kuiweka takatifu kwa Mungu siku aliyoiamuru katika Neno lake; siku moja nzima katika siku saba; ambayo ilikuwa siku ya saba tangu mwanzo wa ulimwengu hadi ufufuo wa Kristo; lakini baada ya Ufufuo wa Kristo imekuwa ni siku ya kwanza ya Juma, na hivyo itaendelea hadi mwisho wa ulimwengu; hii ndiyo Sabato ya Kikristo,(1) na katika Agano Jipya inaitwayo Siku ya Bwana.(2) (1) Kumb. 5:12, 14, 18; Mwa 2: 2-3; 1 Kor. 16: 1-2; Mdo 20: 7; Mt. 5: 17-18; Isa. 56: 2, 4, 6-7 (2) Ufu. 10

Swali la 117: Je! Watu wanapaswa kuitakasa Siku ya Bwana kwa namna gani? 139

Jibu: Siku ya Bwana au Sabato inapaswa kutakaswa kwa kupumzika kitakatifu siku nzima, (1) sio tu kupumzika kutoka kwenye shughuli za kila siku ambazo wakati wote ni ovu, lakini pia hata katika starehe za kidunia;(2) na kuifanya iwe ya kupendeza kwa (isipokuwa kufanya matendo ya rehema au huruma) (3) kufanya ibada mbele za Mungu kibinafsi na hadharani;(4) na kwa sababu hiyo tunahitaji kuandaa mioyo yetu kwa ajili ya kutekeleza kwa uhuru majukumu yale yaliyoelekezwa katika siku hiyo.(5) (1) Kut. 20: 8, 10 (2) Kut. 16: 25-28; Neh. 13: 15-22; Yer. 17: 21-22 (3) Mt. 12: 1-13 (4) Isa. 58: 13-14; 66:23; Lk 4:16; Mdo 20: 7; 1 Kor. 16: 1-2; Zab. 92; Law. 23: 3 (5) Kut. 16: 22, 25- 26, 29; 20: 8; Lk. 23:54, 56; Neh. 13:19

Swali la 118: Je! Kwa nini agizo la kutunza Sabato linaelekezwa zaidi kwa wakuu wa familia, na viongozi wengineo? Jibu: Agizo la kutunza Sabato linaelekezwa zaidi kwa wakuu wa familia na viongozi wengineo kwa sababu hawafungwi wenyewe tu, bali agizo hilo linapaswa kutekelezwa na wale wote ambao wako chini yao; na kwa sababu inawezekana kuwazuia kutunza Sabato kwa sababu ya kazi zao wanazofanya chini yao.(Kut. 20:10; 23:12; Yosh. 24:15; Neh. 13: 15, 17; Yer. 17: 20-22)

Swali la 119: Je! Ni dhambi gani zilizokatazwa katika amri ya nne? Jibu: Dhambi zilizokatazwa katika amri ya nne ni kutokufanya kazi zote zinazohitajika,(1) kufanya kazi zinazotakiwa kwa 140

uzembe;(2) kufanya kazi ngumu ambazo zinazuiwa katika amri hii pasipo kufanya matendo ya huruma na rehema;(3) na kufanya kazi zote zisizo na maana, maneno yasiyo maana, na mawazo mabaya juu ya kazi zetu za ulimwengu na starehe za kidunia.(4) (1) Ezek. 22:26 (2) Mdo 15: 7, 9; Eze. 33: 30-32; Amo. 8: 5; Mal. 1:13 (3) Eze. 23:38 (4) Yer. 17: 24, 27; Isa. 58:13

Swali la 120: Je! Ni sababu gani zilizoambatishwa katika amri ya nne, ambazo zinalazimisha utekelezaji wake? Jibu: Sababu zilizoambatishwa katika amri ya nne ambazo zinalazimisha utekelezaji wake ni lile agizo la Mungu kuturuhusu kufanya kazi kwa siku sita.(1) Kutokana na maelezo ya Mungu mwenyewe, Siku ya saba ni Sabato ya BWANA Mungu;(2) Mfano wa Mungu mwenyewe ambaye kwa siku sita aliumba mbingu na nchi, bahari na vitu vingine ndani yake, na alipumzika siku ya saba; na kutokana na baraka hiyo ambayo Mungu aliweka katika siku hiyo, si tu kwamba aliitakasa siku hiyo kuwa siku ya huduma yake, lakini aliiweka wakfu siku hiyo kuwa njia ya baraka kwetu katika kuitakasa; kwa hiyo Mungu aliibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.(3) (1) Kut. 20:9 (2) Kut. 20:10 (3) Kut. 20:11

Swali la 121: Je! Kwa nini neno "Kumbuka" limewekwa mwanzoni mwa amri ya nne?

141

Jibu: Neno "Kumbuka" limewekwa mwanzoni mwa amri ya nne,(1) kwa sababu ya faida kubwa ya kuikumbuka siku ya Sabato. Kwa kuweka mwanzoni neno "kumbuka' inatusaidia sisi katika maandalizi yetu ya kuitunza,(2) na, kwa kuitunza, huelekeza kushika maagizo mengine yote yaliyo katika amri hii(3) huendelea kutukumbusha kumshukuru Mungu kwa faida kuu mbili; yaani uumbaji na ukombozi;(4) Pia neno "kumbuka' limewekwa mwanzoni kwa sababu wanadamu mara nyingi tuko tayari kusahau,(5) Tunakumbushwa kwamba siku ya Sabato inakuja mara moja kwa siku saba, na biashara nyingi za kidunia zinakuja katikati, na mara nyingi shughuli hizi huondoa akili zetu kufikiria juu ya Sabato, ama kuitayarisha, au kuitakasa;(6) na kwamba Shetani na majeshi yake wanafanya kazi nyingi kufuta utukufu wa Mungu, na hata kumbukumbu yake, na kuleta yote yasiyo ya Kimungu.(7) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7)

Kut. 20:8 Kut. 16: 23; Lk. 23:54, 56; Mk. 15:42; Neh. 13:19 Zab. 92:13-14; Eze. 20:12, 19-20 Mwa. 2: 2-3; Zab. 118: 22, 24; Mdo. 4: 10, 11; Ufu. 1:10 Eze. 22:26 Kumb. 5:14-15; Amo. 8:5 Omb. 1:7; Yer. 17:21-23; Neh. 13:15-23

Sehemu ya IIIA.2. Wajibu wetu kwa Wanadamu

Swali la 122: Je, Amri sita za mwisho zinajumuisha mambo gani yaliyo wajibu kwetu kwa wanadamu wengine? Jibu: Jumla ya amri sita za mwisho zinaelekeza jukumu letu kwa kuwapenda majirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe,(1) na kuwafanyia wengine mambo ambayo tungetaka wafanye wao kwetu.(2) 142

(1) Mt. 22:39 (2) Mt. 7:12

Swali la 123: Je! Amri ya tano ni ipi? Jibu: Amri ya tano ni hii “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.” (Kut. 20:12)

Swali la 124: Je baba na mama katika amri ya tano maana yake ni nini? Jibu: Baba na mama katika amri ya tano sio tu wazazi wa asili, (1) lakini wakuu wote, wakubwa kwa umri(2) au wale ambao Mungu ametupatia katika kazi na wako juu yetu katika mahali pa mamlaka, iwe katika familia,(3) au kanisa (4) (1) Mith. 23:22-25; Efe. 6:1-2 (2) I Tim. 5:1-2 (3) II Fal. 5:13 (4) II Fal. 2:12; 13:14; Gal. 4:19

Swali la 125: Je! Kwa nini wakuu huitwa Baba na Mama katika muktadha wa amri ya tano? Jibu: Wakuu wametajwa kuwa Baba na Mama kwa ajili ya kuwafundisha majukumu yote walio chini yao, kama ilivyo kwa wazazi wa asili, kuwaonyesha upendo na huruma, kulingana na uhusiano wao kadhaa;(1) na kufanya kazi kwa utashi mkubwa na furaha katika kutekeleza majukumu yao kwa wakubwa wao, kama kwa wazazi wao.(2) (1) Efe. 6: 4; II Kor. 12:14; I Thes. 2: 7-8, 11; Hes.11: 11-12 (2) I Kor. 4:14-16; II Fal. 5:13 143

Swali la 126: Je! Ni nini wigo wa jumla wa amri ya tano? Jibu: Wigo wa jumla wa amri ya tano ni utekelezaji wa majukumu ambayo sisi tunadaiwa katika mahusiano yetu kadhaa, kama vile kwa wadogo au wakubwa, au kwa walio sawa. (Efe. 5:21; 1 Pet. 2:17; Rum 12:10)

Swali la 127: Ni heshima gani ambayo wadogo wanapaswa kuwaheshimu wakubwa? Jibu: Heshima ambayo wadogo wanapaswa kuwaheshimu wakubwa ni kuwaheshimu kwa mioyo yao,(1) maneno yao,(2) na tabia zao;(3) kwa sala na shukrani kwa ajili yao;(4) kwa kuiga fadhila na sifa zao;(5)kwa kutii amri na maagizo yao halali;(6) utii halali kwa makaripio yao;(7) kwa uaminifu,(8) kwa kuwatetea (9) na kwa kuwaheshimu kulingana na safu zao kadhaa, na asili ya mahali pao;(10) kuchukuliana nao katika udhaifu wao kwa upendo.(11) (1) Mal. 1: 6; Law. 19: 3 (2) Met. 31:28; I Petro 3: 6 (3) Law. 19:32; I Fal.2:19 (4) I Tim. 2: 1-2 (5) Ebr. 13: 7; Fil. 3:17 (6) Efe. 6: 1-2, 5-7; 1 Pet. 2: 13-14; Rum. 13: 1-5; Ebr. 13:17; Mith. 4: 3-4; 23:22; Kut. 18:19, 24 (7) Ebr. 12: 9; I Pet. 2:18-20 (8) Tit. 2: 9-10 (9) II Sam. 26: 15-16; II Sam. 18: 3; Est. 6: 2 (10) Mt. 22:21; Rum. 13: 6-7; II Tim. 5: 17-18; Gal. 6: 6; Mwa 45:11; 47:12 (11) Zab. 127: 3-5; Mith. 31:23

