UMASKINI NA UTAJIRI: KATIKA MAWANDA MAPANA YA KITEOLOJIA [1, 1 ed.]

Kitabu hiki kwa mara ya kwanza nilikiandika mwaka 2017 katika lugha ya Kiingereza na kilichapiswa katika mtandano wa Ama

873 202 846KB

Kiswahili Pages 155 Year 2021

Report DMCA / Copyright

DOWNLOAD FILE

Polecaj historie

UMASKINI NA UTAJIRI: KATIKA MAWANDA MAPANA YA KITEOLOJIA [1, 1 ed.]

Table of contents :
Yaliyomo
TABARUKU 0
UTANGULIZI 1
SURA YA KWANZA 6
Kwa nini Tuzungumzie mafanikio yanayolenga umasikini na utajiri? 6
Msingi wa kitheolojia kuhusu masuala ya uchumi 13
Nini dhana ya utajiri na umaskini katika jamii tofauti tofauti? 17
Maana halisi ya utajiri kwa mujibu wa maandiko Matakatifu 19
Utajiri ni nini? 20
SURA YA PILI 28
Je Hali Ya Kiuchumi Ya Watu Imetayarishwa? (Predestined?) 28
Je Mipango yetu ya Baadaye Inathirika Vipi Na Dhana Hii ya Kutayarishwa Mapema? 34
Agano la Mungu na Adamu 37
Agano la Mungu na Ibrahim 38
Agano la Waisrael na Mungu (au Agano la Musa) 41
SURA YA TATU 49
Ingawa Mungu Anajua, Lakini Kupanga Ni Kazi Yako Ili Ufikie Malengo Yako 49
Mambo ya kufanya unapotengeneza kesho yako 51
Tengeneza Jina Lako Kwanza Mw. 12:2 51
Chochote Kile Unachokimiliki Hakikisha Kwamba Umekigharimia 54
Usijaribu kuishi maisha yanayokuzidi. I Tim 6:6 57
Thamini kidogo kinachopita mikononi mwako. Yoh. 6:8-12 58
SURA YA NNE 60
Umaskini ni nini? 60
Chanzo cha umaskini 69
Kutokumtii Mungu 69
Kwa sababu ya kudhulumiwa 71
Kwa sababu ya uzembe 74
Mungu anakupima na kukuthibitishia kama utamwacha au hutamwacha 77
Mungu anakutambulisha kwa Shetani 84
Umaskini mwingine ni matatizo ya kiroho tu 85
Magonjwa yaweza kuwa chanzo cha umasikini. 91
Madeni sugu husababisha umasikini usio na kifani. 93
Ulevi kupindukia 98
Sababu mchanganyiko 105
Ni kweli kufa maskini ni ufala? 106
SURA YA TANO 109
Je Kuna Tumaini Lolote La Kutoka Katika Nje? 109
Tufanyaje Sasa 110
Wajibu wa Serikali kuwasaidia masikini 111
Kwa Wanaotaka Kuajiriwa na Walioajiriwa tu 113
1) Hakikisha unakidhi vigezo vya kazi unayotafuta 114
2) Usiwe Mtu wa Kukata Tamaa Mapema 115
3) Uwe jasiri na Ujiamini 116
4) Kubali Ushindani 117
5) Taja moja kwa moja kazi unayotaka kufanya 117
6) Uwe muwazi/ usiwe mwongo 118
7) Kuwa na wapendekezaji wa kuaminika (Referees) 119
8) Omba kazi sehemu nyingi/usiombe kazi sehemu moja tu 120
9) Usilazimishe kupata kazi 120
10) Mwonekano Wako Uwe wa Kuvutia 121
11) Jiajiri mwenyewe ili uwe mwajiri 121
Mbinu za kuilinda kazi yako 122
1) Kuwa na bidii katika kazi 123
2) Epuka kuwa kikwazo kazini 123
3) Epuka Majungu 124
4) Usijaribu kugoma au kushawishi wengine wagome 124
5) Kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzako 125
6) Epuka mapenzi kazini ila uwe na mapenzi na kazi yako 125
7) Usiwe na Mawazo ya Kutafuta Kazi sehemu nyingine 126
8) Usipokee Simu Mbele ya Bosi wako 127
9) Ombea Kazi yako kila siku 128
10) Toa zaka 90% kwa mara ya kwanza na baadaye 10% 129
11. Ongeza Ujuzi wa kazi yako 131
SURA YA SITA 132
Funguo Nne 132
Fungu 1 133
Sawazisha mtazamo wako kuhusu Mungu 133
Fungu 2 137
Tambua mambo ambayo unayoyaweza na yale usiyoyaweza 137
Funguo 3 139
Tambua watu ambao Mungu amewaandaa kwa ajili yako 139
Funguo 4 145
Epuka uchoyo na tamaa ya mali 145
Mwisho 150

Citation preview

UMASKINI NA UTAJIRI

KATIKA MAWANDA MAPANA YA KITEOLOJIA

DANIEL.J. SENI 2

Hakimiliki © 2021 Daniel John Seni Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kuzalishwa tena, au kuboreshwa au kusambazwa kwa njia yoyote au kwa kubadilisha umbo au kunakili na kupeleka katika umbo lingine bila idhini ya maandishi ya mchapishaji, isipokuwa kwa nukuu fupifupi kwa matumizi yasiyo ya kibiashara. Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV). Tafsiri iliyotumika kwenye marejeleo yaliyokuwa kwenye lugha ya kiingereza si tafsiri rasmi; hivyo inaweza kuendelea kuboreshwa kwa kila toleo la kitabu hiki. ________________________

Msambazaji Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam

TABARUKU

Kwa Wazazi mke wangu mpenzi, Esther Cassian.

UTANGULIZI Kitabu hiki kwa mara ya kwanza nilikiandika mwaka 2017 katika lugha ya Kiingereza na kilichapiswa katika mtandano wa Amazon Kindle. Pia nakala ngumu yake inapatikana kwa kuagiza kupitia amazon. Kichwa chake kwa Kiingereza kinaitwa, “THE SCHOOL of POVERTY AND RICHES: A New Hope to the Desperate World. Niliamua kukiandika kwa Kiswahili ili kuruhusu watu wengi kusoma na kuelewa vizuri dhana ya Umaskini na Utajiri; tumaini jipya kwa ulimwengu unaopotoka. Utakubaliana nami kwamba katika ulimwengu huu dhana ya maskini na wanyonge imetawala kiasi kwamba kuwa mnyonge au maskini imekuwa kama ni heshima fulani hivi. Vivyo hivyo, watu kuwa matajiri siku hizi wanahofia kwa kuogopa kwamba pengine labda watu wanafikiri nimewapoka mali zao ndiyo maana nimekuwa tajiri. Yawezekana pia ukakubaliana nami kwamba maskini wengi wamekuwa mitaji ya mitume na manabii; kwa maana ya kwamba maskini wengi ndio ambao huenda kuombewa na kuangushwa na mapepo; (eneo hili bado tunatafiti uhusiano kati ya umaskini na kuangushwa na pepo) lakini huo ndio ukweli. Katika kitabu hiki, nimejadili kwa undani masuala ya umasikini na utajiri kwa kuzingatia muktadha wetu, lakini vilevile nimechukua dhana ya kutangulia kuchaguliwa na kuijadili kwa undani ili kuona kama hatima ya umaskini na utajiri imeamuriwa na Mungu. Karibu tujifunze pamoja

Daniel John Seni Januari 2021 1

Yaliyomo TABARUKU ...................................................................0 UTANGULIZI .................................................................1 SURA YA KWANZA ........................................................6 Kwa nini Tuzungumzie mafanikio yanayolenga umasikini na utajiri?6 Msingi wa kitheolojia kuhusu masuala ya uchumi .................... 13 Nini dhana ya utajiri na umaskini katika jamii tofauti tofauti? ......17 Maana halisi ya utajiri kwa mujibu wa maandiko Matakatifu .......19 Utajiri ni nini? ................................................................ 20 SURA YA PILI ......................................................................................28 Je Hali Ya Kiuchumi Ya Watu Imetayarishwa? (Predestined?) .............28 Je Mipango yetu ya Baadaye Inathirika Vipi Na Dhana Hii ya Kutayarishwa Mapema? ................................................................................................34 Agano la Mungu na Adamu....................................................................37 Agano la Mungu na Ibrahim ...................................................................38 Agano la Waisrael na Mungu (au Agano la Musa) ................................41

SURA YA TATU ................................................................. 49 Ingawa Mungu Anajua, Lakini Kupanga Ni Kazi Yako Ili Ufikie Malengo Yako ................................................................... 49 Mambo ya kufanya unapotengeneza kesho yako ....................... 51 Tengeneza Jina Lako Kwanza Mw. 12:2 ................................. 51 Chochote Kile Unachokimiliki Hakikisha Kwamba Umekigharimia54 Usijaribu kuishi maisha yanayokuzidi. I Tim 6:6 ...................... 57 2

Thamini kidogo kinachopita mikononi mwako. Yoh. 6:8-12 ........ 58 SURA YA NNE......................................................................................60 Umaskini ni nini?....................................................................................60 Chanzo cha umaskini ..............................................................................69

Kutokumtii Mungu .............................................................. 69 Kwa sababu ya kudhulumiwa .................................................................71 Kwa sababu ya uzembe ..........................................................................74 Mungu anakupima na kukuthibitishia kama utamwacha au hutamwacha77 Mungu anakutambulisha kwa Shetani ....................................................84 Umaskini mwingine ni matatizo ya kiroho tu.........................................85 Magonjwa yaweza kuwa chanzo cha umasikini. ....................................91 Madeni sugu husababisha umasikini usio na kifani. ..............................93 Ulevi kupindukia ....................................................................................98 Sababu mchanganyiko ..........................................................................105 Ni kweli kufa maskini ni ufala? ............................................................106

SURA YA TANO............................................................... 109 Je Kuna Tumaini Lolote La Kutoka Katika Nje? ..................... 109 Tufanyaje Sasa......................................................................................110 Wajibu wa Serikali kuwasaidia masikini ..............................................111 3

Kwa Wanaotaka Kuajiriwa na Walioajiriwa tu ....................................113 1)

Hakikisha unakidhi vigezo vya kazi unayotafuta .........................114

2)

Usiwe Mtu wa Kukata Tamaa Mapema .......................................115

3)

Uwe jasiri na Ujiamini ..................................................................116

4)

Kubali Ushindani ..........................................................................117

5)

Taja moja kwa moja kazi unayotaka kufanya ...............................117

6)

Uwe muwazi/ usiwe mwongo.......................................................118

7)

Kuwa na wapendekezaji wa kuaminika (Referees) ......................119

8)

Omba kazi sehemu nyingi/usiombe kazi sehemu moja tu ............120

9)

Usilazimishe kupata kazi ..............................................................120

10) Mwonekano Wako Uwe wa Kuvutia ............................................121 11) Jiajiri mwenyewe ili uwe mwajiri.................................................121

Mbinu za kuilinda kazi yako ............................................... 122 1)

Kuwa na bidii katika kazi .............................................................123

2)

Epuka kuwa kikwazo kazini .........................................................123

3)

Epuka Majungu.............................................................................124

4)

Usijaribu kugoma au kushawishi wengine wagome .....................124

5)

Kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzako ................125

6)

Epuka mapenzi kazini ila uwe na mapenzi na kazi yako ..............125

7)

Usiwe na Mawazo ya Kutafuta Kazi sehemu nyingine ................126 4

8)

Usipokee Simu Mbele ya Bosi wako ............................................127

9)

Ombea Kazi yako kila siku ...........................................................128

10) Toa zaka 90% kwa mara ya kwanza na baadaye 10% ..................129 11. Ongeza Ujuzi wa kazi yako ............................................................131

SURA YA SITA ................................................................ 132 Funguo Nne .................................................................... 132 Fungu 1 .................................................................................................133 Sawazisha mtazamo wako kuhusu Mungu ...........................................133 Fungu 2 .................................................................................................137 Tambua mambo ambayo unayoyaweza na yale usiyoyaweza ..............137 Funguo 3 ...............................................................................................139 Tambua watu ambao Mungu amewaandaa kwa ajili yako ...................139 Funguo 4 ...............................................................................................145 Epuka uchoyo na tamaa ya mali ...........................................................145 Mwisho .................................................................................................150

5

SURA YA KWANZA Kwa nini Tuzungumzie mafanikio yanayolenga umasikini na utajiri? Imewahi kusemwa kuwa “Maisha ni safari kati ya muda mfupi wa uchi: wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa.1” Chagamoto ipo hapa katikati; kati ya kuzaliwa….na kifo…hapa ndipo ugomvi na utata ulipo. Siku ya kuzaliwa kwako, huwezi kujua. Kama ilivyo siku ya kufa kwako wewe hujui. Lakini matukio yote hayo usiyoyajua kuna watu wengine wanahusika nayo kuyashughulikia. Popote pale palipo na kanisa, pana Yesu, popote pale palipo na Yesu pana kanisa! Serikali za duniani zinapokuwa zimeshindwa kutatua matatizo ya kiuchumi-kanisa halishindwi kuwahudumia watu wake kimwili na kiroho ili watoke katika hali yao mbaya. Popote pale ambapo kanisa linatambua nafasi yake, masikitiko na majonzi hupungua sana. Ni taasisi gani inaweza kuleta matumaini kwa watu walio katika hali duni? Ni kanisa peke yake! Kanisa limepewa kazi maalumu na Mungu. Kanisa halikumbatii watu wenye hali duni tu, bali hata walio katika hali ya kawaida na matajiri. Kanisa ni sehemu iliyo salama kwa ajili ya ulinzi 1

John Stott kama alivyonukuliwa na Wright, Christotopher J. H. Sweeter than Honey. Langham. Uk.221

6

wa mali za matajiri, naam, kanisa pia ni sehemu salama ya upatikanaji wa maisha bora kwa watu walio katika hali ya chini. Makundi haya yote yanaposimama mbele za Mungu kanisani; yanakuwa kitu kimoja kabisa! Mojawapo ya misheni ya kanisa ni kuwahudumia watu wa kila tabaka; kimwili na kiroho. Matabaka duniani hayawezi kuisha, ila kuna kupungua tu kwa matabaka hayo. Kwa nini? msikilize ndugu huyu anavyodai: Utandawazi umeweka tofauti kubwa kati ya tajiri na maskini, na kama hali ya maskini wengi duniani inavyosababishwa, kuna haja kubwa zaidi ya kuelewa zawadi na changamoto ya imani ya Kikristo katika kipindi hiki kutokana na mazingira ya maskini na jamii zilizotengwa.2 Katika kambi ya “makanisa ya matengenezo (Reformed Churches)”3 katika kipindi hiki, ukiachilia mbali wale watangulizi wetu,

2

Holman, Susan R. The Hungry Are Dying: Beggars and Bishops in Roman Cappadocia. Oxford Studies in Historical Theology. Oxford; New York: Oxford University Press, p. 13, 2001. 3

Ni tawi kubwa la Kiprotestanti ambalo linafuata mila ya kidini na aina za mafundisho ya Kikristo ya John Calvin wakati wa matengenezo. Katika kipindi cha matengenezo kulitokea kambi kuu mbili: waprotestanti, kambi hii inajumuisha Walutheri (Martin Luther), Makanisa ya matengenezo (reformed churches) (mtangulizi wake ni Zwingli

7

sijaona mtu anayesimama na kuanza kutetea kwa nguvu zote mafundisho ya “mafanikio na utajiri.” (masuala ya uchumi). Lakini unaweza kushangaa kwamba kambi

hii

hujinasibu

kufundisha

mafundisho thabiti ya neno la Mungu, jambo ambalo ama kwa hakika ninakubaliana nalo kwa sababu mimi pia nimo katika kambi hii. Lakini hatari kubwa ya kambi hii ni kwamba, mtu yeyote ambaye ameonekana akifundisha mafundisho ya “mafanikio na utajiri” basi anabambikwa jina la “huyu anahubiri injili ya utajirisho” au “huyu anafundisha mafundisho ya uongo.” Mwishowe waumini wamekuwa hawaelewi ni msimamo upi wasimamie kuhusu masuala haya. Labda kuna kitu ambacho nataka niwakumbushe wana matengenezo wenzangu, John Calvin alipofanya matengenezo ya kanisa kule Geneva, hakuwahi kusema kwamba hapa ndipo matengenezo yameishia. Kwa misingi hiyo ni kwamba kanisa linahitaji kuwa na matengenezo kila siku. Kama kanisa litalala na kutegemea jadi ya matengenezo ya zamani, basi kanisa hilo haliwezi kufaa kwenye

lakini aliyekuja kuweka msimamo ni John Calvin), n ahata Anglican nao waliingia kwenye kundi la protestanti. Kambi nyingine ya Roman Catholic. John Calvin ndiye anayeaminika kuweka misingi na mafundisho ambayo ukristo wa leo unayafuata kwa kiasi kikubwa ingawa wao wenyewe. Katika maeneo mbalimbali katika karne ya 16 na 17 makanisa haya yalijulikana kama makanisa ya matengenezo. Au Reformed Churches.

8

tamaduni zingine kwa sababu kanisa linahitaji kupokelewa na tamaduni tofauti tofauti, na injili inayohubiriwa lazima iwasaidie watu watoke katika shida zao zinazowasumbua kila siku. Changamoto inayokabili makanisa yetu ni kwamba tunajinasibu kufundisha mafundisho ya kweli ya neno la Mungu, jambo ambalo ndio msingi wetu-lakini tusisahau kwamba neno hilo hilo la Mungu lina kila kitu kwa ajili ya maisha ya kila siku ya watu. Kwa sababu hiyo, mchungaji haiwezekani anafundisha toba kuanzia Januari mpaka Desemba, halafu mwaka unaofuata anafundisha imani nk. Professor Yoon Min alipokuwa akifundisha somo “pastoral ministry” aliwahi kukaza kwamba ni lazima makanisa yetu yaweze kuwa na kitu kinachoitwa

“balanced

teachings”

yaani

mafundisho

ambayo

hayajaegemea upande mmoja tu, yaani siyo kwamba wewe kila siku mahubiri yako ni uponyaji tu, au si kila siku mahubiri yako ni utoaji tu, siyo kwamba mahubiri yako ni toba, nk.

Alisisitiza kwamba kama

kanisa haliwezi kuwasaidia watu wanaokuja kuabudu, basi halifai kuwepo hapo. Na hitimisho lake ilikuwa ni kwamba tunapoanzisha makanisa lazima tujue kwamba hayo ni makanisa ni kwa ajili ya watu wasioamini ili waje waamini. Stott aliwahi kusema kuwa wahubiri wa Injili lazima wawe makini sana kuangalia mahitaji ya watu, kwani kuna mahitaji mengi ambayo wanahitaji, na wakati wanapokuja kanisani 9

hawawezi kunyamaza tu bali wanataka kujua kuwa “je kuna neno lolote kutoka kwa Bwana”4 kuhusu hali yao? Kama hakuna neno lolote kutoka kwa Bwana huondoka mioyo yao ikiwa imenyong’onyea sana. Watu wanahangika katika masuala ya uchumi na maisha kwa ujumla, kama tukihubiri neema, ni vyema na ndio msingi wetu wa imani. Msomi mmoja wa masuala ya theologia aliwahi kuuliza maswali haya “Je! ina maana gani kuhubiri kuhesabiwa haki kwa neema katika ulimwengu ambao unasagwa na umaskini? Ni kwa vipi kuhesabiwa haki kunaweza kutangazwa tu katikati ya mataifa yaliyogubikwa na masuala magumu ya kiuchumi? 5 sawa wanapokea lakini bado wanakuambia “mchungaji nataka nikale” utamwambia “kafanye kazi” na utanukuu andiko kwamba “asiyefanya kazi asile” lakini anakwambia “sina kazi” au anakuambia “nitafutie kazi.” Lengo la kuwepo kwa makanisa ni kwamba watu ambao wana mizigo mizito katika maisha yao waweze kuingia. Sasa mojawapo ya mizigo mizito ni hali mbaya ya maisha ambayo inawasumbua hao watu.

4

Stott, John. The challenge of Preaching. Cumbria: Langham Preaching Reasorces. 2013, p.51 5

Bieler, Andrea, and Hans-Martin Gutmann. Embodying Grace: Proclaiming Justification in the Real World. American ed. Minneapolis, MN: Fortress Press, 2010. (nyuma ya kitabu)

10

Matokeo yake ndani ya makanisa kumekuwepo na watu walewale wanaokuja kusali, tena wanavumilia tu kwa sababu wewe mchungaji pengine wanakuhurumia lakini kwa kweli wanatamani kuhamia sehemu nyingine ambako roho zao zitapata ahueni. Kwa hiyo nimekusudia kufundisha somo hili kupitia kitabu hiki ili niweze ku-balance (sawazisha vizuri) mafundisho yetu. Mimi binafsi katika eneo langu la uchungaji sipendi watu wanihurumie, kama siwezi kuwapa kile ambacho mioyo yao inataka kupata ili itulie-basi niwape kibali cha kuhama bila kinyongo. Kwa nini mimi niwe chanzo cha wao kutokuwa na furaha na amani? Lakini naamini kwamba huyu Yesu tunayemhubiri, yeye ni kila kitu. Nilipokuwa ninaandaa kauli mbinu yangu ya “Neno halisi, Injili halisi na Uhuru halisi” nilijikuta najiuliza maswali mengi sana. Mojawapo ya maswali hayo ilikuwa ni kwamba, je ni kwa kiwango gani Neno na Injili vinaweza kumweka mtu akawa huru kweli kweli? Huu uhuru ni wa kiroho tu au na wa kimwili pia? Hivyo basi kitabu hiki pia kinaweza kuwa ni sehemu ya kauli mbiu ambayo nimeisisitiza kila kukicha kwamba watu wanahitaji kuwa huru kweli kweli. Na hakuna kitu kingine ambacho kinaweza kuwaweka huru zaidi ya Yesu Kristo anayehubiriwa kupitia Neno halisi na Injili halisi. Tunapaswa kujua kwamba kama watu tusipowafundisha njia sahihi za kiuchumi za 11

kuweza kujikimu katika maisha yao, shetani yuko tayari kuwafundisha na mwoshowe itakuwa ni uangamivu katika maisha yao. Binafsi nimechukua mtazamo wa Jones, Scott J., na Bruce R. Ough waliowahi kusema kwa nia moja kuwa “Utajiri na umasikini ni masuala ya muhimu wa kujadiliwa katika maisha na mawazo ya kanisa.”6 Mjadala huu lazima ulenge kuwasaidia wale ambao ni matajiri wa sasa, ili kupitia utajiri wao waweze kumtukuza Mungu, lakini pia uwawezeshe wale ambao kwa sasa maisha yao yako katika uchungu wa hali ya umasikini ili waweze kuondokana na hali hiyo kama inawezekana kuwa hivyo. Abraham Lincolin aliwahi kusema kuwa “huwezi kumsaidia masikini kwa kumwangamiza tajiri,” 7 kwa hiyo jamii pamoja na kanisa kwa ujumla tunahitaji kitu kinachoitwa “harmonization” ya hali hii. Hatuwezi kuendelea kuona jamii ikiishi katika mazingira magumu, halafu sisi tunajinasibu kwamba tunapiga gombo la kuwapeleka mbinguni lakini hali zao ni mbaya.

6

Jones, Scott J., and Bruce R. Ough. The Future of the United Methodist Church: Seven Vision Pathways Nashville Tenn: Abingdon Press, 2010. 7

Raymond, Henry J. (2006). History of the Administration of President Lincoln. City: Scholarly Publishing Office, University of Michigan Library.

12

Msingi wa kitheolojia kuhusu masuala ya uchumi Kwa mujibu wa John Calvin, sio imani tu na kanisa ambavyo huleta upya katika maisha kupitia neno la Mungu bali ni vipimo vyote vya maisha ya kila siku vinajumuishwa katika mchakato huu wa upya.8 Kwa sababu hiyo, Ukalivinitist umeonekana kuwa ni chanzo kikubwa cha ushawishi katika jamii kwa ajili ya kufanya maendeleo ya pande zote katika maisha ya mwanadamu. Yaani kimwili na kiroho. Kusudi la kazi ya Mungu ni mwanadamu kuwa huru kabisa, jambo ambalo ni ishara ya kuwepo kwa ukristo wa kweli. Kanisa la Yesu Kristo liko katika ulimwengu ambapo umaskini na utajiri, vinakuwepo. Kazi ya kanisa tangu hapo mwanzo ulimwenguni ilidumu katika kuhudumiana, kwa mana ya Diakonia (Huduma ya Kikristo kijamii), na hii ilitumiwa na kutano katika kanisa la kwanza, nayo ndiyo ilikuwa ishara ya kanisa kuijali jamii (au kujaliana kila mmoja). Maswali ya kiuchumi yana nafasi yake kubwa katikati ya imani ya Kikristo na ni mada muhimu katika theolojia ya kibiblia. Agano la Kale tayari linahusika na maswali ya kiuchumi kama vile, sheria ya majukumu, riba, mikopo na uharibifu, hata vigezo vya kushughulika

8

Matthias Freudenberg, Economic and social ethics in the work of John Calvin. 2009 (Makala)

13

masuala ya uchumi na hukumu (tazama Kutoka 22, Kumbukumbu 24). Kwa njia hii jumuiya ya kijamii na kidini ya Waisraeli ilipaswa kuzingatia kwa umakini sana. Moja ya sheria za msingi za kiuchumi ilikuwa ni kuanzishwa kwa Mwaka wa Yubilee au Mwaka wa Sabato (Walawi 25; Dt 15). Hii ilihusu msamaha wa madeni yote kwa vipindi vya kawaida ili kuzuia mkusanyiko wa utajiri au madeni kwa watu wengine. Katika Biblia uchumi unaonekana kujikita kwenye mtazamo wa umasikini na kuwepo kwa tabaka la watu wanaoishi katika mahitaji ya kiuchumi. Watu masikini wana haki yao ya msingi (Am 2: 6) nao wanaweza pia kutarajia kutendewa vyema na jamii inayowazunguka (Isaya 58: 1-12; 61: 1-11) pamoja na kupunguziwa mzigo mkubwa walio nao (Kutoka 22:2423:10–11; Lawi, 5:7–13; Kumb. 23:20–21; 24:19–22; Neh 5:1–13). Maandiko haya yote yanajaribu kuelezea tu suala la uchumi katika maandiko, haielezi kwa nini kuna masikini ingawa sababu za utajiri zinajibainisha. Mungu alikuwa ameshatoa utaratibu wake wa namna watu wake wanavyoweza kubarikiwa katika nchi ya ahadi lakini ghafla tunaona kundi la masikini wakiwepo, na hapo tunamwona Mungu anaanza kushughulika na kundi hili. Kwa mujibu wa ushahidi wa Agano Jipya, Yesu alichukua dhana ya Mwaka wa Yubile (Lk 4:19). Agano Jipya limesisitiza ujumbe wa Yesu kwa maskini (Mt 11: 5, 25:40, Lk 4:18; 16: 19-31; 18: 18-27), na 14

pia katika kanisa la kwanza tunaona kuwekwa kwa waangalizi wa masikini (Mdo 6), ukisoma hapa utaona kwamba hata kazi ya kwanza kabisa ya mashemasi ilikuwa ni kuwasaidia watu wasiojiweza kwa kugawa mahitaji sawa katika jamii ya waaminio. Lakini cha kushangaza leo unakuta shemasi hajui wajibu wake hata kidogo. (si hoja yangu kujadili kazi za mashemasi hapa). Kwa vyovyote vile mifano hii inaonyesha wazi kwamba masuala ya kiuchumi yanashughulikiwa katika maandiko matakatifu na tahadhari maalumu imetolewa juu ya hatima ya maskini. Katika Ukristo wa mwanzo mojawapo ya ajenda kubwa ili kuwa ni fedha za washirika, usawa wa kifedha kati ya washirika (2 Wakor 89), utendewaji wa watumwa na mwenendo wa matajiri kwa masikini katika chakula cha Bwana (1 Wakorintho 11: 17- 34). Kwa mujibu wa Paulo, Injili inakabiliwa na jinsi washirika wanavyojiona wenyewe na kusudi lao, hivyo basi kutangaza Injili, ushirika wa makutano viliunganishwa pamoja. Hii inatufanya tuamini kwamba kanisa la kwanza lilikuwa makini sana katika hali ya washirika wake. Uelewa huu wa kibiblia kuhusu maswali ya kiuchumi ulichukuliwa na Wakristo wa karne za kwanza na walijitahidi kushughulika

nazo.

