Koja La Lugha

Citation preview

KOJA LA LUGHA

Gia

wa

———

wA / KOJA

LA LUGHA | —.

KIMEANDIKWA

SHAABAN

NA

ROBERT ia

RI

Nairobi OKFORD UNIVERSITY PRESS Lusaka Addis Ababa 1969

nd

Oszford University Press, Ely House, London,

W.I.

N GLASGOW NEW YORK TORONTO MELBOURNE WELLINGTO ADDIS ABABA CAPE TOWN SALISBURY IBADAN NAIROBI LUSAKA BOMBAY CALCUTTA MADRAS KARACHI LAHORE DACCA KUALA LUMPUR SINGAPORE HONG KONG TOKYO

Fil 8 70 Y/

'KBA ei

Jaba uda O Ozford University Press 1969

—— )

SHA

Aa

AA



TAZ

IARARE ASB

536207 JAN 971975 Made in East Africa

UTANGULIZI YOTE yapasayo kuelezwa hapa yamesemwa katika kitabu cha kwanza isipokuwa juu ya sura ya mwisho

ya kitabu hiki ambayo nimefanya tafsiri tu. Kwa asili shairi hili liliandikwa na Francois Marie Arouet de Voltaire aliyeishi zamani za 1694-1778, karne mbili na

nusu zilizopita. Huyu ni mmoja wa walimu wakuu na

waandishi bora kabisa wa Kifaransa. Kwa tafsiri ya Kiingereza iliyofanywa na Joseph McCabe shairi hili lilipangwa kwa beti kumi za mistari 234. Kwa tafsiri ya Kiswahili limepangwa kwa beti 48 za mistari 240, kila ubeti mistari mitano. Usanifu wa shairi hili wapendeza na kufikirisha sana. Nimelifasiri asaa likawapendeza wengine kama lilivyonipendeza mimi.

Juni 1945

Shaaban Robert

WAFU

WENYE

SAUTI

Bwana Mwalimu Kihere, niawini mpwao, Naona kiherehere, piga ramli na bao,

Usiseme kazi bure, itatukuka kaziyo, Upesi jibu lichore, ueleze watu hao.

Abushiri wa Mbwana, tunga kwa vituo, Mistari pima sana, pasiwe ipitanayo, Kisha iwe na maana, ueleze watu hao, Po pote ulipoona, miujiza kama hiyo. Haya bin Hanasa, kina cha Mambo Leo, Kujibu kutakupasa, unitoke mshangao, Ajabu ya hiki kisa, sioni wake upeo, Mfu asemaje hasa, akashinda wazikao? Tena Mzee Waziri, Simulia kwa shairi, Namna ya wasafiri, Tunga kwa mistari,

stadi wetu wa leo, Mombo mji ukaao, wazikao kama hao, isiyopitana cheo.

Fundo niliyofunga, yataka wafunguao, Abdi bin Matunga, haraka nijibu leo, Wengine wakitunga, sitakasirika nao, Mimi kinanitinga, kisa cha mfu huyo.

Nikiwaza ya maiti, na watu wamzikao, Naapa kuwa sipati, usingizi nitakao, Wafu wenye sauti, bado kukutana nao, Nataka madhubuti, kwa watu waelewao, Madhubuti nataka, ili nitulize moyo, Daima nasumbuka, kutafuta siri hiyo, Leo nipeni hakika, msomao Mambo Leo, Kwayo nilipofika, nitangoja wajibuo.

1

USHAIRI USHAIRI ni sudi, mwenye nao ni kipawa, Kipawa cha ustadi, hedaya watu hupewa, Waimbao wana jadi, ya kusema kwa maua,

Maneno huyachagua, yanayokidhi kusudi.

Huchagua na kupima, maneno wanayonena, Mepesi mtu kusema, na kudhibiti maana, Yanayoimbika vema, na sauti kulingana, Hawayapendi sana, maneno ya kukingama. Japokuwa lina kina, neno la kukingama, Huwa halifai sana, mashairini hukwama, Kisha hupoteza maana, uzuri hata kima, Shairi haliwi jema, lugha ikitatizana.

Maneno yakisongana, maanaye huwa kiza, Japo likiwa na kina, shairi litapooza, Maneno yakikosana, hayafanyi mwangaza, Shairi la kutatiza, halina faida sana,

UTUKUFU

MAISHA ya saa moja, maisha ya utukufu, Yapayo watu faraja, hukumbukwa halafu, Kuliko karne moja, miaka mingi mirefu, Isiyo makumbukifu, kwa watu wanaokuja. Hadithi za wanadamu, zo zote ukiziona,

Zilizo mbaya na tamu, au zisizo maana, Asiliye fahamu, zinajengwa kwa majina, Hukuzwa lake jina, mtenda neno muhimu. 2

Hauji usingizini, utukufu wa dunia, Kwa kulala kitandani, kama kuota ruia, Wala haupatikani, pasipo kushindaniwa, Wenda kwa wajaribiwa, utukufu duniani. Jitahidi kujaribu, wajaribuvyo wenzio, Usizichelee taabu, taabu huleta mazao,

Ndiyo njia ya dhahabu, watu waipitayo, Hupata ayatakayo, kila mhimili taabu.

UVIVU UVIVU niepukie, sifahamu faidayo, Kila ukaaye naye, mwisho hulia kilio, Mbele yangu jiondoe, sitaki urafikio, Wakufukuzao wewe, fahamu mimi mwenzao.

Uvivu ninayonena, tia katika sikio, Mimi nafasi sina, kukupa wewe kituo, Kwa sababu. naona, maovu yako mazao, Huwaletea laana, watu wakupendao.

Uvivu sikutamani, naelewa hasarayo, Njaa na umaskini, ndiyo yako matokeo, Wala usitumaini, hapa kupata makao, Tena jitenge njiani, usipinge nitakayo. Uvivu nakufukuza, kama hukwenda mbio,

Fahamu nitaagiza, watoto katika vyuo,

Kuimba wanaoweza, huu uwe wimbo wao,

Nao watakufukuza, utoweke kati yao.

3

|

DUNIA usishike, DUNIA ina koto, wambiwalo namke, mwa a Usiwe kama mtoto, au kam mke, sita Kujibu uwe mzito, neno Ovu mjinga. Mteuzi akumbuke, msemaji si

|

hikike, Dunia ina matata, ambaa usis hoke, usic Na njia za kupita, kuteua toke, yaku i Ukichoka utajuta, machoz anga. mch a Dunia njia zake, sawa kam

Dunia ukiwa juu, kushuka Kila lenye nafuu, kutenda Kabisa usisahau, kuepuka Dunia njia zake, sumbufu

kukumbuke, usichoke, kwao zake, zinatinga.

USAHIBU vu, haoni ajabu, awashwapo na kiwa MTU u, mwiv Wala haoni aibu, kudhihakiwa na maumivu, Ajabu wako sahibu, kukupasha

Moyoni hutia kovu, jeraha la usahibu.

MTU 2

1

Leo mtu ala chema, Hana kichwa wala homa,

LEO mtu amevaa, Nguo za kuteua,

Kesho roho imekoma, Hawezi kuwa mzima.

Kesho yake atakuwa, Katika sanda katiwa.

4

|

3 Leo mtu anapuuza, Makombo yaliyosazwa, Kesho mwenyewe huoza, Ni chakula cha mafunza.

7 Leo ana watumishi, Pake mwangoni haweshi, Kesho wote wabishi, Hawataki utumishi.

4 Leo mtu duniani,

8 Leo mtu anukia, Manukato kama ua, Kesho uvundo atia,

Hutajwa kwa thamani, Kesho hata maskini, Hawezi kumthamini.

Katika kila pua.

5 Leo pake malazini, Ni kitanda cha thamani, Kesho hulala chini, Wala mkeka haoni.

6 Leo afanya mkogo, Nyumba aiona ndogo, Kesho hana hata togo, Ya nyumba hata kidogo.

9 Leo mtu

mtukufu,

Kamili na mkunjufu, Kesho huwa dhaifu, Ukija ubadilifu. 10 Maisha tuyaishiyo, Yamefanana na tao, Kama visemavyo vyuo,

Maisha yetu ni leo.

WIMBO WIMBO usioujua, sikioni unadhuru, Kama mfano wa hewa, mpya ina mkunguru, Kama hukuitambua, thawabu huwa kufuru, Maajabu ya dunia, yameenea vururu. Maajabu yatushinda, kwa kuenea vururu, Wasioweza kupanda, hewani kwenda kuzuru, Wenzao wanapokwenda, huona wanakufuru,

Kikubwa huitwa kitanda, hewani kinapoduru. 5

AAA A AA AAA WA

Wajibu kupambanua, karata pau na uru, Japo zina vimo sawa, itawalayo i huru, Kopa na shupaza pia, hazilingani kwa nuru, Wanyama huteuliwa, tembo haitwi kifaru.

VIBAMBANI

BAADHI ya Wavibamba, kabla kwenda ahera, Walikuwa wakiimba, wakatia wengi fora, Mauti yamevichimba, vibamba vyenye imara, Makaburi hufumba, watu wenye sifa bora. Hapa palikuwa kwao, watu wenye fikira, Hapana dalili zao, sasa zote zimegura, Wakati wa machweleo, jua hufujika sura, Makaburi hufumba, watu wenye sifa bora.

Yalikuwa Wakafika Wakajaa Makaburi

masikani, Vibambani ya sungura, wageni, kutoka pwani na bara, barazani, kuuliza ya busara, hufumba, watu wenye sifa bora.

Hata maradhi mwilini, yasifiwayo kukera, Yalitiwa ugangani, ikabakia kudura, Sifa yao ya zamani, imekuwa matambara, Makaburi hufumba, watu wenye sifa bora. Muumba na Muumbua, Mungu Mbadili sura,

Dua unayepokea, haja ukakidhi mara, Yape nguvu masalia, 'siache yakadorora,

Makaburi hufumba, watu wenye sifa bora.

Mungu zioteshe mbegu, ziwe katika nusura, Katikati ya magugu, uzikuze kwa imara, Watoto wao na ndugu, uwatenge na madhara, Makaburi hufumba, watu wenye sifa bora.

6

MOYO

UNAPOPENDA

KUTUNGA na kukusifu, ni alama ya kupenda, Wala usitie hofu, jambo hili nikitenda, Nalitenda kwa unyofu, wala usidhani inda, Na njia japo ndefu, mimi sitachoka kwenda.

Njia hiyo sitachoka, japo milima 'tapanda, Nitapanda nikishuka, nifike ninakokwenda, Hauchoshwi na mashaka, moyo unapopenda,

Nguvu mpya huzuka, ikahimiza kushinda.

MAITI

ANAYESEMA"

NAULIZA washairi, wasomao Mambo, Pamoja na mashuhuri, wajuao mafunuo, Nataka wanihubiri, moyo upate kituo, Watu watatu hodari, maiti wachukuaor.

Hao watu niwambie, husikii neno Maiti wendao naye, ndiye anenae Haya shime ajuaye, anambie kisa Majina apambanue, maiti na watu

lao, nao, chao, hao.

Labda bin Kibwana, safarini mwambao, Hukosi kuyaona, mambo mfano wa hayo, Nitajie kwa majina, nizibue masikio, Maiti anayenena, na wazishi wazikao. t#Kalamu.

1Vidole vitatu vishikavyo kalamu.

MTI

UNAOCHEZA"

KUULIZA ni thawabu, wanenaji wamenena, Jambo likikupa taabu, usilinyamaze sana, Uliza wenye vitabu, na wajuao maana, Nani aliyeona, mti kucheza tarabu? Mti uchezao ngoma, nimepata kuuona, Umefungwa mahazama, kama kwamba msichana, Achezaye lelemama, kasoro kichwa hapana, Ndivyo nilivyoona, nilipokwenda tazama.

Kazi ya mwanadamu, kujua vitu majina, Kuungama si haramu, maarifa hayo sina, Ndipo nilipoazimu, kuuliza hadhirina, Ili niambiwe jina, ambalo silifahamu. Mti unapewa maji, ingawa kinywa hauna, Tena ni mtafunaji, wa vitu vigumu sana, Nataka watambuaji, wanifunulie jina, Linanisumbua sana, kutafuta kila mji.

Moja hata tatu, pembe za kuviringana,7 Wanazitumia watu, kugonga kwa nguvu sana, Nazo hulia tu! tu! tu! pasipo kusikizana, Hulishwa na wasichana, vitu vigumu tu. Wala si mti mdogo, huo ninaounena, Una kivimbo cha gogo, wala haukuachana, Ukipewa ni mzigo, wa kutoa jasho sana, Utajeni waungwana, katika nchi ya Digo. Nilifika hata bara, ambako wapatikana, Watu wenye busara, ya miti kila namna, Nikatoa na ujira, ili niambiwe jina, Walakini sikuona, pato ila hasara.

8

Katika waelewao, na njia kila aina, a, Nina rafiki upeo, wa moyo kwa kupendan na, Kanambia utakayo, njia ya kupatika Leo, Ni kuuliza mabwana, wasomao Mambo Wakati ni dhahabu, tena mama wa hazina, Yasikawie majibu, nikasumbuka tena, Katika chako kitabu, Mtengenezaji Bwana, Wape shairi vijana, labda watanijibu. Vijana wa Kiswahili, weledi wa maana, , Wenye macho makali, na vichwa vinavyoona

Ninawapa swali hili, kusudi kuchekeshana, Wanaopenda kununa, hawana raha ya kweli. #Kinu.

#Michi.

IDI

LEO ni siku ya Idi, kwa wote Waislamu, Naomba kwa Wadudi, mema atukirimu, Kisha atupe sudi, tushinde mambo magumu, Tuweze kuyafaidi, maisha na afya tamu. Tena napaza sauti, kwa Muumba malaika, Atoaye kwa umati, tunzo isiyovunjika, Atushike madhubuti, tusipate kuanguka, Atusimamishe kati, zituzunguke baraka. KARIBISHO KARIBU kitako, tupate ongea, Unipe tamko, na kicheko pia, Sema furahiko, nakutaradhia, Mrembo sikia, umefika kwako.

9

Karibu useme, tusemezane tamko, Wima sisimame, pumzika pumziko, Kaa utume, ujifanye kama kwako, Mgeni limbuko, mgeni ni mfalme.