144

Swali la 128: Je! 128. Je! Ni dhambi gani za wadogo dhidi ya wakubwa zao? Jibu: Dhambi za wadogo dhidi ya wakubwa zao ni mambo yote yanayohusu kupuuza majukumu wanayotakiwa kufanya; (1) wivu,(2) dharau,(3)na uasi(4)dhidi ya wakubwa(5) katika maeneo yao(6) katika maagizo yao halali,(7)amri, na makaripio yao;(8) kejeli,(9) na kashfa dhidi yao na kwa serikali yao.(10) (1) Mt. 15: 4-6 (2) Hes. 11: 28-29 (3) II Sam. 8: 7; Isa. 3:5 (4) II Sam. 15: 1-12 (5) Kut. 21:15 (6) II Sam. 10:27 (7) II Sam. 2:25 (8) Kumb. 21: 18-21 (9) Mith. 30:11, 17 (10) Mith. 19:26

Swali la 129: Ni nini kinachohitajika kwa wakubwa kufanya kwa wadogo au walio chini yao? Jibu: Inahitajika kwa wakubwa, kulingana na nguvu wanayopokea kutoka kwa Mungu na uhusiano wao; kuwapenda, (1) kuwaombea, (2) kuwabariki;(3) kuwafundisha, (4) kuwashauri, na kuwaonya;(5) kuwasifu, (6) kuwapongeza, (7) na kuwazawadia pale wanapofanya vizuri;(8) na kuwapa mahitaji yao ya kiroho (9) na kimwili:(10) na kwa busara na utakatifu kuwa mifano, kumrudishia Mungu utukufu (11) kuheshimiana (12) ili kuhifadhi mamlaka ambayo Mungu ameweka juu yao. (13) (1) Kol. 3:19; Tit 2:4 (2) II Sam. 12:23; Ayu. 1:5

145

(3) I Fal. 8: 55-56; Ebr. 7:7; Mwa 49:28 (4) Kumb. 6:6-7 (5) Efe. 6:4 (6) I Pet. 3: 7 (7) I Pet. 2:14; Rum. 13: 3 (8) Ayu. 29:12-17; Isa. 1:10, 17 (9) Efe. 6:4 (10) I Tim. 5:8 (11) I Tim. 4:12; Tit. 2: 3-5 (12) I Fal. 3:28 (13) Tit. 2:15

Swali la 130: Je! Ni dhambi gani zinafanywa na wakubwa (wakuu) dhidi ya wadogo (walio chini yao)? Jibu: Dhambi za wakubwa dhidi ya wadogo ni pamoja na kupuuza majukumu ambayo wanapaswa kufanya(1)kuzidi kutafuta mambo yao wenyewe,(2)kutafuta utukufu wao wenyewe,(3)kutafuta faida yao wenyewe,(4)kuamrisha wadogo mambo yasiyo halali,(5)au yale yaliyo nje ya uwezo wao kuyafanya(6) kuwashauri kuelekea mabaya,(7)kuwatia moyo kufanya maovu,(8)au kuwahamasisha kufanya maovu,(10) kuwakaripia isivyo sahihi,(11)kuwaacha katika hali mbaya na hatari,(12) kuwasababishia hasira(13)au kwa njia yoyote ambayo inaweza kuwavunjia heshima.(14) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Eze. 34:2-4 Fil. 2:21 Yn 5:44; 7:18 Isa. 56: 10-11; Kumb. 17:17 Dan. 3: 4-6; Mdo 4: 17-18 Kut. 5: 10-18; Mt. 23: 2, 4 Mt. 14: 8; Mk 6:24 II Sam. 13:28

146

(9) II Sam. 3:13 (10) Yn 7:46-49; Kol. 3:21; Kut. 5:17 (11) I Pet. 2: 18-20; Ebr. 12:10; Kumb. 25: 3 (12) Mwa. 38:11, 26; Mdo. 18:17 (13) Efe. 6: 4 (14) Mwa. 9:21; 1 Fal.1: 6; 12: 13-16; II Sam. 2: 29-31

Swali la 131: Je! Ni majukumu gani ya usawa kwa wakubwa na wadogo? Jibu: Majukumu ya usawa kwa wakubwa na wadogo ni kuzingatia heshima na hadhi ya kila mmoja,(1)kuheshimiana;(2) na kufurahiana.(3) (1) I Pet. 2:17 (2) Rum. 12:10 (3) Rum. 12: 15-16; Fil. 2: 3-4

Swali la 132: Je! Ni dhambi gani wanaweza kufanya wakubwa na wadogo katika uhusiano wao? Jibu: Dhambi kwa wakubwa na wadogo zinazohusu uhusiano ni pamoja na kupuuza majukumu wanayotakiwa kufanya kwa pamoja,(1) kushushiana thamani, (2) kuoneana wivu, (3) kuchukia maendeleo ya mwingine;(4)kutaka kuwa juu ya mwingine (kujiinua) (5) (1) Rum. 13:8 (2) II Tim. 3: 3 (3) Mdo. 7: 9; Gal. 5:26 (4) Hes. 12: 2; Est. 6: 12-13

Swali la 133: Je! Ni sababu gani iliyoambatishwa katika amri ya tano ambayo inaharakisha utekelezaji wake? 147

Jibu: Sababu iliyoambatishwa katika amri ya tano iko katika maneno haya, "ili siku zako zipate kuwa nyingi juu ya nchi akupayo Mungu wako;” (1) amri hii inaelezea ahadi ya maisha marefu na ustawi kwa wale wanaotii amri hii.(2) (1) Kut. 20:12 (2) Kumb. 5:16; I Fal. 8:25; Efe. 6:2-3

Swali la 134: Je! Amri ya sita ni ipi? Jibu: Amri ya sita ni, Usiue (Kut. 20:13)

Swali la 135: Je! Ni majukumu gani yanahitajika katika amri ya sita? Jibu: Majukumu yanayohitajika katika amri ya sita ni (kutunza) kuhifadhi uhai wetu(1)na wa wengine(2) kwa kupinga mawazo yote na makusudi,(3)kushinda tamaa zote,(4)na kujiepusha na matukio yote,(5)majaribu,(6)na mazoea, ambayo huelekeza kuchukua uhai wa wengine;(7)na kwa kuwalinda dhidi ya machafuko yoyote,(8)kuwafariji na kuwasaidia waliofadhaika, na kuwalinda wasio na hatia. (9) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9)

Efe. 5: 28-29 I Fal. 18: 4 Yer. 26: 15-16; Mdo 23:12, 16-17, 21, 27 Efe. 4: 26-27 II Sam. 2:22; Kumb. 22: 8 Mt. 4: 6-7; Mith. 1: 10-11, 15-16 II Sam. 24: 2; 26: 9-11; Mwa 37: 21-22 Zab. 82: 4; Mith. 24: 11-12; I Sam. 14:45 I Thes. 5:14; Ayu. 31:19-20; Mt. 25: 35-36; Mith. 31: 8-9

148

Swali la 136: Je! Ni dhambi gani zilizokatazwa katika amri ya sita? Jibu: Dhambi zilizokatazwa katika amri ya sita ni kufanya tendo lolote lile linaloweza kuchukua uhai wetu,(1) au wa wengine,(2)isipokuwa ikiwa ni hukumu ya kifo,(3)au vita halali,(4)au kujilinda inapolazimu;(5)Amri hii inazuia kuondoa njia halali na muhimu za kuhifadhi uhai; (6)hasira ovu,(7)chuki,(8)wivu,(9)hamu ya kulipiza kisasi;(10)tamaa,(11)kutojali,(12) matumizi mabaya ya nyakula, vinywaji,(13)kazi,(14),na burudani;(15)maneno ya uchochezi,(16)ukandamizaji,(17)ugomvi,(18)kujeruhi,:(19)na kitu kingine chochote kinachoelekea kuharibu maisha ya mtu mwingine. (20) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17)

Mdo 16:28 Mwa 9: 6 Hes. 35: 31, 33 Yer. 48:10; Kumb. 20 Kut. 22: 2-3 Mt. 25: 42-43; Yak. 2:15-16; Mhu. 6: 1-2 Mt. 5:22 I Yoh. 3:15; Law. 19:17 Mith. 14:30 Rum. 12:19 Efe. 4:31 Mt. 6:31, 34 Lk. 21:34; Rumi 13:13 Mh. 2: 22-23; 12: 12 Isa. 5:12 Mith. 12:18; 15: 1 Kut. 18:18; Kut. 1:14

(18) Gal. 5:15; Met. 23:29 (19) Hes. 35: 16-18, 21 149

(20) Kut. 21: 18-36

Swali la 137: Je! Amri ya saba ni ipi? Jibu: Amri ya saba ni, “Usizini. (Kut. 20:14)

Swali la 138: Je! Ni majukumu gani yanahitajika katika amri ya saba? Jibu: Majukumu yanayohitajika katika amri ya saba ni usafi wa mwili, akili,(1)maneno,(2) na tabia;(3)na kujitunza sisi wenyewe na wengine; (4) kujiangalia kwa makini;(5) kuwa na maadili, (6) kutunza ushirika safi, na adabu (7) unyenyekevu; (8) kwa wale wasio watulivu waingie kwenye ndoa, (9) upendo na kushirikiana; (10) kufanya bidii katika wito wetu; (11) kuepuka nafasi zote za kutenda uovu na uchafu.(12) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12)

I Thes. 4: 4; Ayu. 31: 1; 1 Kor. 7:34 Kol. 4: 6 I Pet. 2: 3 I Kor. 7: 2, 35-36 Ayu. 31: 1 Mdo. 24:24 Mith. 2: 16-20 I Tim. 2: 9 I Kor. 7: 2, 9 Mith. 5: 19-20 Mith. 31: 11, 27- 28 Mith. 5: 8; Mwa. 39: 8-10

Swali la 139: Je! Ni dhambi gani zinazokatazwa katika amri ya saba?