Kwa

mfano 15

mtu

mmoja

aliyeitwa

John

Chrystostomos alijiona yeye mwenyewe kama mlinzi wa maskini, akidai kuwa huruma ndiyo alama pekee ya ubinadamu na alitangaza kwamba Kristo mwenyewe hukutana na wanadamu katika kivuli cha maskini.9 Katika miji mingi ya mwishoni mwa miaka ya Kati, asilimia kubwa ya idadi ya watu walikuwa masikini sana na waliishi kwa kuombaomba. Jambo hili liliwapa wasiwasi mkubwa watu waliokuwa matajiri wakati ule, baadaye jamii ilibadilika kwa sababu ya uchumi mpya wa fedha na utofauti wa ustaarabu wa mijini, matatizo ya kijamii hayakuweza kutatuliwa tena na njia za kijadi za ushauri wa kiinjili (wa Kanisa Katoliki). Kwa maneno mengine ni kwamba kuingia kwenye kwenye nyumba za watawa, kutoa sadaka na kufanya matendo mema kwa wasiiojiweza ilionekana jambo la kukosolewa katika jamii.10 Hapa ndipo shida ilipoanzia na watu wakaanza kusahauliana katika matatizo. Na huu sasa tunaweza kusema kwamba ndio ulikuwa mwendelezo wa

9

The glory that was – and is – new Rome: Fifty holy patriarchs witness to the Orthodox faith, viewed on 19 September 2009, from www.orthodoxengland.org.uk/newrome.htm. 10

WARC 2004. A continuing journey towards confessing movement for economic justice nd life on earth: Covenanting for justice in the economy and on the earth (processus confessionis), http://www.kairoseuropa.de/english/continuingjourney.doc.

16

pengo kubwa kati wa aliokuwa nacho na wasio nacho. Yaani mwenye nacho anazidi kupanuka, na asiye nacho anazidi kudorora. Nini dhana ya utajiri na umaskini katika jamii tofauti tofauti? Kila jamii inaangalia suala la hali ya maisha ya mwanadamu kwa namna tofauti kabisa. Jamii ya watu wa Magharibi inaangalia hali ya mtu aliyefanikiwa hasa anapokuwa na vitu kama vile nyumba, gari, afya nzuri pamoja na masuala mengine yanayohusu kumiliki mali. 11 Kwa sababu ya mtazamo huu, kiwango cha utajiri au umaskini mara kwa mara umepigwa kwa kigezo cha watu wa Magharibi. Ninaposema watu wa magharibi ninamaanisha Wazungu. Watu wa Asia pia wana muono wake kuhusu umaskini na utajiri ambayo ama kwa hakika nao umekwisha gubikwa na mawazo ya kimagharibi. Waafrika tumekuwa na dhana ya umaskini na utajiri kwa kuangalia mawazo ya kimagharibi sana. Hiebert anadodosa kuwa utamaduni wa magharibi, na jinsi wanavyoishi inaonekana kana kwamba ni utamaduni wa kibiblia, ambapo hakuna mtu anayeuliza maswali hata kama kuna hitilafu ndani yake.12

11

Hiebert G.Paul. Anthropological Insight for Missionaries. Michigan: Grand Rapids (Baker book House), 1985. Pp 111-137 12

Khj (kama hapo juu)

17

Jamii za hapo kale kabla ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia walikuwa wanapima utajiri kwa namna tofauti na leo. Ukiangalia katika jamii nyingi za kiafrika mtu aliyejulikana kuwa ni tajiri ni yule ambaye alikuwa na wake wengi, (pengine labda kwa kuanza na wake zaidi ya kumi na kuendelea), huyu mtu alijulikana kwamba ni tajiri. Umiliki wa wake wengi ulienda sambamba na upatikanaji wa watoto wangi katika familia. Kazi ya watoto hao ilikuwa ni kulima na kuchunga mifugo. Tamaduni kama hizi kwa sasa zimeshaanza kupotea kwa sababu ya maendeleo ya sayansi na teknoloji. Katika utamaduni wa Kibiblia tunaona dhana hii nayo inajitokeza. Mtu aliyekuwa tajiri (kwa mfano wafalme) alitakiwa kuwa na wake wengi kwa kadri iwezekanavyo. Kwa hiyo si ajabu kuona wafalme wazuri kama akina Daudi wakiwa na wake zaidi ya wanne. Ukiacha Daudi, mwangalie mwanaye sulemani aliyekuwa na wake elfu moja, hii inamaanisha kwamba hiyo ndiyo dhana ya utajiri ilivyokuwa. Katika jamii ambayo nimekulia, nimekuwa tabia ya kumiliki wake wengi kama ishara ya utajiri inaishilizia. Nimewahi kuona wazee wakitaniana kwamba, unakuwa na mke mmoja kama mdomo, au unakuwa na mke mmoja kama mama yako. Dhana hizi zilikuwa kwa namna fulani zinashawishi jamii kujiingiza katika ushindani wa kuwa na wake wengi na kisha kukuza familia na kujijengea heshima. 18

Haya ni maswali ambayo lazima kila mtu ajiulize ni kwamba je ili mtu awe tajiri ni lazima awe na nini hasa? Wakriso wengi wameonekana kuwa njia panda katika suala la umaskini na utajiri, swali je ni kosa kuwa tajiri na ni sifa kujigamba kwa sababu wewe ni maskini? Kwa sababu hii sasa tunawezaje kuelewa masuala haya? Je katika maisha yetu, kusudi ni kupata utajiri au kuwa na pesa za kutusaidia katika mahitaji yetu? Tunawezaje kuleta usuluhishi kati ya utajiri na umaskini? Je umaskini kweli unakuja kutokana na uzembe? Maana halisi ya utajiri kwa mujibu wa maandiko Matakatifu Mojawapo ya masuala yanayojadiliwa sana katika jamii yetu yanahusu suala la utajiri. Watu wengi wanaamini kwamba kuwa na maisha mazuri, lazima uwe tajiri kwa kukusanya kiasi kikubwa cha fedha. Wengine wanaamini kuwa utajiri ni matokeo ya kazi ngumu na kwa kujidhabihu wenyewe. Wengine wanaamini kuwa tajiri ni matokeo ya kuchukua faida ya mtu mwingine. Wakristo wengine wanaamini kuwa kama wewe siyo tajiri, umepoteza kile ambacho Mungu anataka kwako. Kwa mtazamo huu wote, tunapaswa kutafuta jinsi Biblia inavyoelezea juu ya utajiri?

19

Utajiri ni nini? Kwa kuwa maoni ya watu hutofautiana sana juu ya ufafanuzi wa utajiri, hivyo basi ufafanuzi wa kihistoria wa utajiri unahitaji kufanywa. Kamusi ya 1828 ya Webster inafafanua mali kama ifuatavyo (1): "utajiri, (n). 1. Ustawi; furaha ya nje. 2. Mali; kiwango kikubwa cha fedha, bidhaa, au ardhi; yaani wingi wa mali ya kidunia ambayo huzidi mali ya sehemu kubwa ya jamii.13 Kutoka na ufafanuzi huu, tunaona kuwa, ufafanuzi wa kwanza wa utajiri ni ustawi na furaha ya nje. Mafanikio yanajulikana kama (2): kwa kiingereza "PROSPER" ITY, n. [L. Prosperitas.] yaani kupata kitu chochote kizuri au cha kuhitajika. Kamusi ya Webster inasema kwamba furaha nzuri ya nje ni maonyesho ya nje yanayoonyesha furaha ya ndani inayotoka kwa Mungu Kulingana na tafsiri hapo juu ni dhahiri kwamba kwamba utajiri ni kupata kitu chochote kizuri au kinachofaa kwa afya na manufaa ya wengine. Pia tunatambua kwamba ufafanuzi wa msingi na matumizi ya neno neno “utajiri” au “mafanikio” halijafungwa kwenye pesa au utajiri.

13

Webster, Noah (1828) “Wealth”. Webster’s Revised Unabridged Dictionary (1828): American Dictionary of the English Language, Retrieved from http://machaut.uchicago.edu/?resource=Webster%27s&word=wealth&use1828=on

20

Katika historia inaonesha kawmba afya ya mtu ilikuwa ni njia ya kuonyesha uwezo wao wa kutoa mahitaji yao ya kimwili. Hata hivyo, ingawa tumesema kwamba kisawe cha neno “utajiri” ni “mafanikio” biblia inaona vitu hivi viwili kama vitu tofauti. Biblia inatoa tofauti kati ya utajiri na mafanikio kutoka kwa mtazamo wa muda, na wa milele. Vivyo hivyo, Biblia inasema wazi kwamba utajiri wa kidunia hauna thamani ya milele.14 Tunaposhika mtazamo wa kiroho ambapo mali zetu hutoka, tunapata furaha ambayo sio msingi wa kile tulichofanya, badala yake, furaha yetu inategemea ukweli kwamba uhusiano wetu na Mungu ni mzuri.15 Ningependa kutoka maoni ya wadau mbalimbali waliochangia katika mahojiano. Remy16 anasema kuwa “Kwangu mimi mafanikio ni furaha na uwepo wa amani ya ndani... vitu kama magari nyumba mashamba, ni muonekano wa nje ambao wakati mwingine hauakisi ukweli wa mafanikio. Walau kwa kuwa vingi vimepatikana kwa mikopo ambayo bado inalipwa au kwa njia ambazo si za kawaida kama

14

Michael L. Williams, How Does The Bible Define Wealth? 2014

15

Khj

16

Unaweza kufuatilia mtiririko huko katika forumu kwa: http://www.shekinahpct.com/434148594 tarehe 9/7/2019 saa 9:36

21

ushirikina...” Naye Patricia 17 anasema kuwa “kwa mtazamo wangu ili mtu aonekane amefanikiwa ni amani na furaha ya moyo ndivyo vinatakiwa vitawale maisha yake. Pamoja na kwamba kwa mtazamo wa nje watu watapenda kuona mali ili kupata tafsiri kamili ya kufanikiwa ila mali hizo zikiwepo bila kuwa na amani wala furaha ndani ya maisha ya mtu bado tafsiri ya kufanikiwa inakuwa haijakamilika.Mali tuwe nazo kama ishara ya mafanikio ila amani na furaha viambatane navyo.” Ukidadavua Remy na Patricia utagundua kwamba wanaongelea kitu kile kile kwamba mafanikio ya kweli si yale yanayoonekana kwa nje bali kwa ndani. Kwa mtazamo huo tunaweza kugundua kwamba mtu anaweza akawa tajiri si kwa kwa sababu kajikusanyika mali za kutosha, bali ni kwa sababu anaishi maisha ambayo ni ya furaha na amani. Kila mtu Mungu amempa mali na utajiri, na akampa uwezo wa kula, na kuchukua sehemu yake, na kufurahia kwa kazi yake; Hii ni zawadi ya Mungu. Kwa maana hatakumbuka siku za maisha yake; Kwa sababu Mungu anamjibu kwa furaha ya moyo wake (Mhubiri 5: 19-20). Hitimisho fupi kutokana na hoja ya neno utajiri tunaweza kusema kuwa “utajiri” ni neno ambalo linaelezewa hasa kama ustawi na furaha ya nje. Mafanikio sio lazima iwe matokeo ya utajiri , lakini 17

khj

22

badala yake hutoa furaha ambayo ina lengo. Ikiwa mtazamo wetu ni ya jinsi gani tunavyoweza kupata utajiri zaidi na zaidi,wazo hili halipendezi kwa Mungu na halitadumu kwa muda mrefu katika hali ya usalama. Hata hivyo, ikiwa mtazamo wetu wa kupata umelenga kuwabariki watu wengine, kwa kutumia kile tulicho nacho kwa ajili ya ustawi na faida ya wengine, basi hapo humpendeza Mungu na kupata utajiri wa milele. Nini mtazamo wa Kikristo kuhusu utajiri Mtazamo wa Kikristo kuhusu utajiri unapaswa kutolewa kutoka kwenye Maandiko. Kuna sehemu nyingi katika Agano la Kale kwamba Mungu alitoa utajiri kwa watu wake. Sulemani aliahidiwa utajiri na akawa tajiri zaidi ya wafalme wote wa dunia (1 Wafalme 3: 11-13; 2 Mambo ya Nyakati 9:22); Daudi alisema katika 1 Mambo ya Nyakati 29:12: "Utajiri na heshima vinatoka kwako; Abraham (Mwanzo 17-31), Yusufu (Mwanzo 41), Mfalme Yehoshafati (2 Mambo ya Nyakati 17: 5), na wengine wengi walibarikiwa na Mungu kwa utajiri . Hata hivyo, walikuwa watu waliochaguliwa na ahadi za duniani, pamoja na tuzo. Walipewa ardhi na utajiri wote. Katika Agano Jipya, kuna kiwango tofauti. Kanisa halikupewa ardhi au ahadi ya utajiri. Waefeso 1: 3 inatuambia, “utukufu uwe kwa Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye alitubariki…na 23

baraka zote za kiroho ndani ya Kristo." Kristo alizungumza katika Mathayo 13:22 kuhusu mbegu ya Neno la Mungu Kuanguka miongoni mwa miiba na "udanganyifu wa utajiri huchochea neno, na haliiwezi kuzaa. Hii ndiyo kumbukumbu ya kwanza ya utajiri wa kidunia katika Agano Jipya. Kwa wazi, hii si picha nzuri. Katika Marko 10:23, Yesu aliwaambia wanafunzi wake 'ni vigumu sana kwa wale walio na utajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!' siyo kwamba haiwezekani, bali amesema itakuwa ni vigumu. Hii inaamanisha nini? kumbe inawezekana lakini ni vigumu. Kwa nini ni vigumu? Katika Luka 16:13, Yesu alizungumza kuhusu "mammon" (neno la Kiaramu kwa "utajiri"): 18 "Hakuna mtumishi anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa maana atampenda mmoja na kumpenda mwingine, au Atakuwa mwaminifu kwa huyo na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mamoni. Mungu hamhukumu wala hapingi kwa mtu yeyote kwa kuwa ana utajiri. Utajiri huwa na vyanzo vingi, lakini Mungu anawaonya wale wanaotafuta utajiri kila kukicha huku wakimwacha yeye. Nia ya Mungu ni kwamba sisi tuweke mioyo yetu kwake na wala siyo katika utajiri.

18

https://www.gotquestions.org/wealth-Christian.html

24

Kwa hiyo kwa mtazamo wa maandiko matakatifu tumeona kuwa si jambo baya kuwa na utajiri, hata kama ukiwa na utajiri kupindukia ila maonyo yametolewa kuhusu athari yake ambayo baadaye tutaijadili mbele ya safari. Ukisoma Yakobo, anawaonya wale wanaopata utajiri kupitia unyonyaji ambao utajiri wao hulia juu yao. Badala ya kuweka hazina mbinguni, watu wenye tamaa huweka hazina katika siku za mwisho kwa njia ya vitendo vyao vya uharibifu. Wengine huwa matajiri kupitia unyonyaji. Unyonyaji huo hutokea kwa wizi na mara nyingi unyonyaji wa kisiasa. Lakini, hii haipaswi kuwa hali ya kawaida kwa Wakristo, na wala hatupaswi kuwalinda wanaonyonya watu wengine kwa ajili ya kuwa matajiri. Tumeshuhudia watu wengi hata wale wanaojinasibu kuwa ni wakristo wakiwa wanyonyaji wakubwa. Nchi nyingi za Magharibi zimekuwa tajiri kupitia nchi nyingi za barani Afrika kwa kunyonya raslimali za nchi zao. Tulishuhudia mwaka 2017 wakati rais wa Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli alivyokomalia suala la kuibiwa kwa madini ya nchini. Madini haya yalikuwa yakiibiwa kijanja, kwa kusafirisha kitu kilichoitwa “makinikia’ ambayo yalionekana kuwa na ukwasi wa kutosha. Huu ni wizi wa siku zote wa makampuni ya kigeni na ni unyonyaji wa hali ya juu. Wizi huu pia ulipitia mikataba mibovu kwa kuwashirikisha watumishi wa serikali ambao uzalendo kwao ni 25

zero, huku wakijua kile walichokuwa wanakifanya (siyo kama Chifu Mangungo ambaye hakujua chochote), lakini wametumika kunyonya nchi yao. Na hao hao watu cha ajabu ni Wakristo kabisa. Mchungaji Overcomer Daniel siku moja aliuliza kwenye mtandao wa facebook kwamba “hao watu wanasali wapi?” jibu ni fupi tu kwamba wanasali kwenye makanisa haya haya. Kwa hiyo shida siyo utajiri, shida ni namna unavyoupata utajiri na namna unavyoweka moyo wako huko. Hebu tuone kweli hizi kuhusu utajiri; utajiri ni uko maeneo yote kimwili, akili, vifaa, na kiroho. Utajiri hutoka kwa Mungu - yeye ndiye chanzo cha mafanikio na baraka zote (Mathayo 7:11; Kumbukumbu la Torati 8: 8). Utajiri utaweza kusimamiwa - sisi ni mawakili wa mali tuliyopewa (1 Wakorintho 10:26; Mathayo 25: 14-30).

Utajiri

utatumiwa kwa madhumuni ya Mungu (1 Timotheo 6: 17-18; 2 Wakorintho 9:11). Kwa hiyo kulingana na mafungu hayo tunaona kuwa hakuna tatizo lolote kuhusu kuwepo kwa utajiri utokao kwa Bwana. Na utajiri huu ambao mara kwa mara hupatikana kwa sababu watu wamefanya kazi kwa bidi na kujikusanyia mali wakati mwingine huwa ndio msingi pia wa kuwahudumia watu wengine na kutangaza wema wa Mungu. Eldred anasema kuwa "dhana za mabadiliko, kazi, biashara, faida, na 26

mali ni msingi wa kibiblia wa biashara ya ufalme. Ikiwa mtu anafanya biashara kwa ufanisi kama mjumbe wa kueneza injili, mtu huyo lazima kwanza aelewe kwamba Mungu anajali juu ya mabadiliko ya kiroho, kijamii na kiuchumi, ambayo yanafanya kazi katika ulimwengu wa biashara na kwamba umaskini ni ugonjwa wa kijamii unaofaa kushughulikiwa.” 19 Anaongeza kuwa “utajiri unapaswa kuwa katika maeneo yote - kimwili, akili, vitu, na kiroho.”20 Kwa hiyo tunapojadili suala la utajiri na umaskini katika jamii ni lazima kuwa makini sana kwani tunaweza kujikuta tunaangukia katika upotoshaji wa kile ambacho Mungu amekikusudia katika maisha yetu. Tunahitaji mawazo ya kusawazisha hizi pande mbili ili kuwepo na msimamo mmoja uliojikita katika neno la Mungu.

19

Eldred, Ken. God Is at Work: Transforming People and Nations Through Business. Elevate Faith (September 6, 2016) 20

khj

27

SURA YA PILI Je Hali Ya Kiuchumi Ya Watu Imetayarishwa? (Predestined?) “Predestination” (utayarisho) ni dhana ya John Calvin. Kwa mujibu wa John Calvin, kuamliwa mapema ni utaratibu wa Mungu usiobadilika tangu kabla ya uumbaji wa ulimwengu kwamba angewaokoa kwa uhuru watu fulani (wateule), akiwaandalia uzima wa milele kwa uhuru, na wakati wengine watazuiliwa kupata wokovu na kuingia kwenye kifo cha milele.” Hata hivyo maoni haya yanapingwa vikali na baadhi ya wanazuoni. Edward Bahingayi 21 anadai kuwa si mpango wa Mungu uwe masikini wala si mpango wa Mungu uwe tajiri. Mpango wa Mungu ni wewe ufanikiwe tena kama roho yako ifanikiwavyo. Kwa jinsi hiyo itategemea nini maana ya Umasikini au Utajiri ambayo inawza kufungua mjadala. Maana ya utajiri ni kuwa na magari, majumba ya kifahari, na vito vya thamani harafu huku umasikini ukawa kinyume chake bila kijali ni kwa kiwango gani mtu huyo (masikini /tajiri) roho yake imefanikiwa basi huo hauwezi” anaendelea kusema kuwa “Mpango wa Mungu ni kufanikiwa kama roho yako inavyofanikiwa.” Ukiyachunguza maoni hayo utagundua kwamba Edward anachukua mkondo wa mawazo kwamba maisha ya kupata hapa 21

http://www.shekinahpct.com/434148594

28

duniani siyo mpango wa Mungu. Sasa swali tujiulize, je Mungu alijua hali ya masikini na tajiri hata kabla hawajapitia mawazo hali hizo? Na kama alijua, basi hoja ya Edward itakuwa na udhaifu fulani. Hata hivyo, maoni ya kutayarishwa kwa msingi yanatokana na picha za Kibiblia za wito wa Mungu kwa watu waliochaguliwa: watu wa Israeli na kupitia kazi ya Kristo, Israeli mpya. Dhana hii inaungwa mkono na Kumbukumbu la Torati 7 na Warumi 9. Dhana hii ni ngumu sana kuielewa, lakini kile ambacho Calvin alijaribu kukielezea ni kwamba hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kutokea pasipo Mungu kujua. Mungu anajua hatima ya kila mmoja! Anajua kwamba utamwamini Yesu, au hautamwamini! Hakuna jambo ambalo leo linaweza kutokea na kumshangaza Mungu, na kama Mungu anaweza kushangazwa na jambo lolote kwamba limetokea kwa ghafla bila yeye kujua, basi huyo siyo Mungu bali ni mungu. Mungu ni Mwenye nguvu zote, naamini kabisa kwamba hakuna kitu kinachoweza kupita mbali na mapenzi yake. Baada ya kuunda kila kitu kilichopo, yeye ndiye mmiliki kabisa na mtayarishaji wa mwisho wa yote aliyoyafanya. Hii ina maana kwamba Mungu alijua yote yaliyopo hata kabla ya kuumbwa. Ndiyo? Kwa hiyo Mungu alijua Hawa atakula tunda? Hivi vitu unavyoviona vinatokea, Mungu alivijua kabla 29

ya kutokea-naam, hata kabla ya misingi ya ulimwengu kuwepo. Kwa upande wa mwanadamu ni dhahiri kwamba Mungu hahitaji uhai wetu ili atutambue. Anatawala katika ulimwengu na juu ya ulimwengu. Hata vitendo vya dhambi vya wanaume na wanawake hutokea kwa idhini yake ya kibali. Najua umestuka kwa hoja hii! Lakini huo ni ukweli kabisa, kwa sababu ikiwa wewe mwanadamu utaukataa ukweli huu basi Mungu sio mtawala wa ulimwengu. Pia ikiwa kuna mambo ya nje ya udhibiti wake, basi narudia kusema yeye si Mungu bali ni mungu. Watu wengi huchanganyikiwa wanapojifunza habari hizi na maswali

mengi

yanaibuka.

Kwa

mfano

sasa

wale

ambao

hawajachaguliwa kwa ajili ya uzima wa milele itakuwaje? Nani alaumiwe, mbona Mungu bado anawalaumu kwa kutokuamini? Tunaweza kusema kwamba wale ambao si wateule hatimaye watahukumiwa, si kwa msingi wa kuwa wao hawakuteuliwa bali kwa misingi ya kutoamini. Mungu hafurahii kifo cha waovu. Waovu hufa kwa sababu ni kufa kwao! Sasa mwingine anaweza kuuliza, sasa kuna umuhimu gani wa kuhubiri Injili kama Mungu tayari keshachagua wa kwake? Kuhubiri ni lazima kwa sababu Mungu ametuagiza kufanya hivyo. Inawezekana kuwa ndiyo njia pia ambayo huitumia kuwaita wateule wake na pia njia hiyohiyo huitumia ili kuwahukumu wasowateule. Kwa namna yoyote ile unapaswa kuelewa kwamba 30

ninachojaribu kuelezea mahali hapa kuhusu dhana hii ni kwamba Mungu anajua kila kitu. Na hakuna kitu ambacho kinamshangaza. Turudi kwenye mada yetu sasa, je hali ya kiuchumi ya watu imetayarishwa/imeandaliwa mapema? Kwa maana ya kwamba kuna watu wengine ambao Mungu alishaandikia kuwa ni matajiri na wengine kuwa masikini? Hii nimeiweka hapa kama nadharia (hypothesis) ambayo inahitaji kuchunguzwa kwa hali ya juu na kwa utafiti wa hali ya juu sana. John McLeod Campbell, akinukuliwa na Professor Jeong anasema kuwa “tunaposhughulika na masuala ya hali ya mwanadamu kutayarishwa mapema, tunahitaji kuwa makini sana”22 kwani inaweza kuwachanganya watu wengi na kushindwa kuelewa wakae katika msimamo upi. Kwa sababu hiyo, ninapojadili hoja hii ninao umakini mkubwa kwani ninaelewa kwamba yeyote atakayesoma mistari michache katika kitabu hiki hawezi kuelewa isipokuwa amesoma eneo lote husika. Kujibu swali hili siyo rahisi, ila tunaweza kujiuliza maswali mengine zaidi ambayo mengine majibu yake yanaweza kuwa ya ndiyo au hapana. Kwa mfano hebu tujiulize, je kama Mungu alinijua mimi hata 22

Mhadhara wa mafundisho kuhusu Mungu. Chongshin University. South Korea. May 2017

31

kabla ya misingi ya ulimwengu kuwepo, anashindwaje kujua hali yangu ya kiuchumi kwamba itakuwaje? Au atashindwaje kupanga kwamba mimi nitakuwa na sehemu fulani hapa duniani, au siwezi kuwa nayo? Lakini bado swali lingine linakuja, je nitajuaje sasa kwamba Mungu amepanga hali yangu ya uchumi (pengine nzuri au mbaya?), jibu ni kwamba sisi wanadamu hatuwezi kujua kila kitu kutoka kwa Mungu, na kwa sababu hiyo ni Mungu pekee anayejua. Kwa hiyo kazi ya mwanadamu ni kuhakikisha anakusanya maarifa yote yanayohusu uchumi na mafanikio katika maisha kwa ujumla-huku akilenga kwenye mstakabali wa maisha yake ya baadaye, bila kufikiri kwamba kwamba hiyo ndiyo hali yake aliyopangiwa na Mungu. Na ndiyo maana tunakaza kwamba

mwanadamu

anapaswa

kupambana

usiku

na

mchana

kuhakikisha kwamba maisha ya hapa duniani kwa upande wake yanaenda. Ni muhimu sisi kama wanadamu kutimiza upande wetu, na upande wa mtu yeye anajua mwenyewe! Jambo la muhimu kujua pia ni kwamba Mungu hutupatia vitu vyote tunavyohitaji katika maisha yetu. Hii ndiyo inayoitwa “neema ya kawaida kwa watu wote.” Kwa sababu ya neema ya Mungu ndiyo maana unaendelea kuishi, ndiyo maana unakula, unakunywa, unavaa, ni kwa sababu kuna Mungu. kwa sababu Mungu anaishi-basi nasi tunaishi ndani yake. Kama wanandoa Bill na Gloria Gaither walipokuwa katika 32

hali ngumu ya maisha, waliona kwamba katika kila jambo maisha ya kumwangalia Mungu ndiyo muhimu kuliko aina yoyote ile! Kwa hiyo waliimba wimbo ambao umerekodiwa katika vitabu vingi vya nyimbo Kwa sababu anaishi, ninaweza kukabiliana na kesho, Kwa sababu anaishi, hofu zote zimekwenda,

Kwa

sababu

najua

Yeye

anashikilia wakati ujao, Na uhai ni wa thamani kwa walio hai, Kwa sababu Yeye anaishi!23 Kwa sababu hiyo, tunahitaji kuweka kipaumbele chetu kwanza kwa Mungu mwenyewe, yeye ni chanzo cha kila kitu katika maisha yetu. Hata kama hujapata kitu chochote katika maisha yako ni lazima ujue kwamba Mungu pia anajua. Kwa sababu tumesema Mungu anajua kila kitu katika maisha yetu, basi hatupaswi kuwa na wasiwasi na kuishi kwa bahati nasibu, bali tunahitaji kuishi mbele za Mungu kila siku.