TIMOTHEO

KWA

I

EWE Bwana Timotheo, Katika watu wa leo,

Wewe nimekupa cheo, Kwa shairi la kutua. 2 Mawazo namkumbuka, Aliyefariki Kyaka, Kwale wawili tulifika, Tukakaa kwa murua. 3 Ninasikitika sana,

Kwa mauti ya kijana, Hata siwezi kunena, Kwa huzuni kunijaa. 4 Basi namwomba Mungu,

Mwenye kumilki mbingu, Amtiliye mvungu, Kaburini

KWA

mna

taa.

RAFIKI

YANGU

BARUA yako azizi, mikononi imefika, Nakushukuru mpenzi, kuwa umenikumbuka, Mungu akupe majazi, akuongeze baraka, Akulinde Mwenyezi, yasikufike mashaka.

10

Tena ninakupa pole, kwa kuwa uliteseka, Unusurike milele, kwa taabu kuziokoka,

Na maradhi au uwele, yashindwe yakifika, Kila baa liwe kule, lisiweze kukufika. Ningefurahi sana, tarehe ungeandika, Nikajua mbayana, lini huku utafika, Jambo hili lina maana, usiache kukumbuka, Kama likikosekana, nahofu utasumbuka.

MTI MTI ukiwa mkuu, na matawi kukingama, Usiopandika juu, ya kilele kutazama, Msifanyize pashau, maseremala kusema, Mwauweza mti huu, cheo chake kupima.

Msifanye makuu, kushughulika kupima, Siyo huu wala huu, miti iliyo mizima, Wala msidharau, neno moja la hekima, Mti haupimwi juu, shinani umesimama. Milima na vichuguu, kumea iliyokoma, Hupimika kwa juu, cheo kikawa chema,

Mafundi msisahau, miti huzidi daima, Basi msidharau, taabu katika kupima.

MSEMA

PEKE

HAKOSI

MALENGA wa Bagamoyo, mkashifu wanawake, Nami nakujibu leo, ya kuwa usighurike, Maneno niandikayo, dhibiti yadhibitike,

Hajui makosa yake, msema peke hakosi.

gi

Yadhibiti mapokeo, hakosi msema peke, Husema ayatakayo, kusafi upande wake, Sikuzote ana choyo, hampi haki mwenzake, Hajui makosa yake, msema peke hakosi. Hata wanawake nao, wangesema tuandike, Maovu watendewayo, vitabuni yasomeke, Wangekuwa bora wao, jambo hili likumbuke, Hajui makosa yake, msema peke hakosi.

Ubaya ulaumuo, upofu usikushike, Si wa wake peke yao, shika usighafilike, Kila siku watetao, ni mume na mwanamke, Hajui makosa yake, msema peke hakosi. Hatia uisemayo, ni kichekesho tucheke, Uovu hauna kwao, hausemwi hapa pake, Hata wafalme nao, huwaudhi wao wake, Hajui makosa yake, msema peke hakosi. Ushahidi utakao, wa wema wa mwanamke,

Khadija ni madondoo, Muhammad mume wake, Zamani za ndoa yao, hatujui ovu lake,

Hajui makosa yake, msema peke hakosi.

Zamani za majilio, Islamu nuru yake, Masahaba ujuao, Khadija ni mwanamke, Kwanza katika hao, kuzishika nguzo zake, Hajui makosa yake, msema peke hakosi. Na wengine kama huyo, wema wasio makeke, Wachungao vyeo vyao, aibu isiwafike, Wameenea mwambao, peleleza usichoke,

Hajui makosa yake, msema peke hakosi. 12

Ajua Muumba wao, faida ya wanawake, Kama si wema hao, waume wasizuzuke, Watajivunjia vyeo, aibu iwazunguke, Hajui makosa yake, msema peke hakosi.

Siku tuzaliwayo, wana taabu wanawake, Tufikiri dhiki yao, fedheha tusiwapake, Fadhili kama hiyo, haina malipo yake, Hajui makosa yake, msema peke hakosi. Shairi ni kama nguo, ukivaa isiruke, Wala isizidi cheo, chini isiburuzike, Niliyofunua leo, huu ndiyo mwisho wake,

Hajui makosa yake, msema peke hakosi.

KIPENDEZACHO AIBU

HAKITILIKI

NILENGAPO ninafuma, hufuma bila udhia, Shabaha nikipima, macho yangu nafunua, Hufumbua kutazama, shabaha nikichagua, Na leo 'tawatetea, ningojeni kina mama. Ningojeni kina mama, mimi nitawatetea, "Tawatetea lawama, la ovyo lisilo njia, Litaondoka lazima, kwa upesi kukimbia, Mwisho mtajaliwa, nanyi mpewe heshima. Mkono wenye mwiko, umejitenga na moto, Mshikaji wa kishiko, aepa anguko zito, Na mimi madhali niko, msijitie fukuto, Sasa zamu ya mtoto, kuyajibu maandiko.

Ni zamu yangu mtoto, ya kulipa ueleko, Ueleko wa uzito, na chozi na hangaiko,

Sasa mtalipwa pato, ili mpate kicheko, Kicheko na furahiko, yawaepuke majuto.

13

Ninaomba heshima, neno moja kutendewa,

Wakati mkitazama, kazi yangu nawambia, Nitakieni salama, nisishindwe kutetea, Dua mkiniombea,

salama mbele na nyuma.

o, Wanawake wakihama, fahamu Juma Mrish

Itatokea zahama, mashaka na fadhaisho, , Utawaandama nyuma, mbio ukitoka jasho

Tambo lisilo mwisho, waliumbuaje Juma? Mwanamke ukiweka, chelea mapambanisho, Usianze kutoroka, kufanya mabadilisho, Na kama umepotoka, haraka jitie josho, Maisha yataka hasho, upesi tia kiraka. Nakuapia kiapo, muhimu chenye heshima, Elewa hapo ulipo, kina mama wangehama, Wanaume wote hapo, lazima wangelalama, Huzuni pevu lazima, fahamu ingekuwapo. Wanawake nasadiki, wangehama ni uwele, Wanaume mahuluki, wangekuwa ni wawele, Kicheko hakidiriki, labda toba na ole!

Yakumbukiye milele, ninayosema rafiki. Mrisho nastaajabu, hasa hujui umbile, Umbile lenye nasibu, na furaha ya milele, Halitiliki aibu, kusemwa hivi na vile,

Utajiuma vidole, kwa fedheha kukusibu. Kipendezacho viumbe, kina baraka yake, Juma usiyumbeyumbe, kudharau mwanamke, Fahamu yeye kiumbe, haliyo ndiyo yake, Kaletwa tufurahike, ulimwengu aupambe. Leo nalitua tanga, Bagamoyo bandarini, Kisha natia nanga, nangoja watamaduni, Watu unaosimanga, wajipakie chomboni, Utazame masikani, ya peke yako malenga!

14

SI

KITU

SI kitu kuwa tajiri, wala mtukufu sana, Watu wengi fikiri, wametukuka majina, Si kitu kuwa mzuri, kwa umbo kuonekana,

Mambo mengine ya heri, watendaji ni wabaya.

KARATASI, KARATASI

yangu nzuri, kadi ya kuandikia,

Naandika mistari, michache iwe barua, Twe katika safari, hima bila kuchelewa, Kuchelewa ni hatari, ukiwa katika njia.

Kaseme subalheri, wendako ukipokewa, Ukiulizwa habari, sema njema siyo mbaya, Lapendeza neno zuri, baya huzuni hutia, Usijibu kwa kiburi, majibu yako chagua.

Marafiki na wapenzi, wendako nisalimia,

Natamani matembezi, kwenda kuwaangalia, Lakini kwa siku hizi, nafasi imepungua, Wasifanyize chukizi, mfundo kuniwekea,

Mfundo wasiweke, radhi yao niombea, Wala wasikasirike, tuhuma kunifanyia, Nitakuja tucheke, Mungu akinijalia, Nataka ukatamke, yote niliyokwambia.

KWA

PEMBE

MHUNZI

WARAKA wako Mhunzi, mikononi umefika, Nakushukuru mpenzi, kuweza kunikumbuka, Mungu akupe pumzi, akujalie baraka, Umefanya jambo bora, kuniletea waraka. 15

Najilaumu lawama, huzuni ilipofika, Sikufanyiza heshima, kukuletea waraka, Akili ilinihama, sikuweza kuandika, Umefanya jambo bora, kuniletea waraka. Msamaha ninaomba, kuwa nilighafilika, Yakimtoka magamba, samaki huharibika, Wa porini ndiye simba, akishikwa ni mateka, Umefanya jambo bora, kuniletea waraka.

Ahsante nyingi sana, mwisho wa kuandika, Nisalimie mabwana, Forodhani watajika, Nakumbuka waungwana, kwa heshima sijachoka, Umefanya jambo bora, kuniletea waraka,

UOVU MOYO usifanye pupa, kuiga uovu wao, Uovu kama kukopa, iambae deni hiyo, Malipo ya kulipa, mtu mwovu hanayo, Nimezaliwa nao, sina njia ya kuepa.

Inafaa kuwa nao, kuwatupa sihimili, Kuwaacha peke yao, naona ni muhali, Na muhali kama huo, mimi sistahili, Kuonekana awali, nafuata njia hiyo. Uovu una makali, huwakata watendao, Waufanyao amali, usiwafanyie choyo, Moyo usikubali, kuigiza mwendo wao, Uovu si tegemeo, wala hauna kivuli. Uovu kitu dhaifu, moyo sighilibike, Neno linalokashifu, heri ulitanuke, Uandame uokofu, njia njema usitoke, Moyo usihadaike, uovu jambo dhaifu.

16

Uovu una dhima, huwadhuru wafanyao, Sana utawauma, watu siku wapimwayo, Washindwe kusema, mambo waulizwayo, Wateuliwapo wema, waovu watalalama. Atendaye humdhuru, akalalamika sana, Mara moja huduru, ukarudi kukubana, Uovu kama muru, kinywani ukitafuna, Hata ukiutabana, lazima utakudhuru.

Usiwalilie ngoa, waovu hawana shuo, Hao hawakuchagua, mmea wenye mazao, Bure wajizuzua, kuvunja kadiri zao, Hawapati watakayo, labda kulaumiwa.

Uovu Wala Kisha Uovu

njia ya miba, humkita apitaye, hauna shiba, hutapisha aulaye, una misiba, humsibu atendaye, wache pekee, usiufanye sahiba.

Mwovu Huacha Mwovu Mwovu

katika tope, ndimo anamopita, njia nyeupe, akateua matata, hana lepe, usiku yeye hujuta, akikuvuta, dhamiriye akutupe.

Mwovu haoni wavu, njiani akitegewa, Tena hulia wivu, siku akigunduliwa, Usifanye ushupavu, mshupavu huumia, Sikia nakuusia, jihadhari na maovu.

NAMNA

KUMI

ZA

UMASKINI

UKOSEFU wa milki, watu wengine hudhani, Peke yake ndiyo dhiki, hapa ulimwenguni, Wala hawasikitiki, mtu kukosa imani, Ukosefu wa imani, pia ni umaskini.

17

Kama mtu hana haki, chama chake maskini, Japo kuwa hana dhiki, lakini hana thamani, Laana za halaiki, zitamtoa maanani,

Ukosefu wa haki, pia ni umaskini. Asiyejua adabu, hana hadhi duniani, Watu hawamhesabu, zaidi ya mtu duni, Jambo hili la aibu, humweka mtu chini, Ukosefu wa adabu, pia ni umaskini.

Mwingine mwenye sehemu, katika umaskini, Mtu aliyehitimu, mjinga wa vitabuni, Vile vile hakutimu, anaitwa hayawani, Ukosefu wa elimu, pia ni umaskini. Mtu asiye heshima, anayevunja kanuni, Zilizowekwa kwa wema, kuwa mwanga duniani, Kadhalika hana kima, anachukiza moyoni, Ukosefu wa heshima, pia ni umaskini.

Mlipaji wa uovu, kwa deni la hisani, Ajifanyaye mwerevu, mfadhili kumbhini, Hata akiwa mnguvu, jina lake maskini, Ukosefu wa hisani, pia ni umaskini.

Mwengine mwenye makamo, katika daraja duni, Mtu asiye kipimo, na hadhari ulimini, Ulimi mdogo kimo, bali wataka mizani, Ukosefu wa kipimo, pia ni umaskini. Kwa kwao ya mguuni, huna manza hadharani, Manza ya hadharani, ni kwao ya ulimini, Hiyo ina mtihani, ndiyo sumu ya amani, Ukosefu wa amani, pia ni umaskini.

Mkosefu wa akili, naye yumo shirikani, Japo akiwa jamali, kwa sura hana kifani, Naye hana afadhali, ila duni ya thamani, Ukosefu wa akili, pia ni umaskini.

18

Tena izukapo baa, nchi ikiwa vitani, Adui mwenye kichaa, arandapo uwanjani, Ukikosa ushujaa, wa kutetea amani, Ukosefu wa shujaa, pia ni umaskini. Namna za maskini, nyingi mno duniani, Hizi kumi za mwanzoni, wala sizo za mwishoni, Mungu tujaze uoni, tuokoke maskini, Zipunguze hesabuni, aina za maskini.

TAMAA TAMAA za wanadamu, mpaka wake sioni, Wote hutaka kutimu, hawataki kuwa duni, Haba wasioazimu, mambo bora kutamani, Tamaa jambo muhimu, kuwa nalo duniani. Wanaoita haramu, tamaa siwaamini, Watu wote wana hamu, tajiri na maskini, Asiyetaka matamu, natafuta simwoni, Tamaa jambo muhimu, kuwa nalo duniani.

Pangekuwa na mpaka, mwisho wa kutamani, Watu wasingetaka, kukimbia ushenzini, Naona kama baraka, tamaa kuwa moyoni,

Tamaa jambo muhimu, kuwa nalo duniani. Ninasikia kelele, watu wengine hubuni, Kuwa tamaa mbele, mauti huja mwishoni, Wagombana na umbile, watu hawa ninadhani, Tamaa jambo muhimu, kuwa nalo duniani. Kugombana na umbile, sawa na kujihini, Tamaa ina milele, haitoki duniani, Wanaopiga kelele, wafanye kama watani, Tamaa jambo muhimu, kuwa nalo duniani.

19

Tamaa ni gurudumu, zingatia akilini, La gari la binadamu, aishiye duniani, Msikose kufahamu, kuwa tumo safarini, Tamaa jambo muhimu, kuwa nalo duniani. Hakika ziko tamaa, zivutiazo motoni, Na ziko zinazofaa, zipelekazo peponi, Za kwanza ukiambaa, nyingine tia moyoni, Tamaa jambo muhimu, kuwa nalo duniani.