150

Jibu: Dhambi zinazokatazwa katika amri ya saba, mbali na kupuuza majukumu yanayotakiwa, yafuatayo yanakatazwa,(1) uzinzi, uasherati,(2) ubakaji,(3)tamaa zote;(4) mawazo yote machafu; (5) kusikiliza sauti za kingono kwa njia ya kawaida au simu;(6)mwonekano wa kihuni unaovutia umalaya,(7) tabia mbaya au mavazi yasiyo na adabu yenye nia ya kushawishi watu kuingia kwenye dhambi;(8) kuzuia haki ya ndoa,(9) na kuruhusu ndoa zisizoruhusiwa, (kwa mfano ndoa za mashoga na wasagaji)(10)kuweka nadhiri za useja, (11) kucheleweshwa kwa ndoa pasipo na ulazima;(12) kuwa na wake au waume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja;(13)talaka isiyo ya haki,(14) au kuachana; (15) kuangalia picha za uchi, video, na michezo michafu;(16)na matendo mengine machafu yanayofanana na hayo; (17) (1) Mith. 5:7 (2) Ebr. 13: 4; Gal. 5:19 (3) II Sam. 13:14; 1 Kor. 5:1 (4) Rum. 1:24, 26-27; Law. 20: 15-16 (5) Mt. 5:28; 15:19; Kol. 3: 5 (6) Efe. 5: 3-4; Mith. 7: 5, 21-22 (7) Isa. 3:16; II Petro 2:14 (8) Mith. 7:10, 13 (9) I Tim. 4: 3 (10) Law. 18: 1-21; Mk 6:18; Mal. 2: 11-12 (11) Mt. 19: 10-11 (12) 1 Kor. 7: 7-9; Mwa 38:26 (13) Mal. 2: 14-15; Mt. 19: 5 (14) Mal. 2:16; Mt. 5:32 (15) 1 Kor. 7:12-13 (16) Efe. 5: 4; Eze. 23: 14-16; Isa. 3:16; 23: 15-17; Mk 6:22; Rum. 13:13; 1 Pet. 4:3

(17) II Fal. 9:30; Yer. 4:30; Eze. 23:40

Swali la 140: Je!Amri ya nane ni ipi? 151

Jibu: Amri ya nane ni, “Usiibe.” (Kut. 20:15)

Swali 141: Je! Ni majukumu gani yanahitajika katika amri ya nane? Jibu: Majukumu yanayohitajika katika amri ya nane ni yafuatayo; kuwa wakweli, waaminifu, na watu wa haki katika makubaliano na katika biashara kati ya mtu na mtu; (1) kumpa kila mtu kila tuwezacho kufanya; (2) kutoa na kukopesha kwa uhuru, kulingana na uwezo wetu, na mahitaji ya wengine;(3) kuwa na uamuzi mzuri katika masuala kidunia; (4) kupata mali kwa njia iliyo halali, na kuendeleza utajiri wa mali zetu na zile za wengine kwa uaminifu. (5) (1) (2) (3) (4) (5)

Zab. 15: 2, 4; Zek. 7: 4, 10; 8:16-17 Law. 6: 2-5; Lk 19: 8 Lk 6:30, 38; 1 Yoh. 3:17; Efe. 4:28; Gal. 6: 10 I Tim. 6: 6-9; Gal. 6:14 Law. 25:35; Kumb. 22: 1-4; Kut. 23: 4-5; Mwa 47:14, 20; Fil. 2: 4, Mat. 22:39

Swali la 142: Je! Ni dhambi gani zilizokatazwa katika amri ya nane? Jibu: Dhambi zilizokatazwa katika amri ya nane ni pamoja na(1)wizi,(2)kupokea chochote kilichoibiwa;(3)ulaghai,(4) kutumia mzani wa uongo, (5) kuondoa alama za mpaka wa ardhi, (6) ukosefu wa haki na uaminifu katika mikataba kati ya mtu na mtu(7)au katika mambo ya kuaminiana;(8) ukandamizaji,(9) udhalimu,(10) (12) riba,(11) hongo au rushwa mashtaka (13) (14) mabaya, utapeli, kuingiza bidhaa za magendo ili kujipatia faida;(15)uchoyo;(16) wivu katika kufanikiwa kwa wengine; (17) uvivu,(18) michezo ya kubahatisha kwa kutapeli; na njia zingine 152

zote ambazo zinalenga kuchukua mali isiyo halali au kwa njia ya udanganyifu,(19) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17) (18) (19)

Yak. 2: 15-16; 1 Yoh. 3:17 Efe. 4:28; Zab. 42:10 Mith. 29:24; Zab. 50:18 I Thes. 4: 6 Mith. 11: 1; 20:10 Kumb. 19: 14; Met. 23:10 Lk 16: 10-12 Eze. 22:29; Lawi. 25:17 Mt. 23:25; Eze. 22:12 Zab. 15:5 Ayub 15:34 I Kor. 6: 6-8; Mith. 3: 29-30 Isa. 5: 8; Mika 2:2 Ayu. 20:19; Yak. 5: 4; Mith. 21:6 Lk. 12:15 Zab. 37: 1, 7; 73:3 II Thes. 3:11; Mith. 18:9 Mith. 21:17; 23: 20-21; 28:19 Mhu. 4: 8; 6: 2; II Tim. 5:8

Swali la 143: Je! Amri ya tisa ni ipi? Jibu: Amri ya tisa ni “Usimshuhudie jirani yako uongo.” (Kut. 20:16)

Swali la 144: Je! Ni majukumu gani yanahitajika katika amri ya tisa? Jibu: Majukumu yanayohitajika katika amri ya tisa ni, utunzaji na ukuzaji wa ukweli kati ya mtu na mtu, (1) kusema ukweli tu katika maswala yote ya hukumu na haki, (2)na katika vitu vingine vyote 153

ukweli unapaswa kuwa kipaumbele,(3)kuendeleza sifa nzuri ya majirani zetu,(4) kufunika udhaifu wao;(5)kusimama nao katika taabu;(6) kutokukubali taarifa mbaya kuhusu majirani zetu,(7) kutunza ahadi halali;(8)pamoja na mambo mengine yote yanayohusiana na uaminifu. (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Zek. 8:16 Law. 19: 15; Mith. 14: 5, 25 2 Kor. 1: 17-18; Efe. 4:25 Ebr. 6: 9; 1 Kor. 13: 7 1 Kor. 1: 4-5, 7; 2 Tim. 1: 4-5 II Sam. 22:14 Zab. 15: 3 Zab. 15: 4

Swali la 145: Je! Ni dhambi gani zinazokatazwa katika amri ya tisa? Jibu: Dhambi zinazokatazwa katika amri ya tisa ni; dhambi zote zinazohusu kupindisha ukweli, na kuharibu jina zuri la majirani zetu;(1) hasa katika mahakama ya kiraia;(2)kutoa ushahidi wa uongo,(3)kushadidia ushahidi wa uongo,(4) kupindua na kupindisha ukweli(5)kutoa hukumu isiyo ya haki,(6)kubadilisha ubaya kuwa uzuri;(7)kughushi,(8)kuficha ukweli kwa kunyamaza,(9)kunyamaza pale maovu yanapotawala miongoni mwetu kwa kuogopa kufichua ukweli,(10)kulalamika kwa ajili ya wengine; (11) kusema ukweli bila kuzingatia mazingira hatarishi ambapo hekima inapaswa kutumika katika kusema ukweli huo,(12)na mambo mengine yote yanayohusu ukweli kwa majirani zetu. (1) (2) (3) (4)

I Sam. 17:28; II Sam. 1: 9-10, 15-16; 16: 3 Law. 19: 15; Hab. 1: 4 Mith. 6:16, 19; 19: 5 Mdo 6:13

154

(5) Yer. 9: 3, 5; Mdo 24: 2, 5; Zab. 3: 1-4; 12: 3-4 (6) Mith. 17: 15; 1 Fal. 21: 9-14 (7) Isa. 5:23 (8) Zab. 119: 69; Lk. 16:5-7; 19: 8 (9) Law. 5: 1; Mdo 5: 3, 8-9; II Tim. 4:6 (10) I Fal. 1: 6; Law. 19:17 (11) Isa. 59: 4 (12) Mith. 29:11

Swali la 146: Amri ya kumi ni ipi? Jibu: Amri ya kumi ni “Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.” (Kut. 20:20)

Swali la 147: Je! Ni majukumu gani yanahitajika katika amri ya kumi? Jibu: Majukumu yanayohitajika katika amri ya kumi ni; kuridhika na hali zetu wenyewe,(1) na pia kuwa na moyo wa huruma kwa majirani zetu. (2) (1) Ebr. 13: 5; I Tim. 6: 6 (2) Ayu. 31:29; Zab. 122: 7-9; I Tim. 1: 5; Est. 10: 3; 1Kor. 13 4-7

Swali la 148: Je! Ni dhambi gani zinazokatazwa katika amri ya kumi? Jibu: Dhambi zinazokatazwa katika amri ya kumi ni; kutokuridhika na mali zetu wenyewe; (1) kuwa na wivu kwa ajili ya majirani zetu,(2)kuchukia maendeleo ya majirani zetu, (3)pamoja na nia mbaya na shauku ya kuchukua mali za majirani zetu ili ziwe zetu.(4) 155

(1) (2) (3) (4)

I Fal. 21: 4; Est. 5:13; 1 Kor. 10:10 Gal. 5:26; Yak. 3:14, 16 Zab. 112: 9-10; Neh. 2:10 Rum. 7: 7-8; 13: 9; Kol. 3: 5; Kumb. 5:21

Sehemu ya IIIB. Asili ya Dhambi

Swali la 149: Je! Kuna mtu yeyote anayeweza kuzishika amri za Mungu kikamilifu? Jibu: Hakuna mtu awezaye kuzishika amri za Mungu kikamilifu peke yake,(1) au kwa neema yoyote inayopokelewa katika maisha haya kwa kushika maagizo ya Mungu,(2) lakini kila mtu, na kila siku huzivunja amri za Mungu kwa mawazo,(3) maneno na matendo.(4) (1) (2) (3) (4)

Yak. 3:2; Yn. 15:5; Rum. 8:3 Mhu. 7:20; 1 Yoh. 1:8, 10; Gal. 5:17; Rum 7:18-19 Mwa 6:5, 8:21 Rum. 3:9-19; Yak. 3:2-13

Swali la 150: Je! Makosa yote ya sheria ya Mungu yana uzito sawa mbele za Mungu? Jibu: Hapana. Makosa yote ya sheria ya Mungu hayana uzito sawa kwa maana ya kwamba kuna dhambi zingine ambazo zina uzito mkubwa mbele za Mungu kuliko dhambi nyinginezo (Yn.19:11; Eze. 8:6, 13, 15; IYoh. 5:16; Zab.78:17,32, 56)

Swali 151: Je! Ni mambo gani yanayofanya dhambi zingine kuwa mbaya zaidi kuliko zingine?