23

G & W. J. Gaither, (1971) (imenakiliwa katika kitabu cha: Korean English Hymnal. Seoul: KHS 2010, wimbo namba 171

33

Je Mipango yetu ya Baadaye Inathirika Vipi Na Dhana Hii ya Kutayarishwa Mapema? Nimesikia mara kwa mara watu wakisema kwamba “sisi ndiyo waandaji wa hatima yetu wenyewe.” Lakini tumesema kwamba Mungu ameshaandaa masuala ya maisha yetu hata kabla ya ulimwengu kuwepo! Sasa inakuwaje mwanadamu anaanza kuhangaika kuishi kwa kujipanga na kufanya uchaguzi wa mambo kadha wa kadha? Je mwanadamu anaweza kubadilisha mpango wa Mungu katika maisha yake? Kama hawezi kubadilisha, kwa nini anahangaika kwa ajili ya kupanga maisha yake ya baadaye! Mwingine anataka baadaye awe daktari, mwingine awe mkulima, mwingine awe mwalimu, mwingine awe dereva wa ndege. Si mambo yote haya yameamriwa na Mungu kwake,na hivyo kuhangaika juu yake kujisumbua mwenyewe? Ni kweli, mwanadamu hawezi kubadilisha mpango (decree) wa Mungu katika maisha yake, hii inatokana na ukweli kwamba kila mmoja anajenga kwenye msingi ambao Mungu ameutengeneza tayari. Lakini kuandaa kwa ajili ya maisha ya baadaye ni muhimu kwa mwanadamu, hii inatokana na ukweli kwamba yeye hajui kinachoweza kutendeka juu yake. Binadamu hajui hata jambo lililoko mbele yake kwa dakika moja ijayo. Vitu ambavyo Mungu anatupatia; mali, afya pamoja na mambo yote yanayotuzunguka ni kwa ajili ya kutusaidia sisi kufikia kile 34

ambacho amekiandaa kwa ajili yetu. Katikati ya mizunguko hii yote lazima awepo Mungu kwa sababu yeye ndiye kiini cha kila kitu. Tukijiacha

sisi

wenyewe,

bila

Mungu,

sisi

kama

wanadamu

tutachukuliwa katika mzunguko usio na mwisho wa kujaribu kuwa bora, kufanya mambo kwa kasi, na kuwa na vitu vingi. Nimewahi kuona watu wengi wanapohangaika katika maisha yao ya utafutaji na kukosa, mwishoni husema “mimi namwachia Mungu.” Mara kwa mara mimi hupenda kuwatania, mbona unamwachia Mungu mambo kama haya ambayo wewe ndiye unatakiwa kuyafanya kwa wakati huu? Rafiki yangu mmoja tulipokuwa tukisoma mahali fulani alisema “huu mtihani ni mgumu sana, kwa hiyo namwachia Mungu!” Nami nilimjibu, “huyu Mungu wako anayefanya mtihani wako namtaka na mimi!” Changamoto kubwa inayowakabili wanadamu wengi ni kushindwa kufanya upande wao, na kusema kwamba wanamwachia Mungu. Maana ya kuandaliwa mapema siyo kuacha kufanya upande wako. Cha kushangaza ni kwamba binadamu anapofanya kazi kwa muda mrefu, mara anapojikuta katika hali ngumu-basi anasema “namwachia Mungu.” Maana yakeni kwamba mwanzoni hakumwachia Mungu, hakushirikiana na Mungu katika hilo jambo, bali alisimama yeye kama yeye! Watu wengi wanaposhindwa kuamua mambo yao, husema basi namwachia Mungu. huko siko kumtegemea Mungu, bali ni kumfanya 35

Mungu kuwa kama hirizi yako tu! Mungu ni Mungu wa uhusiano, tunapokuwa katika uhusiano naye, hutufundisha mambo ya kufanya. Na mara anapokuwa ametupa mawazo ya kufanya-lazima tufanye. Kuna wengine ambao wakiona mambo yamekuwa magumu, wanasema ngoja tuombe Mungu kwanza. Je unafikiri kweli wanaomba? Watu wengi wamekuwa wakitumia kigezo cha kuomba mapenzi ya Mungu ilhali wanajua wanachopaswa kukifanya katika maisha yao. Chambers aliwahi kusema kuwa “usiulize njia wakati unajua njia iko wapi” 24 kwa kufanya hivyo ni kama kumjaribu Mungu. Kwa hiyo, hakuna kukaa chini na kudai kwamba “mimi Mungu amenipangia hivi” au haya ni mapenzi ya Mungu! Maneno kama haya yasikike kwako tu ikiwa una uhakika na kile unachokisema. Tunapaswa kuzingatia bila kusahau hoja nyingine muhimu tunapozungumzia suala la mpango wa Mungu kwa binadamu. Mungu wetu ni Mungu wa maagano. Kuna maagano kadha wa kadha katika Biblia, na Mungu anapotoa agano, anaweka na ahadi katika Agano. Agano ni kati ya pande mbili. Mungu anapofanya agano nasi, anataka tutembee katika agano hilo. Karibu katika maagano yote katika Biblia, 24

Chambers, Oswald. My Utmost for His Highest. New York: Dodd, Mead & Company, 1935. P, 151

36

Mungu ameweka vigezo vyake. Hii inamaanisha kwamba kama watu hawatembei katika vigezo vya maagano, basi watashindwa kupata vitu vilivyofungashwa kwenye maagano. Hapo sasa hatuwezi kusema kwamba Mungu amebadilisha mpango wake, bali amefuata kile ambacho amekisema. Ngoja tutalii zaidi masuala ya maagano na jinsi Mungu watu waliposhindwa kutunza maagano.

Agano la Mungu na Adamu Hili lilikuwa ni agano la Mungu na Adamu kabla ya anguko. Wanatheolojia wengi wameliita ni “agano la kazi” hili lilikuwa agano la uhusiano wa Kisheria ambapo Mungu mwenyewe aliingia katika uhusiano na Adamu. Mungu, kutokana na wema wake, aliingia katika ushirika na Adamu, akiahidi baraka fulani na kuhitaji majukumu fulani. Mungu kwa uhuru anaweka hali hizo kwa Adamu (Mw. 1:24-30). Ingawa neno “agano” halitumiwi katika Mwanzo 1 na 2. Kuna washirika wawili, yaani Mungu na Adamu, na Adam akiwa kama mwakilishi. Kuna majukumu, kuna masharti na kuna baraka. Vyote hivi ni vijumuishi vya agano. Masharti ya agano la kazi ilikuwa ni “utii tu.” Sasa tukisoma katika Mw.3:1 na kuendelea tunaona namna Adam alivyoshindwa kutunza agano hili. Alishindwa kumtii Mungu kwa kufanya kile ambacho alizuiwa. 37

Ni kweli Mungu hakujadiliana na Adamu kama ataweza kutunza agano hilo, hilo halikuwa jambo muhimu sana kwani Mungu alijali sana ushirikiano na Adamu. Hoja ya msingi hapa ilikuwa siyo kula tunda, bali ni kushindwa kushika kile ambacho Mungu alisema. Yaani kitendo cha kukataa kufanya kile ambacho Mungu alikuwa amewaagiza, kilikuwa ni kitendo cha kutilia mashaka kazi ukuu wa Mungu na uweza wake. Kwa sababu wanadamu walimsikiliza shetani, basi walienda kinyume na masharti ya agano. Na kwa sababu Mungu ni Mungu mwenye haki, ilibidi afuate kile alichosema! Alisema “siku mtakapokula, hakika mtakufa” kwa sababu neno lake halianguki bure, basi alisimamia maneno yake. Sasa hapa nani ambaye alitakiwa kuwajibika? Je Mungu alibadili mpango wake? Jibu ni hapana kwa sababu Mungu alifuata kile alichokuwa amesema, na mwanadamu hakuwa na udhuru wowote.

Agano la Mungu na Ibrahim Tukisoma Mwa. 12, 15 na 17 tunaona uhusiano wa Mungu na Ibrahimu. Mungu alimwita Ibrahimu kwa mapenzi yake mwenyewe. Ibrahimu alikubali kuondoka katika nchi yake na kwenda katika nchi ambayo Mungu alikuwa amemwahidi. Katika sura ya 15 tunamwona Mungu anaweka agano la Ibrahimu. Katika sura ya 17 Mungu anakuja 38

kuthibitisha agano alilofanya naye mwanzo kwa sababu imani yake iliyumbayumba baada ya kutaka kutimiza ahadi ya Mungu kibinadamu. Hata hivyo, kuna shida kubwa juu ya wajibu wa Ibrahimu katika kukubali ahadi za neema za Mungu zilizotolewa kwake katika agano hili, kwa sababu Mungu anamkumbusha Ibrahimu kuwa anahitaji kutembea mbele zake kwa utimilifu. "Nenda mbele yangu, na usiwe na hatia." Mungu hakumwomba Abrahamu awe mkamilifu pale. Lakini anaomba Ibrahimu kutembea mbele Yake kwa moyo wote; Yaani, kujitoa kikamilifu kumfuata na kuamini ahadi alizompa katika Mwanzo 12 na kurudia katika Mwanzo 15. Anamuomba Ibrahimu kuwa mtu mwenye moyo wote, sio kuwa mtu asiye na dhambi. Agano ambalo Mungu ameweka na Ibrahimu ni la neema na wajibu pia. Japokuwa imani ya Ibrahimu katika sura ya 16 ilitikisika, Mungu hakuacha kuthibitisha agano lake. Unajua kwa nini? kuna siri kubwa ambayo unapaswa kuielewa. Iko hivi, katika Mwanzo, 15, Ibrahimu anauliza swali kwa Mungu. Katika mstari wa 8 wa Mwanzo 15, Ibrahimu anasema, "Ee Bwana Mungu, niwezeje kujua kwamba nitaimiliki," hapa anasema juu ya nchi ya Kanaani. "Nawezaje kujua kwamba nipate kuwa nayo?" Na Bwana akamwambia katika mstari wa 9, "'Niletee ng'ombe mwenye umri wa miaka mitatu, na mbuzi wa kike 39

mwenye umri wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na njiwa'. Kisha akamletea hivyo vyote na kuikata vipande viwili na kuweka nusu moja huku na nyingine huku, lakini hakumkata ndege. Kisha ndege wakashuka juu ya mizoga na Ibrahimu akawafukuza, na sasa wakati jua lilipokuwa likishuka, usingizi mkubwa ukamwangukia Ibrahimu, na tazama, hofu na giza kubwa vilikuwa juu yake. Mungu akamwambia Ibrahimu, "hakika kwamba uzao wako watakuwa wageni katika nchi ambayo sio wao watakuwa watumwa na kufadhaika miaka 400. Lakini nitawahukumu taifa ambalo watatumikia na baadaye, watatoka na mali nyingi. Na wewe, utaenda kwa baba zako kwa amani, nawe utazikwa katika uzee mzuri. Kisha katika kizazi cha nne, watarudi hapa, kwa sababu uovu wa Waamori haujajaa bado. Baada ya hayo, na tazama, kuna tanuri ya moto ilipitia kati ya vipande hivi." Hapa maana yake Mungu mwenyewe alipita katika vile vipande, na wakati huo Ibrahimu alikuwa amelala. Kwa namna moja au nyingine ni kwamba Mungu alijifunga mwenyewe hapa, jambo jema ni kwamba Ibrahimu alilala, kwa hiyo hakupita katika vile vitu. Kupita katikati ya vile vitu maana yake ni kwamba kama ukienda kinyume na agano utakatwa vipande vipande kama wale wanyama! Kwa sababu Ibrahimu hakupita katikati ya hivyo vitu, Mungu pekee alipita katikati. Kwa hiyo Mungu ndiye alishika agano lake. Na kweli tunaona anatimiza Agano 40

lake kwa Ibrahimu, mwaka wa 400 wana wa Israel walitoka katika nchi ya Misri na kuwapeleka katika nchi ya ahadi (Kanaani) Kwa hiyo basi, usishangae sana unapoona kwamba ingawa Ibrahimu alikuwa na mapungufu mengi lakini Mungu aliendelea kutimiza agano lake. Alimpatie kile ambacho alikuwa ameahidi kwake. Kwa sababu Mungu alijifunga. Kwa hiyo hapa si sababu kubwa ya Mungu kutimiza mpango wake ni kwa sababu alikuwa anafuata agano lake kama alivyojifunga mwenyewe.

Agano la Waisrael na Mungu (au Agano la Musa) Baada ya Mungu kutimiza ahadi yake ya kuwatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri, aliamua kuthibitisha agano lake tena. Au kwa lugha nyingie kufanya upya agano! Agano la Musa ni agano la masharti lililofanyika kati ya Mungu na taifa la Israeli kwenye Mlima Sinai (Kutoka 19-24). Wakati mwingine huitwa Agano la Sinai lakini mara nyingi hujulikana kama Agano la Musa kwa kuwa Musa alikuwa kiongozi wa Israeli aliyechaguliwa wakati huo. Mfano wa agano hili ni sawa na maagano mengine ya kale ya wakati huo kwa sababu ni kati ya mfalme wa pekee (Mungu) na watu wake (Israeli). Wakati wa agano, Mungu aliwakumbusha watu wajibu wao wa kutii sheria yake (Kutoka 19: 5), na watu walikubaliana na agano na kusema "Yote ambayo Bwana 41

amesema tutafanya!" (Kutoka 19: 8). Agano hili lilitumika kuweka taifa la Israeli mbali na mataifa mengine kama watu wa Mungu waliochaguliwa na ilikuwa sawa na ahadi isiyo na masharti ambayo Mungu alifanya na Ibrahimu kwa sababu pia ni agano la damu. Ikiwa Israeli wangetii, basi Mungu angewabariki, lakini ikiwa wasingetii, basi Mungu angewaadhibu. Baraka na laana zinazohusiana na agano hili la masharti zipo kwa kina katika Kumbukumbu la Torati 28. Maagano mengine yanayopatikana katika Biblia ni maagano ya umoja wa ahadi, ambayo Mungu hujifunga mwenyewe kufanya yale aliyoahidi, bila kujali nini wapokeaji wa ahadi hizo hufanya. Hebu tujiulize maswali haya, je Waisrael walitii kweli kile ambacho Mungu aliwaagiza? Na kama hawakutii nani alitakiwa kuwajibika? Ni dhahiri hawa ndugu baada ya muda mfupi tu walikengeuka kabisa. matokeo yake ilikuwa ni kwamba Mungu aliwaadhibu sawasawa na jinsi alivyokuwa ameahidi. Mungu alisimamia maneno yake hapa. Kwa sababu hiyo, Mungu aliwaadhibu kwa kuzunguka jangwani kwa miaka 40. Safari ya muda mfupi ilichukua muda mrefu sana. Katika maisha yetu, Mungu ameweka vitu vingi kwa ajili yetu na namna ya kuvipata kutoka kwake. Mungu wetu ni Mungu wa agano. Agano la Musa lilibadilishwa kuwa Agano Jipya katika Kristo (Luka 42

22:20, 1 Wakorintho 11:25, 2 Wakorintho 3: 6; Waebrania 8: 8; 8:13; 9:15; 12:24). Agano Jipya katika Kristo ni bora zaidi kuliko Agano la kale la Musa ambalo linabadilika kwa sababu linatimiza ahadi zilizofanywa katika Yeremia 31: 31-34, kama inavyochaguliwa katika Waebrania 8. Kwa hiyo Mungu ameahidi mambo mema kwa ajili yetu. Baraka ya uzima wa milele tunaweza kupokea wote kwa bure kwa sharti la kumwamini Yesu Kristo peke yake, lakini baraka zingine za kimwili zinayo masharti yake ambayo yamepachikwa ili kutufanya sisi tuvipate. Mojawapo ya masharti hayo ni uhusiano wetu na Mungu. Mungu anapofanya agano anataka kuimarisha uhusiano zaidi na zaidi. Katika Agano Jipya, Mungu ametuagiza kuomba ili kupata vitu ambavyo ameviweka kwa ajili yetu. Anasema katika Mathayo 7:7 “ombeni nany mtapewa; tafute, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.” Hapa unaweza kujiuliza, kama Mungu ameandaa vitu vizuri kwa ajili yetu, mbona anatuambia tena tuombe? Kwa lugha nyingine, Mungu anataka kushirikiana na mwanadamu katika masuala yote. Kama nilivyosema hapo awali kwamba kuomba ni uhusiano, kwa hiyo Mungu anataka binadamu akae karibu naye kupitia maombi. Je tusipoomba hatuwezi kupata vitu ambavyo tungepata? Ili kujibu swali hili napenda kurejea katika neno la Mungu. Yakobo 4:2b “wala 43

hamna kitu kwa sababu hamwombi.” Ndiyo! Kulingana na fungu hili watu wengi hawana vitu ambavyo wanapaswa kuwa navyo kwa sababu hawana hawaombi kwa ajili ya vitu hivyo. Unajua tunapokuwa tunaingia katika maombi, tunagusa eneo la vitu vitakatifu vya Kimungu. Professor Imink25 katika mafundisho yake ya “Maombi katika makanisa ya matengenezo” aliwahi kusema “kila mtu anapokuwa anaingia kwenye maombi anapaswa kujua kwamba amekanyaka vitu vitakatifu, chochote kile anachokisema huko vinafanyika.” kubwa

ambayo

Mungu

mwenyewe

Na katika maombi kuna siri hukutana

na

watu

wake

wanaomuitaji kwa uaminifu. Akielezea thamani ya maombi, John Calvin alisema kuwa “katika maombi Kwa maana Kristo hutoa yote; Furaha badala ya taabu zetu, utajiri wote badala ya uhitaji wetu; Ndani yake anafungua hazina ya mbinguni ambayo imani yetu inaweza kumtafakari Mwana wake mpendwa, matumaini yetu yote. Kweli, hii ni falsafa ya siri lakini wenye macho ya Mungu hufunguliwa hakika.”26 Tatizo liko wapi sasa? Yakobo 4:3 anasema “hata mwaomba wala

hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa 25

Intensive course on “Prayers in Reformed Churches” Chongshin University. Korea, 2016. (lecture) 26

Calvin, John. The institute of Christian Religion.( vol 2). Louisville: Westminster John Knox Press, 1960. P. 850

44

zetu.” Yakobo anajibu swali letu kwamba haitoshi kuomba mambo mazuri, lakini ni lazima tuulize kwa roho nzuri na nia njema. Hiki kinaweza kuwa kisiki cha maombi yetu mara kwa mara. Nimewahi kuona watu wengi wakifanya maombi kwa ajili ya kuwakomoa wapinzani wao. Mungu hawezi kusikia maombi ya namna hiyo hata siku moja. Na ukiona umejibiwa maombi ya visasi kama hayo unatakiwa uwe makini sana kwani unaweza kujikuta umeingia kwenye shida ambayo hujawahi kuiona. Ninakumbuka wimbo unaosema kwamba “Mungu nibariki ili adui zangu washangae.” Hili si kusudi la Mungu kubariki maisha yetu hapa duniani, bali Mungu anakuwa na makusudi ya kufaidiana kwa kila mtu na wala siyo kuonyeshana. Kuna wakati mwingine tunapitia vipindi vigumu kwa sababu ya kuwa na nia mbaya katika maombi yetu. Biblia ina mengi ya kusema juu ya nia zetu. Methali 16: 2 inasema, "Njia zote za mtu zinaonekana kuwa safi machoni pao wenyewe, lakini nia njema zinapimwa na BWANA." Kwa sababu moyo wa mwanadamu ni wa udanganyifu sana (Yeremia 17: 9), tunaweza kujipotosha wenyewe kwa sababu ya nia zetu. Tunaweza kujifanya kuwa tunachagua vitendo fulani kwa ajili ya Mungu au faida ya wengine, wakati kwa kweli tuna sababu za ubinafsi. Mungu hapendezwi na ubinafsi wetu na "anafahamu mawazo na makusudi ya moyo" (Waebrania 4:12). 45

Hivyo basi, kwa sababu mioyo yetu ni ya udanganyifu, tunapaswa kuendelea kuchunguza nia zetu na kuwa tayari kuwa waaminifu na kujiuliza kwa nini tunachagua hatua fulani. Nia ni muhimu sana katika jambo lolote. Katika huduma yangu ninapotafuta vijana wa kufuasa mara kwa mara huwa ninawauliza, “je unataka kuwa nani,” majibu ninayopokea ni jibu moja tu “nataka kuwa mchungaji” (isipokuwa kijana mmoja tu hakuwahi kusema anataka kuwa mchungaji). Lakini cha kushangaza sana hakuna hata mmoja ambaye kwa sasa ni mchungaji isipokuwa yule aliyesema kwamba hatakuwa mchungaji anatumika vizuri kuliko wote walioondoka na walikuwa wanasema wanataka kuwa wachungaji. Unajua kwa nini walikuwa wananiambia kuwa wanataka kuwa wachungaji? Sababu ni moja, kusudi lao la kuja kwenye huduma yangu iliuwa ni kupitia mgongo wa uchungaji ili kufanikisha tamaa zao. Lakini kwa sababu Mungu hajaribiwi na mwanadamu, amezuia nia yao mbaya. Hata hivyo ijulikane kuwa mimi sikulazimisha na mpaka leo silazimishi watu kuwa katika nafasi ya uchungaji, lengo ni kuwafuasa kuwa wanafunzi wa Yesu kweli kweli na wanaweza kutumika katika Nyanja mbalimbai katika kanisa. Kwa hiyo unaweza kuona kwamba kwa sababu ya nia zetu Mungu huzuia baadhi ya maombi yetu. Mpendwa katika Bwana, hapa kuna maswali maalum ya kutusaidia kuchunguza nia zetu wenyewe: jiulize; kwanza, je kama hakuna mtu 46

anayejua kile ninachofanya (kutoa sadaka, kuhudumu), je! Bado nitafanya hivyo? Swali hili litakuepusha kujionesha kwa watu badala yake Mungu atakulipia. Pili, je kama hakuna faida inayoonekana kwa kufanya hivyo, je, nitaendelea kufanya? Swali hili litakusaidia kujua nia yako kuhusu kulipwa kwa ajili ya kufanya jambo jema. Tatu, je, ningependa kuchukua nafasi ndogo ikiwa Mungu ataniambia? Swali hili litasaidia kuonesha nia yako kuhusu nafasi yako. Swali letu la msingi ilikuwa kuona ni kwa jinsi gani mipango yetu ya baadaye inaweza kuathirika na dhana ya kutayarishwa mapema. Tumeona kwamba kweli Mungu hawezi kubadilisha kile ambacho ameamuru kwa ajili ya maisha yetu, bali anafuata kile alichokisema. Ili kuthibitisha kile alichokuwa anakisema alikuwa anaweka agano la wake wake ambapo aliwataka watembee katika maagano hayo. Yeyote anayeenda kinyume na maagano hayo shida ilimwangukia-hapo si Mungu tena bali yeye mwenyewe kwa sababu Mungu ameshatamka, basi inakuwa kweli. Tulijiuliza pia suala la nafasi ya maombi katika maisha yetu nini kama hatima ya mwanadamu imetayarishwa. Tuliona kwamba Mungu ametuagiza kuomba, kupitia maombi anataka kutimiza ahadi yake. Kwa kuwa tumeagizwa kuomba, hakuna namna nyingine ya kukwepa suala hili muhimu kwa maisha yetu. Mungu tayari ameshaandaa mambo mazuri kwa ajili yetu. Lakini jambo la msingi 47

kabisa ambalo hupaswi kusahau ni kwamba, kumpata Yesu katika maisha yako ni bora zaidi ya kuupata ulimwengu mzima. Pesa inaweza kupoteza thamani, lakini thamani ya Yesu inapanda kila siku kwa sababu yeye ni Mungu. Soko la hisa linaweza kushuka, lakini soko la Yesu halishuki kamwe kwa sababu yeye yuko juu ya yote! Kila kitu unachokiona ni cha thamani hapa duniani-siyo cha thamani zaidi ya Yesu Kristo peke yake. Unachopaswa ni kukaa kwa uaminifu mbele za Bwana katika maisha yako. Neno linasema kuwa “Bwana atatoa

neema na utukufu, hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu” Zaburi 84:11. Usiache kupanga mambo yako ya kufanya. Panga naye Mungu atakamilisha.

48

SURA YA TATU Ingawa Mungu Anajua, Lakini Kupanga Ni Kazi Yako Ili Ufikie Malengo Yako Kupanga mipango ya kufanikiwa katika maisha ni jambo ambalo linamhusu mwanadamu. Kwa upande mwingine tunaweza kusema kwamba kila mtu lazima awajibike ili kuhakikisha kwamba anafikia malengo sahihi katika maisha yake. Kama usipopanga katika maisha yako, je utajuaje sasa ni jambo gani Mungu amekupangia katika kesho yako? Kwa sababu hujui, basi lazima upange tu. Kama ambavyo nimekwisha kutabanaisha kuwa mara nyingi nimewahi kuwasikia watu wakisema “namwachia Mungu sasa.. mimi nimeshaachana nalo.” Niulize tena, je unadhani watu wanaposema maneno kama hayo wanamwachia Mungu kweli? Hapana! kauli kama hizi hazimaanishi kwamba huyu mtu anamtegemea Mungu bali alikuwa na mipango yake bila Mungu sasa baada ya kuona imeshindikana kutekelezeka ameamua kumwachia Mungu! narudia tena je kwa nini mwishoni unamwachia Mungu? Wewe ndiye unawajibika. Kwa hiyo maandalio ya moyo (mipango ambayo moyo wako unatamani itekelezeke) ni yako mwenyewe! Kwa hiyo lazima upange katika maisha yako kwamba utafanya nini kwa kipindi fulani! (Mithali 16:1, 21:31). 49

Unaweza kushangaa kuona ndani ya kanisa kuwa kuna watu hawajui kesho wanaenda wapi ukiona hivyo, ujue wewe umeshindwa kupanga, na kama ukishindwa kupanga umepanga kushindwa. Lazima uweke tayari farasi kwa ajili ya vita (farasi-ni vifaa ambavyo unavitumia katika mapambano katika maisha) kwa lugha nyingine ni lazima upange mipango yako ya muda mfupi na ya muda mrefu! Hebu ngoja nikupe mifano ya kawaida ili uweze kuelewa; ukitaka kula nyama, lazima upange namna ya kuipata nyama na siyo kukaa chini kuanza kumwomba Mungu aleta nyama! Ukitaka kuoa ni lazima upange kwenda kutafuta mwanamke na siyo kumsubiri Mungu akuletee chumbani mwako. Ukitaka kufanya biashara-lazima ujue bei ya kununulia na bei ya kuuzia kwani katika biashara hatufanyi mabadilishano ya fedha bali tunataka faida Kumbuka kwamba nazungumzia mipango yako ya baadaye. Hoja hii imetokana na dhana ya kwamba Mungu tayari ameshapanga mambo yetu, ya nini kujisumbua kupanga tena. Nimeshaeleza kirefu kwenye sura hii. Nataka nikupe baadhi ya njia za kawaida kabisa lakini zipo katika maandiko Matakatifu ambazo zinaweza kukusaidia kutekeleza mipango yako ya kesho. Jambo la msingi kabla sijazungumzia njia hizo ni lazima ukumbuke kwamba msitakabari wa maisha yetu uko mikononi mwa Mungu. lakini Mungu amekuweka hapa 50

duniani kwa ajili ya lengo maalum. Mungu hajakuweka duniani kama mnyama! Anataka uzingatie mambo fulanifulani ili siku zako za kesho ziwe nzuri.

Mambo ya kufanya unapotengeneza kesho yako Ni

muhimu

sasa

ukumbuke

kurekebisha

mambo

yafuatayo

unapotengeneza kesho yako.27

Tengeneza Jina Lako Kwanza Mw. 12:2 Mungu alipoongea na Ibrahimu alimwambia kwamba “Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka.” Mungu aliahidi kumbariki Ibrahimu kwa namna ya ajabu kiasi kwamba angelifanya jina lake kuwa kubwa. Mungu alijua thamani ya jina la Ibrahimu. Na ndiyo maana kwa kuanza, alipokuwa akifanya agano naye katika Mw. 17 alimbadilisha jina lake ili liendane na kile ambacho Mungu alikuwa amekikusudia kwake. Badala 27

Mambo haya niliyafundisha katika semina ya kanisa la Shekinah Presbyterian Church pale Madale Dar es salaam mwaka 2014 na nusu ya wanasemina walinipa mrejesho ya kwamba wameona hizo ni mbinu mpya kwao. Na wengi wao baada ya muda waliniambia namna ambavyo walianza kutekeleza mbinu hizo. Niliwapa kazi ya kila mmoja awe ananiletea maendeleo yake ili nizidi kuwaombea. Kwa hiyo nawe mpendwa unaposoma mbinu hizi, siyo tu unataka kupata ufahamu wako, bali ni kuzifanyia mazoezi. Najua zingine huwezi kuzifanyia kazi kwa sababu zinahitaji muda mrefu, lakini zile ambazo unaweza kuzifanya sasa, jitahidi sana uzifanye.

51

ya Abram ndipo akawa Ibrahimu. Na mke wake vilevile badala ya kuwa Sarai akawa Sara. Maana ya majina haya yote yalilenga kuwatambulisha kama watu maalum mbele za Mungu. Ni kweli leo Ibrahimu ni baba wa mataifa mengi. Kwanza, tunaona alivyo baba wa Wayahudi wote ambao wametapakaa duniani kote, pili tunaomwona namna alivyo baba wa Waarabu wote ambao nao wametapakaa duniani pote, na tatu tunamwona anavyokuwa baba wa imani kwa waamiini wote (kwamba kwa mfano wa Ibrahim aliyeamini na akawa rafiki wa Mungu) waumini kwa mlengo uleule tunapaswa kumwamini Mungu. Kwa namna moja au nyingine Mungu amelikuza jina lake kwa utukufu wake. Tunapomwomba Mungu kukuza majina yetu hatumaanishi kwamba tunataka kuwa wachoyo kwa kutaka kujulikana na watu wengine duniani! Ingawa pia suala hili nalo huunda sifa ya watu kadhaa hapa duniani. Hoja ya msingi hapa ni kwamba Mungu anapokuwa amelikuza jina lako, wewe unaendelea kubarikiwa zaidi. Unapaswa ujue kwamba Mungu mara nyingi hutumia watu wanaokuzunguka katika kukubariki. (ingawa zipo njia nyingi). Labda nitoe mfano mmoja kwako; ukiwa na biashara ya duka, na watu wakakufahamu wewe katika eneo hilo kwa ajili ya huduma yako nzuri, je watu hawatakuja kununua 52

kwako? nafikiri jibu ni kwamba watakuja bila shaka! Lakini tugeuke upande wa pili, je kama wewe wanakujua kwamba ni mwizi, na pia una chuma ulete katika duka lako, je watu wataendelea kuja? Nafikiri jibu ni dhahiri kwamba wale watakaokuja ni wale ambao hawakujui! Lakini wanaokujua hawawezi kuja kwako. Hivi ndivyo Mungu anavyofungua milango kupitia jina lako. Jina lako lako ni muhimu sana. Fanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba jina lako linabaki kuwa na sifa ile ile ambayo linatakiwa kuwa nalo. Jitahidi sana matendo yako yasije yakahaliribu jina lako. Epuka majina ya pili ambayo ni mabaya na yanaweza kuathiri utambulisho wako; kwa mfano watu wanapoanza kukuita “muongo yule” (baba uongo), kahaba, jambazi, shilawadu! Haya majina yana athari kubwa sana kwako. Huwezi kulibadilisha jina lako kwa maneno tu, bali matendo yako lazima yaambatane na maneno yako. Ukifanya hivyo, Mungu atafungua milango yake. Kila mtu anayekuzunguka atatamani kufanya kitu kwa ajili yako. Hii ni kweli kwa sababu Biblia inasema “Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao” (kwa kiingereza inaamanisha kwamba, Mungu husababisha kila kitu kinachokuzunguka kifanye mema kwa ajili yako).