SARAFU

SARAFU tutumiazo, zimeumbwa kwa duara, Hilo huwapa mawazo, watu wenye fikira, Kuwa zatia mzozo, kushikika kwa imara, Bora ni kuwa nazo, bali zataka busara.

Mali ina matatizo, hutatiza kila mara, Tajiri aliye nazo, hutafuta za fukara,

Fedha ina mshangazo, ufanyizao ishara, Hashibi aliye nazo, pesa yenda mduara.

Fedha zina matukuzo, uzipatapo hufura, Ukapata na uwezo, kutimiza jambo mara, Kucheka wasio nazo, kama walio majura, Yakumbuke mageuzo, tajiri kuwa fukara. Inakwenda mfulizo, sarafu kama majira, Wengi walikuwa nazo, zikawapamba sura, Na sasa hawanazo, zimekwisha kuwagura, Mali ina mageuzo, ya tijara na hasara.

Wakati wa kuwa nazo, hudhani zitagura, Ghafla mtu hanazo, zimeduru kama dira,

Haziachi mburuzo, nyayoze wala ishara, Ajabu ni kuwa nazo, kuponyoka si ibra,

20

SAMBI

NAO

WAMBA yao, mimi sambi, Sambi nao, si walumbi, Walumbao, hawajigambi, Hawajigambi, wema wao.

KIBURI KATIKA mapambo ghali, mojawapo ni kiburi, Lina bei pambo hili, kubwa haina kadiri, Kiburi kina ajali, ikiwa huna nadhari, Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania. Hakifiki bandarini, chombo cha mwenye kiburi, Kitazama baharini, japo upepo shwari, Kinaondoa enzini, watu wengi mashuhuri, Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania. Kitoe katika kichwa, kiburi kina hatari, Ulimwengu una mchwa, wepesi wa kuhasiri, Kiburi chataka fichwa, ndipo kiwapo kizuri, Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania.

Kiburi kina hasara, kinapunguza umri, Pambo hili lina dhara, awali hata aheri, Kiburi mara hukera, watu wanaokukiri, Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania.

Malazi yetu hatima, upana wake shubiri,” Urefu wake ni pima, hauzidi hata wari, Wazeni na kutazama, kama chafaa kiburi,

Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania. 21

Kiburi hakitukuzi, wala hakileti heri, Ni pambo la upuuzi, vazi lisilosetiri, Linaloleta chukizi, na majeraha ya siri, Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania.

Sasa namwomba Mungu, neno langu la kwa heri, Tuokoe Bwana wangu, tuepushe na ghururi, Tupunguzie mchungu, na kitisho cha kaburi, Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania.

Shairi lilipofika, kukoma ndiyo vizuri,

Mengine nitaandika, msichoke kusaburi, Saburi ina baraka, haraka huleta shari, Vibaya kwa binadamu, kiburi kukiwania. “Upana wa mwanandani

katika kaburi ni shubiri moja.

MAISHA MAISHA

jambo la heri, uyapatapo kamili,

Isipungue kadiri, afya katika mwili,

Kisha upate urari, wa hekima kila hali, Maisha ni jambo bora, uyapatapo kamili.

Jambo la kwanza maisha, uhai katika mwili, Lakini hayatatosha, afya ikiwa mbali, Afya inaunganisha, roho na kiwiliwili, Maisha ni jambo bora, uyapatapo kamili. Tena twataka hekima, ili itawale mwili, Tuchague mambo mema, maovu tuweke mbali, Tungalikuwa wanyama, kasoro umbo la mwili, Maisha ni jambo bora, uyapatapo kamili.

22

Binadamu na mnyama, tofauti ya awali, Kila anayesema, kuwa miguu miwili, Shabaha hajaifuma, hajakaribia kweli, Maisha ni jambo bora, uyapatapo kamili.

Tofauti Kipawa Na mtu Maisha

ni hekima, ndiyo inayobadili, hiki mnyama, shida hakitawali, huwa mnyama, akosapo jambo hili, ni jambo bora, uyapatapo kamili.

Mambo niliyotaja, katika beti awali, Yameandamwa na haja, mtu hutaka mali, Ili apate faraja, na kutengeneza hali, Maisha ni jambo bora, uyapatapo kamili.

NIKILALA MUUMBA wangu, bora wa rehema, Malazini pangu, nitunze vema, Unipe langu, fungu la salama, Ondoa uchungu, niyaonje mema. Nikidhie Mola, wema malaika, Saa nikilala, zamu wakishika, Niepushe hila, ngumu kuoneka, Nijalie Mola, asubuhi kuamka.

UA NATAMANI kutamka, Mungu unipe karama, Nipe karama Rabuka, nilisifu ua jema, Lifaalo kusifika, kulisifu huwa vema, Mungu nipe baraka, nijalie kulichuma.

23

Nataka nilichume, liwe langu ua jema, Nilitunze nitazame, nifurahike daima, Liwe ngao niegeme, linifanyie huruma, Wenye wivu wasiseme, baraka imenihama.

Sauti yangu ifike, kwa Mgawaji ncema, Wanipendao wacheke, wafurahike rehema, Nakuomba nishike, mkono usende nyuma, Ua lisiniponyoke, nilishikapo 'tahema. Lina urembo wa nuru, ua ninalolisema, Machoni halidhuru, linavuta kutazama, Sana ningeshukuru, kupata ua la kima,

Kitu kisichodhuru, kukipata ni heshima. Mwenyezi niamru, niombalo liwe tama, Ua liwe na uhuru, liishi maisha mema, Kisha ulinusuru, mwivi asije lichuma, Upendacho si kufuru, kukiombea neema. Hakufuru mwombaji, ambapo neno jema, Muumba ndiwe Mpaji, uliyetupa kalima, Makusudi mahitaji, tuyaweze kuyasema, Nataka unifariji, wala pasiwe lawama.

PEPO HAPANA

mwenye

kuona, Pepo akaikataa,

Kuwa idhini hapana, nimekwisha kusikia, Bali napenda kunena, Mungu atanijalia, Pepo niliyoona, niweze kuiingia. Ingawa haraka sina, wajibu kukwambia, Moyo wangu wasonona, kama ulioumia, Wala siwezi kukana, kweli kukuhadithia, Sivumilii kuona, pepo nisiyoingia.

24

KAZI KAZI ni yenye ijara, kwa watu waitendao, Ama mishahara bora, kufidia jasho lao, Sasa watuma fikira, watumao wana choyo, Tutatenda ndiyo siyo, tuondoane njiani.

Kuondoana njiani, sasa ndivyo ipasavyo, Mtu hana tumaini, bali mashaka ya moyo, Mchana kutwa kazini, hatimizi atakayo, Kazi kwa waitendao, mtendewa hathamini.

Huyabuni matatizo, mengi ya kukutahini, Wapate fanya mzozo, wakiona kosa ndani, Zitanguke bidiizo, na kufukuzwa kazini, Labda hapo mwanzo, sasa kuna kazi gani? Matajiri wana sera, huhesabu wala nini, Kwao neno la hasara, halitoki vinywani, Wajapo pata tijara, neno hili hawaneni, Ila huzidi kukera, bure watu wa kazini.

Hafanyiwi kadiri, mtu hutoshwa na nini, Atengane na usiri, wa kuchelewa kazini, Na kuepuka hatari, ya kuwa katika deni, Kwa hakika ufakiri, jambo duni duniani.

Tajiri hana muhali, kukutosa fedhehani, Tena ukiumwa mwili, na kufariki kazini, Kumbuka hatakujali, wala hatiwi poshoni, Katika zote amali, utumishi jambo duni. Matajiri hawawazi, kama kwamba hawaoni, Hudhani mtu wa kazi, hatunuki hatamani, Nguo njema hawezi, kuvaa mwake mwilini, Riziki yake mizizi, nafaka siyo kifani.

ZI

YA

Chema hakioni tamu, mtumishi wanadhani, Akila kitu kitamu, huwa kiovu kinywani, Shibe yake haitimu, ila kula kitu duni, Tazama dhihaka ngumu, wapewayo maskini.

MOYO

WANAMBIA

MOYO wanambia penda, mtu mjinga sipende, Mjinga ukimpenda, hajui nini atende, Moyo wanambia tenda, lisilotendwa sitende, Fanya wanavyotenda, wenzio wasikushinde.

Moyo Imba Moyo Omba

wanambia imba, wimbo mbaya siimbe, wimbo wa kupamba, uwapumbaze wakembe, wanambia omba, ombi ovu usiombe, Mungu Muumba, dhiki azifanye chembe.

Moyo wanambia tunga, lisilokuwa situnge, Lisilofaa kutunga, karibu yake jitenge, Moyo wanambia jenga, kwa karata usijenge, Jenga jengo la mchanga, kwa mawe kuta ufunge. Moyo wanambia meza, kinachokwama simeze,

Kinachokwama kumeza, kinywani sielekeze, Moyo wanambia uza, roho yako usiuze, Fanya unavyoweza, neno hili jikataze. Moyo wanambia cheza, mchezo mbi sicheze, Cheza wakupendeza, wenzio wakuigize, Moyo wanambia kaza, bidii usipunguze, Usipunguze kuwaza, mawazoni jiingize. Moyo wanambia kopa, deni kubwa usikope, Usiloweza kulipa, siku zote uliepe, Moyo wanambia apa, kwa batili usiape, Wala usifanye pupa, kiapo ukiogope.

26

Moyo wanambia hama, mahali pema sihame, Sihame unapotuma, ili wende ukatumwe, Moyo wanambia koma, kujaribu usikome, Kujaribu ni heshima, watu wote watazame. Moyo wanambia kana, neno la kweli sikane, Kweli unapoiona, fanya bidii unene, Moyo wanambia chuna, ngozi yako usichune, Japo nyeusi sana, bora kuliko nyingine.

IMANI MUNGU wape majazi, wenye kulea vijana, Hao ndio waongozi, wa kuwatenga na laana, Ibariki yao kazi, yakue yao majina, Wafundisheni imani, watoto mkiwalea.

Kuwafundisha imani, ndilo jambo la maana, Na mambo yenye kanuni, viumbe kutendeana,

Watengane na uhuni, wafaulu na kufana, Wafundisheni imani, watoto mkiwalea. Hayahusu peke yao, mambo hayo wavulana, Hata wale wenzao, ambao ni wasichana, Katika maendeleo, wajibu kufuatana, Wafundisheni imani, watoto mkiwalea. Uharibifu wa Ndiyo wakati Sharti walezi Wafundisheni

mtu, huanza tangu ujana, wa kutu, kuota juu ya jina, wetu, waondoe hili shina, imani, watoto mkiwalea.

Watoto ni waigaji, mfano wao hapana, Umbo unalohitaji, wanaweza kufanana,

Udongo ulio maji, ndiyo unaoshikana, Wafundisheni imani, watoto mkiwalea.

27

Wana udhia watoto, maswali hupenda sana, Si akili kuwa nzito, jambo hili mkiona, Ndiyo mwanzo wa uwoto, wa ujuzi na dhana, Wafundisheni imani, watoto mkiwalea. Watoto ni kama tunza, wamekuja ni amana, Mambo mema kuwafunza, ndiyo kushika dhamana, Kuwaharibu ni manza, humchukiza Rabana, Wafundisheni imani, watoto mkiwalea.

Ingawa hapa nakoma, maneno ninayonena, Koleo sijaizima, mengine ninayasana, Kikipata moto chuma, uhunzi mtauona, Wafundisheni imani, watoto mkiwalea.

ANASA ANASA hufukarisha, humeza wingi wa mali,

Inafaa kulipisha, jambo hili kila hali, Mambo ya kufilisisha, kwetu hayastahili, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia. Matumizi ya harija, ni haramu si halali, Kabla ya mali kuja, halifai jambo hili, Anasa zinawafuja, maskini wa akili, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia. Jambo hili ni mkogo, kulikosa si muhali, Akiba japo kidogo, hutengeneza kivuli, Siku ya mvurugo, itakusetiri hali, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia. Afuataye anasa, huchumbia udhalili, Ulimwengu una visa, daima una ajali, Matumizi ya siasa, ni tegemeo kamili, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia,

28

Upatacho kwa jasho, kukifuja si halali, Anasa huvunwa mwisho, si mavuno ya awali,

Dunia ina kitisho, kifaacho si cha mbali, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia. Matumizi ya kiasi, hayaitwi ubahili, Akanushaye huasi, watu hawamkubali, Anasa zinafilisi, zinaleta uthakili, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia. Usiharibu mapato, upatayo kwa amali, Anasa zina majuto, siku ya dhiki kali, Zinatia moyo joto, kama kitu hutawali, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia.

Hapa nilipofika, sihitaji kwenda mbali, Msidhani natoroka, sithubutu jambo hili, Mungu akiniweka, mtasikia kauli, Anasa kwa maskini, vibaya kutangulia.

MLIMWENGU MAMBO ya mlimwengu, magumu kuelezeka, Ujapo panga mafungu, tayari kuyatamka, Huja kizunguzungu, mambo yakatawanyika,

Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka. Furaha ya mlimwengu, daima inakatika, Anakumbuka uchungu, moyoni na kuuweka, Furaha haina fungu, moyoni mwake hutoka,

Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka. Huzuni ina heshima, hutajwa kwa kutukuka, Furaha haina kima, sifa yake hufujika, Tunaacha jambo zima, upungufu tukashika,

Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka.

29

AU



.

ua a

Euraha mara huhama, nyepesi kwa kuyeyuka, Tukakumbukia homa, ya muda kama dakika, Na kusahau uzima, wa miezi na miaka,

Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka.

Tunatukuza machozi, yawezayo kufutika, Na kudharau mapenzi, jambo lisiloondoka, Taabu haina mizizi, na ikiwapo hung'oka,

Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka. Furaha Jambo Lakini Ajabu

ina msinji, mgumu kwa kuvunjika, hili hufariji, tumepewa ni baraka, hatulitaji, sifa yake twafunika, ya mlimwengu, mambo anayokumbuka.

Furaha maji ya mto, vizuri hutiririka, Moyoni huzima joto, na kuondoa mashaka, Lakini haina pato, kwa sifa imepunguka, Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka.

Ajapo pewa milki, ya dunia akashika, Atadhani iko baki, kwake haikufika, Binadamu haridhiki, haachi kusikitika, Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka. Ikiwa hii ni njia, ya kutafuta hakika, Watu watajaliwa, waone wanayotaka, Na mimi nawaombea, wasipatwe na kuchoka, Ajabu ya mlimwengu, mambo anayokumbuka.