156

Jibu: Dhambi zinaleta hatari na utofauti katika uzito ikiwa zitakuwa zimehusisha mambo au mazingira yafuatayo: 1. Kutoka kwa wale ambao wamefanya dhambi hizo:(1) ikiwa ni wazee,(2) ikiwa wana uzoefu wa muda mrefu wa neema ya Mungu,(3)ikiwa wanajulikana kwa imani yao,(4)ikiwa wanajulikana sana,(5) ikiwa wanashikilia nafasi ya juu(6) ofisini,(7) ikiwa ni waalimu,(8) ambao mfano wao utawashawishi wengine.(9) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9)

Yer 2:8. Ayu. 32:7,9, Mhu. 4:13 I Fal. 11:4,9 II Sam 12:14, I Kor 5:1 Yak 4:17, Lk 12:47-48 Yer 5:4-5, Yn 3:10 II Sam 12:7-9, Eze. 8:11-12 Rum 2:17-24 Gal 2:11-14, II Pet 2:2

2. Kutoka kwa wale waliotendwa:(10) ikiwa dhambi inatendwa moja kwa moja dhidi ya Mungu,(11)dhidi ya sifa zake, (12) dhidi ya ibada,(13) dhidi ya Kristo na neema yake,(14) dhidi ya Roho Mtakatifu,(15) dhidi ya shuhuda wake, (16) dhidi ya kazi zake;(17) dhidi ya wale walio juu yetu, watu mashuhuri,(18) na hasa dhidi ya wale ambao tunahusiana nao au tunawaheshimu; (19) na dhidi ya mwamini yeyote, (20) hasa wale walio dhaifu katika imani,(21) dhidi ya mioyo yao au ya mtu mwingine yeyote,(22) na dhidi ya faida ya jumla ya kila mtu.(23) (10) Math. 21:38-39 (11) I Sam. 2:25: Mdo. 5: 4: Zab. 5: 4 (12) Rum. 12: 4 (13) Mal. 1:8, 14 (14) Ebr. 2: 2-3: 7:25 (15) Ebr. 15:10: Math. 12: 31-32

157

(16) Efe. 4:30 (17) Ebr. 6:4-6 (18) Yud 8: Hes. 12: 8-9: Isa. 3: 5 (19) Mith. 30:17: II Kor. 12:15: Zab 55:12-15 (20) Sef. 2: 8, 10-11: Math. 18: 6: Ufu. 17: 6 (21) I Kor. 8:11-12: Rum. 14:13, 15, 21 (22) Eze. 13:19: I Kor. 8:12: Ufu. 18: 12-13: Math. 23: 15 (23) I Thes. 2:15-16: Yosh. 22:20

3. Kutoka kwenye asili na namna dhambi hiyo ilivyo:(24) ikiwa ni kinyume cha sheria,(25) ikiwa inavunja amri zaidi ya moja au inajumuisha dhambi nyingi tofauti tofauti;(26) ikiwa haijakusudiwa kutoka moyoni, bali imeonyeshwa kwa maneno na vitendo,(27) ikiwa ni kwa kudharau wengine,(28) ikiwa haziwezi kusahihishwa,(29) ikiwa ni dhidi ya njia ya neema ya Mungu,(30) rehema zake,(31) au hukumu zake,(32) dhidi ya uelewa wetu wa asili, imani(33) ikiwa ni ushawishi wa dhamiri zetu,(34) ikiwa ni maonyo ya wazi au kibinafsi,(35) ikiwa ni hukumu iliyotolewa na kanisa,(36) au adhabu iliyotolewa na mahakama;(37) na ikiwa ni kinyume cha maombi yetu, makusudi, ahadi,(38) viapo (39) maagano(40) na kujitolea kwa Mungu au wanadamu,(41) Ikiwa ni dhambi inafanywa mara kwa mara na mtu huyo ,(42) au mtu kurudi kwenye dhambi hiyohiyo baada ya kutubu.(43) (24) Mith. 6: 30-35 (25) Ezr. 9:10-12; 1 Fal. 11: 9-10 (26) Kol. 3: 5; I Tim. 6: 10; Mith. 5:8-12; 6:32-33; Josh. 7:21 (27) Yak. 1: 14-15; Mt. 5:22; Mik. 2:1 (28) Mt. 18:7; Rum. 2:23-24 (29) Kumb. 22:22, 28-29; Mith. 6:32-35 (30) Mt. 11:21-24; Yoh. 15:22 (31) Isa. 1: 3; Kumb. 32:6 (32) Amo. 4: 8-11; Yer. 5:8 (33) Rum. 1: 26-27 (34) Rum. 1:32; Dan. 5:22; Tit. 3:10-11 (35) Mith. 29: 1

158

(36) Tit. 3:10; Mt. 18:17 (37) Mith. 23:35, 27:22 (38) Zab. 78:34-37; Yer. 2:20, 13: 5-6, 20-21 (39) Mhu. 5: 4-6; Mith. 20:25 (40) Law. 26:25 (41) Mith. 2:17; Eze. 17:18-19 (42) Isa. 57:17 (43) Yer. 34: 8-11; II Pet. 2:20-22

4. Kutokana na hali ya wakati,(53)na mahali:(54) ikiwa ni kwa siku ya Bwana,(55) au nyakati zingine za ibada ya kimungu, (56) au shughuli zingine za kidini ambazo husaidia kuzuia au kuwa suluhisho la mapungufu ya dhambi; (59) na ikiwa ni kwa wazi au kwenye uwepo wa wengine, ambao kwa sababu hiyo wanaweza kuchafuliwa na dhambi.(60) (53) II Fal. 5:26 (54) Yer. 7:10; Isa. 26:10 (55) Ezek. 23:37-39 (56) Isa. 58:3-5; Hes. 25:6-7 I Kor. 11:20-21 (57) Ezr. 9:13-14 (58) II Sam. 16:22; I Sam. 2:22-24

Swali la 152: Je! Kila dhambi inastahili nini kutoka kwa Mungu? Jibu: Kila dhambi; kubwa au hata ndogo, ikiwa kinyume na mamlaka ya Mungu,(1) wema wake, (2) na utakatifu wake,(3) na pia dhidi ya sheria ya haki yake (4) inastahili ghadhabu na laana ya Mungu,(5) katika maisha haya,(6) na hata yale yajayo; (7) na haiwezi kumalizwa na kitu chochote zaidi ya damu ya Kristo.(8) (1) (2) (3) (4)

Yak. 2: 10-11 Kut. 20: 1-2 Hab. 1:13; Law. 10: 3; 11: 44-45 I Yoh. 3: 4; Rum. 7:12

159

(5) (6) (7) (8)

Efe. 5: 6; Gal. 3:10 Omb. 3:39; Kumb. 28: 15-68 Mt. 25:41 Ebr. 9:22; 1 Pet. 1: 18-19

Swali la 153: Je! Mungu anataka nini kwetu, ili tuepuke ghadhabu na laana Yake kwa sababu ya kuvunja amri Zake? Jibu: Ili tuepuke ghadhabu na laana ya Mungu kutokana na kukiuka sheria Zake, Mungu anataka sisi tutubu kwake, na kuwa na imani katika Bwana wetu Yesu Kristo,(1) na kutumia kwa bidii njia ambazo Kristo hutumia kuwasilisha kwetu faida za upatanisho Wake. (2) (1) Mdo 16: 30-31; 20:21; Mt. 3: 7-8; Lk 13: 3, 5; Yn 3:16, 18 (2) Mith. 2: 1-5; 8: 33-36

Sehemu ya IIIC. Njia za Neema

Swali la 154: Je! Ni njia zipi za nje ambazo Kristo hutumia kuwasilisha kwetu zile faida za upatanisho wake? Jibu: Njia za nje na za kawaida ambazo Kristo hutumia kuwasilisha kwetu zile faida za upatanisho wake, ni maagizo yake yote; hasa Neno, Sakramenti, na Sala (maombi); na yote ambayo yametekelezwa kwa wateule kwa ajili ya wokovu wao. (Mt. 28: 19-20; Mdo 2:42, 46-47) Sehemu ya IIIC.1. Neno

Swali la 155: Je! Neno la Mungu linakuwaje na ufanisi kwenye wokovu? Jibu: Roho wa Mungu huweza kutumia usomaji wa Neno la Mungu kwa ajili ya kuwaleta watu katika wokovu, lakini hasa 160

mahubiri ya Neno la Mungu, ndiyo njia ya kuijua kweli,(1) Neno huwashawishi wenye dhambi;(2)huwavuta watu kwa Kristo;(3) na kuwafanya wafanane na sura ya Kristo,(4)na kuwanyenyekesha chini ya mapenzi Yake;(5) vilevile Neno huwaimarisha dhidi ya majaribu na uovu;(6) na kuwajenga katika neema,(7) na kuimarisha mioyo yao katika utakatifu na faraja kupitia imani iletayo wokovu.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Neh. 8: 8; Mdo 26:18; Zab. 19: 8 I Kor. 14: 24-25; II Nyak. 34: 18-19, 26-28 Mdo. 2:37, 41; 8: 27-39 II Kor. 3:18 II Kor. 10: 4-6; Rum. 6:17 Mt. 4: 4, 7, 10; Efe. 6: 16-17; Zab. 19: 11; 1 Kor. 10:11 Mdo 20:32; II Tim. 3: 15-17 Rum. 1:16; 10: 13-17; 15: 4; 16:25; 1 Thes. 3: 2, 10-11, 13

Swali la 156: Je! Neno la Mungu linapaswa kusomwa na watu wote? Jibu: Ingawa watu wote hawataruhusiwa kusoma Neno hadharani (hasa kanisani),(1) bado, watu wa kila aina wanapaswa kusoma Neno la Mungu peke yao,(2) katika familia zao:(3) Vilevile Maandiko Matakatifu yanapaswa kutafsiriwa kutoka lugha ya asili hadi kwenye lugha za makabila.(4) (1) (2) (3) (4)

Kumb. 31: 9, 11-13; Neh. 8: 2-3; 9: 3-5 Kumb. 17:19; Ufu. 1: 3; Yn 5:39; Isa. 34:16 Kumb. 6: 6-9; Mwa. 18:17, 19; Zab. 78: 5-7 II Kor. 14: 6, 9, 11-12, 15-16, 24, 27-28

Swali la 157: Je! Neno la Mungu linapaswa kusomwa kivipi?