53

Chochote

Kile

Unachokimiliki

Hakikisha

Kwamba

Umekigharimia Hakikisha kile ambacho umekimiliki ni mali yako kweli na kwa halali. Usikubali ofa za ajabu ajabu zitakugharimu! Badala ya kukigharimu hicho kitu wewe kitakugharimu. Maana yangu ni kwamba hata kama mtu anakupa kitu, basi kuwepo na sababu nzuri ya kukupa kitu hicho. Je lengo lake ni nini hasa kwa kukupa bure? Je unastahili kitu hicho kupokea? Ukishindwa kubainisha sababu hizi, ujue kwamba maisha yako ya baadaye yatakuwa katika hatari, ama ya mazoea kupokea burebure, au kwa kupewa kitu ambacho pengine si halali kwako na kuingia kwenye mtego wa adui. Kuna mifano kutoka katika maandiko Matakatifu vitu vya burebure! Ibrahimu alikataa mateka. Mw.14:21-23, Ibrahamu alikataa shamba la bure. Mwa. 23:7-14. Daudi naye alikataa kupokea vitu vya bure. 2 Sam. 24:18-25. Hii inanifanya niseme kwamba kama mtu akikupa mtaji; Ukipata faida rudisha mtaji wake ili asije akajivuna kwa kukusaidia. Unapaswa uiweke katika akili ya kwamba chochote unachopokea leo siyo cha bure. Maana ya dhana hii ni kwamba kuna mtu mwingine amegharimia na ndiyo maana wewe unakiona kama ni cha bure. Kwa hiyo kama hujatambua thamani ya kitu kile, basi hata siku ukipata cha kwako huwezi kutambua thamani ya kitu hicho. 54

Nimewahi kuwaona watu wengi wanavyotumia vibaya sana mali ambayo hawajaigharimia na wala hawajui inatoka wapi. Ninakumbuka mfano mmoja nilipokuwa kwenye masomo yangu Korea kusini; kulikuwa na rafiki yangu ambaye kila akienda bafuni alikuwa anatumia zaidi ya saa moja kuoga. Sasa siku moja nikataka kujua, huyu jamaa mbona anatumia muda mrefu sana bafuni huwa anafanya nini? Nilikuja kugundua kwamba anapokuwepo bafuni anajimwagia maji mwili mzima kwa muda wa zaidi ya nusu saa! Yaani hapo maji yanatiririka tu. Nikamuuliza siku moja, “ndugu yangu, mbona unamwaga maji kiasi hicho bafuni?.” Alinijibu kwamba “ndugu hapa kila kitu ni bure, maji haya ni ya bure kabisa, sasa kuna shida gani kumwaga maji mimi bafuni?” Baadaye nilimwambia kwamba “usichukulie kila kitu ni cha bure, kuna watu wamelipa.” Ndiyo! Kuna watu wanatoa sadaka kwa ajili ya chuo hicho, na mojawapo ya matumizi ya hiyo sadaka ni pamoja na kulipia maji. Ninayo mifano mingi sana juu ya namna watu wanavyoshindwa kuthamini vitu na kuviona ni vitu vya bure. Mfano mwingine, namkumbuka mtu mmoja alikuwa anafanya kazi katika kampuni fulani. Alikuwa anapenda sana kunipigia simu muda wa mchana kwa kutumia namba ya TTCL. Siku moja nikamuuliza, ‘….nakuhurumia sana kwa sababu unatumia gharama kubwa sana kwa ajili ya kunipigia simu, maana naona mtandao tofauti’ 55

alinijibu ‘aaaah usiwe na wasiwasi hii siyo hela yangu ni pesa za kampuni wanaweka vocha nyingi na hivyo nimeamua kukupigia wewe’ nami kwa sababu kipindi kile nilikuwa mdogo, basi tuliendelea kulonga! Sasa unaonaje hapo? Yaani huyu alichukulia poa matumizi ya simu kwa sababu siyo pesa zake, kwa sababu hajagharimia! Nataka nikwambie kwamba, kuna watu wanagharimia chochote ambacho wewe unakitumia bure. Lakini watu wanaopenda kumiliki na kutumia vitu vya bure, wakitendewa vile huwa wakali sana. Nilisimuliwa hadithi moja ya familia moja. Familia hiyo wote walikuwa wafanyakazi wa serikali. Pale nyumbani aliyekuwa anabaki ni mfanyakazi wa ndani peke yake. Kulikuwepo na simu ya mezani ambayo ama kwa hakika ilikuwepo pale kwa ajili ya kumpigia mfanyakazi wa ndani kwa ajili ya kujua hali ya hapo nyumbani. Siku moja baba wa familia aliichunguza simu na kukuta inatumika sana, na akajikuta kumbe huwa anaweka salio kubwa sana kwa mwezi. Akawaita wanafamilia wote na kuanza kuwaeleza kuwa, “mimi huwa situmii kabisa simu hii, maana natumia simu ya ofisini hata kupiga kwa rafiki zangu, je nani anayetumia simu hii?” kila aliyemuuliza alijibu hivi “baba mimi sijawahi kutumia simu hii, natumia simu ya ofisini kwangu, gharama zote hulipwa na ofisi.” Baba yule alipokosa majibu kwa wanafamilia wake, akamwita mfanyakazi wa 56

ndani na kumuuliza “Je wewe unatumia simu gani?” akajibu “natumia simu ya ofisini!” Baba akahamaki! Una ofisi wapi? Binti akamwambia, “si hapa ndio ofisini kwangu, kwa hiyo natumia simu hiyo hiyo kama ninyi mnavyotumia simu za ofisini!” Katika hali ya kawaida nafikiri walijifunza kutokana na majibu ya binti yule. Hakuna kitu cha bure! Halijikuta wamelipia gharama! Mara kadhaa nimewahi kuwaambia wapendwa kwamba hata wokovu wetu siyo wa bure, kuna mtu aligharimia-Yesu Kristo mwana wa Mungu aligharimia wokovu wetu kwa gharama kubwa ya kumwaga damu yake pale msalabani. Acha nyimbo za kizamani za kucheza na wokovu kwa kisingizio kwamba ni cha bure. Hakikisha kila unachomiliki, umekigharimia. Utasema, mbona wachungaji tukiwapa kitu mnapokea? Nikuulize swali, unajua mzigo aliona nao mchungaji kwa ajili yako? Kama huujui, basi nenda kamuulize na ulinganishe na vijisenti unavyompa!

Usijaribu kuishi maisha yanayokuzidi. I Tim 6:6 Biblia inasema “lakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.” Mahitaji ya mtu katika maisha yamefungwa na tamaa zake. Kwa hiyo hawezi kuridhika kabisa. katika mstari wa 5 unaona uovu wa tamaa. Watu ambao hawaridhi na vile wanavyotumia humpa Shetani fursa ya 57

kuwajaribu, kuwaongoza kwa kutumia njia za uaminifu, na njia nyingine mbaya, kuongeza mafanikio yao. Unakuta mtu mwingine hata hela hana za kutosha lakini anataka aishi kama mtu mwenye hela nyingi sana. kama unahitaji kula mboga siku hiyo, basi ule mboga za majani siyo kulazimisha kwenda kununua nyama. Kama wewe hoteli yako ni wali wa 500 usijaribu kwenda kwenye bei kubwa zaidi maana utakula hasara zaidi. Usijaribu kuiga maisha ya watu wengine. Kuna watu wengine ambao ukijaribu kujilinganisha nao utaumia tu. Acha kuishi maisha ya kufuata mkumbo mtu. Ishi maisha yako kwa kadri wewe ulicho nacho. Mungu amekupa uwezo mkubwa sana wa kuweza kutawala maisha yako. Ukitaka kufikia malengo yako lazima usiishi maisha ya zaidi yako.

Thamini kidogo kinachopita mikononi mwako. Yoh. 6:8-12 Kuna watu ambao hawapendi kuthamini kitu wanachopata, kwa hiyo kila kinachopita mikononi mwao, wao hukitumia vibaya bila thamani kabisa. Katika fungu hilo hapo juu tumeona kuwa Bwana Yesu aliwaagiza wanafunzi waweze kukusanya mabaki. Tunapaswa kujifunza kutokana na hili kuwa kile ambacho Bwana hutoa; iwe kidogo au ni kikubwa, yeye anataka kitunzwe vizuri. Hata ingawa anaweza kutoa

58

zaidi kuliko tunavyohitaji, hatupaswi kupoteza au kutumia vibaya. Yesu alisema ‘Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee chochote’

59

SURA YA NNE Umaskini ni nini? Ukiangalia kamusi mbalimbali zinatoa karibu maana sawa kwamba “ni hali ya kuwa na pesa kidogo, bidhaa, au kukosa njia za msaada au upungufu wa vitu muhimu katika maisha.”28 Tafsiri kama hii imeegemea sana kwenye mawazo ya watu na mashirika ambao wanaona umasikini katika masuala ya kiuchumi. Umaskini (kutoka neno la Kiarabu) ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, maji salama, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua. Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara.29 Umaskini wa kadri ni kuwa na raslimali chache zaidi au mapato madogo zaidi kulingana na watu wengine katika jamii au nchi au hali ya kadiri duniani. Hali hii pia hujulikana kama umaskini halisi au unyonge. Umaskini linganishi ni hali ya kuwa na rasilimali chache au kipato cha chini kuliko wengine kwenye jamii au nchi, au ikilinganishwa na wastani duniani kote. 28

http://www.dictionary.com/browse/poverty

29

Poverty | United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization. Iliwekwa mnamo 2015-11-04.

60

Kulingana na maelezo ya hapo juu tunaweza kugawa umasikini katka makundi mawili;

umasikini wa kwanza ni “umaskini wa

kawaida”, hapa mtu anao uwezo kidogo wa kufanya shughuli zake za kila siku, anaweza kukithi baadhi ya mahitaji yake ya msingi lakini kama likitokea jambo la dharura hawezi kabisa. Kwa mfano mtu huyu hawezi hata kulipia madawa hospitalini. Anategemea nguvu zake mwenyewe. Kama siku moja asipoenda kufanya kazi,basi familia inalala njaa! Lakini jambo lingine la msingi kwa mtu huyu ni kwamba hawezi kumsaidia mtu mwingine. Huyu mambo yake yamejichanganya kidogo tu, siku akufunguka anaweza kuwa mtu mwingine kabisa. Yaani anaweza kujikithi mwenyewe tu. Umasikini wa pili tunauita “fukara” hapa mtu hawezi kabisa kupata mahitaji yake maalumu. Na fukara wakati mara nyingi siyo kosa lake kwamba kwa nini amekuwa fukara bali ni kwa sababu maalum. (Yaani Sababu za Kimungu kama Yesu alivyosema ‘Maskini mnao tu sikuzote’ lakini pia Mungu Baba alijua kuwa miongoni mwa jamii kutakuwepo na maskini (Walawi 19:10, 23:22, 25:35; kumb. 15:7,8) Uebert Angel 30 alitoa maana pana ya umasikini. Yeye alidai kuwa “tafsiri ya umasikini siyo kwamba wewe huna gari au huna 30

Tafsiri hii iko kwenye mtandao wa yutubu katika chaneli yake inayopatikana kwa https://www.youtube.com/watch?v=n6PIM99ROgo

61

nyumba, ni jambo moja tu; kama huna uwezo wa kuwasaidia wengine wewe bado ni masikini. Kama una vitu vinavyokutosha wewe mwenyewe tu; gari moja,nyumba moja, hata kama ukiwa na basi dogo linakupeleka kazini kila siku, wewe bado ni masikini, ni tajiri kama unavyo hivyo lakini pia uweze kuwasaidia wengine, tunao watu wengi wenye pesa lakini suala la msingi je unaweza kuwasaidia watu wengine. kama wewe huna uwezo wa kununua angalau kwa fulana kwa mtu, basi wewe ni masikini.” Tafsiri hii inalenga kumwona mtu tajiri kama mtu anayeweza kumsaidia/kumlisha mtu mwingine. Katika tafsiri hii, mtu yeyote ambaye anaweza kumlisha mtu mwingine (nje ya familia yako) basi wewe ni tajiri au kwa lugha nyingine umefanikiwa! Watu wenyewe wanauzungumzia umasikini katika hali ya kupungukiwa kiuchumi, yaani hawana mahitaji ya kutosha. Jarida la Hakikazi Catalyst 31 linadai kuwa watu tofauti hufasiri maana ya umasikini kwa njia mbalimbali. Viongozi kwa kawaida hufikiria juu ya umasikini kwa kuangalia uwezo wa watu katika kununua mahitaji yao na kuuza bidhaa zao. Lakini fasiri ya umasikini ni kubwa zaidi. Kuna

31

Ukisoma katika tovuti hii, kuna mpango wa serikali ya Tanzania wa kupunguza umaskini wa mwaka 2001. Kama unahitaji taarifa zaidi unaweza kuzipata hapa, mimi nimechagua taarifa chache tu. http://www.hakikazi.org/tbu/preface.htm imepakuliwa tarehe 2/7/2017 saa 6:30 pm

62

fasiri ya kuzingatia matatizo ya kuwa na mgawanyo sawa katika kupata elimu na afya bora, kuwa na heshima na hadhi katika jamii, kujisikia kuwa una uwezo wa kutatua tatizo lolote linalotokea katika maisha yako, na hivyo kuwa na matumaini ya maisha. Kwa hiyo kuna mengi ya kufikiria wakati unapotaka kuondoa umasikini. Kwa hakika fikra nyingi haziko wazi mpaka unapofikiria kwa makini yanayotendeka katika jamii. Watu wa kawaida, wafanyabiashara, wafanyakazi serikalini, Mawaziri na viongozi wa nje wana mawazo tofauti kuhusu swali la umasikini ni nini. Wana mawazo tofauti kuhusu sababu za umasikini na jinsi ya kuuondoa. Katika dunia ya sasa watu hununua mahitaji yao kwa kutumia pesa. Kama hawana njia za kupata pesa watakuwa maskini. Umasikini mbaya zaidi ni ule ambao unawafanya watu wasiweze kupata chakula. Kwa hali hiyo, wanakuwa dhaifu na wanaweza kufa kwa njaa. Hali nyingine ya umasikini ni ile ambayo watu wanaweza kuwa na chakula kiasi au kidogo lakini hawana maji salama, huduma za matibabu, nyumba au mavazi bora. Watu wa kawaida walipoulizwa wajiepushe na nini ili wasiingie katika hali ya umasikini walitoa mawazo yafuatayo: Wamiliki ardhi, wapate zana za kilimo na teknolojia inayofaa, wapate misaada na 63

mikopo, wawe na usafiri mzuri (barabara na magari), waweze kupata masoko kwa urahisi, wawe na mipango bora ya matumizi ya maji, kujenga uwezo wa kuweka akiba , usalama kazini ,wapate huduma bora za jamii na miundo msingi (hasa afya ya elimu) , kupunguza rushwa, kuwe na uwazi zaidi, kuimarisha uwajibikaji na ushirikishwaji katika kuchangia kutoa maamuzi katika kiwango cha serikali za mitaa na serikali kuu, kujijengea fikra za kimaendeleo, kujenga uwezo wa mipango mizuri katika ngazi ya kijiji,

kuunda upya na kuimarisha

vyama vya ushirika, kuwawezesha wanawake wawe na madaraka zaidi katika kudhibiti mali ya familia, kujenga umoja, mshikamano, kuaminiana na hali ya kushirikiana 32 na kuondoa chama tawala na kuweka chama cha upinzani madarakani. Hata hivyo inasemekana kwamba mtu masikini ndiye anayeweza kutoa maana ya umasikini, kwa hiyo hat hiyo tafsri imeegemea na kuonekana imetolewa na mtu masikini au aliyefanya utafiti kwa watu masikini na wakampa majibu hayo. Shirika moja linaloshirikiana na benki ya dunia lilifanya mahojiano na watu wa nchi 47 ambapo kila

32

khj

64

mmoja alitoa maelezo yaliyoashiria umasikini. Nimechambua kauli kumi na moja hapa chini namna watu hao walivyojibu.33 1. “Usiulize nini maana umaskini kwa sababu umekutana nami nje ya nyumba yangu. Angalia nyumba na uhesabu idadi ya mashimo. Angalia vyombo vyangu na nguo ambazo nimevaa. Angalia kila kitu na uandike kile unachokiona. Unachoona ni umasikini wenyewe” Mtu mmoja nchini Kenya, 1997 2. “Umaskini ni udhalilishaji, maana ya kuwa tegemezi juu yao, na ya kulazimishwa, kukubali udanganyifu, matusi, na kutojali wakati tunatafuta msaada” -Latvia 1998 3. “Ninapoondoka asubuhi kwenda shuleni huwa sinywi kifungua kinywa chochote. Wakati wa mchana sili chakula, na inapokuwa jioni huwa ninapata chakula kidogo, na hiyo haitoshi. Hivyo wakati mimi ninapomtazama mtoto mwingine akiwa anakula, huwa moyo wangu unaumia, nadhani mimi nitakuwa na njaa siku moja.” Mtoto wa miaka 10, Gabon 1997 4. “Tajiri ana kazi moja ya kudumu; Maskini ni matajiri katika kazi nyingi.” – Pakistan 33

World Bank, Poverty Group, PREM December 1999 imepakuliwa katika http://siteresources.worldbank.org/INTPOVERTY/Resources/3356421124115102975/1555199-1124115187705/ch2.pdf tar. 2/7/2017 saa 3:39pm

65

5. “Kuwa maskini ni kuwa daima umechoka kwa kazi ngumu” Kenya 1996 6. “Mtu maskini lazima awepo ili aweze kumtumikia mkuu, tajiri. Ndiyo Mungu alivyopanga.” -Brazil 1995 7. “Umaskini ni suala la kurithiwa. Ikiwa umezaliwa kwa familia masikini, kamwe huwezi kuwa tajiri hata siku moja, kila kizazi kitakachofuatia kitakuwa masikini tu” -Uganda 1998 8. “Katika familia yangu ikiwa mtu ni mgonjwa sana, tunajua kwamba tumeshampoteza huyo, kwa sababu hatuna fedha za kutosha kwa ajili ya chakula, je tunawezaje kupata pesa ya kununua dawa? “-Vietnam 1999a 9. “Niliuza ardhi yangu na sasa sina kitu. Siwezi kamwe kuinunua ardhi yangu tena kwa sababu bei za ardhi zinaongezeka kila mwaka.” -Tanzania 1997 10. “Masikini hana ratiba, hata kama ulikuwa umepanga kwenda sehemu fulani, ukiitwa na bosi wako lazima ukimbie haraka na kuacha ratiba zako zote, hakuna uhuru wowote, hofu tu”Tanzania-2017 11. “Watu wameweka matumaini yao kwa Mungu, kwani serikali haifai tena katika masuala ya kuwasaidia watu wake”- Armenia 1995 66

Kulingana na kauli hizo hapo juu, ni wazi kwamba upungufu wa mahitaji maalumu katika maisha ndicho kitu kinachoitwa umaskini. Biblia ina mengi ya kusema juu ya kuwa maskini, na tuna mifano mingi ya watu masikini katika Maandiko. Hata hivyo kuwa maskini sio lazima ishara ya kukataliwa na Mungu. Kwa kweli, inawezekana kuwa maskini katika mambo ya kimwili lakini matajiri katika mambo ya kiroho (angalia Ufunuo 2: 9). Uchunguzi unaonesha kwamba kuna matumizi ya neno masikini (poor) katika Biblia mara 178. Ingawa kuna tofauti tofauti kidogo, neno “masikini” limeenda sambamba na masuala ya kiuchumi kama vile: kukosa chakula, kushindwa kumudu mahitaji fulani, kushindwa kujitegemea, kukosa mavazi, kuwa na madeni, nk. Hebu chunguza mistari ifuatayo hapa chini:1. “Lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao

maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni. (Kut. 23:11) 2. “Tena kwamba ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na 67

sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;” ( Law. 14:21). 3. “Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake

umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri.” (Law. 25:35). 4. “Mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake;

kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako.”(Kumb. 24:15) 5. “Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze

ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.” (Math. 19:21) 6. “Maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya

changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini.” (Rum 15:26) 7. “Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye

mavazi mabovu;” (Yak. 2:2) Katika mafungu yote hapo juu, tunaona kwamba neno maskini katika linahusu hali ya kiuchumi, lakini sababu zinazohusiana na hali 68

hiyo ni ngumu. Hazijabaininishwa wazi. Lakini kupitia maandiko mengine ya Biblia tunaweza kupata sababu za umasikin.

Chanzo cha umaskini Nimeona ni vyema tukaangalia Biblia inasema nini juu ya chanzo cha umasikini. Kusudi langu la kutalii kibiblia ni kukufanya wewe kama uko kwenye kundi hili uangalie kama kuna chanzo chochote ambacho kinakugusa. Ingawa biblia haijasema kwamba umasikini ni dhambi, lakini bila shaka pia wakati mwingine kuwa maskini ni matokeo ya uchaguzi mbaya.

Kutokumtii Mungu Hiki ni chanzo kikubwa cha umasikini hapa duniani. Tukianza kusoma kitabu cha Mwanzo kinatuambia chanzo kuwa masikini ni kwa sababu mwanadamu wa kwanza alimkosea Mungu na hivyo hakuja jema lolote ambalo linaweza kupita mikononi mwake lisiwe na uchungu. Mw. 3:17-18 neno linasema “kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale, ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni.” Ukiangalia msitari huu unadhihirisha kwamba anguko la binadamu ndilo lililovuruga kila kitu kabisa. ni dhahiri kwamba kabla ya 69

anguko maisha ya mwanadamu hayakuwa ya taabu hata kidogo, lakini baada ya hawa wanadamu kushindwa kumtii Mungu, tunaona ardhi inaambiwa badala ya kuzaa mahindi-inazaa miiba, hata kula kwenyewe ni kwa shida, halafu angalia sehemu ya mwisho inavyoonesha kwamba kumbe Adamu alikuwa anakula nyama kiurahisi tu, lakini sasa kaongezewa majukumu ya kula mbona za kondeni. Kwa mtu ambaye anaishi mazingira magumu hii hoja anaweza kuielewa vizuri sana, mtu anakula nyama baada ya mwaka mmoja na pengine anakula kwa jirani. Kwa sababu ya anguko ndiyo maana mambo yalivurugika kabisa. mojawapo ya hoja tano za misingi ya Ukaliviniti ni kwamba mwanadamu ameharibika kabisa, kila kitu kiko hovyo hovyo. Hii hoja haimaanishi kwamba matokeo ya dhambi yako kiroho tu, bali n ahata kimwili pia mwanadamu ni mgonjwa, chanzo chake ni anguko, na anguko ni pale binadamu aliposhindwa kumtii Mungu. Mungu alipokuwa amewachagua wana wa Israeli kuwa taifa lake teule aliwaagiza kutii neno lake na pindi walipokataa iliwalazimu kupata shida na mahangaiko kutoka kwa maadui zao. Hii iliambatana na kula kwa shida, magonjwa na mapungufu mengi katika maisha yao. Kumbukumbu la Torati 28: 47-48 inasema kuwa “kwa kuwa hukumtumikia Bwana kwa furaha na moyo wa kushukuru kwa ajili ya 70

ule wingi wa vitu vyote, kwa hiyo utawatumikia adui zako atakowaleta Bwana juu yako, kwa njaa na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote (umasikini)…”Ukiangalia hapa unagundua kabisa kwamba shida ni kule kushindwa kumtii Mungu wetu na ndiyo maana mashindano wa kupata na kukosa yameendelea kuwepo hapa duniani.

Kwa sababu ya kudhulumiwa Kuna mazingira mengine ambayo umasikini husababishwa na kudhulumiwa na watu wenye nguvu zaidi, siyo watu hata nchi mbalimbali zimedhulumu nchi zingine katika hali ya juu sana, na matokeo yake pengo hili limeendelea kuwepo. Hii haimaanishi kwamba kila

aliye

tajiri

amedhulumu

mtu,

lakini

kuna

wale

ambao

wamedhulumu. Kuna ushahidi katika jamii inayotuzunguka namna wajane wanavyotendewa na shemeji zao; kabla ya mume wake kufariki maisha yalikuwa mazuri, lakini baada ya kufariki wanamnyang’anya kila kitu. Je unafikiri mama huyu ataishia wapi? Tena bora labda akiwa na watoto wakubwa, asipokuwa na mtoto itakuwaje? Hii ndiyo changamoto ya jamii inayotuzunguka. Nimewahi

kusimuliwa

habari

ya

ndugu

wa

marehemu

walipokuwa kwenye msiba wa kaka yao, baadhi yao waligawana majukumu-huku mke wa marehemu analia, wengine wanatafuta hati ya 71

nyumba, viwanja na hata mali zingine. Baada ya mazishi, siku mbili, mama wa watu akaanza kuangalia nyaraka, hakukuta hata karatasi moja, vyote wamekusanya. Baada ya muda siyo mrefu mama wa watu aliambiwa “hii nyumba siyo yako, unatakiwa kuondoka haraka sana” kumbe hao jamaa wameshauza kila kitu. Dhuruma ya hali ya juu! Wamama niwashauri tu, unapokuwa umefiwa, usijidai kwamba wewe unajua sana kulia na unasahau kila kitu, acha ujinga huo. Chukua vitu vyaraka muhimu kama vile vyeti vya ndoa, hati za viwanja na vyumba nk. Ni kweli ulimpenda mumeo, lakini ndio hivyo tena hunaye. Ukizubaa utaona baadaye! Lakini kuna waajiri wengine ambao siyo wazuri sana, wanadhulumu wafanyakazi masikini ambao wameenda pale kwa ajili ya kujitafutia vipato vidogo vidogo ili mkono uende kinywani. Nimewahi kuona waajiri wengi wakiwadhulumu wafanyakazi. Sasa fikiri mtu amefanya kazi kwa muda wa miezi zaidi ya mitano, halafu mwishowe hapokei mshahara na baadaye anafukuzwa kazi. Unaonaje? Kama asipokuwa makini ataishia kuwa ombaomba mtaani. Kwa hiyo dhuluma kwa watu wengine ni mbaya sana na inaweza kusababisha watu wengine wawe masikini. Yakobo aliwahi kuwaonya wakristo matajiri kwa habari ya kudhulumu wafanyakazi. Anasema “angalieni ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na 72

vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi” (Yak. 5:4). Hapa tunaona kwamba hawa matajiri walifanyiwa kazi na watu bila kuwalipa mishahara yao. Yakobo anawaambia kwamba haki ya masikini haipotei bali Mungu anasikia kilio chao. Ninakumbuka nilipokuwa na umri wa miaka kama kumi na mbili mpaka kumi na saba hivi, pale kijijini kwetu Tindabuligi tulikuwa tunafanya kazi ya kushindilia magunia ya pamba. Wakati wa mavuno ya pamba, magari mengi yalisomba pamba hizo. Kwa hiyo kila tukiona gari tulikuwa tunakimbia haraka kwa ajili ya kwenda kushindilia magunia. Nakumbuka gunia moja lilikuwa linabeba kama kilo hamsini. Sasa usifikiri kilo za pamba ni za kuweka tu, unashangaa rundo la pamba haliwezi kufikisha hizo kilo! Maelezo haya yote nataka tu kukuambia kwamba haikuwa kazi ngumu. Lakini jambo la kushangaza, baada ya kuhangaika kushindilia usiku kucha, karani anapokuja asubuhi hajali kabisa hali ya watu walioshindilia,na hapo anajali wale wanaopakia ili gari liondoke. Sasa mnaanza kuomba hela yenu kwa kubembeleza! Mara nyingi sana tulikuwa tunadhulumiwa. Umeshindilia magunia yako kumi usiku kucha, ambayo kwa miaka ya 1990 gunia moja ilikuwa ni kama shilingi 50 x 10= 500. Sasa usifikiri hiyo hela ni kidogo! Kipindi kile chai ilikuwa ni shilingi 10 na chapati shilingi 20, sasa hapo unakula chapati za shilingi 80 na chai kikombe kimoja, unatumia shilingi 90 tu. 73

Lakini jambo la kusikitisha kabisa, mara kwa mara tulikuwa tunadhulumiwa hela zetu. Na ndiyo maana pengine ndiyo maana hata vyama vya ushirika vilikufa, kwa sababu ya dhuluma. Siyo hivyo tu, kuna watu wengine walikuwa wakiuza pamba zao wanaambiwa kwamba pesa itakuja jioni. Wanapoenda jioni, karani haonekani eneo hilo! Yaani mkulima amehangaika miezi zaidi ya minne akihangaikia pamba yake, halafu mwishowe anadhulumiwa. Haya mambo tumeyashuhudia. Kwa hiyo Yakobo anapoonya habari za matajiri kudhulumu watu wengine, anajua na pengine maskini walienda kulalamika kwake kwa sababu alikuwa ni kiongozi wa kanisa. Maandiko yanazungumzia dhuluma ambayo inasababisha mtu mwingine awe masikini. Mithali 13:23 inasema kuwa “chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.” Mwandishi hapa bado anaonesha tatizo la dhuluma katika jamii.