MAREHEMU

KAIMA LIWALI WA PANGANI

PEPO wa maombolezi, nakuomba niauni, Niongoze waziwazi, ufasaha sinihini, Moyoni nina majonzi, kutangaza natamani, Tumefiwa na mpenzi, Liwali mwema Pangani.

30

Amekufa ana kazi, miaka sita na arobaini, Ila ndogo kama uzi, hakuacha duniani, Yamiminika machozi, tukikumbuka hisani, Tumefiwa na mpenzi, Liwali mwema Pangani. Wakati wake wa kazi, haufutiki moyoni, Kwa mengi msaidizi, kwa wenyeji na wageni, Alikuwa ni azizi, kwa watu wote mjini, Tumefiwa na mpenzi, Liwali mwema

Pangani.

Alipenda simulizi, na dhihaka barazani, Japo alipanda ngazi, hakudharau wa chini, Hakufanya uchaguzi, kila mtu ni mwandani, Tumefiwa na mpenzi, Liwali mwema Pangani.

Mazishi aliyaenzi, Bazter wa Bomani, Alikuja kubarizi, kumuaga kaburini, Na watu wengi vikozi, walifika mazikoni, Tumefiwa na mpenzi, Liwali mwema Pangani.

Poleni ndugu wazazi, na walizi matangani, Na H. H. Azizi, rafiki yake zamani, Futeni yenu machozi, mshukuru Rahmani, Tumefiwa na mpenzi, Liwali mwema

Pangani.

Mwisho wa maombolezi, kalamu naweka chini, Nakuomba Mwenyezi, kabuli iwe makini, Umbariki majazi, marehemu, ya Peponi, Tumefiwa na mpenzi, Liwali mwema Pangani.

USINGIZI USINGIZI nipakate, nataka kupumzika, Yasinipalie mate, nilale na kuamka, Maburudiko nipate, na kuamka nataka, Usingizi uwe pete, valika na kuvuka.

31

KWELI SALAMU

IKITOKEA

zako Mzee, zimewasili Pangani,

Vijana hata wazee, wameniomba mjini,

Ili nikuelezee, swali lako gazetini, Kwayo nimetamani, kuyajibu matafiti. Nataka nijaribu, kukueleza mwandani, Ikuepuke muhibu, dhiki iliyo moyoni, Kushindwa si aibu, asiyekosa Manani, Asiyekosa Manani, neno hili thabiti. Leo nafuasa hamu, nijaribu gazetini, Samahani walimu, nikitia kosa ndani, Hapana aliyetimu, viumbe wa duniani, Yote ajua Manani, yote bila tofauti. Mzee na mauti, na huyo mchanja kuni, Wote kwa thabiti, wamefanana yakini, Ukiona tofauti, ni lafidhi manenoni, Sahihi mtema kuni, ni mzee na mauti.

Nasikia hapo kale, huyo mtu wa kuni, Alizifunga tele, kuni nzito mzigoni, Akapiga makelele, alipokuwa taabani, Nimechoka duniani, njoo upesi mauti.

Mauti yalitokea, pale pa mtema kuni, Yakawa kumwambia, nimekuja watakani? Utakalo litakuwa, unasema neno gani? Ni cha mtema kuni, kweli ikithibiti! Dhihaka ya kufariki, ilitoka moyoni, Akasema kirafiki, nitwike hizi kuni, Basi katika dhiki, binadamu atamani, Mauti yawe auni, kumbe hanayo dhati.

32

Kweli ikitokeza, huwa ya mtema kuni, Mfano Waingereza, wakipiga Wajermani, Maadui watawaza, tuliponzwa na nini? Ni cha mtema kuni, uongo ukifeleti!

Mambo unayoyaona, yote hapa duniani, Karibu yamefanana, bara na baharini, Lafidhi za kunena, hufanana maanani, Tafsiri naidhani, itakuwa madhubuti.

Ninakuaga sahiba, kuwa hapa kituoni, Hizi ni beti haba, ziliopo mwandani, Shairi la miraba, halizidi kipimoni, Toka juu hata chini, haifai tofauti.

UJANA UJANA

na nguvu, mwilini ukigawiwa,

Tumia kwa welekevu, ukiteua murua,

Jihadharishe uvivu, kila ukikujia, Ujana wa ulegevu, uzeeni husumbua. Ujana kitu muhimu, vema ukitumiwa, Wakati huo magumu, yafaa kujaribiwa, Ujana una zamu, mara moja hutujia, Kabla kwisha hamu, huwa umekimbia.

Ujana ni wakati, wa akiba kuandaa, Uzeeni hupati, nguvu ila kupungua, Nguvu yako haisiti, uzee ukiingia, Haya ni madhubuti, tena yamekubaliwa.

33

PANGANI PANGANI Kuondolewa

tangu zamani, mji wa uliwali, mjini, jambo hili idhilali,

Hamkutani kwani, watu wenye akili? Mkaomba kwa Jalali, Mpaji wa maskini,

Kuomba ndivyo ilivyo, wanadamu duniani, Mambo yakiwa ovyo, tegemeo ni Manani, Ombeni iwapasavyo, na mikono inueni, Msidhani hawaoni, Bwana Mungu mtakavyo.

Kuomba si udhaifu, mwenye kuomba hupewa, Hupewa mambo nadhifu, mabaya humwondokea, Akashukuru halafu, kwa kupokelewa dua, Mungu apendalo kuwa, halitiwi hitilafu.

UKULIMA KAZI bora Afrika, yenye cheo na heshima, Inayoleta baraka, bara hii na neema, Yapasa kukumbuka, kuwa ni ukulima, Vibaya kuzohalika, kushika jembe kulima. Japo tunayo mifugo, kila aina wanyama,

Japo tunayo magogo, na misumeno ya chuma, Sharti tulime mihogo, njaa isije tuuma, Tukiupa kichogo, ukulima tutazama.

Wachimbaji wa dhahabu, pia njaa huwauma, Waandishi wana taabu, wakikosa kula sima, Kilimo kina thawabu, tena kazi ya rehema, Kuutupa ni aibu, Afrika ukulima.

34

Wavuvi wa samaki, wakirudi hulalama, Samaki hawaliki, bila wishwa wa mtama, Haifai kudhihaki, kudharau ukulima, Mkulima ni rafiki, wa watu dunia nzima.

Mtu hawezi kulipa, fadhili ya mkulima, Japo fedha ukimpa, ni sarafu siyo kima, Fedha imepigwa chapa, kurahisisha huduma, Kubadili na kulipa, bali si chakula chema. Hapana mtu kabidhi, mbele ya mkulima, Watu wote huwa radhi, fedha yao kuituma, Ili wapate faradhi, chakula cha daima, Ukulima huhifadhi, maisha dunia nzima. Mtu akilima shamba, mimea ikisimama, Husaidia Muumba, vitu kuvipa uzima, Ana haki kujigamba, kuwa ni mtu mwema, Aipaye kila nyumba, furaha ya daima.

Hagawiwi na mtu, fungu la mkulima, Huvuna katika mwitu, ambao aliulima, Njia hii kwa watu, ni moja yenye heshima, Kupata riziki zetu, kutoka kwa Mungu mwema.

Watu wengi wa asili, walikuwa wakulima,

Ubora wa jambo hili, yapasa kuutazama, Isipotee asili, makabila yakazama, Ukulima ni halali, siyo kazi ya lawama.

Shairi likenda mno, machozi yananichoma, Nchi ya kumea ngano, kila mimea athama,

Ipayo watu unono, wakaweza cheza ngoma Imeenea miguno, njaa watu yawauma,

39

ri

WASIA

AWA

AAA

MA

UVIVU

HAUNA

SUDI

BWANA MUNGU nahitaji, maarifa ya kalamu, Nina hoja na wenyeji, nawataka wafahamu, Walio katika miji, na vitongoji vya humu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika? Wenyeji una heshima, katika mastakimu, Bali sisi tuko nyuma, kwa kukosa darahimu, Tujitahidi kuchuma, umaskini ni SUMU, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika?

Sifanyizi itikadi, ila nataka wahimu, Tuweze kulipa kodi, mwaka ukisha timu, Uvivu hauna sudi, jaza yake ni hukumu, ka? Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushi Ninasikitika sana, kwa kuwaona kaumu, Ambao tumeungana, kwa uzazi hata damu, Wengi kitu hawana, ila shida ngumungumu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika? , Katika nchi za pwani, ambazo nazifahamu u, mdim iliki hawam ni, maski Watu wengi

Umwendeaye taabani, mfuko wake mgumu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika?

Jambo hili halibidi, ni hasara likidumu, Shime tufanye juhudi, moyoni tutie hamu, Najua hapana budi, Mungu atatukirimu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika?

Tujitahidi kwa kazi, na ukabidhi adhimu, Tuache upuuzi, na anasa za wazimu, Bwana Mungu ni mjuzi, hatutakosa sehemu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika?

36

Nikikaa nasaili, sisi lini tutatimu? Kila tulacho kikali, lini tutaonja tamu? Fikira ya udhalili, inanikausha damu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika?

Dhiki zimetuzunguka, nafasi kwetu adimu, Kila tunachokishika, kwetu sisi hakidumu, Mara moja kitaruka, kwa uchache wa fahamu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika? Nilipofika kiasi, imebaki kuhitimu, Haifai kwenda kasi, shairi hili la mimu,

Maneno mengi najisi, au huitwa haramu, Huwaje mtu mwenyeji, akakosa cha kushika?

SALAMU SALAMU haishi hamu, wasemaji wamenena, Laiti ningehitimu, ningetanabahi sana, Ya kuwa uliazimu, kwenda bila kuonana,

Ningejitahidi sana, haja yako isitimu. Nilidhani nitaweza, mimi nawe kuonana, Kila njia hafanyiza, hakusudia kunena, Mbele yako kueleza, wakati wa kuagana, Jambo muhimu sana, jema la kusikiliza. Umenihini nafasi, ndogo ya kunenezana, Sitakulipa kisasi, kisasi siyo uungwana, Ni sheria halisi, ya kuzidi kutengana,

Nikiwaza ninaona, jambo hili halipasi. Kwa kuwa ninapenda, kuwaza tutakutana, Wajibu kujilinda, nisiseme mengi sana, Japo kuwa umetenda, neno lisilofanana, Nakuombea mwanana, safari uliyokwenda. 37

ZAWADI jina langu, ZAWADI imewasili, ndani limo mbingu, Limeandikwa mahali, kama nyota ya kwangu, Thamani ya jambo hili, haikadiriki Sitasahau fadhili, akinijalia Mungu. i yangu, Maneno ni mapungufu, fahamu rafik ngu, Hata ukiyasarifu, kwa kuyapanga mafu , Hayawezi kuarifu, pasipo kizunguzungu mwengu. Na huu ni upungufu, mkubwa kwa wali

HASARA kwenda, MAISHA yetu mapito, kila siku tuna inda, tush yana yo amba o, Katika mambo mazit , unda kuya zayo tuwe to, Na yale mambo mato nda. kute la sa kuko Hasara iliyo nzito, ni da, Maisha hayatulii, siku zote yanakwen nda, kupa ni uka kush si Na sababu ya uhai, nda, matu a akos utay Usipofanya bidii, Hasara iliyo nzito, ni kukosa la kutenda.

Dunia ukijilaza, lazima itakuponda, Lakini ukijikaza, utapata japo shinda,”

Yafaa kujihimiza, woga huleta kukonda,

Hasara iliyo nzito, ni kukosa la kutenda.

da, Nenda katazame chungu, wakusanyavyo magan nda, kujipi amu binad , Mungu avyo Ndivyo apend Akikabili machungu, mwisho hupewa kushinda, Hasara iliyo nzito, ni kukosa la kutenda.

38

Mema Maovu Lakini Hasara

tukiyatafuta, maovu yanatuwinda, yana matata, ushindani yanapenda, tutayapita, tukijaribu kupanda, iliyo nzito, ni kukosa la kutenda.

Sasa namwomba Mungu, asiache kunilinda, Na walimwengu wenzangu, awajaliye matunda, Watokane na machungu, ndivyo ninavyopenda, Hasara iliyo nzito, ni kukosa la kutenda.

Tupe nguvu tuhimili, tucheleweshe kuvunda, Zirutubishe na hali, wake wazae makinda, Dua hii ikubali, utuepushiye inda,

Hasara iliyo nzito, ni kukosa la kutenda. Niliyosema si haba, kusitawisha kiwanda, Haba na haba kibaba, pishi na pishi kikanda, Baadaye mtashiba, mfurahi na kuwanda, Hasara iliyo nzito, ni kukosa la kutenda. kshinda — nusu.

HADHARI

HADHURIWI alinyongwa, mapokeo yanasema, Ulimwengu una nongwa, hadhari ni jambo jema, Kudai sana ubingwa, mwisho huleta nakama, Hadhari ina malipo, hata katika salama.

Ukichukua mzigo, heri kwanza kuupima, Dunia ina mitego, mtu hakawi kukwama, Dharau japo kidogo, mwisho huvunja heshima, Hadhari ina malipo, hata katika salama. 39

Unapopewa shubiri, usijitwalie pima, Mtu kujua kadiri, ndiyo kutukuza kima,

Dunia ina hatari, haraka siyo kuchuma, Hadhari ina malipo, hata katika salama. Hatari kwa binadamu, kufuata kila tamaa,

Jambo hili kwetu sumu, mwisho wake siyo mwema, Yote hayatulazimu, mengine yatatuchoma, Hadhari ina malipo, hata katika salama. Njia zetu zina miba, ukisafiri tazama,

Tena zina ghiliba, huelekea vilima, Hadhari kwetu akiba, ukichoka utahema, Hadhari ina malipo, hata katika salama. Kutojali Si jambo Hadhari Hadhari

ni hasara, wanena wenye hekima, lenye ijara, kutojali kunauma, ndiyo busara, ndiyo njia ya uzima, ina malipo, hata katika salama.

Wachezaji wa karata, wana maneno husema, Mchezo wenye matata, ni kushika ulitima, Kushinda hutakupata, ushabiki utavuma, Hadhari ina malipo, hata katika salama. Mengine nitayasaza, Nadhani hayataoza, Mungu ikimpendeza, Hadhari ina malipo,

akiba huleta neema, mwakani mtayasoma, kutubakisha wazima, hata katika salama.