161

Jibu: Neno la Mungu linapaswa kusomwa kwa heshima kubwa;(1) na kwa imani thabiti kwamba hilo ndilo Neno la Mungu,(2) na kwamba ni Mungu peke yake anayeweza kutuwezesha kuelewa Neno Lake;(3) vilevile, Neno linapaswa kusomwa kwa nia ya kujua, kuamini, na kutii mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa ndani yake;(4) linapaswa kusomwa kwa bidii,(5) na kwa kuzingatia upeo wa msomaji;(6) kwa kutafakari,(7)na kulitumia kwa usahihi katika maisha yetu, (8) na kwa kujikana wenyewe,(9) na kwa maombi.(10) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10)

Zab. 19:10; Neh. 8: 3-10; Kut. 24: 7; II Nyak. 34:27; Isa. 66:2 2 II Pet. 1: 19-21 Lk. 24:45; II Kor. 3:13-16 Kumb. 17:10, 20 Mdo. 17:11 Mdo. 8:30, 34; Lk 10: 26-28 Zab. 1: 2, 119:97 II Nyak. 24:21 Mith. 3: 5; Kumb. 33:3 Mith. 2: 1-6; Zab. 119: 18; Neh. 7: 6, 8

Swali la 158: Je! Neno la Mungu linapaswa kuhubiriwa na nani? Jibu: Neno la Mungu linapaswa kuhubiriwa tu na wale walio na vipawa vya kutosha, (1) na pia wamepitishwa kwa haki na kuitwa kwenye huduma hiyo.(2) (1) I Tim. 3: 2, 6; Efe. 4:8-11; Hos. 4: 6; Mal. 2: 7; II Kor. 3:6 (2) Yer. 14:15; Rum. 10:15; Ebr. 5: 4; I Kor. 12:28-29; I Tim. 3: 10; 4:14; 5:22

Swali la 159: Wale walioitwa kwa ajili ya huduma ya Neno wanapaswa kuhubirije Neno la Mungu? 162

Jibu: Wale ambao wameitwa kufanya kazi katika huduma ya Neno wanapaswa kuhubiri mafundisho sahihi kutoka kwenye Neno la Mungu,(1) kwa bidii,(2) kwa wakati ufaao na ule usiofaa;(3) waziwazi,(4)sio kwa maneno ya kushawishi ya hekima ya wanadamu, lakini kwa udhihirisho wa Roho;(5) kwa uaminifu, (6) kwa kuweka wazi shauri la Mungu;(7) kwa busara,(8) kwa kulitumia Neno huku wakizingatia mahitaji na uwezo wa wasikiaji;(9) kuhubiri kwa wivu,(10) kwa kumpenda Mungu kwa bidii,(11) na roho za watu wake; (12) kuhubiri kwa dhati, (13) huku wakilenga kurudisha utukufu kwa Mungu,(14) na uongofu wale wanaohubiriwa(15) na kwa uadibishaji; (16) na wokovu. (17) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17)

Tit. 2:1, 8 Mdo. 18:25 II Tim. 4: 2 I Kor. 14:19 I Kor. 2: 4 Yer. 23:28; I Kor. 4:1-2 Mdo. 20:27 Kol. 1:28; II Tim. 2:15 I Kor. 3: 2; Ebr. 5:12-14; Lk 12:42 Mdo 18:25 II Kor. 5: 13-14; Fil. 1:15-17 Kol. 4:12; II Kor. 12:15 II Kor. 2:17; 4:2 I Thes. 2: 4-6; Yn. 7:18 I Kor. 9:19-22 II Kor. 12:19; Efe. 4:12 I Tim. 4:16; Mdo. 26: 16-18

Swali la 160: Je, nini kinahitajika kwa wale wanaosikia Neno linalohubiriwa?

163

Jibu: kwa wale wanaosikia Neno linalohubiriwa wanahitajika kulipokea;(1)kujiandaa kwa:(2) maombi;(3) na kwa kuchunguza: Kile wanachosikia kutoka kwenye Maandiko;(4) na wanapaswa kupokea ukweli kwa imani,(5) kwa upendo,(6) kwa unyenyekevu,(7) na kuweka sawa utayari wa akili, (8) kwenye Neno la Mungu;(9) kwa kutafakari,(10)na kuliweka mioyoni mwao(12) na mwishowe lazima lizae matunda katika maisha yao.(13) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13)

Mith. 8:34 I Pet. 2: 1-2; Lk 8:18 Zab. 119: 18; Efe. 6:18-19 Mdo 17:11 Ebr. 4:2 II Thes. 2:10 Yak. 1:21 Mdo. 17:11 I Thes. 2:13 Lk 9:44; Ebr. 2: 1 Lk 24:14; Kumb. 6:6-7 Mith. 2:1; Zab. 119:11 Lk. 8:15; Yak. 1:25

Sehemu ya IIIC.2. Sakramenti

Swali la 161: Je, ni kwa jinsi gani Sakramenti zinakuwa njia zenye ufanisi za wokovu? Jibu: Sakramenti zinakuwa njia zenye ufanisi za wokovu sio kwa nguvu yoyote ile iliyo ndani yake au namna yoyote ile ya kiungu ndani yake au nguvu yoyote ya yule anayefanya utekelezaji wake, bali inatokana na Kazi ya Roho Mtakatifu na baraka ya Kristo (I Pet. 3:21; Mdo. 8:13, 23; I Kor. 3: 6-7; 12:13) 164

Swali la 162: Sakramenti ni nini? Jibu: Sakramenti ni agizo takatifu lililowekwa na Kristo katika kanisa lake,(1) kuashiria na kuonyesha(2) kwa wale walio ndani ya Agano la Neema,(3) faida za upatanisho wake;(4) kuimarisha na kuongeza imani yao, na neema zingine zote,(5) kuwalazimisha kutii;(6) kushuhudia na kuthamini upendo wao na ushirika wao kati ya mmoja na mwingine;(7) na kuwatofautisha na wale walio nje ya kanisa.( 8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mwa. 17: 7, 10; Kut. Sura ya. 12; Mt. 26: 26-28; 28:19 Rum. 4:11; 1 Kor. 11: 24-25 Rum. 15: 8; Kut. 12:48 Mdo 2:38; 1 Kor. 10:16 Rum. 4:11; Gal. 3:27 Rum. 6: 3-4; 1 Kor. 10:21 Efe. 4: 2-5; 1 Kor. 12:13 Efe. 2: 11-12; Mwa. 34:14

Swali la 163: Je! Sakramenti ina sehemu ngapi? Jibu: Sakramenti ina sehemu kuu mbili; ishara ya nje na ya ndani. Ile ishara ya nje, inatumika kulingana na miadi ya Kristo mwenyewe; ishara ya ndani ni ile neema ya ndani na ya kiroho inayowakilishwa. (Mt. 3:11; 1 Pet. 3:21; Rum. 2:28-29)

Swali la 164: Je! Kristo alianzisha Sakramenti ngapi katika kanisa lake chini ya Agano Jipya? Jibu: Chini ya Agano Jipya Kristo ameanzisha Sakramenti mbili tu katika kanisa lake; Ubatizo na Meza ya Bwana. (Mt. 26: 26-28; 28:19; 1 Kor. 11:20, 23)

165

Sehemu ya IIIC.2.1. Ubatizo

Swali la 165: Ubatizo ni nini? Jibu: Ubatizo ni Sakramenti ya Agano Jipya, ambayo Kristo ameamuru kwa kuosha kwa maji kwa jina la Baba, na Mwana, na la Roho Mtakatifu,(1) kuwa ishara na muhuri ndani yake Kristo, (2) ishara ya ondoleo la dhambi kwa damu yake,(3) na kuzaliwa upya na Roho wake;(4) ishara ya kufanywa Wana,(5) na ishara ya ufufuo wa uzima wa milele; (6) ambapo wanaobatizwa kimsingi wanajiungamanisha na kanisa linaloonekana, (7) na kuingia katika uhusiano kamili na Kristo.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mt. 28:19 Gal. 3:27 Mk 1:4; Ufu. 1:5 Tit. 3:5; Efe. 5:26 Gal. 3:26-27 I Kor. 15:29; Rum 6:5 I Kor. 12:13 Rum. 6:4

Swali la 166: Je nani anayestahili kubatizwa? Jibu: Si kila mtu anaweza kubatizwa isipokuwa yule aliye ndani ya kanisa linaloonekana, ambapo anamkiri na kumtii Kristo.(1) Vile vile watoto ambao wazazi wao wote, ama mmojawapo anamkiri Kristo anaweza kubatizwa kwa sababu watoto hao kwa msingi wa wazazi wao, nao wako ndani ya agano (2) (1) Mdo 2:38; 8:36-37 (2) Mwa. 17: 7, 9; Gal. 3:9, 14; Kol. 2:11-12; Mdo 2:38-39; Rum. 4: 11-12; 11:16;1 Kor. 7:14; Math. 28:19; Lk 18:15-16

166

Swali la 167: Je! tunawezaje kuona maana ya ubatizo katika maisha yetu? Jibu: Tunaweza kuona maana ya ubatizo katika maisha yetu kwa kukumbuka kwamba tumetiwa muhuri katika ubatizo na kwa kushika nadhiri yetu ya ahadi iliyowekwa ndani yake Kristo;(1) tumebatizwa kwa yeye, kwa uharibifu wa dhambi, na uzima wa neema;(2) na kwa kujaribu kuishi kwa imani,(3) kuwa na mazungumzo yetu kwa njia ya utakatifu na haki,(4) na kutembea katika upendo wa kindugu, kama kubatizwa kwa Roho mmoja na kwa mwili mmoja. (5) (1) Kor. 2: 11-12; Rumi 6: 4, 6, 11, Rum. 6: 3-5, 1 Kor. 1: 11-13; 6: 23, 4: 11-12; 1 Pet. 3:21 (2) Rum. 6:3-5 (3) Gal. 3:26-27 (4) Rum. 6:22 (5) I Kor. 12:13, 25-27

Sehemu ya IIIC.2.2. Meza ya Bwana

Swali la 168: Meza ya Bwana ni nini? Jibu: Meza ya Bwana ni Sakramenti ya Agano Jipya,(1) ambayo, kwa kutoa na kupokea mkate na divai, kifo cha Kristo kinaonyeshwa; na wale ambao wanashiriki pasi na mawaa hunufaika kiroho kwa mwili na damu ya Kristo;(2) umoja wao na ushirika naye unathibitishwa;(3)na wanashuhudia na kuhuisha shukrani zao,(4) na ushirika wao na Mungu,(5) na upendo wao, kama viungo vya mwili huo wa fumbo.(6) (1) Lk 22:20 (2) Mt. 26: 26-28; 1 Kor. 11: 13-26 (3) 1 Kor. 10:16

167

(4) 1 Kor. 11:24 (5) 1 Kor. 10: 14-16, 21 (6) 1 Kor. 10:17

Swali la 169: Jinsi gani Kristo anataka mkate na divai vitolewe na kupokelewa katika Sakramenti ya Meza ya Bwana? Jibu: Kristo amewateua wahudumu wa Neno lake katika usimamizi wa Sakramenti hii ya Meza ya Bwana. Katika kushirikisha Meza ya Bwana wahudumu huweka wakfu mkate na divai kutoka kwenye matumizi ya kawaida, kwa kutumia maneno ya uanzishwaji wake, kwa shukrani, na sala; kwa kuchukua na kumega mkate, na kuwapa wote wanaoshiriki mkate na divai: ambao kuchukua na kula mkate, na kunywa divai, kwa ukumbusho kwamba mwili wa Kristo ulikuwa amevunjwa na kutolewa, na damu yake ilimwagika kwa ajili yao. (I Kor. 11:2324; Mt. 26: 26-28; Mk 14:22-24; Lk 22:19-20)