Kwa sababu ya uzembe Umaskini mwingine ni kwa sababu ya uvivu au upumbavu wa maadili, yaani mtu anakuwa mpumbavu na kushindwa kujipatia mahitaji ya kila siku na kutegemea msaada kutoka sehemu nyingine. (2 Wathesalonike 3:11, Waefeso 4:28, Luka 15: 11-24). Viongozi wa 74

kanisa walitakiwa kuwaonya wajinga katika makanisa haya (1 Wathesalonike 5:14) na kurekebisha miendo ya wavivu (Tito 1: 12-13, 1 Wathesalonike 4: 11-12). Uzembe katika maisha ya mwanadamu huleta uvivu wa hali ya juu kiasi kwamba mtu anashindwa kufanya kazi yoyote ya kumwingizia kipato. Mithali 10:4-5 inasema kuwa “Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha. Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.” Maelekezo ya mistari hii miwili yanaonyesha jinsi mtu mmoja anavyofanikiwa na mwingine anashindwa. Mtu mvivu ni tofauti sana na mtu mwenye bidii. Pia katika Mithali 12:24, anasema jambo hilo hilo kuhusu uzembe na uvivu. “Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.” Mstari wa 27, “mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.” Na 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.” Mafungu haya yote yanakemea tabia ya kuwa mvivu na mzembe kwa sababu matokeo yake kuwa masikini. Hebu tafakari namna uzembe ulivyokupotezea fursa nyingi katika maisha yako. Kuna watu wengi wamefukuzwa kazi kwa sababu ya kuwa 75

wazembe. Kuna wakulima wengi mashamba yao yanazidiwa na palizi kwa sababu ya kuwa wazembe wa kuamka mapema na kwenda kulima. Kuna wanafunzi wengi wanafeli katika masomo yao kwa sababu ni wazembe wa kusoma nakala za waaalimu na vitabu, wao husoma mtihani ukikaribia-je inawezekanaje kufanana na aliyesoma tangu akiwa mwanzo. Kuna watu wengi tunawashuhudia kwa sababu ya uzembe wao wanakuwa ni watu wanaopenda kulalamika juu yaw engine, wanaona kana kwamba hawatendewi haki na jirani zao, rafiki zao na hata nchi zao. Wavivu wengi ni wambea! Ukiona mtu ambaye ni ana majungu mtaa mzima, ujue yule kuna uwezekano ana uzembe fulani! Kwa taarifa yako, kufanikiwa kwa mzembe ni kama ngamia kupita katika tundu la sindano. Wazembe ni watu wanaojua kutembelea ndugu zao nyakati zote bila kujali kwamba wako kazini au la, na wakifika huko wasipotendewa mema kama walivyotarajia,, basi utasikia wanaanza kusema maneno lukuki. Wazembe hawafai hata katika mambo ya ibada. Mtume Paulo aliwaonya Wathesalonike kuhusu kuwa wavivu (2 Wathesalonike 3: 7-12). Hawa waumini wa Thesalonike walikuwa ni wakristo kuliko hata wewe! Walikuwa wanamsubiri Yesu Kristo aje mapema iwezekanavyo, kwa hiyo waliachana na kazi za kila aina. Maana yake kama ni kushinda kanisani wakipiga sala – walishinda! Kama ni kwenye mikesha-walishinda, kama ni kwenye kutembelea 76

waumini wenzao-hawakuwa nyuma. Hayo mambo yote ni mazuri sana na lazima kila mkristo ayafanye, lakini Paulo hakulitaka miongoni mwao. Wao walijisahau kabisa wakaona kanisani ndo wamefika! Washirika, wachungaji-ni wakati wa kanisa kuchangamka sasa. Kama unamuona mtu kila siku kanisani; asubuhi mpaka jioni, muda wa miezi miwili, muulize “ndugu vipi siku hizi, kazi huna?” Ukifanya hivyo unaweza kumwokoa na roho ya uzembe. Wakristo wanapaswa kushiriki kazi za kanisani zote pasipo kukosa, lakini kanisa pia linahitaji kuwa na ratiba ya kufanya mambo yake ili kuwaruhusu watu kufanya kazi zao binafsi. Kwa upande wa watumishi wa Mungu, tujifunzeni kwa Paul, yeye ni mfano wa mtu aliyekomboa wakati aliokuwa nayo na kuitumia vizuri.

Mungu anakupima na kukuthibitishia kama utamwacha au hutamwacha Wakati mwingine kupungukiwa katika maisha yetu kunakuja kutokana na kusudi la Mungu la kutaka kutupima sisi kama tutaendelea katika imani zetu. Mungu ameahidi kutimiza mahitaji yetu ya kila siku. Inapotokea tumekosa mahitaji hayo, anatarajia kutuona tukiwa tumesimama pasipo kuyumbayumba. Ninahitaji kufafanua zaidi juu ya hili ili usichanganyikiwe! 77

Maandiko matakatifu yanasema kwamba Mungu hamjaribu mtu kwa maovu na wala yeye hajaribiwi. Maana yake ni kwamba, hakuna sababu ya mwanadamu kuanguka katika dhambi na kudai kwamba hilo lilikuwa ni jaribu la Mungu. lakini ninachotaka kuzungumza mahali hapa ni kwamba wakati mwingine Mungu huruhusu hali ngumu katika maisha yetu ili atupime. Agano la Kale na Jipya, maneno yaliyotafsiriwa kwa ajili ya kumpima mtu ni "mtihani" inamaanisha "kuthibitisha kwa majaribio." Kwa hiyo, wakati Mungu anajaribu watoto wake, kusudi lake ni kuthibitisha kwamba imani yetu ni ngangari. Sio kwamba Mungu anahitaji kuthibitisha kwamba eti hakujua itakavyokuwa kwako (tumeshajadili kwamba Mungu anajua yote kabisa) lakini yeye anatuhakikishia kwamba imani yetu ni thabiti, yaani hapo Mungu anakutangazia wewe ushindi, ili unapokumbana na mambo mazito katika maisha yako, basi uwe umeshajua kiwango chako cha imani. Pia anataka kututhibitishia kwamba sisi ni watoto wake kweli, na kwamba hakuna jaribio litakaloshinda imani yetu. Katika mfano wa mpanzi, Yesu anawatambua wale ambao huanguka kuwa ni wale wanaopokea mbegu ya neno la Mungu kwa furaha, lakini, mara tu wakati wa majaribu unakuja, huanguka. Yakobo 78

naye anasema kwamba kupimwa kwa imani yetu kunaendeleza uvumilivu, kisha ukomavu katika safari yetu ya mbinguni (Yakobo 1: 34). Yakobo anaendelea kusema kwamba kujaribiwa ni baraka, kwa sababu, wakati majaribio yanapokuwa wamekwisha, tutapokea taji ya uzima, ambayo Mungu amewaahidi wale wanaompenda" (Yakobo 1: 12). Mitihani katika maisha hutoka kwa Baba yetu wa mbinguni ambaye anafanya kazi zote kwa ajili ya wema kwa wale wanaompenda na ambao wanaitwa kuwa watoto wa wake (Warumi 8:28). Kwa hiyo unaweza ukaona kuwa; majaribu ya shetani hulenga kukuangusha katika dhambi, lakini majaribu ya Mungu (tuite mitihani) hulenga kututhibitishia imani yetu na kutupatia mema zaidi. Mwalimu mzuri huwapa wanafunzi wake mitihani ili awafanye wajipime wenyewe viwango vyao vya ufaulu na siyo kwamba anataka waanguke. Ukikuta mwalimu anatoa mitihani kwa lengo la wanafunzi waanguke huyo ni shetani mdogo! Nilipokuwa nasoma katika chuo kikuu cha Dar es salaam nilipata kusimulia hadithi ya ukweli ya mhadhiri mmoja pale chuoni. Yeye alikuwa anatunga mitihani ya kuwakomoa wanafunzi wake ili waanguke. Katika kila mtihani wake asilimia tisini na tisa walikuwa wakishindwa kabisa. Siku moja mwanafunzi mmoja alitaka kujua kwa nini wanashindwa sana. Hivyo akamfanya mpango wa kuiba mwongozo wake wa usahihishaji (marking scheme). Mwanafunzi huyo alifanikiwa, 79

na siku ya mtihani alibahatika kuingia na mwongozo huo na kunakili kila kitu kilichokuwa katika mwongozo huo. Matokeo yalipotoka, huyo mwanafunzi alishika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia hamsini ya alama zote! Sasa wakamuuliza mhadhiri huyo, je kama wewe mwenyewe umepata hamsini, je sisi wanafunzi wako tutapata ngapi? Habari hii ilinistua sana, lakini pia iliniweka sawa kama ujuavyo mwanafunzi wa mwaka wa kwanza anapenda kusikiliza kila kitu. Ninachotaka hasa kukueleza ni kwamba Mungu hafanani na huyo mhadhiri, wala Mungu hafanani na shetani mwenye lengo baya siku zote katika maisha yetu. Mungu hutaka kututhibitishia imani zetu kupitia mitihani. Na lengo la Mungu ni kwamba wewe ufaulu. Kwa hiyo unapoingia katika maisha magumu lazima ujue kwamba pengine Mungu anataka kukusimamisha namna unavyoendelea katika imani yako. Ukisoma katika Waamuzi 3:1-2 tunaona baadhi ya mataifa katika nchi ya Kanaani ambayo Mungu aliyaacha kuyaondoa ili kuwajaribu (kuwapima) na kuwafundisha vita wana wa Israeli. Ukiendelea kusoma utagundua kwamba mataifa hayo yaliwasumbua sana wana wa Israeli, wakati mwingine waliteswa kwa zaidi ya miaka arobaini na hata zaidi. Lengo la Mungu liko palepale; alitaka kuwapima na kuwafundisha vita. Kwa hiyo shida na mikasa ya umaskini mingine hupaswi kulia lia bali 80

unahitaji kuwa na misuli ya kuvumilia ili ukitoka hapo utakuja kuwa kama dhahabu. Ukisoma historia ya matajiri wengi ambao wametajirika kwa njia halali (katika kitabu hiki sitaki kujadili utajiri wa nguvu za giza) watakueleza namna walivyovumilia mapito magumu katika maisha yao. Ukiwauliza vizuri watakueleza namna walivyokuwa wakiuza maji ya kwenye mifuko ya nailoni. Watakwambia namna walivyotembeza pipi mtaani. Watakwambia namna walivyofanya kazi ya umama ntilie kwa miaka mingi. Watakwambia namna walivyolima vibarua mashambani mwa watu kwa siku nyingi! Haya mambo yapo kabisa. Lakini katika hayo, Mungu anaangalia stamina yako ya kuvumilia huku ukiendelea kumtegemea yeye peke yake. Jambo kama hili liliwahi kunitokea katika maisha yangu hapo nyuma! Mimi siyo mtu tajiri lakini pia siyo mtu masikini! Ila ninavyo vitu vyote ninavyohitaji kwa sababu Bwana hunipa kila nikihitaji. Nisipokuwa na kitu chochote maana yake Mungu hahitaji niwe nacho, na kama nikihitaji Napata kwa muda mfupi. Uwe makini, usiige! Nakumbuka miaka ya 1992 nilikuwa na uwezo wa kupalilia ekari moja kwa siku mbili tu. Na nilikuwa ninafanya kwa uaminifu kweli kweli, kwa hiyo mabwana wengi walinipenda na kunikaribisha kulima kwenye 81

mashamba yao. Nakumbuka nilipoamua kwenda kusoma chuo cha Biblia Kolandoto, Shinyanga, sikuwa na hela kabisa. nilikamata kibarua cha kufyatua tofali kwa mwalimu mmoja pale kijijini. Kufyatua tofali moja miaka ya 2002 ilikuwa shilingi 10 (tofali la udongo), hapo wewe mwenyewe ndio unasomba maji, wewe mwenyewe ndio unachnganya, kwa kifupi kila kitu unapaswa kufanya. Kama yangu alinisaidia kufanya kazi hiyo. Mwisho wa kazi tulifyatua tofali 3000 na kugawana pesa hiyo. Pesa hiyo ilikuwa nusu ya ada ya chuoni; nikajikusanyia kusanyia vishilingi, yule mwalimu akanisaidia nauli na pesa ya kulala njiani, kaka yangu akatoa kiasi fulani. Nikaenda chuoni! Nikiwa chuoni mambo yalikuwa mazuri tu. Lakini baada ya likizo ningefanyaje? Nani atanisaidia kulipa ada ya chuo? Nilirudi nyumbani kwa furaha lakini furaha yangu iliisha muda mfupi baada ya kuanza kujiuliza maswali hayo. Hapo napo nikaanza kujishughulisha! Nikaanza kusoma mahindi na kuanza kuuza mtaani (kwa kisukumakugalagaja). Nilikuwa naendesha baiskeli kwa mwendo wa kilometa 50 mpaka 60 kwa siku, huku nimebeba gunia la mahindi! Pesa niliyoipata kutokana na kazi hiyo haikutosha kulipa ada, lakini niliamua kwenda tu. Katika

maisha

nilikuwa

nimejifunza

kutokumwomba

mwanadamu yeyote zaidi ya Mungu. kwa sababu pesa haikutosha, ilibidi 82

niombe baiskeli kwa mmisionari mmoja pale chuoni ili niende angalau nikapate pesa kijijini kwa kipindi cha likizo fupi. Mmisionri huyo kwa huruma akaniuliza “kweli wewe unataka kwenda kutafuta pesa au unataka kurudi nyumbani tu?” nilijibu kwa ujasiri kwamba “nataka kufuata pesa.” Basi akaniambia kwamba kuna kazi ya kufanya! Mimi pamoja na wanafunzi wengine waliokuwa na matatizo kama mimi tukapewa kazi ya kufuata mbuzi katika mnada fulani maeneo yale. Safari hiyo sitaisahau katika maisha yangu yote. Ilikuwa ni mwendo wa saa moja kwa gari, nasi tulipaswa kurudi kwa miguu tunaswaga mbuzi. Nafikiri unaweza kuona namna shughuli ilivyokuwa pevu na ilihitaji kuvumilia kwa namna ya ajabu sana. Unajua kwa nini nimekushirikisha hadithi yangu? Nataka nikuambie kwamba, Mungu anayo mipango mizuri kwa ajili ya maisha yetu, na mipango hiyo iko mbele yako! Ushuhuda unajenga na kutia moyo. Hebu naomba utiwe moyo na neno la Mungu pamoja na ushuhuda niliokushirikisha na ninataka nikuhakikishie kwamba mimi siyo yule wa miaka ile. Nimeendelea kuuona mkono wa Mungu. Kama ambavyo nimekuwa nikisisitiza, mimi nina kila kitu! Maana yake ni kwamba kama nikihitaji kitu, Mungu atanipa-kama hanipi maana yake sikihitaji! Kwa hiyo, mojawapo ya sababu za kupungukiwa na kuwa 83

katika hali ngumu katika maisha yetu ni Mungu anataka kukuthibitishia kwamba wewe hautamwacha au utamwacha.

Mungu anakutambulisha kwa Shetani Mungu anataka kutambulisha imani yako kwa shetani. Ayu. 1:8-11. Mungu hupenda kujivunia watu wake walio na uwezo wa kuvumilia majaribu. Si kwamba Ayubu alikuwa amefanya jambo lolote lakini kwa sababu ya mazungumzo ya Mungu na Shetani basi akaangukiwa na mzigo huo.Aliyeanzisha mazungumzo yale ni Mungu na wala siyo shetani- Sasa katika mambo kama haya huwezi kuanza kufunga na kuomba kwa sababu Mungu mwenyewe ndiye ameanzisha. Pia huwezi kukemea pepo kwa sababu pepo huyo kapata kibali kutoka ikulu! Mungu anapenda kujivunia watu wake kwa shetani anapoona kwamba wanaishi maisha yanayompenda yeye. Mungu anataka kuona uvumilivu wako na namna unavyompenda yeye. Waru. 5:3-5 Mungu hupima uvumilivu wetu na namna tunavyompenda wakati anaporuhusu mambo magumu kutokea katika maisha yetu. Mungu hupenda kujivunia watu wake na kumwambia adui yako kwamba, unamwona fulanijapokuwa hana kitu chochote sasa hivi lakini bado ananitegemea! Anataka kumthibitishia adui yako kwamba utegemezi wako kwa Mungu

84

hautegemei mali ulizo nazo. Uwe umepata, au umekosa-utabaki kusimama na Mungu siku zote za maisha yako

Umaskini mwingine ni matatizo ya kiroho tu Biblia wakati mwingine imetueleza vyanzo vya matatizo ya kiuchumi na umaskini kwa ujumla kuwa unaweza kusababishwa na matatizo ya kiroho. Katika 2 Samuel 21:1-2 tunasoma hivi “Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.” Tukiangalia hapa tunaona ni mfululiza wa matatizo ya ukame wakati wa utawala wa mfalme Daudi. Mwaka wa kwanza ulipitia-Daudi akaona ni hali ya kawaida tu, labda hali ya hewa imebadilika kidogo, hamna shida mwakani mvua itanyesha! Mwaka wa pili unafuatia, hali inaendelea vile vile, na pengine Daudi alijisemea “hii ni hali ya kawaida tu, maana tunasoma hata historia inatuambia kwamba kulikuwa na njaa zingine hata miaka saba, sasa hapa ni miaka miwili tu.” Hayawi hayawi, mwaka wa tatu huo! Ukame ndo unazidi kupamba moto, hakuna nyasi wala nini! Daudi akastuka, akasema hebu ngoja nimwombe Bwana! Jibu alilolipata kutoka kwa Mungu lilikuwa ni tatizo la kiroho. Najua sasa tunaenda vizuri! 85

Tatizo tunaambiwa ni kwa sababu ya Sauli kushindwa kutunza agano na Wagibeoni. Wagibeoni ni watu wenye kuvutia zaidi sana. Waandishi wanawaelezea kama Waamori (21: 2), lakini wanajulikana zaidi kama Wahivi (Yoshua 9: 1, 7; 11:19). Hawa Wagibeoni walikuwa kati ya wale watu walioishi Kanaani, ambao Mungu aliwaamuru Waisraeli kuwaangamiza (Kutoka 33: 2; 34:11; Kumbukumbu la Torati 7: 1-2). Chini ya uongozi wa Yoshua, Waisraeli walikuwa wamevuka tu mto Yordani (Yoshua 3) na kuutwaa mji wa Yeriko (sura ya 6), halafu Ai (sura ya 7 na 8). Mji uliofuatia baada ya miji hiyo ilikuwa ni Gibeoni, na Wagibeoni waliijua ratiba hiyo mapema. Wakagundua kwamba hapo wasingepona bila kuwaingiza Waisraeli kwenye mambo ya kiroho ya kufanya agano pamoja nao. Tumekwisha kuona kwa sehemu kuhusu maagano. Katika historia ya Agano la Kale na Jipya, Mungu alihusika na watu aliofanya nao agano. Wakati Mungu aliokoka Nuhu na familia yake, alifanya agano nao na kutoa upinde wa mvua kama ishara ya agano hilo (Mwanzo 9: 1-17). Mungu baadaye alifanya agano na Ibrahimu, na ishara yake inayoambatana na kutahiriwa (Mwanzo 12: 1-3; 17: 1-22). Kisha Mungu alifanya agano na Israeli kupitia Musa, na ishara yake ilikuwa Sabato (Kutoka 19-20, 31: 12-17; Kumbukumbu la Torati 5). Mungu alifanya agano na Daudi kumjenga nyumba ya milele (2 86

Samweli 7: 12-17). Kisha kuna Agano Jipya lililofunguliwa na Bwana wetu Yesu Kristo kupitia kumwaga damu yake (Yeremia 31: 31-34; Luka 22:20, 1 Wakorintho 11:25, 2 Wakorintho 3: 6; Waebrania 9: 1122). Mungu hakuwahi kushughulika na wanadamu kwa kiholela tu bali daima ameshughulika pamona na watu wake kulingana na agano. Kwa hiyo agano lilikuwa ni suala la kiroho kabisa! Kinachosikitisha ni kwamba Sauli alisahau kabisa agano hili! Mahala pengine Sauli alikuwa makini na masuala haya. Kwa mfano katika 1 Samweli 15: 5-6, tunaambiwa kwamba Sauli alikumbuka kwamba Wakeni walitoa msaada kwa Israeli wakati wa kutoka Misri, na hivyo aliwaokoa wakati alipopigana na Waamaleki. Sasa swali la msingi, je Sauli aliwezaje kusahau agano la Waisraeli walilofanya na Wagibeoni? Ni vigumu kuamini kwamba alisahau bali tunaweza kusema kwamba alipuuzia tu. Labda aliona upuuzi waliofanya babu zake kuingia agano la Wagibeoni? Kweli ulikuwa ni upuuzi mtupu, kwani hawakumuuliza Mungu wakati wa kufanya agano hilo. Lakini hiyo haisaidii

kabisa-ukishaingia

kwenye

agano,

umejifunga!

Tayari

walitakiwa wafuate makubaliano ya Agano! Mungu anafanyia kazi maagano. Inashangaza kuona kuwa Sauli alikataa kuwaangamiza kabisa Waamaleki, ambao Mungu alimwamuru awaue wote (1 Samweli 15), na 87

akajaribu kuwaangamiza Wagibeoni, ambao hakuwa na kibali cha kuwaua. Njaa kubwa ilitokea kwa sababu ya upuuzi huu. Daudi hakujua kabisa shida ya njaa mpaka alipoamua kumwomba Mungu kwa uaminifu, na Mungu alimwambia tatizo hilo la Wagibeoni, tatizo ambalo lilisababishwa na mfalme wa kwanza wa Israeli. Daudi hakuanza kukemea na kudai “unajua Mungu mimi sikuwepo, sasa unaletaje njaa kwenye utawala wangu?” Neno linasema hivi “ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaaambia..niwatendee nini? Na kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa Bwana?” (2 Sam.21:2-3). Wagibeoni walitangaza wazi kwamba hawakuhitaji fedha. Pesa haiwezi kufuta damu ambayo Sauli alikuwa ameimwaga. Walisema pia kwamba "hatuwezi kumwua mtu yeyote katika Israeli" (mstari wa 4). Kwa kuwa wao walikuwa chini ya kongwa la Wayahudi, hawakuwa na kibali cha kumuua Myahudi yeyote. Wagebeoni waliomba suluhisho lao liwe kupewa watoto saba wa Sauli ili wawaue kwa kuwatundika juu ya mti. Kutundikwa juu ya mti ilikuwa adhabu inayotumiwa kwa uhalifu mkubwa (angalia Mwanzo 40:19, Kumbukumbu la Torati 21: 22-23; Yoshua 8:29; 10:26). Daudi aliwapatia hayo mahitaji yao nao wakatimiza matakwa yao kama walivyosema (Daudi alikuwa makini sana alipokuwa anawakabidhi hao 88

Wagibeoni wana wa Sauli34 kwa sababu alitaka kutunza agano lake na Yonathani mwana wa Sauli (mst 7) kwa hiyo alimtorosha Mefiboshethi. Baada ya kutatua shida hii, hatuoni tena suala la ukame katika Israeli katika kipindi cha Daudi. Ni kwa sababau alishughulikia tatizo la kiroho ambalo lilikuwa limesababisha ukame wakati wa utawala wake. Nafikiri umeshaanza kuelewa sasa kwamba kuna wakati mwingine hali ngumu zinanaweza kutukumba kwa sababu kuna matatizo ya kiroho ambayo yanapaswa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo. Matatizo ya kiroho yanaweza kusababisha hatari kubwa katika jamii kwa ujumla. Nimewahi kusimuliwa na watu kadhaa kuwa miji ambayo ina wachawi wengi huwa hakuna maendeleo. Na mtu mwingine aliwahi kuniuliza swali kama nimewahi kumwona mchawi ambaye ni tajiri au amefanikiwa kabisa katika maisha yake ya kimwili. Hata akiwepo, utajiri wake ni wa kishirikina ambao matokeo yake ni maumivu na magomvi maishani mwake. Jamii inayokuzunguka inasumbuliwa na matatizo mengi ya kiroho ambayo yameenea miongoni mwa watu. Pengine kuna maagano wa mababu wa zamani waliyoyafanya na

34

Wana "hutumiwa kwa mawanda mapana, hii haimaanishi wale watoto aliowazaa Sauli tu. Kwa sababu Sauli hakuwa na wana saba, kwa hiyo ilijumuisha na wana wa Merab, ambao kwa kweli walikuwa wajukuu wa Sauli.

89

mizimu, sasa kila mnapojaribu kufanya jambo la maendeleo halifanikiwi kwa sababu eneo ya nguvu ya ushindani wa kiroho inakusumbua. Jamii nyingi za kiafrika zinakabiliwa na matatizo haya ya kiroho ambapo sasa zinahitajika jitihada za kanisa kusimama katika nafasi yake na

kuharibu

mikataba

hiyo.

Ninaposema

matatizo

ya

kiroho

ninamaanisha kwamba; tatizo hilo liko nje ya hali ya kawaida! Usiposhughulikia matatizo ya kiroho, hutasogea popote katika kazi zako. Tumeshuhudia watu wengi wakianzisha hata biashara hazisogei popote kwa sababu kuna changamoto za kiroho za maeneo yale! Na cha kushangaza hata miongoni mwa wapendwa unakuta kwamba hawaoni mambo kama haya kuwa ni ya muhimu kuyashughulikia. Zamani wapendwa walikuwa na utaratibu wa kuweka wakfu nyumba zao wanapotaka kuhamia ili kuwepo na baraka za Mungu kupitia watumishi wake, lakini siku hizi utasikia tu “mpendwa fulani keshahamia Madohe,” unauliza, “kahamia lini?’ hakuna anayejua! Tunamshukuru Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwa sababu ndani yake matatizo yote ya Kiroho yanaweza kutatuliwa kupitia damu yake ya pale msalabani. Tunapokuwa tunahisi hali ambayo siyo ya kawaida, ni vizuri zaidi kumwomba Mungu kama Daudi alivyoomba ili tuweze kupewa maelekezo na Bwana. Wakati mwingine unaweza 90

kumwomba Mungu na akakwambia pengine labda hujamsamehe mtu fulani! Unaweza kumwomba Mungu na akakwambia kwa sababu pengine wewe umekuwa hutoi zaka na sadaka ndiyo maana unakabiliwa na changamoto katika maisha yako. Kuna sababu nyingi za kiroho ambazo nyingi zinasababishwa na nguvu za giza. Kila mkristo anapaswa kuwa makini katika masuala ya kiroho. Mpendwa katika Bwana nakushauri kabisa kwa moyo wote, usicheze na mambo ya kiroho. Unapohisi kuna tatizo-shughulikia mapema.