HAYA HABARI nimesikia, kuwa haya yachukiza, Watu wanakusudia, upesi kuifukuza, Sababu huwazuia, haja zao kuzikuza, Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia. 40

Kuna watovu wa haya, ambao wanaeleza, Kuwa haya jambo baya, si mmea wa kukuza,

Haya haina hatia, bure kuipatiliza, Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia. Haya ni kama utaji, nyusoni inapendeza, Watu inawafariji, ni pumbao hupumbaza, Inaposhika vipaji, sura zetu huangaza, Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia. Maisha yasiyo haya, hakika yanaumiza, Moyoni yana kinaya, na machozi yanaliza, Kila jambo huwa baya, haya ikijipoteza, Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia.

Haya inakazaniwa, watu wanaikimbiza, Nyusoni inang'olewa, yauzuliwa baraza, Wanatafuta ukiwa, watu hawa peleleza,

Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia. Haya inaitwa woga, watovu wanaeleza, Makusudi kuvuruga, wenzao kuwatatiza, Ili wapate kuiga, wazame katika kiza, Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia.

Haya ina thamani, ni akiba ya kusaza, Usiitoe moyoni, si jambo la kupoteza, Ni ngao ya nuksani, haya ukiifanyiza, Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia. Hapa nilipofika, ninatamani kutuza, Mengine nitaandika, sijachoka ninawaza, Mambo yanayosomeka, na mema kusikiliza, Maisha yasiyo haya, yanaharibu tabia.

41

HADAA

WAUNGWANA

NA

HIANA

wenye vyeo, nawaarifu waraka,

Mdogo wa mausio, ambao ninaandika, Wende katika eneo, lote la Tanganyika, Hadaa na hiana, ni hasara kutumia.

Mambo Kuacha Maana Hadaa

hayo ya dunia, wajibu kuyaepuka, kuyatumia, si hasara ni baraka, yatazuia, heri kwetu kufika, na hiana, ni hasara kutumia.

Jambo la kwanza hadaa, lazima kulitanuka, Hadaa huleta baa, matumaini huruka,

Si jambo la manufaa, rada yake kuhizika, Hadaa na hiana, ni hasara kutumia. Hadaa ina batili, moyoni ukiiweka, Huwi mtu wa kweli, ila utaharibika, Haki ukiibadili, mwisho utaaibika, Hadaa na hiana, ni hasara kutumia. Jambo la pili hiana, si neno la kulishika,

Hiana ina fitina, moyoni mtu kuweka, Wenzio mtakosana, habari ikiwafika, Hadaa na hiana, ni hasara kutumia.

Watu ukiwaghilibu, wajivutia mashaka, Hiana ina aibu, wakati wa kubukuka, Watu hawakuhesabu, jina lako litanuka, Hadaa na hiana, ni hasara kutumia.

Hiana si faida, mtu akiishika,

Itamtia husuda, mwisho atajitundika, Jambo hili lina rada, vigumu kusameheka, Hadaa na hiana, ni hasara kutumia, 42

Leo haya yanatosha, nitaacha kuandika, Waraka nimefupisha, uwe mwema kusomeka, Kama nitazidisha, wasomaji watachoka, Hadaa na hiana, ni hasara kutumia.

TABIA KIOO kwa binadamu, katika hii dunia, Watakao tufahamu, wanatazama tabia, Tabia jambo muhimu, tunza na kuangalia, Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia.

Sidanganywe na pumzi, haikawi kukimbia, Yakakutoka mapenzi, watu ukawachukia, Jifunze uwe azizi, mahali ukiingia,

Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia. Fanya adabu kwa watu, adabu husaidia, Adabu libasi kwetu, kashifa inazuia, Kisha hutukuza utu, jambo hili huwaniwa,

Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia. Adabu ni mtumishi, milele husaidia, Faida yake haishi, kila siku huzidia, Adabu ina ucheshi, watu huifurahia, Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia. Wapo watu maskini, hawana cha kutumia, Lakini wana thamani, kwa ubora wa tabia, Watu hao duniani, ni chumvi ya kutumia, Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia.

Wapo wenye milki, watakavyo hutumia, Lakini si marafiki, kwa ubaya wa tabia, Hao hawachukuliki, hatari kukaribia, Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia. 43

Tena wapo wanyonge, ambao ni maridhia,

Hawadhuru kama nge, wala hawana udhia, Wajipatiao tonge, kwa njia yenye sheria, Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia.

Kisha wapo wenye nguvu, wajinga kuitumia, Wajitiao ubovu, kwa mambo ya kurukia, Wakamuliwapo mbavu, huilaumu dunia, Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia. Zaidi yake wadogo, waelekevu wa njia, Wajipatiao togo, kwa mambo yenye murua, Hawashikwi na mitego, waendapo hupokewa, Utatukuka jina, kwa uzuri wa tabia.

MPATANISHAJI

BORA KULIKO MTEKAJI

BWANA Chamberlain, Waziri wa Uingereza, Twakushukuru yakini, kwa mambo kuyatuliza, Kuirudisha amani, roho zimetoka kiza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji.

Taa zilizimika, Ulaya ikawa kiza, Furaha ilitoweka, hofu ilijieneza, Dunia ilistuka, kwa wingi wa virigiza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji. Afrika na Amerika, tisho lilijitambaza, Nchi za Ushirika, pia halikusaza, Kwa kuchelea shabuka, iliyotaka tokeza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji.

Yalitaka ubalozi, mambo yale kutuliza, Yalitaka uongozi, ustadi wa kuwaza, Ama sivyo uchokozi, dunia ungalimeza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji. 44

MJI

Ufunguo ulitiwa, ukabaki kugeuzwa, Ahera kufunguliwa, umati kujiingiza, Chamberlain alizuia, ukarudi mwangaza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji. Wa Chekoslovakia, wamefanya miujiza, Sadaka waliyotoa, haijatendeka kwanza, Imeokoa dunia, Mungu awape ijaza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji.

Mtekaji humwaga damu, kama mpira kucheza, Moyo wake mgumu, Shetani humwongoza, Furaha yake udhalimu, haki huipuuza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji. Tulikuwa ukingoni, nusura kukitimizwa, Alitawala Shetani, karibu kutupoteza, Tumerudi furahani, twaweza kuzungumza, Mpatanishaji bora, kuliko mtekaji mji.

WAINGEREZA

WATASHINDA

1

3

WAINGEREZA taratibu, Hawajisifu harubu, Fahamu wataharibu, Adui wa uhuria.

Kila mpinga uhuru, Atafuta kujidhuru, Mungu hatamwamuru, Kuwa juu ya dunia.

2 Zi wazi zake sababu, Kwa mweledi wa kitabu, Hili si jambo la taabu, Mara moja humwelea.

4 Kauli hii thabiti, Bighairi tofauti, Washindi madhubuti, Waingereza watakuwa. 45

8

5 Mungu nipe buruhani,

Patakutana umati, Wasiohofu baruti, Waone heri mauti, Kuliko kudhulumiwa.

Unibakishe mwakani, Niadhimishe amani, Na wenzangu huria.

9

6

Na jamii halaiki, Mungu wape riziki, Uwaepushe na dhiki, Bwana pokea dua.

Usinitoe usoni,

Uniongoze kizani, Kiumbe wako sioni, Msaada niridhia.

10

7 Mungu hatamnusuru, Wala hatampa nuru, Mwenye kutaka kudhuru,

Beti kumi zitakifu, Shairi kama mkufu, Si vizuri kuwa refu,

Uwezo

Mengine nitazuia.

humkimbia.

TAFSIRI

YA

NDOTO

NDOTOYO bin Kibwana, ya watoto ishirini, Ni dola zenye majina, zilizo sasa vitani, Kwa nguvu zinapigana, zote zimo harakani, Ndivyo ninavyoona, wala si kama nadhani.

Mchezo wao wa mawe, kuyatupa manyasini, Uliokujia wewe, kwa ndoto usingizini, Ni ghadhabu na mayowe, ya watu wengi vitani, Kila dola upandewe, yasema sina kifani.

Kwa mawe kumalizika, ni dhiki ya Jermani, Ambayo itawafika, na hivi imo njiani,

Nguvu ikimalizika, watasema laitani, Dhiki hii itafika, imalize ushindani.

Kijana aliyesaza, mawe mengi kilembani, Fahamu ni Mwingereza, na wenziwe shirikani, Hao watawaviza, maadui Jermani,

Kama mayai viza, Italia na Japani.

Kwa kofia kuvuliwa, na kapu kuwa motoni, Ni adui kaondolewa, na kunyang'anywa mkononi, Nchi alizochukua, kwa kuziteka vitani, Wenyewe watarudishiwa, nchi zao mwishoni. Kwa saa alfajiri, ndoto kuja kichwani, Inasema tafsiri, tokeo lake jirani, Kwayo hapana usiri, atashindwa Jermani, Ndoto yako ina heri, sijui utuzwe nini.

Sasa natoa mfano, wazo langu la moyoni, Mzigo mzito mno, kama wendako jirani, Na makali mapigano, ushindi uko usoni, Hii kweli siyo ngano, imani yangu rohoni. Bwana Salehe Kibwana, usikate tumaini, Ndoto yako ina maana, bora sana ufichoni, Naona fahari sana, kwa kukujia kichwani, Tumwombe

Mungu

Bwana,

atuonyeshe

mwishoni.

Kusema kweli thawabu, japo kuwa mashakani, Shairi nililojibu, sikutajwa jina ndani, Kwayo naona aibu, kusutwa uwanjani, Hukupewa karibu, kakwita nani Shaaban? Kwa kuwa nimecharibu, kujitia barazani, Nastahili adhabu, ya wakuu gazetini, Wala sitaona taabu, kujiona masutoni, Maana siye sahibu, sikutajwa orodhani.

47

A

HAPOTEZI MTU anayeweka, kwa Mungu hapotezi, Milele hufurika, hazina ya Mwenyezi, Kwa wema na baraka, iliko hafiki mwizi, Kutu shida kushika, mchwa kula hawezi.

HURUMA HURUMA inanong'ona, kuwa sasa imechoka, Moyoni inasonona, yatamani kutoroka, Kwa mambo inayoona, magumu kuvumilika, Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia.

Huruma usituache, tushike na kutuweka, Imani yetu ni chache, ndivyo tulivyoumbika, Tusetiri tusichache, tusije tukaumbuka, Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia. Japo hatustahili, msamaha tunataka, Huenda tukabadili, tukapata kuokoka, Waijua yetu hali, mtu hakukamilika, Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia,

Kukosa na kupotea, mwanadamu kahusika, Lakini tunayo nia, twatamani kuokoka, Kama watusaidia, twatumai kusafika,

Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia.

Kuomba si jambo duni, ni thamani ya kutaka, Haja haijulikani, ila kwa kuitamka, Neno ninalotamani, vita ni kukatika, Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia.

48

un

Vikatike kwa heshima, si aibu kutufika,

Waingereza kusimama, ndivyo tunavyotaka, Moto wanaouzima, ukome tena kuwaka, Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia.

Ndipo yaje mapatano, tuishi wote shirika, Yatoweke mapigano, kama mvua kuanuka,

|

Yashikane kwa mikono, mataifa na kucheka,

Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia. Yashikane kwa mikono, mataifa na kucheka, Pasiwe manung'uno, ya watu kutoridhika,

Yafuate mapatano, ya vita kutozuka, Huruma

usiondoke, zidi kutuhurumia.

Shairi hili la kafu, kituoni limefika, Tunaomba tahafifu, tulale na kuamka, Mungu usitukashifu, twapenda kusetirika,

|

Huruma usiondoke, zidi kutuhurumia.

GAZETI

HALINA

NAFASI

AHSANTE Bwana Edi, salamu nimeziona, Nitafanya jitihadi, utenzi uzidi tena,

|

Beti elfu idadi, zimekwisha patikana, Na nyingine zaidi, kiwandani nazisana.

|

Nasikitika gazeti, sasa nafasi halina, Karatasi hatupati, zimekuwa shida sana, Tunazopata katiti, hazitoshi kama jana, Zikichapwa nyingi beti, habari zitabanana.

Moyoni ninayo dhati, nafasi ikija tena, Likikua gazeti, kwa urefu na upana, Nitazizidisha beti, na kuzidi kukazana, Ahadi hii thabiti, akiniweka Rabana.

49

Tumwombe Mungu wetu, upepo uwe mwanana, Ushindi uje kwetu, Hitler apate laana,

Na Mfalme wetu, apewe amani tena,

Turudiye raha zetu, za usiku na mchana.

Hitler na wenzake, nataka wapigwe sana, Hata walalamike, nguvu hatuna tena,

Tunataka tuandike, sasa vita hapana, Tendo hili lifanyike, ninakuomba Rabana.

HAZINA MASHAIRI ni hazina, katika kila msemo, Huongoza kuona, mambo mengi yaliyomo, Katika dunia pana, mfano kama masomo, Tena huwafaa

sana, watu wa kila makamo.

MWINGEREZA HAKUBALI UTUMWA SELEMANI wa Kabunji, tangu utaje Pangani, Na mimi katika mji, kujibu nimetamani, Usidhani nahitaji, sifa za gazetini, Ndege ni Mwingereza, kisiwa Britania.

Naandika Sijigambi Uliyetupa Ndege ni

mistari, mwisho herufi ya eni, uhodari, ila naeleza nyuni, habari, na kumtia fumboni, Mwingereza, kisiwa Britania.

Umbo ulilosema, la rangi tatu mwilini, Ni bendera ya heshima, ipepeayo angani, Jina lake linavuma, Union Jack shani, Ndege ni Mwingereza, kisiwa Britania.

50

Uhuru ndiyo uhai, na damu ya huyu nyuni, Utumwani hatulii, mtu wa Britani, Amefanana na tai, siyo kuku wa nyumbani, Ndege ni Mwingereza, kisiwa Britania. Swali la beti saba, umetupa Selemani, Nikizidisha miraba, itakuwa si kifani,

Maneno yakiwa haba, maana kubwa huwa ndani,

Ndege ni Mwingereza, kisiwa Britania, Jibu langu 'tafupisha, niifuate kanuni,

Sitaki kubadilisha, mapokeo ya zamani, Deni ulichokopeshwa, usichokopa si deni, Ndege ni Mwingereza, kisiwa Britania,

Kama jibu si mufti, lawama kwangu begani, Jina langu madhubuti, wa mbali sikilizeni, Ni Shaaban Robert, nimehamia Pangani, Sifa sikujizoeza, nafuata mazoea.