Swali 170: Je! Ni jinsi gani wale ambao wanashiriki Meza ya Bwana wanakula mwili na kunywa damu ya Kristo ndani yake? Jibu: Kwa kuwa mwili na damu ya Kristo havipo katika uhalisia wake.(1)Hata hivyo, mkate na divai vipo kiroho kwa imani ya mpokeaji;(2)kwa hiyo, wale ambao wanashiriki kwa usahihi Sakramenti ya Meza ya Bwana hula mwili na damu ya Kristo siyo kimwili bali ni katika hali ya kiroho. Ingawa ni katika hali ya kiroho, mkate na divai vinabaki kuwa ni vitu halisi,(3) lakini kwa imani wanapokea na kutumia katika maisha yao, kwamba Kristo alisulubiwa kwa ajili yao. (4) (1) Mdo 3:21 (2) Mt. 26:26, 28

168

(3) 1 Kor. 11: 24-29 (4) 1 Kor. 10:16

Swali la 171: Je! Ni jinsi gani wale wanaoshiriki Sakramenti ya Meza ya Bwana wanapaswa kujiandaa kabla ya kushiriki? Jibu: Wale wanaopokea Sakramenti ya Meza ya Bwana wanapaswa kujitayarisha, kwa kujichunguza katika;(1)uwepo wao katika Kristo,(2)dhambi zao;(3) ukweli na kipimo cha maarifa yao,(4) imani,(5) toba,(6) upendo wao kwa Mungu na ndugu,(7) huruma kwa watu wote,(8) kusamehe wale ambao wamewafanyia vibaya;(9)nia yao kwa Kristo,(10) na kuhuisha utii wao;(11) na kwa kufanya mazoezi mambo haya,(12)kwa kutafakari sana,(13)na sala zisizokoma.(14) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14)

I Kor. 11:28 II Kor. 13: 5 I Kor. 5: 7; Kut. 12:15 I Kor. 11:29 I Kor. 13: 5; Mt. 26:28 Zek. 12:10; I Kor. 11:31 I Kor. 10: 16-17; Mdo 2: 46-47 I Kor. 5: 8; 11:18, 20 Mt. 5: 23-24 Isa. 55: 1; Yn. 7:37 I Kor. 5: 7-8 I Kor. 11: 25-26, 28; Ebr. 10: 21-22, 24; Zab. 26: 6 I Kor. 11: 24-25 II Nyak. 30: 18-19; Mt. 26:26

Swali la 172: Mtu aliye na wasiwasi ikiwa yupo ndani ya Kristo, au ana mashaka na matayarisho yake, je anaweza kushiriki Meza ya Bwana au la? 169

Jibu: Mtu aliye na wasiwasi ikiwa yupo ndani ya Kristo au ana mashaka na matayarisho yake kwa kushiriki Sakramenti ya Meza ya Bwana; mtu kama huyu anaweza kuwa ameshampokea kwa kweli Kristo, ingawa bado hana uhakika au bado hajahakikishwa;(1) hata hivyo, anapaswa kushughulikia kutokuamini kwake(2)na kutatua shida yake(3)na katika kufanya hivyo, anaweza kushiriki meza ya Bwana, na akishiriki anaweza kuimarishwa.(4) Sakramenti imetolewa hata kwa ajili ya wale dhaifu, na Wakristo wenye mashaka ili watiwe nguvu katika imani yao.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Isa. 1: 10; 1 Yn 5:13; Zab. 77: 1-12; Sura 88; Yona 2: 4, 7 Isa. 54: 7-10; Mt. 5: 3-4; Zab. 31:22; 73:13, 22-23 Fil. 3: 8-9; Zab. 10:17; 42: 1-2, 5, 11 II Tim. 2:19; Isa. 1: 10; Zab. 66: 18-20 Isa. 40:11, 29, 31; Mt. 11:28; 12:20; 26:28

Swali la 173: Je! Mkristo ambaye ana kashfa, lakini anataka kushiriki Meza ya Bwana anaweza kuruhusiwa kushiriki? Jibu: Wote wanaopatikana na kashfa, bila kujali imani zao na nia zao za kutaka kushiriki Meza ya Bwana, Kanisa, kwa mamlaka yaliyotoka kwa Kristo linapaswa kuwazuia kushiriki Meza ya Bwana na kuwatenga(1)hadi hapo watakapopokea maelekezo zaidi au mpaka hapo watapojirekebisha.(2) (1) 1 Kor. Sura. 5; 11: 27-31; Mt. 7:6; Yud. 1: 23; I Tim. 5:22 (2) II Kor. 2:7

Swali la 174: Je! Wale wanaoshiriki Sakramenti ya Meza ya Bwana wanapaswa kufanya nini wawapo katika ibada yenyewe?

170

Jibu: Wale wanaoshiriki Sakramenti ya Meza ya Bwana wakati wa ibada yake wanapaswa kushiriki kwa heshima na utakatifu wote wakimngojea Mungu katika agizo hilo(1) ili washiriki kwa uangalifu na vitendo(2)na kwa kutambua mwili wa Bwana ulioteswa,(3)na kutafakari kwa upendo juu ya kifo chake na mateso yake,(4) na hivyo kuhuzunika juu ya dhambi zao;(5) na kuwa na hamu ya kumfuata Kristo,(6) kula kwake kwa imani,(7)kupokea utimilifu wake,(8) kuamini sifa zake,(9) kufurahi katika upendo wake, (10) kushukuru kwa neema yake;(12) katika kuhuisha agano lao na Mungu, na upendo kwa watakatifu wote.(13)[katika muktadha huu, watoto hawaruhusiwi kushiriki Meza ya Bwana, wala watu ambao wamejulikana kupata shida ya akili] (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13)

Law. 10: 3; Ebr. 12:18; Zab. 5: 7; I Kor. 11:17, 26-27 Kut. 24: 8; Mt. 26:28 I Kor. 11:29 Lk 22:19 Zek. 12:10 Ufu 22:17 Yn 6:35 Yn 1:16 Fil. 1:16 Zab. 63: 4-5; II Nyak. 30:21 Zab. 22:26 Yer. 1: 5; Zab. 1: 5 Mdo 2:42

Swali la 175: Ni nini jukumu la Wakristo baada ya kupokea Sakramenti ya Meza ya Bwana? Jibu: Jukumu la Wakristo baada ya kupokea Sakramenti ya Meza ya Bwana ni kufikiri kwa makini kama wamepata chochote kutoka kwenye Meza ya Bwana,(1) au kama wamehuishwa kiroho 171

baada ya kushiriki. Kumshukuru Mungu kwa ajili ya Sakramenti, (2) kuomba mwendelezo wa Sakramenti,(3)kujilinda na mambo yanayoweza kuwarudisha nyuma,(4) kutimiza viapo vyao,(5)na kujitia moyo wenyewe ili waendelee kuhudhuria mara kwa mara katika Sakramenti,(6)kama wasipoona matokeo yoyote basi wanahitaji kujichunguza katika maandalizi yao(7)kama wanaweza kujithibitisha wenyewe mbele za Mungu na kwa dhamiri zao; basi wanapaswa kusubiri matokeo yake kwa wakati(8)lakini wasipoona matokeo yoyote kwa wakati, basi wanapaswa kujinyenyekeza,(9)na kuhudhuria mara nyingine kwa umakini zaidi na uaminifu.(10) (1) Zab. 28: 7, 85: 8; I Kor. 11:17, 30-31 (2) II Nyak. 30:21-16; Mdo 2:42, 46 (3) Zab. 36:10; Wimb. 3: 4; I Nyak. 29:18 (4) I Kor. 10: 3-5, 12 (5) Zab. 50:14 (6) I Kor. 11: 25-26; Mdo 2:42, 46 (7) Wimb. 5: 1-6; Mhu. 5: 1-6 (8) Zab. 42: 5, 8; 43: 3-5; 123: 1-2 (9) II Nyak. 30: 18-19; Isa. 1:16, 18 (10) II Kor. 7:11; I Nyak. 15: 12-14

Swali la 176: Je! Sakramenti ya Ubatizo na Meza ya Bwana zinakubalianaje? Jibu: Sakramenti ya Ubatizo na Meza ya Bwana zinakubaliana kwa kuwa mwanzilishi wa vyote ni Mungu;(1) sehemu zake za kiroho ni Kristo na faida zake;(2) zote ni mihuri ya agano moja,(3) vinahitaji kufanywa na wahudumu wa injili, na hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kufanya;(4) na vinapaswa kuendelezwa katika kanisa la Kristo hadi kuja kwake mara ya pili.(5) 172

(1) (2) (3) (4) (5)

Mt. 28:19; I Kor. 11:23 Rum. 6: 3-4; I Kor. 10:16 Rum. 4:11; Kol. 2:12; Mt. 26: 27-28 Yn 1:33; Mt. 28:19; I Kor. 4: 1; 11:23; Ebr. 5: 4 Mt. 28: 19-20; I Kor. 11:26

Swali 177: Je! Sakramenti ya Ubatizo na Meza ya Bwana hutofautianaje? Jibu: Sakramenti ya Ubatizo Meza ya Bwana hutofautiana, kwa maana ya kwamba ubatizo unapaswa hutolewa mara moja tu, na kwa maji, kuwa ishara na muhuri wa kuzaliwa upya na kuandikishwa kuwa Wakristo wa kanisa linaloonekana,(1)na kwamba ubatizo hutolewa hata kwa watoto wachanga;(2)Lakini Meza ya Bwana inatolewa mara nyingi na kila mara. Mkate na divai humwakilisha na kumuonyesha Kristo kama lishe ya kiroho kwa roho zetu,(3)na kudhibitisha mwendelezo wetu na ukuaji ndani yake, (4)na kwamba Meza ya Bwana si kwa watoto, bali ni wale wanaoweza kujichunguza wenyewe.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Mt. 3:11; Tit. 3: 5; Gal. 3:27 Mwa 17: 7, 9; Mdo 2: 38-39; I Kor. 7:14 I Kor. 11: 23-26 I Kor. 10:16 I Kor. 11: 28-29

Sehemu ya IIIC.3. Maombi

Swali la 178: Maombi ni nini? Jibu: Maombi ni toleo la matamanio yetu kwa Mungu,(1) kwa jina la Kristo,(2) kwa msaada wa Roho wake;(3) kwa kukiri dhambi zetu,(4) na kwa shukrani na rehema zake.(5) 173

(1) (2) (3) (4) (5)