Magonjwa yaweza kuwa chanzo cha umasikini. Katika Luke 8:43 tunaambiwa kwamba “na mwanamke mmoja ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu yeyote. Hoja ya msingi hapa ni namna ugonjwa wa mwanamke huyu ulivyosababisha umasikini katika familia yake. Akimzungumzia mwanamke huyu Reinhard Bonnke35 anasema kuwa “kutoka damu mara kwa mara kwa mwanamke huyo lilikuwa janga. Janga ambalo lilimletea matatizo ya kuishiwa, udhaifu, wa kupumua na ugumu kutembea. Kwa

35

Imepakuliwa katika ukurasa wake maalumu wa https://www.facebook.com/evangelistreinhardbonnke tarehe 5/7/2017 saa 9:17

91

sababu hakuwa na pesa hakuwa na uwezo wa kula chakula cha kutosha ili kulipa fidia kwa upotevu wake wa nguvu zake” Mojawapo ya eneo muhimu la mafanikio ya binadamu ni afya. Wakati tunapokuwa na afya mbovu hatuwezi kufanya jambo lolote lile. Magonjwa yamekuwa chanzo cha umasikini kwa watu wengi kwa sababu ya kutumia mali zao zote kwa ajili ya kujitibu,na wakati mwingine magonjwa hayo pia hayaponi kama tulivyosoma andiko la hapo juu. Tuna ushahidi wa kutosha namna jamii inavyoangamia kwa magonjwa makubwa kama kansa, Ukimwi pamoja na magonjwa-lishe ambapo baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakitumia magonjwa hayo kujitajirisha huku wengine wakiangamia kwenye dimbwi la umasikini wa kutisha. Tumeshuhudia katika kipindi hiki kiliniki nyingi zinazodai kuponya magonjwa mbalimbali. Wagonjwa wengi wanapoenda hudaiwa pesa kiasi kikubwa mno ambacho hawawezi kumudu kuzilipa. Lakini kwa sababu ya ahadi ya madaktari feki, basi wako tayari kwenda kuuza viwanja, magari, nyumba na hata vitega uchumi vingine ili mradi wapone tu. Hali kama hii inapoikumba familia, basi ujue kwamba umasikini umepiga hodi. Kwa sababu hiyo basi, kuna kila sababu kwa kila mtu kujilinda afya yake na matumizi mabaya ya vyakula 92

vinavyoharibu miili yetu na kujitahidi kufanya vitu ambavyo vinaweza kuimarisha afya zetu. Mungu tayari amekwisha kutupatia afya miilini mwetu, ni jukumu letu kujitunza na kujilinda. Tunaamini kwamba Mungu anatulinda kila siku kwa upendo wake kwetu, lakini ni wajibu wetu kujiepusha na mambo yanayoweza kuharibu afya zetu; kwa mfano kula vyakula vyenye sukari nyingi kila siku (soda, juisi, sukari nyingi kwenye chai, keki) na vingine vingi. Je unataka Mungu aje akwambie kwamba usitumie vitu hivi kwa sababu vinaweza kudhuru afya yako vinapokuwa vimezidi mwili? Tujaribu kuepuka vyakula vya viwandani kwani ndivyo vimekuwa vyanzo vya matatizo mengi yanayowakumba watu wengi. Mambo mengine ni kama vile uvutaji wa sigara; hata kwenye pakiti wazalishaji wake wametoa onyo kabisa kwamba “ni hatari kwa afya yako,” lakini unakuta mtu anavuta hata pakiti tano kwa siku. Sigara ni hatari mno kwa afya. Je unataka Mungu aje ashuke kwako akwambie “fulani, acha sigara?” hiyo kitu haipo hata siku moja.

Madeni sugu husababisha umasikini usio na kifani. Hakuna andiko linalosema kwamba kukopa ni dhambi au kuwa na madeni sugu ni dhambi! Hakuna kabisa! Lakini athari ya madeni sugu na madeni limejadiliwa. Tunazo habari za watu walioingia katika 93

madeni na baadaye mambo magumu yaliwapata. Katika 2 Wafalme 4:1 tunasoma kuwa “basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wale wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Mungu; na ALIYEMWIA amekuja ili AJITWALIE wana wangu kuwa watumwa.” Katika fungu hili, maneno ambayo nimeyaandikwa kwa herufi kubwa yamebeba maana ya mstari mzima. Hatuna mashaka na uaminifu wa mtumishi wa Mungu ambaye kwa sasa alikuwa tayari marehemu. Mke wake anamsifia kwa Elisha kwamba “alikuwa mcha Mungu” tena “nawe Elisha unalijua hilo.” Lakini pamoja na kuwa mwaminifu, huyu mtumishi wa Mungu alikuwa “deni” (sina hakika kama ni deni sugu, lakini deni ni deni). Baada ya kifo chake kulingana na sheria ilikuwa inataka watoto kuwa watumwa wa yule anayewadai. Vile vile, tunaposoma mazingira ya familia hii inaonekana ilikuwa ni masikini sana labda ndiyo maana ilikuwa imeingia kwenye madeni makubwa. Ukisoma mstari wa pili utagundua kwamba familia hii ilimiliki chupa ya mafuta tu. Ni dhahiri kwamba familia hii likuwa katika hali ya umasikini mkubwa sana. Kwa sababu hiyo, Elisha alimwambia aende akaazime vyombo sehemu nyingine ili ajaze mafuta kwa muujiza. Na kweli alifanya hivyo na baadaye tunaona familia yake inatoka kwenye deni hilo kubwa na kubakiwa na bakishishi. 94

Maisha ya madeni tumeyashuhudia kwa watu wengi sana. Viwango vya madeni vinatofautiana; wafanyabiashara wengi wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa pasipo kukopa mahali fulani ili kukuza mitaji yao. Mimi siyo mfanyabiashara lakini ninaamini kwamba kwa mtu anayeanza biashara mkopo unaweza kumchimbia kaburi la biashara yake. Ni watu wachache sana wanaoweza kutumia vizuri mikopo yao lakini wengi wao huishia kukopa na matokeo yake kufilisiwa kabisa. Kuna watu wengi wamekimbia miji ya kwa sababu ya kudaiwa madeni makubwa. Nimewahi pia kuwaona watu wakichukua mikopo benki na kununua magari, viwanja, nyumba na wanabadilisha hata mlo pale nyumbani kwao; kama alikuwa anakula ugali na dagaa kila siku, basi anakuwa anakula wali nyama kila siku. Lakini baada ya muda benki wanataka pesa yao! Matokeo yake hana kitu cha kurudisha, hapo kwa vyovyote vile mali hizo lazima zipigwe mnada na watu wa benki. Tatizo la watu wengi wa kawaida, hata madeni yao siyo makubwa sana; unakuta kwenye duka fulani anadaiwa elfu mbili, duka fulani anadaiwa mia tano, kwa Mangi anadaiwa, elfu tano kwa sababu alikopa unga, kwa Mpemba anadaiwa elfu saba kwa sababu alikopa nyama. LUKU ya Tanesco inasoma umeme umekaribia kuisha, anaenda kwa Mchaga kukopa elfu tatu kwa maelezo kwamba atamrudishia ndani ya siku mbili, akitoka pale anakuta wasomaji wa mita ya maji wanampa 95

siku mbili za kulipa na kama hatalipia maji yatakatwa! Ili ajinasue na suala la maji-basi anaenda tena kwa Mgogo kukopa elfu thelathini ili akalipe maji! Ni orodha ndefu (unaweza kuiongezea wewe). Sasa hawa watu wote wanapoanza kudai, na wewe ulitegemea kibarua ili ufanye kazi na ulipe-lazima utakiona cha mtema kuni! Lakini nina historia ya watu wengi ambao wana tabia ya kukopa. Ukimkuta mtu mwenye tabia ya kukopa huwa wanafanya hivi; hata kama ana hela hapendi kununua kitu kwa keshi, anachokifanya ni kwamba anamwambia mwenye duka “hebu nipe sabuni hapo, jioni nakuletea hela yako,” wakati huo siyo kwamba hana pesa! Anayo mfukoni lakini unajua kwa nini hataki kulipa kwa wakati huo? Anatengeneza mazingira ya kukopa baadaye; kwa maana ya kwamba kwa sababu hiyo hela anayo, jioni kweli atakuja kulipa. Mwenye duka (au mkopeshaji) ataona kwamba “oh huyu jamaa ni mwaminifu sana, yaani alisema ataleta hela saa kumi jioni, na kweli ameleta.” Siku nyingine hivyo hivyo, lakini baadaye atakopa na kutokomea, anabadilisha na njia ya kupita. Na ndiyo maana mtu mwenye madeni mengi mtaani hutembea akiwa makini sana, akisikia mluzi nyuma yakehageuki ng’o, yaani ndiyo anatokomea kabisa. Hii ni tabia ambayo husababisha si tu umasikini bali ni ufukara kabisa. 96

Kitu kingine ambacho sasa unaweza kushangaa ni kwamba, wakati mwingine anapokopa, ni kwa riba kubwa! Anajikuta kwamba lile deni la kawaida analodaiwa ni dogo kuliko riba ilizaliwa. Hii inatokana na tabia ya mtu anayependa madeni kufanya upya/kuhusisha madeni yake, analipa la zamani-anakopa sehemu nyingine ili liwe jipya. Kwa lugha nyingine wanasema “kuvuta muda wa deni.” Nakumbuka nilipokuwa nasoma katika chuo kikuu cha Dar es salaam watu wengi sana walinishawishi nichukue mkopo kutoka kwenye bodi ya mkopo. Nilishawishika kabisa kwa sababu ya ubembelezi wa rafiki zangu chuoni. Kwanza walidai kuwa “yaani hiyo pesa ni ya serikali, na serikali ni ya kwao, na hakuna mtu ambaye amewahi kulipa deni hilo.” Nilichukua fomu na nikaenda kulipia ile fomu. Lakini nilipofika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo, nilijiuliza swali, “je kwa nini wanaita ni mkopo?” Je kama kweli ni bure wangesema “ni mkopo?” nilisubiri kama saa moja hivi pale ofisini, watu zaidi ya mia mbili wanasubiri kushughulikiwa masuala yao ya mikopo! Baada ya kuzingatia moyoni mwangu nikaona huu mkopo niachane nao, maana kama ni mkopo, basi kuna siku natakiwa kulipa tu! Sasa wakati wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli, suala la kulipa mikopo alilikaza sana. Tuliona hata majina yalikuwa yanabandikwa kwenye mbao za matangazo ya halmashauri husika. Ni aibu gani ningepata kama jina 97

langu lingekuwepo pale! Sasa hivi wale waliokuwa wananicheka wakati wanapoenda kuangalia kwenye akaunti zao kama bumu (boom) limeingia, wanajuta. Achana na madeni yasiyo ya lazima. Mpendwa katika Bwana, sisemi kabisa kwamba usikope kiasi fulani cha pesa wakati unapokuwa umezidiwa. Ni sawa kabisa kukopa, kwa sababu hata mwanzoni mwa hoja hii nilisema kukopa siyo dhambi. Lakini kuwa makini! Ukiendelea kufanya hivyo itakusababishia dhambi kubwa ya kuwa mwongo, na mafaniko yako yote yatapukutika kwa sababu ya madeni. Hebu jipime wewe mwenyewe, je uko katika hali kama hii? Basi naona umefungwa kwenye kifungo ambacho hakuna atakayekutoa zaidi ya kuzifanyia mazoezi kanuni zilizo ndani ya kitabu hiki.

Ulevi kupindukia Kuna

ulevi

wa

aina

mbalimbali,

hata

hivyo

ulevi

ninaozungumzia mahali hapa ni ulevi wa pombe. Ninajua suala hili miongoni mwa Wakristo limekuwa na mjadala mkubwa. Pia ni suala la kimaadili kwa sababu kila jamii ina muono wake kuhusu unywaji wa pombe. Hoja za kuhusu unywaji wa pombe nimezijadili kwa undani katika kitabu kingine cha kinachohusu maadili ya Kikristo cha “Niamue

98

Lipi.” 36 Naomba uangalie kwa makini hoja zifuatazo za wale ambao wanakubaliana na unywaji wa pombe na baadaye ulinganishe na wale wanaokataa, kisha nitakueleza madhara ya kiuchumi yanayotokana ulevi. Wanadai kuwa Biblia haikatazi unywaji wa pombe bali inakataza ulevi wa pombe. Ndiyo maana katika I Tim 3:3 ‘si mtu wa kuzoelea ulevi’ kuzoelea ni kitenzi cha ‘kuzoea’ maana yake kuendekeza tabia ya kufanya hivyo. Na hapa Paul anatoa sifa za kiongozi wa kiroho. Kumbe wakiristo wengine wasio viongozi wanaweza kunywa pombe. Wanakazi pia kuwa Biblia imeagiza mkristo aweze kujitawala sio kuacha kunywa pombe, hivyo basi kama mkristo anaweza kunywa bia moja na akalala bila kumbughudhi mtu basi anaweza kunywa ili mradi tu atawale hali yake. Vile vile wanajitutumua kwa kusema kuwa Biblia inatambua kwamba pombe inaweza kutumika kama dawa, basi si mbaya kunywa pombe kwa ajili ya afya. Na kwamba Si kila mtu anayekunywa pombe anakuwa mlevi. Na biblia imekataza ulevi sio unywaji wa pombe. Pia

36

Seni, Daniel John. Niamue Lipi. Dar es salaam: Shekinahpress. 2015. Pp. 19-21

99

hudai kuwa kukataa kunywa pombe unaweza kujitenga na jamii. Kwa mfano kuna jamii zingine kama ukienda kwenye sherehe lazima uzimue kidogo ndipo uonekane unashirikiana nao. Hoja nyingine inayoibuliwa ni kuwa suala la kunywa pombe halihusiani na masuala ya uzima wa milele. Kwa kuwa mtu amempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake basi amehesabiwa haki na ana uzima wa milele. Je umeshawishika kwa hoja hizo? Ngoja nikupe hoja za upande wa pili namna wanavyojitutumua na wao. Zifuatazo ni hoja zao za msingi. Wanadai kuwa; Biblia inaonya juu ya matokeo ya matumizi ya pombe. Mtu aliyeweka nadhiri haruhusiwi kunywa kileo. Hes 6:2-3. Makuhani hawakuruhusiwa kunywa vileo. LAW 10:9. Wafalme hawakupaswa kunywa vileo katika falme zao. MIT 31:4. Kileo hupotosha watumishi wa Mungu wanaojaribu kunywa. ISA 28:7. Si vizuri mtu aliyekusudiwa kuwa mkuu kutumia kileo. LK 1:15. Kunywa pombe kwa mkristo ni kuonyesha na kuendelea kuishi maisha ya zamani. 1PET 4:3-4. Pombe huleta magomvi katika nyumba za watu na kuvunja ndoa zao. Ulevi huua idadi kubwa ya watu. Nadhani hata wewe umeshuhudia watu ambao wamekufa kwa sababu ya pombe. Hakuna anayeanza kunywa pombe na kusema kwamba hatakuwa mlevi bali 100

hustukia mlevi tu. Matokeo ya ulevi ni mabaya mno. Mfano kwa habari ya Lutu kulala na watoto wake wakati wa ulevi na Nuhu wakati wa ulevi alilaani mjukuu wake Kanaani. Kila mlevi unayemwona alianza kama mnywaji halafu polepole akawa mlevi mkubwa. Je umeshawishika na hoja hizi? Pande zote mbili zina Maandiko ya kusimamia. Kwa sababu hiyo hatuwezi kusimama tu bila kuwa na hoja za msingi na kuanza kukemea upande mmoja eti kwa sababu tunaamini upande wa pili. Kwa mujibu wa madhehebu yangu, kwa vyovyote vile Mkristo haruhusiwi kunywa pombe, hivyo nami nina msimamo huo. Nakumbuka rafiki yangu Daniel Heke tulipokuwa katika chuo cha Theolojia tuliwahi kubishana kuhusu suala la kunywa pombe. Yeye alihitimisha kwamba “pombe siyo dhambi ila ni tabia mbaya” halafu mimi nikaongeza kuwa “tabia mbaya ni dhambi!” Hata hivyo katika kitabu hiki nataka niwe na msimamo kati ambao haujikiti katika maandiko bali unajikita katika masuala ya kimaadili. Katika msimamo wangu wa kati, nataka nikupe hoja tatu muhimu zinazoweza kukushawishi uoione pombe kama adui mkubwa wa maendeleo. Kwanza, Ulevi kupindukia husababisha watu wengi wauze mali zao. Katika jamii tumeshuhudia watu wengi ambao hawapigi hatua kwa 101

sababu ya ulevi. Watu wengi wameuza mashamba yao kwa sababu ya ulevi. Ninakumbuka vizuri sana kijijini kwetu namna wazee walivyokuwa wanauza mashamba, na hata chakula kwa ajili ya kwenda kununu chupa moja ya pombe. Tena pombe ambayo wanakunywa ni ile inayoitwa “moshi” (kwa kisukuma). Pombe ile ni kali kupita kiasi, na zaidi ya hayo ni “pombe haramu” kwa maana ya kwamba serikali ilishapiga marufuku kunywa pombe kama hizo. Watu wameuza mifugo yao kwa ajili ya kwenda kunywa pombe! Watu wameweka rehani kwa ajili ya kwenda kunywa pombe. Ngoja nikupe mfano hai ili uweze kuelewa! Wakati tukiwa bado vijana wadogo, baba yetu alikuwa ameathirika na pombe, kiasi kwamba alikuwa anaweza kuuza kitu chochote kilichoonekana ili mradi akanywe pombe. Nakumbuka siku moja alienda akachukua pesa kwa mtu mmoja pale kijijini na akatulazimisha kwenda kupalilia shamba la yule jamaa alikochukua pesa. Kwa muda wa wiki nzima hatukuweza kukanyaga kwenye shamba letu kwa sababu tulikuwa tukienda kulima kwenye shamba la mtu mwingine. Jambo hili halikutokea mara moja wala mara mbili lilijirudia mara kwa mara. Tulikuwa tunaenda kulima huku tunalalamika, lakini ndiyo mzazi wako, inabidi utii sheria bila shuruti! Jambo hili kama tusingelistukia mapema lingeleta madhara makubwa sana, lakini ashukuriwe Mungu aliyetutoa katika hali hiyo. 102

Jambo kukumbuka ni kwamba usijaribu hata kuonja pombe hata siku moja! Kama tulivyosema hapo juu kwamba hakuna mlevi ambaye hakuanza kwa kunywa kidogo. Usikubali mtu akuambie kwamba “onja kidogo.” Achana na ujanja wa watu wanaoweza kukwambia kwamba “zimua moja.” Pili, ulevi hulemaza akili ya kufanya kazi. Mtu anapoanza kuwa mlevi wa kupindukia huwa hajijui. Hata watu wakimwambia kwamba “wewe ni mlevi” atakataa. Na zaidi ya hayo ulevi hufanya watu wengi wasifanye kazi. Hii inatokana na kwamba kuanzia asubuhi hadi jioni wanakunywa pombe tu. Matokeo yake ni kudorora kwa uzalishaji mali katika

jamii

n

ahata

kushusha

chini

kiwango

cha

familia.

Ninawakumbuka rafiki zangu ambao wamekuwa ni walevi kupindukia, leo ukikutana nao utafikiri wamenyeshewa mvua! Namwomba Mungu kwa ajili yao kwamba watoke katika hali hii mbaya inayowakabili. Hawawezi kufanya kazi kabisa. Swali la msingi, je wanapata wapi pesa za kunywa? Wengine kununuliwa na marafiki zao, wengine ni mikopo ya pombe kila mahali-pamoja na sababu zinginezo. Jamii isipopiga ulevi unywaji

wa

pombe,

taifa

litakosa

nguvu

kazi

kwani

watu

hawatajihusisha na shughuli za uzalishaji mali. Tusikomee kupiga marufuku matumizi ya shisha na madawa mengine ya kulevya-pombe ni adui mkubwa. 103

Tatu, ulevi kusababisha watu wafanye matukio yasiyofaa katika jamii. Watu wengi wmefungwa magerezani kwa sababu ya ulevi. Ukienda gerezani wengi watasema kwamba “unajua ni sikujielewa nilipofanya jambo hili kwa sababu ya pombe!” Watu wengi wamebaka na kubakwa kwa sababu ya ulevi. Sasa umeshajua ukishabaka, wewe ni gerezani tu. Je unapokuwa gerezani nani anahudumia familia yako? Kwa hiyo hii ni shida kubwa ambayo inaweza kusababisha umasikini katika jamii. Hivyo basi kulingana na hoja hizo, ni wachache sana wanaoweza kusema kwamba wao tangu waanze kulewa bado hawajawahi kuathiriwa na pombe! Kwa sababu hiyo, napenda kuwashauri vijana na wazee, tuacheni pombe! Ni kazi ngumu kuacha tabia ambayo umeizoea! Hebu ile hela ambayo unataka kwenda kunywa safari lager, mpe mkeo akanunue unga. Ile hela unayopanga kwenda kununua sanduku la bia kwa ajili ya rafiki zako, mpe mtoto wako akanunue vitabu vya shule. Hilo pengo la pesa unayotumia kunywa, halafu baada ya muda unaenda kuitoa yote kwa njia ya mkojo-nani analiziba?

104

Sababu mchanganyiko Wakati mwingi umasikini huweza kusababishwa na sababu nyingi kwa pamoja. Melkisedeck Shine37 aliorodhesha tabia mchanganyiko ambazo zinaweza kusababisha umasikini kama ifuatavyo na maelezo yake:Kutokujaribu, katika kutafuta mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita. "Chagua kufa, au kupambana". "Siogopi kufa, naogopa kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna aliyezaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa. Woga anayeogopa

na

Wasiwasi,

gizani,

lakini

"Tunaweza sio

mtu

tukamsamehe mzima

mtoto

anayeogopa

mchana"(Plato). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe. Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha halali na kina manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu ambacho hakijatokea.

37

http://www.ackyshine.com/uchumi:tabia-za-kuepuka-ili-uweze-kuwa-tajiri

105

Kuweka vinyongo, "Kuweka chuki na kinyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine". Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli. Starehe na anasa kupindukia, Ni ngumu sana kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. "Sisi ni kile tunacho kula". Mafanikio ya kwanza huanzia kwenye afya yako". Afya ni utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. "Mavuno ya uzee, ni swaga za ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana"(Nikki Mbishi,). Lawama na umbea, watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu. Tusilamike, tupambane, lawama hazisaidii chochote.Ukiweka malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia ndoto zako.

Ni kweli kufa maskini ni ufala? Haya ni maneno ya kejeli kutoka kwa mchungaji Antony Lusekelo (aka mzee wa upako) wa kanisa la GRC-Dar es salaam. Mchungaji

Lusekelo

alisema

hayo

alipokuwa

akiongea

na

mtangazaji wa kipindi cha ujenzi kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV kila Jumapili, Mzee wa Upako alisema mtu 106

anapokufa akiwa ameacha mali za kutosha ni jambo jema kwani familia yake nyuma haiwezi kupata taabu wala watoto hawawezi kupata shida tofauti na yule anayekufa akiwa na kitanda tu kwani watoto wake watapata shida na mateso. Hapa nanukuu kauli yake "Watu wanamsifu mtu amekufa bila mali eti alikuwa mwadilifu yaani unakuta mtu amefanya kazi serikalini miaka na miaka, sijui miaka 35 au 40 anakufa hata kitanda hana, wapo watu wanasema huyu jamaa alikuwa mzalendo na muadilifu sana hata kitanda hana, hamna mtu huyo alikuwa fala umenielewa huyu alikuwa fala na hastaili kuwa kielelezo cha msingi tuhoji mtu kapata mali wapi? Ndiyo jambo la msingi sababu unaacha watoto duniani unadhani wataishi vipi? Mama anakuwa na nyumba pale anachota kodi anapeleka watoto shule maisha yanaendelea." Pale juu nimeanza kwa kusema kwamba hayo ni maneno ya kejeli kwa maana ya kwamba yanakejeli hali ya mtu alivyo, na kuona kwamba kila anayekufa hana mali za kuachia kizazi kijacho basi yeye ni fala. Kauli hii tunaweza kuichunguza kupitia andiko la Luka 12:13-21. Hapa Yesu alitoa mfano wa mtu tajiri ambaye alijikusanyia mali nyingi na kujisifu kwa roho yake. Ukisoma vizuri utaelewa kwamba huyu mtu alitegemea utajiri wake kama kigezo cha maisha yake, na ndiyo maana anasema kuwa “Ee nafsi yangu, 107

una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.” (mst19). Hapa tunaona huyu jamaa anajisifu kwa sababu ya kujipatia mali nyingi na kujitakia roho yake ikae kwa amani na kupumzika. Hii ina maana kwamba huyu jamaa alitumia miaka yote kujikusanyia mali na wala hakumkumbuka Mungu wake. Je nini jibu la Mungu kwa watu wa namna hii? “ Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako” (mst 20). Maana yake ni kwamba maisha ya hapa duniani ni ya muda mfupi sana. Mtu anapojirundikia mali kwa uchoyo bila kujitajirisha mbele za Mungu, wakati wowote anapokufa-tumaini la mali yake haliwezi kumsaidia. Hoja yangu hapa siyo kuzuia watu wasiweke akiba, kila mtu anatakiwa aweke akiba, lakini lazima akumbuke kwamba “uzima wa mtu haupo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo” (mst 15). Mali ya hapa duniani kamwe haitoshi. Nimekutana na watu wenye mali zaidi kuliko wanavyoweza kuhitaji na hata hivyo, bado wanahitaji zaidi. Wale ambao huona maisha mazuri kwa kuangalia wingi wa mali walizo nazo, kamwe hawatayapata maisha hayo mazuri. Maisha

108

mazuri hayawezi kupatikana kwa sababu tuna mali nyingi, bali ni kwa sababu tunaye Mungu ambaye yeye kila kitu kinatoka kwake. Kwa lugha nyingine ni kwamba unapokuwa umempata Mungu katika maisha yako, wewe unacho kila kitu kwa sababu yeye ni zaidi ya kile unachohitaji hapa duniani. Neno la Mungu linasema “na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna sikuzote” (2 Kor. 9:8). Hapa tunagundua kwamba kumbe Mungu hutupatia mahitaji yale tunayohitaji kwa wakati wetu bila kujali mazingira tuliyo nayo

SURA YA TANO Je Kuna Tumaini Lolote La Kutoka Katika Nje? Suala la matatizo binafsi ya kiuchumi ambayo yanasababisha watu kuwa masikini na fukara si jambo dogo, kwani lina upana wake katika kulijadili. Mahatma Gandhi aliwahi kusema kuwa “umaskini ni aina mbaya ya vurugu.”38 Mwalimu Nyerere aliwahi kusema “ni ghali sana kuwa masikini.” Pia mwalimu Nyerere baada ya uhuru mwaka 1961 alitangaza maadui watatu; ujinga, maradhi na umasikini. Nelson

38

https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/m/mahatmagan150720.html

109

Mandela aliwahi kusema kwamba kwa kadri umasikini, ukosefu wa haki na ukosefu mkubwa wa usawa upo katika ulimwengu wetu, hakuna hata mmoja wetu anayeweza kupumzika kweli.

Kwa hiyo unaweza

kugundua kwamba suala la umasikini ni suala la Kihistoria.

Tufanyaje Sasa Kuna wengi hufikiri kwamba wanapokuwa na pesa wanaweza kuondokana na umasikini, hayo ni mawazo hasi kuhusu kuondokana na umasikini. Mtu akipewa pesa inawezaje kumsaidia kuondokana na hali ngumu ya maisha? P. J. O’Rourke aliwahi kusema kuwa "huwezi kuondokana na umasikini kwa kuwapa watu fedha.39" Tunajua

kwamba

Biblia

inatuamuru

kuwasaidia

masikini.

Usijiweke kwenye kundi wa watu masikini ambao wanahitaji kusaidiwa bali jiweke kwenye kundi la watu wanaoweza kuwasaidia wengine. kwa vyovyote vile tunahitaji kujiuliza je tunawezaje kufanya matokeo ya kweli ambayo yanaheshimu hali ya masikini? Tunawezaje kuwasaidia waondokane na mzunguko wa umasikini?

39

O'Rourke, P.J. (January 7, 2014). "The Baby Boom: How It Got That Way...". Grove/Atlantic, Inc. – via Google Books.

110

Tunahitaji kujua wajibu wa makundi manne kwa ajili ya kushughulika na watu masikini; 1) wajibu wa serikali kusaidia masikini 2) wajibu wa kanisa kuwasaidia masikini 3) na wajibu wa masikini mwenyewe kuondokana na hali yake.

Wajibu wa Serikali kuwasaidia masikini Katika kipindi hiki ni muhimu kujadili majukumu ya serikali kwa masikini. Biblia iliandikwa katika kipindi ambacho mipango ya ustawi wa jamii ya ustawi wa serikali haikuwepo. Maelekezo ya Kibiblia kuhusu maskini yaliandikwa na dhana kwamba msaada wowote uliotolewa kwa maskini ungekuja moja kwa moja kutoka kwa wanachama wa jamii husika.

Hata hivyo mafundisho ya Kibiblia

yanaonyesha kazi na kanuni za serikali kuwa ni kusimamia haki bila upendeleo (Mambo ya Walawi 19:15). Kwa namna yoyote ile, serikali imepewa wajibu na Mungu wa kusimamia shughuli zote zinazohusu haki za makundi mbalimbali katika jamii. Kwa sababu hiyo, ni lazima serikali ifanye kazi ya kuondoa umasikini katika jamii. Muundo wa serikali una lengo la kuondoa umasikini. Tumeshuhudia namna serikali ambavyo inajaribu kutimiza wajibu wake kwa kuwasaidia masikini katika jamii. Hata hivyo kiwango cha 111

umasikini nchini Tanzania kiko katika hali ya juu sana. Kwa mfano waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu umasikini alisema katika bajeti ya mwaka 2016/17, alisema kuwa Kigoma, Geita, Kagera, Mwanza pamoja na Singida ndiyo mikoa masikini zaidi Tanzania. Dk. Mpango alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na umaskini mkubwa wa asilimia 48.9, ukifuatwa na Geita (asilimia 43.7), Kagera (asilimia 39.3), Singida (asilimia 38.2) na Mwanza (asilimia 35.3). Kusudi langu si kukosoa serikali katika utendaji wake bali ni kusisitiza tu kwamba ni wajibu wa serikali kuondoa umasikini. Hata hivyo nitoe onyo kwamba masikini yeyote anayetegemea serikali impatie pesa, basi imekula kwake! Kazi ya serikali ni kuweka mitandao wa kukusaidia wewe utoke, siyo ikushike mkono utoke kwenye umasikini Serikali na kanisa vishirikiane kuondoa hali hii (yale ya serikali ishughulikie-yale ya mtu binafsi ashughulikie na upande wa kanisa ushughulike. Kujifunza kwa nchi zilizofanikiwa. Je ilikuwaje? Je ni kweli nchi zote zimehusika katika unyonyaji? Hapana. (ukiachilia ule umasikini binafsi lakini kuna nchi tajiri sana). Huduma za kijamii nk.