MOYO MOYO wa mtu msitu, ndani una kila feli, Usisadiki tu, kila neno la awali, Hata akisema mtu, aliyeandikiwa kweli, Usoni haiwi kitu, bila tendo na dalili.

MUNGU

NICHUNGE

EE! Mungu nichunge, njia yangu nielewe, Wala sitaki niringe, mkononi mwako Wewe, Ulimi wangu ufunge, kwa mambo yangu mwenyewe, Lakini nipige yowe, kwa dhuluma ya wanyonge.

”Ji

Nakutaka Muumba, nifanye mnyenyekevu, Mnyenyekevu kuomba, wala nisiwe mvivu, Lakini nifanye simba, mbele ya uonevu, Unione uonevu, mbele yake kama mwamba,

Nakuomba Mungu, nifanye niwe mtii, Nivumilie machungu, taabu hii na hii, Nipatapo dogo fungu, nisidai nikinai, Lakini niwe adui, kwa mpunjaji wenzangu. Napenda niwe laini, mbele ya watu wakuu, Sidai kuwa kifani, wala sitaki dharau, Siku zote niwe chini, wao wakiwa juu, Bali kutaka nafuu, ya wenzangu natamani.

MAPUMZIKO MAPUMZIKO ya watu, duniani sifikiri, Mapumziko yetu, yamo ndani ya kaburi, Huko mwili wa mtu, utatulia vizuri,

Maisha nafasi tu, ya kazi kujitendea.

KIZITO

HAKIUMIZI

WENGI wanaposhika, kizito hakiumizi, Kama una mashaka, nieleze waziwazi, Nitakuwa mshirika, katika yako majonzi, Uso mzuri kucheka, haupendezi machozi. Maisha yamezunguka, dunia ina uwazi, Roho zimeungika, kwa mkufu wa mapenzi,

'Tunapopata mashaka, yapo na masaidizi, Sema lililokufika, nilifahamu mpenzi. 32

T

WEMA PANDA mbegu ya wema, yaote mapendeleo, Panda mbegu ya heshima, ili uvune cheo, Uovu si mbegu njema, zao lake machukio, Tena hupata lawama, apandaye mbegu hiyo. Panda Hapati Haraka Wengi

ungoje majira, usivune mbio mbio, mazao bora, mwenye pupa na choyo, ina hasara, wamesema wasemao, wamedorora, kwa kupuuza yapasayo.

NDOA

YA

1 BISMILAHI nasema, Mungu Mgawa rehema, Kwako naomba salama, Nisemayo yawe sawa.

2 Tena naomba kabuli, Nyoosha yangu kauli, Mambo yanayodhili, Niweze kusimulia.

3 Niongoze Mwongozi, Nisemayo yawe wazi, Yafike kwa wasikizi, Wajue ilivyokuwa,

SIRI 4 nyuni, umewapa Mungu Wakaao misituni, Sauti tamu vinywani, Nami nipe robo moja. 5 Nipe pumzi niheme, Na sauti niseme, Ulimi usiteteme, Kusita na kupotea. 6 Nipe sauti niimbe, Kisa hiki nikipambe, Wimbo wende kila pembe, Ya nchi tunayokaa. 53

13

7 Nipe maneno matamu, Yatiayo watu hamu, Kusoma na kuazimu, Kutenda yanayofaa.

Kisa cha ndoa ya siri, Nataka kukifasiri, Jinsi kinavyohasiri, Wanawake wakiwa.

14

8 Nipe maneno laini, Yaliyo na buruhani, Waimbe wana mekoni, Na nje wakitembea.

9 Nipe maneno muhimu, Niandike kwa kalamu, Wala yasiwe magumu, Kwa watoto kuelewa.

Hifadhi ya wanawake, Nataka niitamke, Nipe moyo nisichoke, Muumba pokea dua.

15 Ingawa wana hiari, Kutenda wanavyokiri, Lakini shauri zuri, Ni chumvi ya kuungia.

16

10 Naandika kiwe kito, Wimbo huu kwa watoto,

Waelewe na mapito, Mema

katika dunia.

Tungo hii ya awali, Juu ya jambo hili, Bwana Mungu tafadhali, Zidi kuniangazia. 17

11 Naandika iwe tunu, Wimbo kwa akina nunu, Ili wawe na fununu, Ya kuweza jiokoa.

Ndiyo mwanzo naanza, Jambo hili kueleza, Naomba

18

12 Naandika

ni akiba,

Katika njia ya miba, Inayoleta misiba, Labda wataambaa.

mwangaza,

Nende bila kujikwaa.

Nuru

nimulikie,

Ili nendako nijue, Wala nisiwayewaye, Nikapotewa na njia.

19

25

Niongoze nendako, Nirudi na nitokako, Nisikose matamko, Aibu nyuma ikawa.

Nilitaka nibaini, Habari ya mtaani, Nikafika kwa fulani, Karibisho nikapewa.

20

26 Nilipotaka habari, Mwenyeji kanihubiri, “Hapa palizuka shari, Mwanzo wake ni ndoa.”

Hatari ukigundua, Watu usipowambia, Kama watatumbukia, Lawamani utatiwa.

21

27 “Bibi mmoja mzuri, Mwenye umbo la fahari, Kwa ghiliba alikiri, Kwa siri kuolewa.”

Kwa hivi nimefikiri, Kuficha si jambo zuri, Bila neno la hadhari, Watu kuwatolea.

28

22 Wapo watakaoshika, Pengine na kuokoka,

“Ati aliona sifa,

Ndipo nami

Kaolewa kwa kashifa, Bila wazazi kujua.”

Bila ya taarifa,

nikashika,

Kalamu kuhadithia.

29

23

“Wazazi wasikitika, Huzuni imewashika, Binti kughilibika, Jambo hili kuridhia.”

Sidai ushahidi,

Lakini yaliyobidi, Nilifanya jitihadi, Kwenda kuangalia.

30

24

“Kwanza hawakukubali, Kusadiki jambo hili, Waliona si la kweli, Bure alisingiziwa.”'

Nilikuwa nahitaji, Moyo kuufariji, Basi nikahojihoji,

Ili nipate elewa.

39

31

37

“Wazazi kupeleleza, Wakapata mwangaza, Binti amejioza, Bila wao kuambiwa.”

Hizi ni siku za hati, Ndoa zina masharti, Ni hasara kwa binti, Siri akiolewa.

32 “Hili liliwakasiri, Pakazuka kubwa shari, Ila kwa bahati nzuri, Watu wakaamuliwa.'

38 Japo kuwa ni suna, Ndoa ya siri fitina, Mwisho mwema

haina,

Wajibu kuzingatia.

33

39

Alipokwisha hutubu, Nikaona ni wajibu, Juu ya uharabu, Onyo lazima kutoa.

Ndoa isiyodhihiri, Wala kufanyiwa ari, Watu hawataikiri, Matata yakitokea.

34

40

Japo kuwa hukubali, Vyuo kusema halali, Ndoa isiyo dalili, Pengine ina udhia.

Matata yakitokea, Huna pa kukimbilia, Japo mwana umezaa, Kurithi atazuiwa.

35

41

Kama haijui baba, Ndoa haina haiba, Mama hali na kushiba, Wakati akisikia.

36

Kusikia bintiye, Kaolewa asijue, Hasira na uchunguwe, Kichwani mvi hutia,

Mtoto atatabika, Wenziwe katika rika, Milele watamcheka, Aibuni atatiwa.

42 Na wewe mama lazima, Utavunjiwa heshima, Jua hawana huruma, Watu wakiona doa.

49

43 Utatolewa maanani, Watu wasikuthamini, Udunishwe hesabuni,

Hati ikikosekana,

Hili si jema kuwa.

Ndoa hii kujitia.

Utashindwa msichana, Heri kuambaa sana,

44 Kuozwa hukukatazwa, Hoja gani utatoa, Sababu kujiumbua, Binti mwenye murua?

50

Tena tufanye methali, Kama mume wa pili, Kwa baba akiwasili, Dhahiri kutaka oa.

51

45 Kwamba watu wazoea, Kwa siri kuolewa, Lakini si sawasawa, Mwisho dhiki hutokea.

Mahari yakitolewa, Wazazi wakipokea, Tuseme wana hatia, Kwa jambo wasilojua?

46

52

Ndoa ya siri hatari, Inapoteza mahari, Kama hili likijiri, Wapi pa kushitakia?

Kwa sheria si halali, Mke waume wawili,

Lizukapo jambo hili, Wapi pa kukimbilia?

47

53

Madai yako batili,

Huyu ataka mkewe,

Mbele ya Serikali, Kama huna dalili, Ushahidi wa kutoa.

Yule adai maliye, Hapo lazima ujue,

48 Serikali itasihi,

Hati yako ya nikahi, Ili itie sahihi, Kuwa uliolewa.

Nazaa

itatokea. 54

Mama atatamani, Kukurudisha tumboni, Na baba atatamani,

Kuwa usingezaliwa.

61

55

Maisha ya wanawake, Namna ya peke yake, Kuwafanya waanguke, Ni jambo lenye hatia,

Mmoja katika mia, Siri wanaoolewa, Bahati humtokea,

Mambo yakawa sawa.

62

56

Mara nyingi nimeona, Mabinti waungwana, Sifa yao ya majina, Hawana imepotea.

Na tisiini na tisa, Hukutana na visa,

Vinavyotisha Misibani

hasa,

wakawa.

63

57

Waanzao mambo haya, Ni wanaume wabaya, Halafu huwaumbua, Wanawake bila njia.

Huachiwa ulezi, Pasipo msaidizi, Aliyemwita mpenzi, Amekwisha kukimbia.

64

58 Amekwisha kukimbia, Mke mwingine kaoa,

Wanawake ni wakiwa, Wajibu kusaidiwa, Tena tumeumbiwa, Ili watoto kuzaa.

Na wewe wawayawaya, Watoto njaa walia.

65 Wazeni tabu ya mimba,

59 Ukienda kushitaki, Watu hawatasadiki, Na hii ndiyo haki, Wajinga wanayopewa.

Mtaona ya kwamba, Mti haushindi shamba, Juu ulipomea.

66

60

Tunda halishindi mti, Msiumbue mabinti, Kwa matendo na sauti, Lazima kusaidiwa.

Usifuate ubembe,

Waume wengi wazembe, Hawana hata chembe, Mapenzi ila hadaa.

38

67

70 Angetaka aliweza, Kuzuia kutokeza, Nisione mwangaza, Leo katika dunia.

Mabwana nawasihi, Msione ikirahi, Kesho mtafurahi, Sifa nikiwatolea.

7 Mama alivyonitunza, Kumlipa sitaweza, Shukurani kufanyiza, Ni deni limebakia.

68

Leo siku ya mabibi, Ya kufutiwa madhambi, Natumaini kwa Rabi, Kuwa wataokolewa.

72 Haya niliyobaini, Yanatendeka yakini, Mtungaji Shaaban, Robert baba elewa.

69 Mama yangu Mwanamwema, Namtukuza daima, Na jamii kina mama, Heshima nawatolea.

MSITU MAISHA robo tatu, twapapasa hatuoni, Katikati ya msitu, usio na nuru ndani, Na robo moja tu, tunapopata uoni, Umekwisha tia kutu, uzee mwetu mwilini.

Kipawa cha akili, japo kuwa ni fahari, Lakini wembe mkali, hukata na kuhasiri, Sana huhasiri mwili, uzito wa kufikiri, Na hii si afadhali, unapowaza vizuri. Na uzito wa ujinga, kadhalika ni hasara, Huu ujinga hufunga, hujui lililo bora, Hasa ujinga ni jangwa, baya kuliko Sahara, Ujanani tunatanga, ndani yake kila mara.

99

BARUA MUSA RASHID somo, barua nimefahamu, Nimesoma yaliyomo, hata nikahitimu, Kwa kutunga nawe umo, katika sifa muhimu, Kukutolea ungamo, hapa imenilazimu. Nimependezwa na kimo, beti zilivyotimu, Tezi hata omo, zimeundwa kwa elimu, Na maana ndani imo, iletayo tabasamu, Kubwa katika midomo, kwa maneno maalumu.

Umefikia kipimo, kwa watu wengi adimu, Bora hakina mashimo, na maneno si magumu, Usemapo kuwa humo, ushairini haramu, Mimi nahesabu umo, wala hutoki mwalimu. Masuto hayawi fumo, hasa ya wenye wazimu, Japo kuwa si chumo, mashairi ni matamu, Katika kila masomo, ya watu wataalamu, Mashairi ni kilimo, na mbegu ya fahamu. Nimepatwa na mshomo, kwa kusikia muamu, Kuwa kitandani yumo, kwa maradhi kumsumu, Ipe kabuli midomo, Bwana Mungu mkirimu, Atoke katika shimo, kijana tena adumu.

Mrefu kwa kipimo, mkono wako Karimu, Mwokoe asiwemo, ndani ya dhiki ngumu, Dunia haina shimo, usiloweza hukumu, Kutoka kiliyomo, na kuamuru kidumu.

Nilialikwa niwemo, juzi katika karamu,

Nikakuta Harvey yumo, anaagwa na walimu, Nikasikia msemo, wa hotuba moja tamu, Iliyotia tetemo, kwa shairi maalumu.

60

Nitafuliza msemo, hata beti zitimu, Nyuma kusibaki zumo, kushutumu wanadamu, Kuhesabiwa kuwamo, katika choyo si tamu, Sifa mbaya siyo chumo, kuwania mwanadamu.

Beti nane kwa kipimo, shairi lako mwalimu, Na hili chake kimo, beti tisa zimetimu, Kuzidisha msemo, sasa hailazimu,

Basi hiki ni kikomo, pamoja na wasalamu,

MAJIBU NAKUSHUKURU muhibu, kwa barua ashrafu, Ambayo naihesabu, haina ulinganifu, Bora kuliko dhahabu, hata vito vitukufu, Haya sasa ni majibu, kama ulivyoarifu. Na mimi ningefurahi, kukuona mtukufu, Utiaye moyo zihi, mwili ukawa mnyofu, Na kama sikusitahi, fahamu ningekukifu, Kuja kwako asubuhi, kabla hujaarifu.

Kujivunjia heshima, niliona upungufu, Wenye hekima husema, mwenye haraka kipofu, Na mwenda pole daima, husafiri njia ndefu,

Maneno haya ni tama, usidhani usanifu.