Zab. 62: 8 Yn. 16:23 Rum. 8:26 Zab. 32: 5-6; Dan. 9: 4 Fil. 4: 6

Swali la 179: Je! Tunapaswa kuomba kwa Mungu peke yake tu? Jibu: Kwa kuwa Mungu ana uwezo wa kuchunguza mioyo yetu: (1) kusikiliza maombi yetu,(2) kusamehe dhambi zetu,(3) kutimiza haja za wote;(4)ni yeye peke yake wa kuaminiwa,(5)na kuabudiwa;(6) maombi ni sehemu maalum,(8) na hivyo maombi yote yaelekezwe kwake na si kwa mwingine. (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

I Fal. 8:39; Mdo 1:24; Rumi 8:27 Zab. 65: 2 Mika 7:18 Zab. 145: 18-19 Rum. 10:14 Mt. 4:10 I Kor. 1: 2 Zab. 50:15

Swali la 180: Nini maana ya kuomba katika jina la Kristo? Jibu: Kuomba katika jina la Kristo ni kutii agizo lake, na kwa imani juu ya ahadi zake;(1) sio kwa kutaja jina lake tu;(2) bali kwa kuteka faraja yetu ya kuomba, kwa ujasiri, na tumaini la kupokelewa kwa maombi yetu kutoka kwa Kristo na huduma yake ya Upatanisho.(3) (1) Yn 14: 13-14, 16:24; Dan. 9:17 (2) Mt. 7:21 174

(3) Ebr. 4: 14-16; 1 Yoh. 5: 13-15

Swali la 181: Je! Kwa nini tunapaswa kuomba kwa jina la Kristo? Jibu: Dhambi zetu zimeshatutenganisha na Mungu kiasi kwamba hatuwezi kupata uwepo wake bila mpatanishi;(1) na kwamba hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyeteuliwa kwa ajili ya kufanya upatanisho, au anayefaa kuwa mpatanishi bali ni Kristo peke yake;(2)hivyo basi, hatupaswi kuomba kwa jina jingine ila jina lake peke yake.(3) Dhambi zetu zimeshatutenganisha na Mungu kiasi kwamba hatuwezi kupata uwepo wake bila mpatanishi kuondoa utengano huo, na hivyo hakuna mtu mbinguni au duniani aliyeteuliwa au anayefaa kwa kazi hiyo tukufu isipokuwa Kristo pekee. (1) Yn. 14: 6; Isa. 59: 2; Efe. 3:12 (2) Yn. 6:27; Ebr. 7: 25-27; I Tim. 2: 5 (3) Kol. 3:17; Ebr. 13:15

Swali la 182: Je! Roho Mtakatifu hutusaidiaje katika kuomba? Jibu: Kwa kuwa hatujui kuomba au kile tunachopaswa kuomba kama itupasavyo, Roho Mtakatifu hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa kutuwezesha kuelewa juu ya nini cha kuomba, na jinsi maombi yanavyopaswa kufanywa na hufanya kazi ya kuhuisha mioyo yetu (ingawa sio kwa watu wote, na wala si kwa wakati wote na kwa kipimo kile kile). (Rum. 8: 26-27; Zab. 10:17; Zek. 12:10)

Swali la 183: Je, tunapaswa kuomba kwa ajili ya akina nani?

175

Jibu: Tunapaswa kuombea kanisa la Kristo duniani;(1)kwa mahakimu,(2)na wachungaji;(3)sisi wenyewe,(4)ndugu zetu,(5)maadui zetu;(6)na kwa watu wa kila aina walio hai,(7)au watakaoishi baadaye;(8)lakini sio kwa wafu,(9)wala kwa wale wanaojulikana kuwa wamefanya dhambi ya mauti.(10) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10)

Efe. 6:18; Zab. 28: 9 I Tim. 2: 1-2 Kol. 4: 3 Mwa. 32:11 Yakobo. 5:16 Mt. 5:44 I Tim. 2: 1-2 Yn. 17:20; II Sam. 7:29 II Sam. 12: 21-23 I Yn. 5:16

Swali la 184: Je, ni vitu gani tunapaswa kuomba? Jibu: Tunapaswa kuomba vitu vyote vinavyoleta utukufu kwa Mungu;(1) vitu ambavyo ni kwa ajili ya ustawi wa kanisa,(2) kwa vitu vyetu(3)au vya wengine;(4)lakini hatupaswi kuomba vitu ambavyo si halali.(5) (1) (2) (3) (4) (5)

Mt. 6: 9 Zab. 51:18, 122: 6 Mt. 7:11 Zab. 125: 4 I Yoh. 5:14

Swali la 185: Je, tunapaswa kuomba vipi? Jibu: Tunapaswa kuomba kwa hofu mbele za ukuu wa Mungu, (1) na kwa hisia nzito kwa kutokustahili kwetu mbele zake,(2) kwa 176

mahitaji yetu,(3)tukiwa na hisia kwa ajili ya dhambi zetu;(4)kwa toba,(5) kwa kushukuru,(6)kwa mioyo iliyoinuliwa kwa Mungu,(7)na kwa ufahamu kamili,(8) kwa imani,(9) kwa uaminifu,(10) kwa bidii,(11) kwa upendo,(12)na kwa uvumilivu,(13)tukimsubiri Bwana,(14)kwa kutii mapenzi yake.(15) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15)

Mh. 5: 1 Mwa 18: 27; 32:10 Lk 15: 17-19 Lk 18: 13-14 Zab. 51:17 Fil. 4: 6 II Sam. 1:15, 2: 1 I Kor. 14:15 Mk. 11:24; Yak. 1: 6 Zab. 17: 1; 145: 18 Yak. 5:16 I Tim. 2: 8 Efe. 6:18 Mik, 7: 7 Mt. 26:39

Swali la 186: Je, Mungu ametoa kanuni gani kama mwongozo kwetu katika jukumu la kuomba? Jibu: Neno la Mungu ndilo linalotuelekeza katika jukumu la kuomba;(1) lakini kanuni maalum ya mwongozo ni yale maombi ambayo Mwokozi Wetu Kristo aliwafundisha wanafunzi wake. Maombi haya yanayojulikana kama, "Sala ya Bwana.” (2) (1) I Yoh. 5:14 (2) Mt. 6: 2-13; Lk. 11: 2-4

Swali la 187: Je, Sala ya Bwana inapaswa kutumikaje? 177

Jibu: Sala ya Bwana sio tu kwamba ni mwongozo, kama kielelezo ambapo kila ombi tunapaswa kufanya kwa njia hiyo; lakini pia inaweza kutumika kama sala, ili kwamba ifanyike kwa ufahamu, imani, heshima na sifa zingine muhimu katika utendaji sahihi wa jukumu la maombi. (Mt. 6: 9; Luka 11: 2)

Swali la 188: Je, Sala ya Bwana ina sehemu ngapi? Jibu: Sala ya Bwana ina sehemu tatu; utangulizi, maombi, na hitimisho

Swali la 189: Je, Utangulizi wa Sala ya Bwana unatufundisha nini? Jibu: Utangulizi wa Sala ya Bwana (wenye maneno haya "Baba yetu uliye mbinguni.")(1)unatufundisha kuwa tunapoomba tunapaswa kumkaribia Mungu kwa ujasiri, juu ya wema wake wa ubaba;(2)na kwa heshima, na hisia kama za watoto,(3)hisia za mbinguni,(4)na kwa hofu ya uweza wake mkuu:(5)pia, kuomba kwa ajili ya wengine.(6) (1) (2) (3) (4) (5) (6)

Mt. 6: 9 Lk 11:13; Rum. 8:15 Isa. 64: 9 Zab. 123: 1; Omb. 3:41 Isa. 63: 15-16; Neh. 1: 4-6 Mdo 12: 5

Swali la 190: Je, tunapaswa kuomba nini katika ombi la kwanza? Jibu: Katika ombi la kwanza (ambalo ni “Jina lako litakaswe (litukuzwe)”) (1) tunapaswa kukiri udhaifu wetu, na kwamba watu wote wanapaswa kumheshimu Mungu,(2)tuombe kwamba Mungu 178

kwa neema yake atuwezeshe kujua, kumkiri, na kuthamini sana,(3) vyeo vyake,(4)sifa zake,(5)maagizo yake,(6)na chochote kile anachopenda kujitambulisha nacho; (7) na kumtukuza kwa mawazo, maneno,(8)na matendo yetu (9) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9)

Mt. 6: 9 II Kor. 3: 5; Zab. 51:15 Zab. 67: 2-3 Zab. 83:18 Zab. 86: 10-13, 15 II Thes. 3: 1; Zab. 138: 1-3; 147: 19-20; II Kor. 2: 14-15 Zab. sura. 8; na sura. 145 Zab. 19: 14; 103: 1 Fil. 1: 9, 11

Swali la 191: Je, tunapaswa kuomba nini katika ombi la pili? Jibu: Katika ombi la pili (ambalo ni “ufalme wako uje,”) (1) tunapaswa kutambua kwamba wanadamu wote kwa asili tuko chini ya utawala wa dhambi na Shetani; (2) tunapaswa kuomba kwamba, ufalme wa dhambi na Shetani uharibiwe, (3) Injili ya Kristo ienezwe ulimwenguni kote;(4) kwa ajili ya kuwabadilisha wale walio dhambini;(5)na kwamba Kristo atawale mioyoni mwetu;(6)na kuharakisha kuja kwake kwa mara ya pili na kutawala pamoja naye milele: (7) (1) (2) (3) (4) (5)

Mt. 6: 10 Efe. 2: 2-3 Zab. 68: 1, 18; Ufu 12: 10-11 II Thes. 3: 1 10. Mdo 4: 29-30; Efe. 6: 18-20; Rum. 15: 29-30, 32; II Thes. 1:11; 2: 16-17 (6) Efe. 3:14-20 (7) Ufu 22: 20

179

Swali la 192: Je, tunapaswa kuomba nini katika ombi la tatu? Jibu: Katika ombi la tatu (ambalo ni, “Mapenzi yako yafanyike hapa duniani, kama ilivyo mbinguni.”) (1)Tunapaswa kukiri kuwa, kwa asili, wanadamu wote sio tu kwamba hatuwezi kabisa kufanya mapenzi ya Mungu,(2)bali pia tunaasi Neno lake,(3)tunanug'unika kinyume na mapenzi yake, (4) na tumeamua kabisa kufanya mapenzi ya miili yetu na ya Ibilisi:(5)tunapaswa kuomba kwamba Mungu aondoe upofu wetu wote,(6)udhaifu,(7) na upotovu wa mioyo;(8) na kwa neema yake atupe uwezo wa kujua, kufanya, na kutii mapenzi yake, (9) kwa unyenyekevu,(10) kwa furaha, (11) kwa uaminifu, (12) kwa bidii, (13) kwa wivu,(14) kwa moyo safi,(15) na kwa uvumilivu, (16) kama malaika wanavyofanya huko mbinguni. (17) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16) (17)