112

Kwa Wanaotaka Kuajiriwa na Walioajiriwa tu Katika maisha ya utumishi kupitia eneo la ushauri kwa watu wa Mungu nimekuwa nikiwashauri mambo mbalimbali kuhusu ajira. Wengi ambao wametumia mbinu hizo wamefaidika nazo kwa hali ya juu sana. Wengine wananipigia simu ni kushukuru kwa ushauri wangu. Wengine wanafikiri kwamba ili apate kazi anahitaji kwenda kwa mganga wa kienyeji na kufanyiwa matambiko mbalimbali. huku wengine wenye imani haba wakienda kwa watumishi wajiitao mitume na manabii ili waombewe na kupata ajira! Yawezekana kweli ulipofanyiwa hivyo ulipata kazi. Lakini hata kama ukiombewa kwa namna gani kama hushiki kanuni za kupata kazi huwezi kupata kazi hata siku moja. Nakusihi usome kwa makini na uweze kuzifanyia mazoezi uone matunda yake. Labda kabla sijaendelea nataka nikwambie kwamba katika kila jambo lazima umtangulize Mungu kwanza kwa sababu yeye ndiye anayeweza kukupa maarifa na mbinu za kutekeleza wajibu wako. Kwa hiyo omba Mungu bila kukoma katika maisha yako yote hata kama umepata kazi au hujapata, maombi kwa Mungu wako ni muhimu sana. Mimi sijui unamwomba Mungu yupi lakini omba sana kwa Mungu wako. Mbinu hizo ni hizi zifuatazo:-

113

1)

Hakikisha unakidhi vigezo vya kazi unayotafuta Mbinu hii ninaanza nayo kwa sababu ndiyo mbinu ambayo

inazibeba na zile zitakazofuata. Kila kazi ina sifa zake na vigezo vyake. Hakikisha kazi unayoomba una sifa za kuifanya kwa namna yoyote ile. Usijaribu kuomba kazi ambayo huna vigezo nayo hutapata. Kwa mfano ukiwa unataka kazi ya ulinzi, ni vizuri zaidi ikiwa angalau umepitia mgambo hata miezi sita au hata jeshi. Maana kazi ya ulinzi ni zaidi ya kufungua geti, kuna wakati unaweza kuingia katika vita na majambazi, sasa wewe kama hujawahi kwenda hata mgambo, utatimua mbio haraka sana na kusababisha hasara kwa kampuni. Kazi zipo nyingi sana ila watu hawana vigezo vya kazi hizo. Kwa mfano unatafuta kazi ya kufundisha hesabu lakini wewe hujui hata hiyo 2x2. unatafuta kazi hospitalini lakini hujui hata kipimajoto! Kila kazi ina vigezo vyake. Kazi zingine zinahitaji viwango tofauti tofauti vya elimu. Kwa mfano siku hizi ofisi nyingi zinaomba mtu mwenye shahada ya umahiri ndipo aweze kuajiriwa. Kama una shahada ya awali soko linaanza kupotea sasa hivi. Kwa hiyo hakikisha una vigezo vya kazi unayoomba kuifanya na kama huna sifa na kazi hiyo, huwezi kupata kazi.

114

Kwa taarifa yako hata vibarua wa kubeba tofali kuna vigezo vinavyotakiwa. Wewe ukiwa legelege kwa mwonekano wako huwezi kupata kazi hiyo. Kila ukienda kutafuta kazi watakwambia hamna kazi kwa sababu mwonekano wako tu unaonekana kwamba unahitaji kusaidiwa na wala siyo kufanya kazi. Kazi kama hizo lazima uonekane baunsa hapo lazima watakupa tu. Kwa hiyo kila kazi ina vigezo vyake.

2)

Usiwe Mtu wa Kukata Tamaa Mapema Kuna watu wengine wana sifa nzuri za kupata kazi lakini tatizo

lao wanakata tamaa mapema sana. Yeye akikosa kazi sehemu mbili tu anaanza kusema ‘loo! Mimi nina mkosi, kwa nini huyu apate nami nikose’ acha mawazo hayo. Kama umekosa hapo kazi, tafuta sehemu nyingine hauna haja ya kuanza kulalamika kwa sababu pengine hujui kwa nini umekosa hapo kazi. Wakati mwingine Mungu hutaka kutujaribu kuona kama hatukati tamaa kwa hiyo usijaribu kukata tamaa. Niliwahi kuona fulana imeandikwa ‘Marufuku kukata tamaa’ niliipenda sana kwa sababu kukata tamaa ni dhambi kubwa mno katika maisha yako ya mafanikio. Huwezi kufanikiwa kama una tabia ya kukata tamaa.

115

3)

Uwe jasiri na Ujiamini Jambo hili nimelijadili sana katika sura ya kwanza. Labda

niseme kwamba kujiamini ni muhimu sana kwa ajili ya kupata kazi. Kama huwezi kujiamini wewe mwenyewe unataka nani akupe kazi? Ukifika kwa mwajiri jiamini kwamba wewe ndiye mtu wa pekee kabisa katika ofisi hiyo hakuna mwingine wa kufanana nawe hapo. Jieleze kama ukitakiwa kujieleza kwa ujasiri mwingi. Mungu alimwambia Joshua katika Joshua 1:1-8 uwe hodari na moyo wa ushujaa. Ukianza kutetemeka mbele ya mwajiri wako unaonekana kwamba hata kazi huwezi kufanya. Niliwahi kumwona kijana mmoja alikuwa anatafuta kazi ya ualimu katika shule moja hapa Dar es salaam, mwajiri akamwambia kazi ya ualimu ipo. Kijana alionekana kufurahi sana. Mwajiri akamwambia kwamba waende darasani akamwone jinsi anavyofundisha. Kijana akakubali, lakini cha kushangaza alipoingia darasani alianza kutetemeka! Chaki zinaanguka ovyo! Tena hiyo ilifanyika mbele ya wanafunzi, kama unavyojua wanafunzi hawakujizuia walianza kumcheka. Kwa haraka haraka tu unafikiri angeweza kupata kazi hiyo? Hapana. Hata kama unajua kila kitu lakini unaposhindwa kujiamini na kuwa jasiri utakosa kazi.

116

4)

Kubali Ushindani Kuna watu wengine wanaogopa kuomba kazi kama akisikia watu

wengi wameomba. Nataka nikwambie kwamba hata kama watu elfu tano wameomba kazi hiyo na wewe omba tu maana hujui ni nani ambaye atachaguliwa kupata kazi hiyo. Tunahitaji kuiga kwa wafanyabiashara, hata kama kuna mtu anauza viazi karibu naye anaanza biashara pale pale na kitu kile kile na wateja wananunua mali yake. Sasa wewe kama ukiogopa eti kwa sababu kuna wengi wameomba kazi hiyo, hutapata kazi. Kumbuka kwamba mwajiri huruhusu maombi yawe mengi ili aweze kuchuja ni nani anayestahili. Kwa kuwa kupata kazi ni mchujo basi kubali kushindana na watu wengine walioomba kazi kama yako.

5)

Taja moja kwa moja kazi unayotaka kufanya Kila unapoomba kazi hakikisha kwamba kazi unayoomba

unapewa kazi hiyo hiyo. Kuna watu wengi ambao huomba kazi wakisema nataka kazi yoyote. Mara nyingi mwajiri hupenda kuona mwajiriwa akitaja moja kwa moja kazi anayotaka. Sasa unapoanza kumpa mafumbo mwajiri anaweza kukupa kazi yoyote hata ile ambayo huwezi kuifanya.

117

Unaposhindwa kutaja kazi unayotaka, inaweza kukupa matatizo makubwa kwa sababu mwajiri anaweza kukupa kazi ambayo huiwezi hata kidogo. Nazungumzia hasa kwa wale wanaotafuta kazi maofisini. Kama mwajiri akishindwa kubaini unataka kazi gani anaweza kuachana na maombi yako.

6)

Uwe muwazi/ usiwe mwongo Kuna watu wengine wakati wanatafuta kazi ni waongo sana.

Wanajieleza kweli kweli lakini kwa njia ya uongo. Mtu mwingine anaanza kueleza kwamba nilifanya kazi mahali fulani kumbe uongo tu! Nakumbuka jamaa yangu mmoja alinieleza kwamba anatafuta kazi ya kuendesha gari. Alinieleza kwamba amewahi kuendesha magari ya kwenda mikoani na hata mabasi ya mikoani na daladala amewahi kuendesha. Mimi wakati huo nilijua kampuni fulani walikuwa wanatafuta dereva mwenye uzoefu kama wake. Basi jamaa nilipeleka maombi yake nao wakamkubali kwamba aende kazini. Kwa kuwa jamaa alijieleza vizuri siku ya kwanza basi hapakuwa na tatizo. Alipewa gari kuendesha na kuwapeleka ili awapeleke sehemu ya kazi. Mungu wangu huwezi amini jamaa huyo aliweka gia namba moja kwa muda wa dakika kama tano kwenye lami! Sasa mmojawapo wa hao watu akamuuliza, mbona hubadilishi gia? Akajaribu kubadilisha gia akashindwa! Jamaa 118

wakamwambia shuka kwanza tuendeshe sisi wenyewe wewe utajifunza siku nyingine! Unajua tatizo la jamaa yangu? Ni kwa sababu alionesha kwamba anajua kuendesha gari lolote kumbe sivyo. Jamaa alijua kuendesha automatic sasa ile ilikuwa ni manual tena left hand. Kwa kifupi hakupata kazi hiyo.

7)

Kuwa na wapendekezaji wa kuaminika (Referees) Mara nyingi unapoomba kazi mwajiri hupenda kuona ni akina

nani wanakupendekeza katika kazi hiyo. Kama una watu wenye historia mbaya huwezi kupata kazi. Hakikisha una watu wenye majina ya pili ili waweze kukupendekeza. Niliwahi kufundisha kanisani siku moja kwamba kila mtu ajitahidi kuwa na jina la pili. Kwa mfano Daktari, Profesa,

Mwalimu,

Mchungaji.

Sasa

kama

wewe

wale

wanaokupendekeza wana majina ya kwanza tu huwezi kupata kazi. Majina ya pili yanawatambulisha wale watu zaidi na hivyo wanaweza kufahamika

zaidi

ya mahali

wanapoishi

na hivyo

wananapokupendekeza unaweza kujenga imani zaidi kwa mwajiri wako. Kama huwezi kupata mtu mzuri wa kukupendekeza huwezi kupata kazi kwa sababu watu wengi siku hizi hawaaminiki.

119

8)

Omba kazi sehemu nyingi/usiombe kazi sehemu moja tu Vijana wengi wanapenda kuomba kazi sehemu moja na hivyo

wanapokosa kazi sehemu ambayo waliamini kwamba hawatakosa kazi wanakata tamaa ya kutafuta kazi nyingine. Ni vizuri kama umeamua kuingia katika ulingo wa kutafuta ajira tuma maombi sehemu nyingi za kazi. Kama ikitokea kwamba wamekuita kwa mpigo sehemu zote, basi chagua ni wapi uende yaani sehemu ambayo ni chaguo lako la kwanza na sehemu zingine toa udhuru. Kama ukipata sehemu nyingine basi uwe mwaminifu kwa sehemu zingine kusema kwamba ulipata kazi sehemu nyingine. Ukifanya hivyo hata kama ukifukuzwa au ukiacha mwenyewe sehemu uliyopata basi wanaweza kukuajiri wao.

9)

Usilazimishe kupata kazi Kuna wakati mwingine watu hulazimisha kupata kazi fulani.

Kama unataka ufanye kazi kwa raha mstarehe, nakusihi usikubali kutoa rushwa kwa ajili ya kupata kazi. Wasichana wengi hutoa rushwa ya ngono kwa ajili ya kupata kazi maofisini, jambo hili ni baya mna na linaweza kuleta madhara makubwa katika kazi yako. Kama hupati kazi hiyo kwa sababu unapaswa kutoa rushwa achana nayo.

120

10)

Mwonekano Wako Uwe wa Kuvutia Ni vizuri kama unaomba kazi ukawa na mwonekano wako

mzuri. Wakati mwingine mtu mwingine haajiriki kwa sababu ya mwonekano wake tu. Kwa mfano mtu mwingine anakuwa mchafu kupita kiasi, nani atakuajiri? Unapoenda kuomba kazi jitahidi angalau hata tai au suti mara moja siyo mbaya ili angalau uvutie macho ya mwajiri wako.

11)

Jiajiri mwenyewe ili uwe mwajiri Kama umetafuta kazi ukakosa kabisa kabisa, mimi naona bado

hujakosa kazi! Ili nijue kama umekosa kazi, basi labda nisikie fulani amefariki! Namaanisha kwamba maadam uko hai, bado hujakosa kazi. Jiajiri mwenyewe ili uwaajiri wengine! Hakuna hajai ya kuanza kulalamika eti kwa sababu umekosa kazi ndo unataka na kujinyonga. Acha mawazo hayo. Jiajiri mwenyewe kwa kufanya hata biashara ndogo ndogo baadaye biashara hiyo itakkuwa kubwa tu. Amini kwamba Mungu anaweza kukupatia kazi ili uje uwapatie wengine kazi. Kwa taarifa yako ni kwamba hakuna mtu ambaye amefanikiwa kwa kiasi kikubwa huku akiwa ameajiriwa labda kama atakuwa ameajiriwa naye ameajiri watu wengine kwa ajili ya kuingiza kipato! 121

Labda jambo la kujiuli, je wote tuwe waajiri? Hapana! Na ndiyo maana nimekufundisha mbinu za kupata kazi. Kwa kawaida tunaishi kwa kutegemeana. Kwa hiyo kila mtu hapa duniani anaweza kupata ajira kwa namna moja au nyingine inategemea yeye ameamua apate ajira ya namna gani. Mungu wetu ni mwaminifu, unapoendelea kusoma kitabu hiki nakuombea Mungu akubariki sana na kama una biashara yako utaenda kubarikiwa sana. Kwa kuwa ni muhimu uandike barua kwa mwajiri wako ili kutafuta kazi, jitahitahidi sana mara baada ya kuandika barua hiyo iombee au ipeleke kwa mchungaji wako akaiombee au mtu yeyote unayemwamini kwamba akiomba maombi yatasikiwa! Huyu Mungu tunayemtukia ni mwaminifu atatenda!

Mbinu za kuilinda kazi yako Watu wengi wakiisha kupata kazi huwa ni watu wa ajabu sana. Wanafanya kazi kwa bidii kwa muda mfupi tu lakini baada ya muda kidog wanageuka na kuwa watu wengine kabisa. Hali hii mara nyingi husababisha watu wengi kufukuzwa kazi. Watu wengi ambao nimewashauri na kuwaombea na kupata kazi mara nyingi nimekuwa nikiwashauri na kuwapa mbinu hizi ambazo nawe nataka nikupe ili 122

uepuke kufukuzwa kazi. Mbinu kuu ambayo ndiyo inabeba mbinu zingine ni kuwa na nidhamu katika kazi. Ndani ya mbinu hii tunapata mbinu nyingine ndogo ndogo kama ifuatavyo:-

1)

Kuwa na bidii katika kazi Mara unapopata kazi hakikisha kwamba unafanya kazi zako

ambazo umepangiwa kwa bidii. Acha kutumia muda wako vibaya kwa kuchati na simu muda mrefu huku kazi zinazidi kukulemea. Watu wengi wakipata kazi kwa mara ya kwanza huwa wana bidii sana lakini baada ya kuzoea eneo la kazi wanaacha maadili ya kazi zao na kufanya mambo yao.

2)

Epuka kuwa kikwazo kazini Wakati mwingine unaweza kuajiriwa mahali fulani ukajikuta

wewe ndiye umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya kampuni au taasisi. Kwa mfano kama wewe umeajiriwa kwa kazi ya mapokezi lazima uvutie wateja katika kampuni hiyo ili wasione wewe kuwa ni kikwazo kwao. Watu watapenda huduma yako na kuendelea kuwa wateja wa kampuni hiyo. Kila siku hakikisha kwamba haujawa kikwazo katika asasi uliyopo. Umekuta watu wanaendelea basi nawe jiunge kuendesha gurudumu la maendeleo. 123

3)

Epuka Majungu Majungu

ni

maneno

maneno

kuhusu

watu

wengine.

Kuzungumzia watu wengine wakati wao hawapo hayo ni majungu. Kuna watu wengine wakipata kazi baada ya kufahamiana na wafanyakazi wenzao kwa muda mfupi tu huingia katika majungu. Huanza kuzungumzia maisha ya watu wengine. Mara fulani anatembea na fulani! Mara bosi anatembea na fulani! Sasa wewe unayeongea pengine huna hata uhakika nayo ya nini hayo? Je uliomba kazi au uliomba kwenda kupiga majungu? Kama watu wanafanya mambo yao hayo hayakuhusu, wewe fanya kazi zako umalize. Utakuta mtu huyu huyu anayepiga majungu hata kazi zake hakamilishi. Ukifanya hivyo utafukuzwa kazi siku moja tu.

4)

Usijaribu kugoma au kushawishi wengine wagome Migomo na maandamano kama nilivyosema hapo awali kwamba

hayana faida yoyote ile. Usijaribu kugoma kazini hata kama unaonewa wala usijaribu kuwashawishi wengine wagome kwa sababu ukifanya hivyo utafukuzwa kazi peke yako na wengine utawaacha hapo. Kama kuna tatizo katika kazi yako, jaribu kufuata utaratibu mzuri wa kuonana na viongozi wa ngazi zote lakini usifanye mgomo wowote. Kitendo cha kugoma kinaonesha kwamba wewe huna nidhamu 124

ya kazi na kitasababisha ufukuzwe kazi. Vile vile usikubali mtu mwingine akushawishi kufanya mgomo kwani mtafukuzwa kazi haraka. Fimbo ya bosi huwa ni moja tu! Kukutimua kazini ili ukahangaike mitaani!

5)

Kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzako Uhusiano mzuri na watu wengine ni jambo la lazima katika kazi

yako. Usijaribu kuchagua watu wa kuongea nao. Najua kuna ile kushibana na baadhi ya watu lakini hakikisha hata kama kuna mtu umeshibana naye kazini wengine pia uwe na uhusiano mzuri nao. Unapokuwa na uhusiano na mtu mmoja tu kazini kama siku haupo na kukatokea tatizo lolote kazini wengine hawawezi kukwambia na pengine hata unayeshibana naye hayupo wakati huo. Hakikisha kila mtu unaongea naye kwa lugha nzuri. Ukifanya hivyo watu watakupenda na utakuwa mtu wa watu.

6)

Epuka mapenzi kazini ila uwe na mapenzi na kazi yako Mapenzi na kazi huwa haviendi pamoja. Nazungumzia mapenzi

kati ya mwanaume na mwanamke au kwa lugha nyingine ngono! Watu wengine hufukuzwa kazi kwa sababu ya mambo ya mapenzi. Kuna watu ambao hawawezi kutulia na wake zao au waume zao au siju watu 125

wao….? Sijui lakini ninachotaka kukwambia ni kwamba ukianza kuhusisha kazi na mapenzi tayari umeliwa! Unakuta mtu mwingine amekuta watu wametulia lakini akifika yeye anajiona kidume au kijike kila mtu anambeba tu! Ukifanya hivyo ipo siku utafukuzwa kazi maana unaweza kuvamia hata mke wa bosi! Mapenzi yanayoruhusiwa ni kuipenda kazi yako tu. Mapenzi na kazi yak o ndilo jambo la maana kuliko jambo lolote lile. Ukiipenda kazi yako utaithamini na wala hutafanya mchezo wowote kazini.

7)

Usiwe na Mawazo ya Kutafuta Kazi sehemu nyingine Kama unakumbuka vizuri nilisema kwamba kwa ajili ya kupata

kazi ni vizuri ukaomba kazi sehemu nyingine na kama ukipata uwe mwaminifu uwajulishe wale watu kwamba umepata sehemu nyingine. Lakini hoja hii hapa ni baada ya kupata kazi. Ukishapata kazi acha mawazo ya kutokuridhika na kazi yako. Maana kama ukifanya hivyo hutapata faida yoyote. Wewe utaendelea kuwa mgeni kila ofisi. Nimewahi

kuwaona

watu

ambao

hawamalizi

mwaka

wanaondoka kazini kwa sababu wanatafuta kazi kila siku sehemu nyingine. Mimi naamini kwamba ili uweze kujipanga vizuri ni lazima ukae muda mrefu kazini kwako ili uweze kupata angalau maendelea. 126

Unaweza kutafuta kazi sehemu nyingine kama mwajiri wako atakudhulumu. Nataka nikutahadharishe jambo hili, kwa kuwa umepata kazi usifikiri kwamba kila siku utapewa mshahara wako kwa muda muafaka! Wakati mwingine hata serikali inachelewesha mishahara. Sekta binafsi mara nyingine huchelewesha mishahara hata zaidi ya miezi mitatu, sasa siyo wakati wa kukimbia huku na huku kutafuta kazi, maana hata utakapoenda unaweza kukuta mambo ni yale yale. Kama mwajiri huwa analipa madeni ya wanafanyakazi, ya nini sasa kukimbia huku na huku kutafuta kazi. Kuna wakati mwingine mishahara inaweza kuchelewa kutolewa. Usijaribu kwenda kila mahali unamtangaza tangaza mwajiri wako kwani hali hiyo ni ya kawaida sana labda pengine ulikuwa hujui!

8)

Usipokee Simu Mbele ya Bosi wako Nimeona jambo hili niliweke bayana. Kuna watu wengine

pengine ameitwa na bosi kwenda kuzungumza mambo fulani fulani na mara simu inaita, bila aibu wala haya anapokea simu mbele ya bosi! Ni kosa kubwa sana ambalo linaweza kusababisha ufukuzwe kazi. Usifikiri kwamba kufukuzwa kazi mpaka uibe tu. Wakati mwingine unashangaa eti mtu anapigiwa simu ndani ya ofisi ya mtu huku anaongea na bosi 127

unashangaa anachukua simu na kuanza kuongea! Ni makosa makubwa hayo. Wakati mwingine hata mimi huchukizwa na watu wanaokuja katika ofisi yangu kwa ajili ya ushauri na maombezi, huku mkiendelea kuzungumza mara mtu anapokea simu na kuanza kuzungumza mambo mengine kabisa. Yaani mimi inabidi nimsubiri amalize mazungumzo yake ndipo nami tuendelee! Tafadhali kama unataka udumu katika kazi, uwe makini sana na matumizi ya simu ofisini.

9)

Ombea Kazi yako kila siku Maombi kwa kila jambo ni kumshukuru Mungu ni muhimu sana

katika maisha. Ili uilinde kazi yako ni lazima uwe unaiombea. Maombi yako yasiwe ya kinafiki ya kutaka kupandishwa cheo tu. Maana kuna watu wengine wakifika katika maombi wanaomba wenzao washushwe halafu wao wapandishwe! Nilimsikia mtu mmoja anaomba hivi ‘ninaangusha mapepo yanayoshusha kiwango changu cha kazi, nawaangusha wote waliopo hapo kazini ili mimi niwe kichwa, maana Mungu alisema hatutakuwa mikia bali vichwa.’ Maombi haya yaliniacha hoi bin taaban! Ni kweli ahadi kama hiyo ipo katika Biblia lakini ni katika mazingira gani sasa? 128

Na sisi wachungaji tunahitaji kuwaelewesha watu wetu ili wajue namna ya kuomba. Kama unataka kupandishwa cheo, ombea bosi wako kila siku. Kama bosi wako akipandishwa cheo wewe unaweza kushika mahali pake. Ombea wafanyakazi wenzako. Ombea shughuli zote za kampuni/shirika au shughuli zote za kazini. Hakikisha unapofungua ofisi yako unafanya maombi hata dakika moja. Hata kama watu wanakusubiri waambie kwanza wasubiri. Ukifanya hivyo utapata kibali kazini na kuendelea vizuri. Kuna watu wengine wanafukuzwa kazi kwa sababu ya ushindani wa kiroho tu. Watu wengine wanaenda kwa waganga wa kienyeji usiku kucha wanataka ufukuzwe kazi. Kazi kwako ni kuomba tu.

10)

Toa zaka 90% kwa mara ya kwanza na baadaye 10% Kutoa ni sehemu kubwa kubarikiwa katika maisha yetu. Kama

ukipata kazi kwa mara ya kwanza, mshahara wako wa kwanza unapaswa utoe asilimia tisini. Kuna siri katika hili. Ukisoma historia ya watu waliofanikiwa kwa njia ya haki wametoa zaka asilimia tisini ya mshahara wao wa kwanza katika kazi mpya.

129

Mtu fulani alienda kuuliza ushauri kwa mchungaji kwamba afanye nini ili kampuni yake iendeleee. Aliambiwa atoe zaka asilimia kumi. Jamaa akasema ‘kwa nini Mungu apokee kidogo nami nipokee kubwa’ akasema ngoja mimi nampa Mungu kwa mara ya kwanza asilimia tisini. Alipofanya hivyo alibarikiwa sana. Leo hii kampuni yake iko dunia nzima! Baada ya kutoa hiyo asilimia tisini basi miezi inayofuatia usikose kutoa zaka ya asilimia kumi kwa mapato yako. Kuna unaona kwamba nakudanganya basi jaribu mara moja uone. Hakuna mafanikio yoyote makubwa pasipo kutoa kwa Mungu na kwa ajili ya kazi yake. Sasa ukisikia akina Mengi wametoa shilingi milioni mia moja kwa ajili ya ujenzi wa kanisa inakuuma sana! Heee! Hujui? Lazima atoe kwa Mungu ili apate zaidi na zaidi. Usifikiri anachezea hela. Kwa taarifa yako, tajiri yoyote asipotoa kwa Mungu hutoa kwa mganga wa kienyeji. Sasa wewe unataka utajiri wako ulindwe na mganga wa kienyeji ambaye anweza kufa wakati wowote ule badala ya Mungu asiyekufa milele? Ukifuata kanuni za kutoa Mungu atailinda kazi yako. Kuna mambo mengi sana yanayolinda kazi ya mtu isiyumbe lakini haya niliyoyaweka hapa ni makuu mno kiasi kwamba mtu akiyafuata atafanikiwa sana.

130

11. Ongeza Ujuzi wa kazi yako Jambo la kuongeza ujuzi ni muhimu mno mtu wa Mungu unapoendelea na kazi yako. Watu wengi wamepata ajira na kubweteka, wamekaa na vidigirii vyao kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na tano katika ajira ile ile, jambo ambalo ni hatari kubwa sana. Unapaswa uongeze ujuzi katika fani yako. Kama huwezi kuchukua masomo ya hali ya juu, basi jitahidi sana angalau ujisomee vitabu mbalimbai kuhusu Nyanja yako, na hata Nyanja zingine. Rais wa Tanzania wa awamu ya tatu, Bwana Benjamini Mkapa aliwahi kusema kuwa kujisomea vitabu ni jambo la muhimu mno kwani unaweza kuongeza maarifa ambayo hukuwahi kuwa nayo na hivyo unaweza kusaidia jamii. Ndugu yangu, ninakupa changamoto kwamba, usibweteke, soma vitabu, ongeza maarifa. Tena siku hizi huhitaji kuna vitabu vingi katika mitandao. Unaweza kuingia katika mitandao yenye vitabu vya bure, unasoma kimoja kwa kingine. Lakini pia unaweza kununua vitabu. Ninataka niongeee zaidi kuhusu usomaji wa vitabu. Nilipokuwa nasoma masomo yangu Korea Kusini, kila nilipokuwa nikiingia kwenye ofisi na wahadhiri nilikuwa nakuta vitabu vingi sana mezani, na vingine havihusiani kabisa na Nyanja niliyokuwa naisomea (theologia). Baadaye nilikuja kugundua kwamba wenzetu wanakusanya maarifa mengi kutoka katika Nyanja mbalimbali. Hii inasaidia sana kujua mambo mengi 131

yaliyotokea, yanayotokea na pengine yatakayotokea baadaye! Tatizo wapendwa utakuta tu anasoma Biblia (sikatai kabisa na ninakusihi uisome kila siku-hii ni mada nyingine) lakini hata Biblia hiyo anaisoma kwa kudonoa donoa tu. Mara leo Marko, kesho Mwanzo (tena kimstari kimoja kinasomwa huku akisinzia). Hapana! Tunapaswa kujitahidi kuongeza maarifa kutoka sehemu mbalimbali ili tumudu soko la ajira liliko mbele yetu. Usipojiendeleza, basi kuna mambo mawili yanaweza kutokea kwako: 1) kutokupandishiwa msharaha wako. 2) Kupunguzwa kazi kwa taarifa kwamba tutakupigia simu. Amua mwenyewe, kusuka au kunyoa. Che Guava mpaka anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, Nkrumah library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asubuhi lazima asome kitu kipya.