Usidhani ni dhihaka, maneno haya turufu, Endaye kwa haraka, hatokani na uchofu, Mwenye pupa kulishika, tunda bivu takilifu,

Mwenye saburi hufika, kati ya ukamilifu. 61

VILEO MTENGEZA Mambo Leo, radhi niwie Bwana, Nafasi ukiwa nayo, nipe ruhusa kunena, Ukiona mapoteo, shairi halina kina, Sahihisha kila tao, liimbike dana dana.

Tena litie vituo, liwe jepesi kunena, Lipendeze masikio, kwa sauti kulingana, Hata watu wasomao, wadhibiti na maana, Kama tembo kileo, nguvu hulevya sana.

Watu nguvu Mambo hasa Amani kwao Kama bangi

walewao, daima huchokozana, wapendayo, mzozo na kuuana, chukio, hawapendi kuiona, kileo, mali hulevya sana.

Mali nayo ni kileo, lakini bahati ina, Watu walewao hiyo, hudai sana ubwana, Huwadharau wenzao, ambao kitu hawana, Kama mvinyo kileo, elimu hulevya sana. Elimu wailewao, ajabu ukiwaona, Hujifanya kama wao, mfano wao hapana, Hapa nawapa funuo, kiza huzaa mchana, Kama kasumba kileo, uwezo hulevya sana. Uwezo aliye nao, ana shani kubwa sana, Hutaka ayasemayo, hata ikiwa fitina, Yawe katika sikio, wimbo wenye maana, Kama divai kileo, mapenzi hulevya sana.

Mapenzi pia kileo, lakini ni bora sana, Huunga watu ambao, nasaba moja hawana, Yakipenya watu hao, hujiona walingana,

Kama pombe kileo, sifa hulevya sana. 62

Hakika sifa kileo, wazi bila kubishana, Kunguru ana mlio, usiopendeza sana, Aliposifiwa nao, hadhari hakuiona, Kama kangara kileo, dharau hulevya sana. Dharau ndicho kileo, kizuio cha kuona, Huziba na masikio, ikabaki kujivuna, Hali ujivuniayo, pengine hayana maana, Kama moshi ni kileo, nasaba hulevya sana. Wale wajinasibuo, kabila na uungwana, Na wale wadunishwao, kama walio na laana,

Adam baba yao, chini alipatikana, Kama mbege ni kileo, neema hulevya sana. Sisemi kuwa vileo, vimeniashiki sana, Na watu watumiao, kupatiliza nakana, Wengi hushinda wao, kuwashinda shida sana, Nimevisema vileo, kuonya si kubishana.

Ningeandika vileo, vyote nilivyoviona, Nikawapa waimbao, lakini nafasi sina, Hali namna hiyo, mwaelewa waungwana, Mtu akiwa nayo, mengi hawezi kunena.

Basi natia komeo, Mungu tupe mwanana, Tupe mambo tuwezayo, yasiwe mazito sana, Vikitokea vileo, kutaka kugombana, Vitukute tuna ngao, na zana za kupigana.

JIBU ONYO nawatolea, maneno haba hekima, Na jibu pole ni dawa, swali kali hulizima, Hulizima likapoa, lililotaka kuchoma, Na matone nawambia, ndiyo mito na visima.

63

Nawambia kuwa mito, ni bahari na maziwa, Kuku hawapi watoto, maziwa anapozaa, Lakini kwa fukuto, makinda yake hukua, Mwanzo wa kila kizito, vidogo vingi pamoja. Vidogo vingi pamoja, ndiyo mwanzo wa kigumu, Kila linalotajwa, kwa upole huwa tamu, Neno pole ni faraja, halitii joto damu, Ulimi mno hufuja, kama hauna hatamu.

Neno kali huwasha, mwasho mwingi mbaya, Kila ukijibisha, maneno yako chagua, Chagua na kunyoosha, kombo palipoingia, Maisha yetu yakisha, majina nyuma hukaa. Sema na kufananisha, kama uso na kioo, La matata badilisha, waitike watu ndiyo, Neno la kuchangamsha, watie katika moyo, Hapo yako maisha, watakumbuka wajao. Tia maneno mafuta, hata yawe laini, Midomoni yakipita, yasiwe na mshindani, Hata kama unateta, adui awe haoni, Neno la kukusuta, wala la kukufitini.

Kabla ya kutamka, kufikiri ni halali, Ovu likikuponyoka, mara sema tafadhali, Radhi anayetaka, si mwoga ana akili, Rahisi kununulika, siache kikawa ghali. Katika masihara, kweli nyingi hutolewa, Usifanye hasira, hasira hupotoa, Inapotoa harara, hata haki hupotea, Si woga ni busara, jibu pole ukitoa.

Nimelitunga koja, kwa maua mbalimbali, Liwe tunu kwa wambeja, walio bara Swahili, Ni mimi nisiye haja, mtu mmoja dhalili, Shaaban najitaja, mwisho wa shairi hili. 64

ASALI SALAMU zimewasili, kuwa wataka barua, Kukusahau muhali, halipati kutokea, Twaungana mara mbili, mapenzi na kuzaliwa, Yote mawili asali, hapana la kuchagua.

Lipi la kuchagua, nieleze nifahamu? Katika mawili haya, lipi lililo muhimu? Kipimoni nikitia, yote naona matamu, Mpendwa uso kunjua, upate kutabasamu. Mungu atakujali, kila neno liwe sawa, Ndiye ajuaye feli, apendalo huandaa, Mtu hawezi badili, analolitaka kuwa, Hustawisha la mbali, la karibu likavia.

Nitaacha kalamu, nifupishe barua, Waraka mfupi tamu, na rahisi kuelewa, Mungu atatukirimu, siku itatokea, Badala ya kalamu, pamoja tutaongea.

TANGU

NILIPOKOMA

TANGU nilipokoma, kupata kwako barua, Furaha imenihama, machungu navumilia, Moyoni nina tuhuma, labda umechukiwa, Kama nimekosa sema, ndiyo hali ya dunia. Kama nimekosa sema, ili nipate elewa, Nitafute kisima, au lilipo ziwa, Nguo yangu ya lawama, nikajaribu kufua, Kosa moja si lawama, huweza kuvumiliwa.

65

Nakuarifu wa ama, unapopata barua, Niletee jibu hima, moyo upate tulia, Moyo unaniuma, jibu likija 'tapoa, 'Tapoa niwe mzima, jibu lako kwangu dawa. Niletee jibu jema, usivunje mazoea, Mzoefu wa huruma, hahitaji kuambiwa, Kuwa tone la wema, si hazina ya dunia, Hazina inapohama, wema hukumbukiwa. Nakumbuka

ulisema, kuwa unahitajia,

Mashairi kuyasoma, nami nikakuletea, Yapata mwezi mzima, jibu hujaniletea, Yamewasili salama, ama yamepotea, Hili silo lawama, sithubutu unajua, Nalinda kinywa daima, hilo lisije tokea, Lakini watu husema, kuhimizana sheria, Hili ukilitazama, pande mbili utajua. Hili ukilitazama, hutakosa kutambua, Kuwa hukuona nyuma, ndilo ninalochelea, Twende sawa daima, wengine walie ngoa, Wakati wakitazama, twalingana sawasawa.

Mashitaka nimesema, na ushahidi kutoa, Kama una hoja njema, waweza kujitetea, Wala usifiche nyuma, udhuru wako kutoa, Ningefurahi daima, kuona huna hatia. Nikijaliwa uzima, nitakwenda kupumua, Nimwone Mwanamwema, bibi aliyenizaa, Tangu nilipomhama, siku nyingi zimekuwa, Na mjumbe ametuma, kuwa anihitajia. Mama anitaka hima, nende bila kukawia, Kuvunja wito lawama, sheria tumewekewa,

Unapoitiwa jema, ukisiri huwa baya, Akwitaye amechuma, hupunguza ukikawa.

66

MZURI NILIPOPATA barua, una homa yakukera, Wasiwasi nilijaa, na masikitiko mara, Mikono nikainua, kukuombea nusura, Mzuri poa, tutengeze yetu sera. Naomba iwe dawa, dua kwa mwenye kudura, Inshalah maradhi haya, yatakuepuka mara, Kufumba na kufumbua, iwe kama masihara, Urudi ulivyokuwa, katika afya bora.

Wasalam natia, barua fupi ni bora, Haba anayetumia, hawi katika hasara, Mfano tumewekewa, kuwa uzi ndiyo jora, Kufahamu ya dunia, kwa machache ni busara.

MUUAWA

NA

WAVUVI

MAMBO LEO nimesoma, ya Agosti sikia, Mdanzi mwenye heshima, kuwa anihitajia, Kimya kukaa si vema, jibu linapotakiwa, Swali ulilosema, jibu lake kama hivi. Watu wa kale husema, visa ukivisikia, Vina ncha daima, tangu saba hata mia, Na watu wanavisema, kwa ncha wanazojua, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi. Wavuvi na mkulima, marafiki walikuwa, Mkulima akasema, “Wavuvi mkenda vua, Watoto wenu lazima, chakula 'tawaletea, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi.

67

y Na wavuvi walisema, 'Kuvua tukirejea, Tutakupa mkulima, samaki kutoelea, Ada ya wema ni wema, bure bila kununua, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi. Ahadi ya mkulima, kama alivyoitoa, Alitimiza kwa wema, bila kasoro kutia,

Ila wavuvi kwa tama, ahadi walipindua, Alikuwa

Kwisha Wavuvi Akabaki Alikuwa

mkulima,

muuawa

na wavuvi.

kwa mkulima, mavuno yake kutoa, walikingama, wote wakamkimbia, kulalama, na njaa inamuua, mkulima, muuawa na wavuvi.

Hujulikana daima, mvuvi ana hadaa, Wala hatazami nyuma, pato likimtokea, Huwa na uso wa chuma, huzuni usiyojua, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi.

Tembo jina adhama, lakini kwangu si sawa, Mdanzi punguza ruma, propaganda yaua, Wote tucheze ngoma, bila mtu kutishiwa, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi. Tembo jina la mnyama, mtu akimtokea, Mwili wote hutetema, asiweze kukimbia,

Kunita hivyo si vyema, umbo langu walijua, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi.

Shubiri haiwi pima, kulingana hukataa, Ratili unapopima, katika tani si sawa, Jina hili ukisema, watu utawazuzua, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi.

Wajua sipati pima, ya nini kunishaua? Cheo kikubwa

lawama, mtu asichofikia,

Kama nina kilema, nite vivyo 'taridhia, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi.

68

Wawindao wanyama, manyoya wanatumia, Kuonyesha heshima, kuwinda wanavyojua, Bwana Mdanzi kufuma, mashairi waelewa, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi.

Majibu haya ya hima, mwenzio nina fadhaa, Nimo katika kuhama, kituoni sijakaa,

Hapa niliposimama, yaningoja motakaa, Alikuwa mkulima, muuawa na wavuvi.

VITABU NAWATAJA wafalme, watawalao dunia, Wake na wanaume, wapate kufunukiwa, Watoto wawe na shime, heshima kuwafanyia, Hapana wafalme, wanaoshinda vitabu. Vitabu vina enzi, daima vinaenziwa, Mtu kama hawezi, kuvisoma ni mkiwa, Maisha siku hizi, bila elimu nazaa,

Katika vitu azizi, kimojawapo kitabu. Katika rafiki bora, kitabu nashuhudia, Humpa mtu busara, maarifa na wasia, Asomaye kila mara, faida hujivunia, Kutokujua hasara, lugha katika kitabu. Vitabu vinahukumu, na sheria vinatoa, Usihitaji vigumu, hata vyepesi hufaa, Nyayo zetu za fahamu, bila kitabu hukwaa, Na uchi wa binadamu, ni kutojua kitabu.

Vitabu vina hekima, asomaye humjia, Asiyejua kusoma, hapati kutangulia, Katika dunia nzima, kama utaangalia, Milele hukaa nyuma, asiyejua kitabu. 69

Haya ninayosema, naona sikuambiwa, Hata akiwa na kima, na ubora wa uzawa, Dunia humpima, hapati robo wakia, Asiyejua hekima, maarifa ya kitabu. Vitabu vimehifadhi, kila tunu na hidaya, Ndiyo haina kabidhi, ya mambo ya dunia, Soma upate hadhi, uwe ndege wa kupaa, Ufunguo wa ardhi, ni kuelewa kitabu. Wako

walio wajuvi, udhuru wanaotoa,

Kuwa huotesha mvi, kazi ya kujisomea, Watakuwa kama jamvi, siku zote kukaliwa, Maisha hayana chumvi, kwa mjinga wa kitabu. Vitabu husetiri, kama libasi kuvaa, Huongoza kufikiri, mtu akaendelea, Kitabu ni mshauri, faraghani ukikaa, Kutojua msitari, ni hasara wa kitabu.

Mengi mtu humshinda, pasipo nguvu ya kichwa, Na njia ya kuyatenda, vitabuni imefichwa, Uteuzini ukenda, kitabu si cha kuachwa, Kichwa shamba la kupanda, maarifa ya kitabu. Hasikitiki hajuti, mpenzi wa kurasa, Asipokuwa mufti, au kutukuka hasa, Miongoni mwa umati, hupata yake hisa, Kimeshinda sauti, ya kutamka kitabu. Maisha yana adhabu, kusoma usipojua, Mtu huitwa kidhabu, madanganyo hajatoa, Na kufanywa kama bubu, hali kinywa amepewa, Kila tunda la dhahabu, limo katika kitabu. Wana ulimi wa pili, kusoma wanaojua, Hunenezana

kwa mbali, mmeziona

barua,

Mjinga hana kauli, wa mbali akasikia, Chakula nguvu ya mwili, na ya akili kitabu.

70

Kitabu ndiye rafiki, nipendaye kumkumbatia, Tena mimi nasadiki, kuwa kinasaidia, Nikiwa katika dhiki, njia hunitatulia, Hunitatulia haki, nisionewe kitabu.

Tazameni ibra, ya kitabu nawambia, Hakidai ijara, ukisha kukinunua, Na kila wakati bora, msaada kinatoa, Hakika hana hasara, mnunuzi wa kitabu.

Vitabu hutengeneza, na watu kuwainua, Tazama Waingereza, kimo walichofikia, Stadi wa kuongoza, kwa maarifa dunia, Hili wasingeliweza, bila kuwa na kitabu. Ngazi isingalipanda, ya heshima Arabia, Kama kisingalikwenda, chuo kuwahubiria, Yanayopasa kutenda, na kuzuia mabaya, Mengi mtu hatatenda, kama hana kitabu.