Mt. 6: 10 Rum. 7:18; Ayu. 21:14; I Kor. 2:14 Rum. 8: 7 Kut. 17: 7; Hes. 14: 2 Efe. 2: 2 Efe. 1: 17-18 Mt. 26: 40-41 Yer. 31: 18-19 Zab. 119: 1, 8, 35-36; Mdo 21:14 Mik. 6: 8 Zab. 100: 2; Ayu. 1:21; II Sam. 15: 25-26 Isa. 38: 3 Zab. 119: 4-5 Rum. 12:11 Zab. 119: 80 Zab. 119: 112 Isa. 6: 2-3; Zab. 103: 20-21; Mt. 18:10

Swali la 193: Je, tunapaswa kuomba nini katika ombi la nne? 180

Jibu: Katika ombi la nne (ambalo ni, “Utupe leo liziki yetu.”)(1) Tunapaswa kukiri kwamba, kwa sababu ya dhambi zetu wenyewe tumepoteza haki yetu ya baraka zote za nje za maisha haya, na tunastahili kunyimwa kabisa na Mungu;(2)na kwamba baraka zenyewe haziwezi kutusaidia;(3)Wala hatustahili kuzipata baraka hizi;(4) na zaidi ya hayo, tunavutwa na hamu ya kupata,(5)ili tuzitumie kwa njia isiyo halali. (6) Kwa hiyo, tunapaswa kujiombea sisi wenyewe na wengine;(7)kwa pamoja tusubiri mapenzi ya Mungu kila siku katika matumizi ya njia halali, na bora ya vitu tunavyopewa. (8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mt. 6:11 Mwa. 2:17, 3:17; Rum 8: 20-22; Yer. 5:25; Kumb. 28: 15-68 Kumb. 8: 3 Mwa 32:10 Kumb. 8: 17-18, Yer. 6:13; Mk 7: 21-22 Hos. 12: 7 Yak. 4: 3 Mwa 28:20; 43: 12-14; Efe. 4:28; II Thes. 3: 11-12; Fil. 4: 6

Swali la 194: Je, tunapaswa kuomba nini katika ombi la tano? Jibu: Katika ombi la tano (ambalo ni, “Utusamehe deni zetu, kama tunavyowasamehe wadeni wetu.”) (1) Tunapaswa kukiri kwamba tuna hatia ya dhambi ya asili na dhambi za kutenda, na hivyo tunakuwa na deni kwa haki ya Mungu; na kwamba sisi, wala kiumbe chochote kingine, hatuwezi hata kidogo kulipa deni hilo:(2) kwa hiyo tunapaswa kujiombea sisi wenyewe, na wengine, kwamba, Mungu kwa neema yake ya bure, kupitia utii wa Kristo, atuondolee sisi hatia na adhabu ya dhambi;(3)atukubali katika Mpendwa wake Kristo;(4) na aendeleze neema yake ndani yetu,(5)na atusamehe makosa yetu ya kila siku,(6)na utujaze amani na furaha, kwa kutupatia kila siku uhakikisho wa 181

msamaha;(7)ambao tunaomba huku tukiwa na ushuhuda ndani yetu pia kutoka mioyoni mwetu kwamba tumewasamehe wengine makosa yao.(8) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8)

Mt. 6:12 Rum. 3: 9-22; Mt. 18: 24-25; Zab. 130: 3-4 Rum. 3: 24-26; Ebr. 9:22 Efe. 1: 6-7 II Pet. 1: 2 Hos. 14: 2; Yer. 14: 7 Rum. 15:13; Zab. 51: 7-10, 12 Lk 11: 4; Mt. 6: 14-15; 18: 35

Swali la 195: Je, tunapaswa kuomba nini katika ombi la sita? Jibu: Katika ombi la sita (ambalo ni, “Na usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.”) (1) Tunapaswa kukiri kwamba Mungu mwenye busara, haki, na neema; kwa madhumuni ya haki takatifu anaweza kutayarisha mazingira ambayo huwa shabaha ya majaribu. (2)Kwamba Shetani,(3)ulimwengu,(4)na mwili, viko tayari kwa nguvu kutuweka kando na kutunasa;(5)na kwamba sisi, hata baada ya msamaha wa dhambi zetu, kwa sababu ya ufisadi wetu,(6) na udhaifu, (7)vinaweza kusababisha tujaribiwe,(8)na sisi wenyewe hatuna uwezo wa kupinga majaribu hayo, (9) na tunastahili kuachwa chini ya nguvu ya majaribu.(10)Hivyo basi, tunahitaji kumwomba Mungu aweze kuongoza ulimwengu na vyote vilivyomo,(11) kwa ajili ya kushinda mwili,(12)na kumzuia Shetani,(13)na kwamba Mungu atusaidie tuweze kushinda majaribu ya dhambi;(14)au, pindi tujaribiwapo, Roho wake aweze kututia nguvu; (15) au pindi tuangukapo, tuinuliwe tena;(16) na kuwa na nguvu baada ya majaribu:(17) ili utakaso wetu na wokovu wetu ukamilike, (18) na Shetani akanyagwe chini ya miguu yetu,(19) na

182

kuwa huru kabisa kutoka kwenye dhambi, majaribu, na maovu yote, milele. (20) (1) Mt. 6:13 (2) II Nyak. 32:31 (3) I Nyak. 21: 1 (4) Lk. 21:34; Mk 4:19 (5) Yak. 1:14 (6) Gal. 5:17 (7) Mt. 26:41 (8) Mt. 26: 69-72; Gal. 2: 11-14; II Nyak. 18: 3; 19: 2 (9) Rum. 7: 23-24; I Nyak. 21: 1-4; II Nyak. 16: 7-10 (10) Zab. 81: 11-12 (11) Yn 17:15 (12) Zab. 51:10; 119: 133 (13) II Kor. 12: 7-8 (14) Mt. 26:41; Zab. 19:13 (15) Efe. 3: 14-17; I Thes. 3:13; Yud. 1:24 (16) Zab. 51:12 (17) I Pet. 5: 8-10 (18) II Kor. 13: 7, 9 (19) Rum. 16:20; Zek. 3: 2; Luka 22: 31-32 (20) Yn. 17: 15; I Thes. 5:23

Swali la 196: Je! hitimisho la Sala ya Bwana linatufundisha nini? Jibu: Mwisho wa Sala ya Bwana (ambao ni, “Kwa maana ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.”(1)Maneno haya yanatufundisha kupeleka maombi yetu kwa hoja.(2) Hoja zinapaswa kupelekwa kwa Mungu;(3)na kwamba katika maombi yetu tunaungana katika sifa,(4)kwa Mungu wa milele, mwenye nguvu zote.(5) Kwa heshima hiyo, kwa kadiri ya uwezo na utayari wake wa kutusaidia,(6)imani yetu inatufanya tuwe na ujasiri 183

kumsihi kwamba atusaidie(7)na kwa utulivu tunategemea kujibiwa maombi yetu..(8) Kwa kushuhudia kuwa tunataka kusikilizwa, na kuwa na ujasiri kwamba Mungu amesikia maombi yetu, tunasema Amina.(9) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9)

Mt 6.13. Rum 15:30, Ayu. 23.3-4, Yer 14.20-21. Dan 9.4,7-9,16-19. Fil. 4.6. 1 Nyak 29.10-13. Efe 3.20-21, Lk 11.13, Zab 84.11. II Nyak. 20.6,11, Efe 3.12, Ebr 10.19-22. II Nyak. 14.11, 1 Yn 5.14, Rum 8.32. I Kor 14.16, Ufu. 22.20-21.

________________ꭥ_________________

184

Viambatisho 1. Imani ya Mitume Namwamini Mungu Baba Mwenyezi, Muumba wa Mbingu na Nchi, Na Yesu Kristo Mwana Wake Pekee, Bwana Wetu, aliyechukuliwa mimba kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu, Akazaliwa na Bikra Mariamu, Akateswa zamani za Pontio Pilato, Akasulubiwa, Akafa, Akazikwa, Akashuka mahali pa wafu, siku ya tatu Akafufuka, Akapaa mbinguni, Ameketi mkono wa Kuume wa Mungu Baba Mwenyezi, Kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu. Namwamini Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu lililo moja, Ushirika wa Watakatifu, Ondoleo la dhambi, kiyama ya mwili na uzima wa milele. Amina.

2. Imani ya Nikea (AD 325) Tunamwamini Mungu mmoja Baba, Mwenyezi, Muumba wa Mbingu na Nchi, na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Tunamwamini Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, mzaliwa wa milele wa Baba, Mungu kutoka kwa Mungu, Nuru kutoka kwa Nuru, Mungu wa kweli kutoka kwa Mungu wa kweli, aliyezaliwa, lakini hakuumbwa, ni nafsi moja na Baba. 185

Kupitia yeye vitu vyote viliumbwa. Kwa ajili yetu na kwa ajili ya wokovu wetu alishuka kutoka mbinguni; kwa nguvu za Roho Mtakatifu alichukua mwili kutoka kwa Bikira Mariamu, na akafanywa mwanadamu. Kwa ajili yetu alisulubiwa chini ya Pontio Pilato; akafa na akazikwa. Siku ya tatu akafufuka tena kama yasemavyo Maandiko; akapaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Baba. Atakuja tena

katika utukufu kuhukumu walio hai na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho. Tunamwamini Roho Mtakatifu, Bwana, mpaji wa uzima, ambaye anatoka kwa Baba na Mwana. Pamoja na Baba na Mwana huabudiwa na kutukuzwa. Amezungumza kupitia Manabii. Tunaamini kanisa moja, takatifu, la ulimwenguni pote, na la kitume. Tunakubali ubatizo mmoja kwa msamaha wa dhambi. Tunatazamia ufufuo wa wafu, na maisha ya ulimwengu ujao.

3. Sala ya Bwana Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni, utupe leo riziki yetu, utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea, usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu na hata milele. Amina.

4. Amri Kumi (Kut. 20:1-17) 1. Usiwe na miungu mingine ila Mimi. 2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga. 3. Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako. 186

4. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 5. Waheshimu baba yako na mama yako. 6. Usiue. 7. Usizini 8. Usiibe. 9. Usimshuhudie jirani yako uongo. 10. Usitamani…cho chote alicho nacho jirani yako.

187