SURA YA SITA Funguo Nne Nilipokuwa nikieleza vyanzo vya umasikini na kupungukiwa katika maisha yetu, nilikuwa naeleza chanzo hicho, lakini pia nilikuwa naweka na angalizo kwa watu wote wanaopitia katika changamoto hii, kwamba kama mtu akiepuka sababu hiyo,basi anaweza akachomoka pale alipokwama. Katika surah ii nimekuletea funguo nne, ambazo 132

zaweza kuwa kama majumuisho lakini kuna tofauti ndani yake. Funguo hizi ni elimu yenye upeo kwako na ukisoma vizuri katika funguo hizi utagundua mambo matatu muhimu 1) utagundua nafasi ya Mungu kwako 2) utagundua nafasi yako wewe kama wewe, na 3) utagundua nafasi ya watu wengine kwako. vyote hivi vinashirikiana na kumpa Mungu utukufu.

Fungu 1 Sawazisha mtazamo wako kuhusu Mungu Mungu ni Mungu wa utaratibu, tunaamini katika nguvu zake na kwamba anaweza kufanya jambo lolote lile ambalo lipo katika shabaha yake. Biblia imejaa matendo makuu ya Mungu, miujiza katika Biblia inathihirisha ukuu wake. Hata sasa Mungu anaweza kufanya miujiza katika maisha yetu kwa namna ya ajabu sana. Tumeshuhudia watu wengi wakifunguliwa katika matatizo yao ya kiuchumi, magonjwa pamoja na matatizo mengine. Tunapoona mambo haya tunajenga matarajio kwamba pengine Mungu atafanya kwetu kwa njia ile ile au atafanya hivyo hivyo kama alivyofanya kwa mtu fulani katika Biblia! Ndiyo anaweza kufanya lakini si lazima afanye hivyo hivyo! Huu ndio ukweli kuhusu Mungu.

133

Hivyo basi, tunapoingia kwenye maombi, tusimlazimishe Mungu na kumwelekeza kwamba “Mungu fanya hivi kama ulivyofanya kwa huyu jirani yangu.” Hii siyo imani bali ni “tamaa tu.” Unapomwelekeza Mungu afanya jambo fulani kama alivyofanya kwa mtu mwingine ni maana yake ni kumzuia kufanya jambo ambalo ni zuri zaidi kuliko la huyo mtu mwingine. Kila mtu atatendewa kivyake na Mungu kulingana na namna ambavyo Mungu ameamua kufanya katika shauri lake na pia katika imani ya mwombaji. Matarajio yako yanaweza kuwa matarajio yasiyofaa kama hautakuwa makini. Katika maandiko Matakatifu tunaona mambo mengi ambayo Mungu aliyafanya kwa watu fulani fulani lakini watu wengine kwenye matukio kama hayo hawakuondolewa. Mungu alimwokoa Yusufu kutoka gerezani lakini yule mwokaji alikatwa kichwa (Mwanzo 40). Mungu alimwokoa Musa kutoka kwenye kifo kwenye Mto Nile lakini wapo watoto wengi waliuawa kwa njia hiyo. Mungu alimtunza Yeremia asiuawe na umati lakini nabii Uria aliuawa na mfalme Yehoakimu (Yer 26). Petero aliokolewa kutoka gerezani lakini Yakobo alikatwa kichwa (Mdo 12). Yesu aliponya wengi lakini hakumponya Paulo kwenye mwiba wake. Yako matukio mengi sana ya namna hii katika Biblia. Jambo la kujiuliza tufanye nini sasa? Ni kusimama na Bwana peke yake. Kama Bwana alimwokoa fulani si lazima nami 134

aniokoe kwa njia ile ile lakini Mungu atabaki kuwa Mungu. hebu sikiliza Shadrack Meshaki na Abedinego walivyosema “…hata kama Mungu asipotusaidi, hatuko tayari kuabudu sana yako ee Mfalme” (Dan. 3:17-18). Je Mungu aliwaacha? Hapana! Aliwapigania vijana hawa na tanuru la moto. Huo ndio mtazamo ambao unapaswa uwe nao wewe. Mtu mmoja aliwahi kuniambia kwamba kama mtu asiponibariki mwaka huu najinyonga! Nikamuuliza, kwani lazima Mungu akubariki? Nikamuuliza kwani Mungu alikwambia atakubariki na kitu gani? Hakuwa na majibu. Mtu mwingine aliniambia “mchungaji yaani mwaka huu kama nisiponunua gari naachana na mambo ya wokovu.” Hii ni mitizamo mibaya sana kuhusu Mungu. yaani unamfanya Mungu kana kwamba ni mwanadamu? Je hiyo ndiyo imani? Lazima ifike mahali useme kwamba “hata kama Mungu asiponisaidia, sipo tayari kutenda uovu huu ili nijipatie faida.” Unachotakiwa kujua ni kwamba, Mungu anataka watu wake wamtumainie katika maisha yao yote, lakini kwa vile amesema hivyo, siyo kwamba amejifunga, bado Mungu ana uhuru wake wa kufanya mambo. Lakini yote katika yote lazima usimame kwa imani na mtazamo wako kuhusu Mungu lazima uwe sahihi, vinginevyo utaingia kwenye manung’uniko mbele za Mungu kwa kumwona Mungu kuwa ana 135

upendeleo. Mungu hana upendeleo, anachokifanya hukifanya kwa sababu kipo katika shauri lake. Ukiwa na mtazamo huu, imani yako itapiga hatua moja kwenda nyingine na utadumu kumtegemea Mungu siku zote. Unapata chakula kwa taabu? Sawa, lakini kumbuka kuna mwingine ambaye ana chakula cha kutosha lakini amelazwa! Sasa wewe ungependa ipi? Ukalazwe au utafute? Hayo yote anayajua Mungu peke yake. Huna mtoto? Sawa, lakini kuna mwingine anao watoto lakini wote wanamsumbua sana, maisha yake yamekuwa ya uchungu, unakuta mtu anatoa kauli kama “kuzaa ni kutoa uchafu tumboni!” Lakini katika mambo yote, tunapaswa kumwacha Mungu ashughulike na maisha yetu kama alivyopanga. Kama umekosa kitu fulani, usiwe mtu wa kunung’unika mbele zake bali uwe mtu wa kushukuru. Ninaamini katika utafutaji mtu hupaswi kukata tamaa, lakini pia naamini kwamba Mungu yuko kazini muda wote. Siamini katika bahati ya Mungu (majaliwa ya Mungu) ila naamini katika “Uhuru wa Mungu” na maamuzi yake. Hoja hii si “fatalisimu” 40 bali ni predestination ya

40

Ingawa Fatalisim na Predestination zinafanana katika tafsiri kwamba ni imani kwamba kila kitu kimepangwa na Mungu, lakini katika utendaji wake ni tofauti kabisa. Fatalism wanaamini kuwa mwanadamu hana kitu cha kufanya kabisa kuhusu suala mstakabari wake, kwa hiyo inategemea nguvu ya bahati ambayo imepangwa kwake. Lakini predestination ni mzizi wake ni kwa Mungu mwenyewe (siyo nguvu fulani) katika tabia ya Mungu binafsi na mwenye haki, Bwana wa historia. Mtu yeyote

136

Kimungu kwa watu wote. Wale wanaokataa mawazo ya kipredestination huishi kwa hofu sana kwa sababu wanafikiri kuna nguvu fulani ya bahati ambayo haijawaangukia. Nitaeleza jambo hili katika kitabu kingine. Lakini narudia kusema Mungu anabaki kuwa Mungu, mwanadamu anabaki kuwa mwanadamu. Maswali ya kwa nini tuombe, au tufanye kazi majibu yake nimeshayatoa ni kwamba kwa sababu Mungu ametuagiza kufanya hivyo. Sasa kama ameagiza kuombausipoomba ni dhambi. Kwa hiyo Mungu hushirikiana pamoja nasi katika kutimiza kusudi lake katika maisha yetu.

Fungu 2 Tambua mambo ambayo unayoyaweza na yale usiyoyaweza Mojawapo ya mistari pendwa katika Biblia ni Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Je mstari huu unamanisha nini? Watu wengi wamekuwa wakinukuu mstari huu nje ya mazingira yake. Maana ya mstari huu siyo kupewa uwezo wa kupata mambo mazuri tu katika maisha yako, bali ni kupewa nguvu ya kupitia katika mapito. Kwa hiyo unaposoma mstari huu lazima usome kuanzia mstari wa 11-12 anaposema “Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina ambaye anataka awe na amani moyoni mwake na maisha yajayo, lazima aamini katika predestination.

137

mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.” Sasa kupitia mapito hayo, Paulo anasema anayaweza mambo yote, yaani katika shida anaweza kuishi na katika raha anaweza kuishi. Katika maisha yetu, ni vizuri sana kujua kuna mambo gani ambayo huyawezi. Siyo tu kusema eti nayaweza mambo yote! Je wewe unaweza kutengeneza simu? Unaweza kufanya biashara zote? Je wewe unaweza kufanya mambo yote? Kama ingekuwa hivyo tusingehitaji watu wengine. Jambo la msingi kujua ni kwamba unapaswa kujua maeneo ambayo wewe unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko maeneo mengine. Kuna mwingine anaweza kuimba vizuri lakini mwingine anaweza kupiga gitaa na kinyume chake. Sasa tunapozungumzia masuala ya kujikwamua kiuchumi, haiwezekani wewe unakuwa unafanya kila kitu wakati mtaji wenyewe umekopa. Kuna maeneo katika kazi zako unaweza kufanya vizuri sana, kwa mfano kuna watu wengine wanaweza kufanya biashara ya mama Ntilie vizuri mno kuliko wengine. Na kupitia biashara hizo, watoto wao wanaenda shule; sasa wewe iga uone! Utaishia kulaumu kazi za watu. Tukisema watu wajitahidi kujua mambo wanayoweza kufanya vizuri, watu wengi na wewe hupenda 138

kusema ‘’usikubali udhaifu’’ huo sio udhaifu ni kujitambua! Kujitambua siyo udhaifu bali ni ujasiri wa kukufanya uwe mtu anayejitathmini kila wakati.

Funguo 3 Tambua watu ambao Mungu amewaandaa kwa ajili yako Si mara zote lakini mara kwa mara Mungu anatumia watu kwa ajili ya kutimiza kusudi lake. Tunaposoma Biblia tunaona katika matukio mengi, Mungu alipotaka kuwasaidia watu wake ili kutimiza kusudi lake aliwatumia au aliandaa watu kwa ajili ya kushirikiana nao. Tuangalie mifano kadhaa katika Biblia:Mungu aliandaa watu mbalimbali kwa ajili ya Yusufu (mfano, Simon, Potifa, Mnyweshaji na Farao), Mungu alimwandaa Haruni kwa ajili ya Musa. Musa alibishana na Mungu, kwa sababu hakuwa na ujasiri wa kuzungumza, Mungu alimteua Haruni kuwa msemaji wa Musa (Kutoka 4: 14-16). Mungu anapokuwa ameinua watu kwa ajili ya yako usiwadharau hata kidogo. Utakapowadharau ni sawa na kumdharau Mungu mwenyewe na kushindwa kuwa mtu wa shukurani. Tunaona namna 139

Mungu anavyowatumia watu kukuinua wewe, sasa hao watu usifikiri wamejileta tu, eti na wewe una ngekewa sana, hakuna kitu kama hicho bali Mungu anakupatia kwa ajili ya kutimiza kusudi katika maisha yako. Hebu tujifunza kupitia misheni ya Gideoni kwa undani zaidi ili uweze kuelewa ninachosema. Kwanza unapaswa ukumbuke kwamba wakati Mungu alipomwambia Gideoni ajiandae kuwaokoa waisraeli alikataa kwa sababu ya kabila lake. Soma Waamuzi 6 -7. Ukisoma hapo utaona namna Gideoni alivyojiona dhaifu, na hafai, na alimuuliza Mungu nawezaje kuwaokoa? Kwa sababu kabila lake la Manase ni dogo na yeye ndiye hohehahe katika familia yao. Kwa kuwa Gidioni alikuwa na wasiwasi na wito wake, ilibidi ambane Mungu kwenye kona ili amhakikishie kama ni kweli au la! Gidioni akamwomba Mungu kuwepo kwa umande juu ya ngozi tu na sehemu nyingine iwe kavu 6:37— Mungu akafanya kama alivyoomba. Gidioni hakuridhika na jibu la kwanza, akaomba tena ngozi iwe kavu na sehemu nyingine iwe ilowane maji. Mungu akafanya hivyo. Kile ninachotaka kusema kwa sasa ni kwamba Mungu huandaa mazingira kwa ajili yakow ewe. Mazingira haya yote yalikuwa elekezi kwa ajili ya Gidioni kuwa na uhakika na kile alichoomba kwa Mungu.

140

Mungu aliandaa mazingira haya kwa ajili ya kumtia Moyo Gidioni ili aende katika vita hivyo. Mungu alikusudia kumpatia ushindi mkuu Gidioni kupitia wanajeshi wachache sana! Lakini Gidioni hakujua hilo na badala yake akakusanya wanajeshi 32,000! Ni wengi sana. Lakini Mungu akatoa wazo; Wanaopaswa kuondoka kwa hiari yao wenyewe.. (wanaoogopa, na kutetemeka)—hawa walipaswa kurudi nyumbani kwa hiari yao wenyewe! Watu 22,000 wakarejea nyumbani na wakabaki 10,000 nao walionekana kuwa wengi. Hey! Ingekuwa mimi ningeanza hata kulia! “Jamani sasa nitafanyaje watu wanaisha, nani atanisaidia jamani!” labda pengine ningewaambia waliobaki, “Jipeni moyo jamani twendeni!” jibu la Mungu ni hapana, ninataka nichague kundi la watu maalumu kwa ajili yako! Kuweka mchujo kwa vigezo. Mungu akafanya jaribio dogo pale mtoni—wanajeshi watakaoramba maji kama mbwa wachukuliwe. Biblia inasema watu 300 tu ndio walioramba na watu 9700 wakanywa kwa kulala chini kabisa! Hao 300 walikuwa tayari kwa lolote lile litakalotokea. Hapa ndipo tunaweza kusema Mungu hahitaji watu wengi ili aweze kutenda muujiza kwa ajili ya watu wake. Kama wakiwepo watu wawili tu wenye imani Mungu anatenda kazi! Mungu akipandisha vigezo tu, wataondoka wenyewe wala huhitaji kuhangaika saana! 141

Mungu alifanya haya kwa ajili ya kumhakikishia Gidiaoni ya kwamba atashinda! Mungu akamwandalia watu wachache wa kuvuka naye katika vita ile. Mungu ameandaa mtu gani kwako kwa ajili ya kukuvusha? Wakati mwingine inakuwa ni vigumu sana kujua watu ulio nao lakini wapo tu. Gidion aliendelea kuwa na wasiwasi! Biblia inasema “Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako Lakini, ukiogopa kushuka, shuka pamoja na Pura mtumishi wako kambini; (7:10). PURA-Mtumishi huyu aliandaliwa mahali hapa kwa ajili ya kumtia moyo Gidioni ili asiogope. Kama ilivyokuwa kwa Baraka alipoogopa kwenda kumpiga Sisera, Mungu tayari alikuwa amemwandaa Debora kwa ajili yake. Amuzi 4:8. Umeona nini katika kuhusu Gideoni? Ndiyo, Mungu wakati anaweza kuwaondoa watu wasiohitajika katika kushirikiana na wewe katika safari ya mafaniko-ukiona wanaanza kuondoka, acha kulia lia, pengine Mungu anataka afanye mazingira ya kukufanya utoke ulipokwama. Unaweza kuwa na wafanyakazi wazuri ambao umeshibana nao katika kazi yako, lakini wakati wa kuondoka unapofika, waache waondoke, kwa sababu misheni yao ya kuwa nawe imeishia hapo. Tarajia kwamba Mungu anaendaa kukupa mtu wa kuambatana naee: 142

anaweza kuwa mke wako/mume wako, rafiki yako, mchumba wako nk lakini yule yule unayepewa na Mungu ndiye ambaye mtavuka naye, naye atakutia nguvu—usimdharau! kumbuka Baraka alimng’ang’anie Debora waende wote! alijua kuna kitu kwake. Kuna vitu vingi sana Mungu ameweka ndani ya watu wanaokuzunguka vitu vingi kwa ajili yako. Usiwadharau hata kidogo. Thamini wale unaokuwa nao kila wakati. Tunayo mifano mingi ya Kibiblia kabisa kuhusu Mungu anavyoandaa watu wengine kwa ajili yako, hebujaribu kukumbuka Mwanamke wa Sarepta alivyotumiwa na Mungu kumpa chakula Eliya, lakini Eliya huyohuyo alifanyika baraka kwa mama huyu na chakula hakikupungua kimiujiza. Katika huduma ya Yesu Kristo hapa duniani, kuna wanawake ambao waliandaliwa kutoa mahitaji kwa Yesu.( ieleweke kwamba Yesu alikuwa katika nafsi ya ubinadamu pia), kwa hiyo wanawake hawo alimtoa "rasilimali" zao. Akina Mariam Magdalena, Yoanna aliyekuwa mwanamke mwenye cheo cha juu aliyeolewa na mwanamume aliyekuwa mwenye akili na mwenye uwezo wa kutosha kusimamia nyumba ya Herode Antipa, mwana wa Herode Mkuu. Hawa wote walilisha kundi la Yesu na wanafunzi wake. Je Yesu hakuwajali wamama hawa? Yesu aliwajari sana (Luka 8:1-3). 143

Tunahitaji watu wa kila namna katika maisha yetu ili yaweze kusonga mbele. Unaweza kumuona mtu leo hafai, lakini mtu huyo ni wa muhimu sana, na Mungu ndiyo amemleta karibu nawe ili kukusaidia wewe. Naomi Mduma41 alitoa mada kwenye mtandao mmoja wa kijamii na kudai kuwa kila mtu anahitaji watu wa aina saba, kama ifuatavyo 1) mtu aliyekuzidi kipato,elimu,maarifa viwango vya kiroho

na hata

muonekano ili uzidi kusonga mbele,ujifunze kutoka kwao

na

usibweteke, 2)mtu uliyemzidi kipato,elimu,viwango vya kiroho,maarifa ili upate moyo wa kusonga mbele na kuona kuwa unapiga hatua, 3) mtu anayekupinga,ili uweze kutambua,kuona,kusahihisha na kuongeza umakini ktk kila ufanyalo 4) mtu anayekusifu/kutiana moyo ili upate sababu ya kusonga mbele hasa pale unapokatishwa tamaa na wakosoaji wako. 5) Adui, huyu anakusaidia kuishi na kufanya kila jambo kwa tahadhari na umakini wa hali ya juu. 6) Rafiki,huyu hukupa sababu ya kusonga mbele,hucheka pamoja nawe na hulia pamoja nawe, ni msiri wako,ni mfariji ni mshauri na mwelekezi mzuri 7) wa kukuombea huyu kukuinua katika ulimwengu wa kiroho na anakusaidia vita ambayo kwa silaha za kawaida haiwezekani.

41

https://www.facebook.com/search/str/naomi%2BMduma/keywords_blended_posts? Imepakuliwa 8/7/2017 saa 12:46

144

Ukiangalia kwa umakini hoja za Mduma utangundua kwamba zina uhalisia ndani yake, kwani maendeleo hayapatwi kwa mtu kukaa peke yake, bali ni kwa kushirikiana na wetu wengine wanaomzunguka. Na watu wanaokuzunguka wana tabia tofauti tofauti, kama wewe ulivyo na tabia tofauti nao. Kwa hiyo ni lazima uwathamini watu walio karibu nawe. Hao wote Mungu amewainua kwa ajili yako.

Funguo 4 Epuka uchoyo na tamaa ya mali Kwa yeyote yule anayetaka maendeleo ni lazima aepuke roho ya uchoyo. Kwa kawaida roho ya uchoyo ndiyo inayosababisha tamaa ya mali, hii inatokana na ukweli kwamba mtu huyu akiwa na tamaa ya namna ya hawezi kuridhika hata siku moja. Yeye kila siku ni hasara tu. Nafikiri umewahi kukutana na watu wanaosema wamepata hasara hata kama wameuza kwa kiwango kikubwa na kwa faida kubwa. Kwa mfano unakuta mtu anasema “unajua jana nilipata hasara kubwa sana,” lakini ukweli anaujua mwenyewe kwamba amepata faida kubwa. Huo ni uchoyo, na roho hii inapoendelea kustawi ndani ya mtu husababisha awe na tamaa ya pesa ambayo inakemewa na maandiko. Ingawa nimesikia watu kadha wa kadha wakisema kwamba “pesa ni mbaya sana” lakini maandiko matakatifu hayajawahi kusema kwamba pesa ni mbaya. Somo 145

moja la Biblia ambalo wengi wetu hawaelewi kuhusu pesa. Mistari mingi inayohusu pesa mara nyingi inapotoshwa kwa sababu ya tamaa za watu walioshindwa kutawala maisha yao. Kwa kwa mfano “kwa maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; wambao wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi” (1 Timothy 6:10). Umeelewa nini hapa? Shida kubwa ya hapa ni “kupenda fedha” siyo “fedha yennyewe” au kwa lugha nyingine shida iliyopo hapa ni “yule mtu anayependa fedha” na wala siyo fedha yenyewe. Wasomaji wa Paulo walijua kuwa nia za kifedha na uchoyo zilikuwa zimesaidia kuharibu ushuhuda wa baadhi ambao waligeuka (labda) kutoka nafasi za uongozi katika kanisa kuwa walimu wa uasi. Kufuatiwa na tamaa, wapinzani "walipoteza njia yao," mfano mzuri wa jinsi tamaa ya utajiri inavyomgawanya mwamini na Mungu (Mt 6:21, 24; 13:22; Luka 12: 1621). Kwa hiyo unaweza kugundua kwamba pesa kama pesa siyo mbaya, tatizo linakuja pale mtu anapopenda pesa na kujawa na uchoyo. Uchoyo wa mali unapokuwa umeongezekana madhara yake ni makubwa mno. Ni bora kutokuwa na mali kabisa kuliko kujawa na roho ya uchoyo wa mali.

146

Paulo anaelezea mchakato wa hatua tatu: (1) tamaa ya pesa; (2) Udanganyifu wa fedha; (3) uharibifu unaosababishwa na fedha. Kanuni iko hivi “mzizi huamua matunda.” Mzizi husababisha mti uzae matunda ya aina fulani. Kwa sababu ya kupenda pesa, kila kitu kinachozaliwa kinakuwa dhambi kabisa. Uchoyo ni tamaa ya kumiliki vitu vyote badala ya kumpenda Mungu aliyefanya vitu hivyo. Paulo alionyesha kwamba mali ni upumbavu kwa sababu inashindwa kufanya maandalizi kwa maisha ya milele na inaongeza huzuni kubwa katika maisha ya hapa duniani. Paulo anaweka onyo kwa wale wanaopenda pesa na uchoyo umewakalia ndani yao. Pesa siyo lengo kuu la maisha yetu, na ndiyo maana mtume Paulo aliwaonya wasomaji wake kuhusu pesa. Kama pesa umeiweka kuwa lengo la maisha yako, basi wewe umepoteza lengo la maisha yako! Unahitaji kujisahihisha na kubadilisha mtizamo wako kuhusu pesa unazopata. Watu wengi walio wachoyo wa mali hujifikiri wao kwanza na jinsi ya kupata faida yao binafsi kwa haraka haraka. Watu wanapokuwa wameingiwa na uchoyo, hutamani kila kitu kiwe cha kwao. Yaani anapoona hata shamba la mtu mwingine, anataka liwe la kwake! Akiona gari limepita, anataka liwe la kwake! Akiona nyumba nzuri, anataka iwe yak wake! Akiona mke wa mtu mzuri, anataka awe wa kwake! Chochote kile anachokiona anataka awe nacho. Hiyo ndiyo tamaa ya kupenda 147

pesa. Unajua sasa matokeo yake? Mtu huyu yuko tayari kuacha imani yake kwa sababu tu ameahidiwa pesa. Unapaswa kujiangalia sana katika maisha yako kama tamaa ya pesa haijakutawala. Ukishaingiwa na tamaa ya pesa, kila siku utataka kutengeneza faida tu. Mtu mwenye tamaa ya pesa hata urafiki hata siku moja. Nimewahi kuwasikia watu kadha wa kadha wakisema “hakuna urafiki juu ya pesa.” Nimethibitisha mambo haya kwa sababu mtu mwenye uchoyo wa pesa, basi yuko tayari hata kumuua mzazi wake kabisa ili apate pesa. Tumeshuhudia vijana wengi wakiwaua wazazi wao, n ahata ndugu zao wa karibu kwa sababu wameahidiwa pesa. inabidi umwombe Mungu kila siku kwa ajili ya kushinda tamaa ya pesa. Ukishinda tamaa ya pesa, unaweza kupata pesa zaidi-ukishindwa na tamaa ya pesa, unaweza kupata pesa zaidi lakini itakufarakanisha na imani yako. Akifafanua katika kitabu cha Mhubiri 5:8-20, Wright42 alieleza yafuatayo kuhusu uchoyo; uchoyo unapoungana na tamaa ya utajiri huzalisha kitu kinachoitwa “kutoka chini kwenda juu” kwa maana ya kwamba fedha hutiririka kutoka kwa watu masikini kwenda kwa watu tajiri tu. Na anaendelea kusema kuwa “kwa kadri unavyozidi kuwa tajiri, basi ndiyo ujue kwamba masikini wanazidi kukuzunguka” na hivyo 42

Wright, Christopher J. H. Sweeter than Honey; preaching the Old Testament. Cumbria: Langham Preaching Resources, 2015. Pp. 258-59.

148

tamaa yako ya pesa inakufanya usiwe na amani tena kwa sababu ya kundi kubwa linalokuzunguka. Lakini maisha yanapaswa kufurahiwa kama zawadi kutoka kwa Mungu kwa hiyo vitu vyote ambvyo vinatoka kwa Mungu havichukuliwi kwa uchoyo bali hupaswa kufurahiwa kwa kushirikiana na watu wengine ambao kwa wakati huo bado hawajapata nafasi ya kumiliki vitu ambavyo Mungu amekupa. Kwa hiyo, pesa kama pesa haina tatizo, kama ukiweza kukwepa uchoyo wa kujikusanyia mali kwa ajili yako mwenyewe tu, unaweza kushinda. Mali ambazo Mungu ametupa ni kwa ajili ya watu wote, ingawa tunaonekana kwamba ni mawakili wa Mungu lakini lazima tujue kutumia mali za Mungu kwa pamoja na watu wengine. Nilisikiliza mahojiano ya kijana mmoja anayeitwa Benjamin Fernandes,43 (baba yake ni yule mchungaji wa kanisa la AGAPE). kijana huyu alitamka maneno yaliyogusa moyo wangu sana. Alikuwa anahojiwa kwa nini ameamua kurudi Tanzania ilhali alikuwa anasemo kule Marekani alikuwa amepata kazi ya kulipwa kwa mwaka milioni 425. Pamoja mambo mengi aliyoeleza kijana huyu lakini alikaza kitu kimoja kwamba “pesa siyo lengo lake katika maisha” kwa hiyo alisema 43

https://youtu.be/GvLf_us919Q imepakuliwa tarehe 9/7/2017 saa 3:50pm

149

ameamua kurudi nyumbani kwa sababu anaipenda nchi yake. Alieleza vitu vingi sana lakini alisema pia kuwa bidii kujumlisha mambo ni mafanikio katika maisha. Lakini muhimu sana ni kushinda uchoyo wa fedha. Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa “fedha ina matairi, unapoifuatilia kwa bidii na uchoyo, inakuacha mbali sana.” Mwisho Ndugu mpendwa, jambo la msingi katika maisha yetu; ama tuwe na vitu vingi, ama tusiwe navyo, ni muhimu kuwa na ushirika na Mungu wetu wa karibu sana. Tunaweza kuwa matajiri kupindukia, inafaa nini kama uhusiano wetu na Mungu ni mbovu? Unaweza ukawa na bidii ya kutafuta utajiri kwa njia yoyote ile lakini inafaa nini kuishi maisha ya raha hapa duniani, maisha ambayo hayazidi miaka mia moja na ukaishi maisha ya milele Jehanam? Haisaidii kitu kabisa, ninakushauri utafute mali kwa bidii zote lakini usimsahau Mungu wako! Mungu anapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza katika maisha yetu. Tunaweza kufanya mambo mengine yote lakini jambo la kutiliwa mkazo ni kwamba lazima tuishi na ushirikiano na Mungu wetu. Hakuna jambo zaidi ya hilo katika maisha ya hapa duniani. Kumbuka kwamba kuna wakati utakufa tu, je kama umejikusanyia mali zako binafsi na kwa uchoyo wako ambao umekugubika, hutaki hata kutoa mali uliyo nayo 150

kwa ajili ya kazi ya Mungu, je mali hizo zitakusaidia mbele za Mungu? Usijivunie mali uliyo nayo yote inatoka kwa Mungu.

151