Mwasikia Misri, kuwa ilifanikiwa, Hili lisingedhihiri, kama isingalijua, Elimu ya misitari, na michoro kutumia, Mtu hana nadhari, anayekosa kitabu. Sifa ya Plato, mpya katika dunia, Hasifiwi kwa mapato, na nasaba ya uzawa, Ila alikuwa kito, nuru ya kumulikia, Kwa elimu yake nzito, na kuelewa kitabu.

Socrates mwalimu, mfadhili wa dunia, Aliyenywishwa sumu, bure kwa kusingiziwa, Mungu amrehemu, watu wanamwombea, Huwezi kumfahamu, ila uwe na kitabu. William mshairi, Shakespeare Ulaya, Aliyekuwa johari, katika Britania, Kwa kutunga mashairi, kuliko wengine pia, Ameacha misitari, bora katika kitabu. 71

Kila jambo huteleza, baada ya kutokea, Katika kikuu kiza, tusiweze kumbukia,

Lakini kwa mwangaza, wa kitabu twajua, Hili linatukuza, ubora wa kitabu.

Wanaofanya kipenzi, kitabu kukitumia, Ndiyo walio na enzi, katika maisha haya, Mtu mwingine hawezi, kuwa nao sawasawa, Asemalo kama njozi, bubu katika kitabu. Vitabu vinatawala, watu wote ni raia,

Bendera kila mahala, ya vitabu hupepea, Afrika makabila, ilani yatangaziwa, Utahesabiwa ila, usipojua kitabu. Haya machache yatosha, natamani kupumua, Leo nimewakumbusha, kitu chenye manufaa, Nikijaliwa maisha, mengine 'tawatungia, Haraka mara huchosha, mwendo mwema taratibu

TAPISHI TAPISHI tamu, ikiwa na mzoaji, Siri hudumu, kama ina mwekaji, Lakini sumu, siri kwa mpayukaji, Na wazimu, pendo lisilofariji.

JINA

LANGU

NIMEWAPA

NILIZALIWA Tanga, kumi na Tangu ujana natanga, kwa safari Kila nitiapo nanga, nitulie moyo Safari mpya hupasa, nisiyoweza

72

tisa na tisa, kunipasa, hasa, kukinga.

Nilipelekwa kusoma, Dar es Salaam mjini, Nikaona taadhima, ya malezi ya chuoni, Kupata utu uzima, baada ya mtihani, Nilikwenda Forodhani, kujaribu kujituma. Miaka kumi na nane, nilifanya kazi hizo, Mimi na watu wengine, bila ovu na mzozo, Nia yangu waone, watu wenye mawazo, Rangi siyo chukizo, kuwa sawa na wengine.

Miaka minane na kumi, kazi ya mfululizo, Mimi wa rangi ya lami, na wa rangi nyinginezo, Ninapotumwa sikimwi, wala sifanyi mchezo, Sikupata machukizo, wala sikuudhi mimi.

Nashukuru kila wema, walionipa mabwana, Pamoja na heshima, kwa kuaminiwa sana, Sikuachwa nikakwama, nuksani sikuona, Na kila nililonena, kwao lilikuwa jema. Katika hii Idara, sikupata kufahamu, Kufanyiwa hasira, wala neno moja gumu, Niliona kila mara, mabwana kutabasamu, Nami nikawaheshimu, kwa tabia yao bora. Tena nilipata hadhi, ya kushika ufunguo, Mabwana wakawa radhi, kuitunza fedha yao, Neno moja la kuudhi, sikulisikia kwao, Nilipoagana nao, wote walikuwa radhi.

Jina langu nimewapa, nami nakumbuka yao, Moyo umepiga chapa, fadhili ya watu hao, Kwa moyo naapa, miaka yote niishiyo, “Tafanya makumbukio, ya mema waliyonipa. Idara ya Forodhani,

nimekwisha

badiliwa,

Bila ya nuksani, fedheha wala udhia, Nina huzuni moyoni, nakumbuka mazoea, Lakini kuvumilia, ni wajibu duniani.

73

Nimo katika Idara, sasa ya kutibu ng'ombe, Bora kupata ijara, uwekwapo usigombe, Hawi mkulima bora, anayechagua jembe, Maisha ya kiumbe, kugeuka si ibra. Kama yo yote yuko, apendaye kusikia, Mahali leo niliko, anwani namwambia, Kuwa Pangani siko, nimekwisha jihamia, Anayetaka kujua, Mpwapwa ndiko niliko.

Hadithi ningetunga, kwa mashairi ikawa, Tangu mwanzo wa uchanga, wakati wa kuzaliwa, Kwa maneno nikapanga, awali na aheria, Lakini nawaachia, wengine wapate tunga. Naachia waamuzi, kisa changu waamue, Wakipange waziwazi, kila jambo wafunue, Mtu yo yote hawezi, kujiamua mwenyewe, Mungu nizidishie, saburi ya uamuzi.

TENDO

BORA

BISIMILAHI barua, kwa wapenzi nipendao, Jamii ya mashujaa, walioacha makwao, Vitani wakajitia, kuwatetea wenzao, Leo nawaandikia, ari yangu nionayo. Sihitaji kusifu, mambo yote mtendayo, Lakini nawaarifu, tarehe tuliyo nayo, Tendo bora msahafu, husoma watu wajao, Na hapana utukufu, ulio sawa na huo.

Tangu mliposafiri, kuandama shambulio, Sijasoma msitari, uonyeshao punguo, Wa sifa ya askari, hayo ndiyo tuombayo, Hili latupa fahari, wote tuwatumaio.

74

Tangu mwanzo wa utesi, sijasikia tokeo, Sijasikia tetesi, na lawama hamnayo, Mwasifiwa ufuasi, unaozaa mazao, Na hii ndiyo halisi, heri niwaombeayo.

Kila mnapoteta, sifa kwetu huja mbio, Na majina tunapata, ya watu watukukao, Jambo hili huleta, heshima katika moyo, Hapana cha kufuta, sifa namna ya hiyo.

Mwasifiwa makini, bidii katika moyo, Hasa mkiwa vitani, hapana endaye mbio, Tusomapo gazetini, sifa kadiri ya hiyo, Huja fahari moyoni, kubwa isiyo na cheo. Mwasifiwa uthabiti, imara katika moyo, Na harufu ya baruti, inapofanya tokeo, Mara hupiga magoti, mkatenda yapasayo, Hufurahisha mabinti, habari wasikiao. Mwasifiwa utii, na heshima mfanyayo, Alia wivu adui, tabia mliyo nayo, Askari sifa hii, ndiyo imhusuyo,

Ndugu zenu wakinai, wanaposikia hayo. Mazungumzo hayeshi, haya yatosha kwa leo, Nadhani huu ubishi, mwaka huu mwishilio, Tuna hamu na utashi, ya kuona siku hiyo, Ya kuvunjiwa mashi, Hitler aliyo nayo.

Kwa siri nitatamka, mkinipa masikio, Japo mwakumbuka, kukumbushana ni ngao, Msivunje ushirika, bora mlio nao, Huu mwisho wa waraka, kwa watu niwapendao. 75

KUNDI

KUNDI moja wanakaa, wadudu wadogo sana, Na ndege wenye manyoya, kundi moja hupatana, Wanadamu vibaya, kutengana kwa fitina, Kwani hatuna haya, siku zote kugombana?

Hatukuumbwa na kucha, mfano kama wa simba, Wala meno yenye ncha, kama papa au mamba, Sababu gani twaacha, alivyotaka Muumba, Ambaye tunamcha, na daima kumwomba?

Mtu hakupewa pembe, aina kama ya mbogo, Hafanani na ng'ombe, mtu hata kidogo,

Twaigaje nyama kumbe, wanavyofanya zogo, Kama wana wakembe, kugombana kwa madogo? Hasara na majuto, huja kwa tunayotenda, Hupenya katika keto, kutia moyo madonda, Nyayoni hatuna kwato, namna kama ya punda, Hupigaje teke zito, kupigwa usikopenda?

Mwilini hatuna miba, kama mfano wa nungu, Twafanyaje ghiliba, izae mambo machungu, Yanayoleta misiba, kuwadhuru walimwengu, Kwa choyo cha kushiba, kuwania kubwa fungu? Vinywani hatuna sumu, mshabaha kama nyoka, Mtu hufanyaje hamu, akataka kugeuka, Awe si binadamu, Muumba alivyotaka, Kusudi adhulumu, na kuvunja ushirika?

AA ——— Ma a———A ———

Wala hatuna mikonga, mfano kama wa tembo, Hutamanije kutunga, kuburuga kila jambo, Kwa kusudi la kugonga, wenzetu kwa makumbo, Na kuwavutia janga, tufananao kwa umbo?

76

aa aa AA ”

Sisi wanadamu, ni wasafiri pamoja, Na vitu vilivyo humu, hatuchukui kimoja, Tutaacha vinadumu, safari yetu ikija, Kwa hakika ni wazimu, hiki choyo kutufuja. Huko Kuwa Nani Hitler

tunakokwenda, ukizuka ushahidi, nani ametenda, mambo yasiyo muradi, atakayependa, kushuhudiwa hasidi, utakonda, jambo hili likibidi.

NDOA

YA

SIRI

UDHIA

NDOA ya siri si bora, haishindi ya dhahiri, Ndoa ya siri hasara, kubwa Mzee Waziri, Neno lisilo fikira, mwerevu halikariri, Haina hata ishara, ya heri ndoa ya siri. Kutunga ni jadi kwangu, sikupokonya sikwiba, Amenijalia Mungu, nashukuru haiba, Ipambayo jina langu, kama shingo na kikuba, Ndoa ya siri machungu, inachoma kama mwiba

Lipi la kunikimbiza, ningependa kuelewa, Mzee umeteleza, kiburi chakuzuzua, Kwa hili wajipuza, na mwisho utazomewa, Ndoa ya siri manza, haifai kutetewa. Jina la mtu hukua, wengine wakimsema, Na mimi napendezewa, kwa shabaha kuifuma,

Kudhani nitakimbia, umepotea kupima, Ndoa ya siri udhia, si ndoa iliyo njema.

Mke hulazimu eda, na mume akitengana, Na kujitenga kwa muda, ndoa ikijulikana, Mwawapa wazazi rada, kwa jambo wasiloona, Manufaa na faida, ndoa ya siri haina. 77

Ndoa ya siri payo, kweli si masihara, Tamaa wote tunayo, moyoni inatukera, Bali kufuasa moyo, si jambo la busara, Na kukimbilia mbio, ndoa ya siri ujura. Kama haijulikani, fulani ameolewa, Wanaume hamsini, hata zaidi ya mia, Wanaweza kutamani, bibi mmoja kuoa, Ndoa ya siri sheriani, ina nyembamba njia. Uchokozi sianzi, sababu kidogo mwoga, Lakini bila ajizi, nikipigwa nitapiga, Na sasa nimebarizi, Mzee funga njuga, Ndoa ya siri upuzi, mwenye akili kuiga. Ubongo wangu wenda, si kama umetulia, Wala haukuganda, nitungalo naelewa, Tena damu hupanda, mwilini na kuchelea,

Ndoa ya siri kupenda, ni ulafi wa dunia.

Shetani nitakupunga, Mzee upate poa, Sababu bila uganga, huwezi kupambanua, Wapi panapofunga, na wapi pa kutokea, Ndoa ya siri ujinga, kuivutia sheria.

TUMBO TUMBO limeumbwa kati, ya mwili tulio nao, Tena mbali limeketi, ya macho na masikio, Halisikii sauti, ya ulimi usemao, Linapodai sharti, lipate liyatakayo. Tumbo halina kungoja, linapodai lipewe, Japo huna pesa moja, lataka linunuliwe, Wala halitaki hoja, deni lake lichelewe, Njaa deni la kioja, lisilo na mfanowe.

78

Tumbo ni mashine kali, isagayo mbio mbio, Iliyowekwa mbali, na ubongo uwazao, Kabisa halikubali, kuhiniwa litakayo, Ukifanya ubahili, utaona mlegeo. Tumbo halina mfupa, laini sana mwiliwe, Deni lake ukilipa, kusudi usidaiwe, Mara moja hutupa, lataka liongezewe, Ndiyo nguvu ya mishipa, na vitu vinginewe. Tumbo hupenda uhondo, puani unukiao, Na kushawishi matendo, pengine ambayo siyo, Usipotazama kando, ukawaza yaliwayo, Litakulisha uvundo, na mengine yadhuruyo. Tumbo lataka lishibe, daima liandaliwe, Papunguapo lizibe, mwili usipungukiwe, Naomba tupate shibe, kwa halali turidhiwe, Mungu tupe tusiibe, wala tusiadhiriwe.

Wakati unapotimu, na njaa ukiwa nayo, Tumbo halina fahamu, wala makumbukio, Halikumbuki karamu, jana ulokuwa nayo, Cha jana si kitamu, kuliko ulacho leo. Katika yasumbuayo, wajibu ikumbukiwe, Tumbo limezidi cheo, kuliko yote wenziwe, Haliamuru kituo, na kudai litiiwe, Likitawaliwa leo, kesho mpya udhiawe. Tumbo likipekecha, mtu hana kituo, Utadhania makucha, ndani yanakwenda mbio, Na lishibapo huacha, matata yote hayo, Mungu tunayekucha, tupe shibe wanayo. Kila tukiwa wazima, huo ndiyo mwendowe, Mungu tupe neema, na baraka tujaliwe,

Deni hili la lazima, likija lilipiwe, Bila kupata lawama, na heri tubarikiwe.

79

HERI HERI acha kujaribu, ukijaribu litende, Jaribu lenye thawabu, mazoea mbele yende, Jihadharishe aibu, njia mbaya usiende, Mazoea yana taabu, yadhuruyo usitende. Heri acha kuanza, ukianza limalize, Ahadi ukifanyiza, wajibu uitimize, Uonalo waliweza, fanya ndipo utangaze, Usilojua uliza, wajuzi wakueleze.

Heri kutofadhiliwa, kufadhiliwa jilinde, Fadhili unapopewa, hata ikiwa kipande, Wajibu kukumbukiwa, moyoni mwako igande, Na wema ukitendewa, uovu usiutende. Heri acha kujisifu, ukijisifu yaweze, Yaweze kuyasarifu, mambo hata yatokeze, Walio watukufu, vinywa vyao si mazeze, Huzifunga kwa mkufu, ndimi zisiwapoteze.

Heri kukataa shari, usitamani ushinde, Shari haina heri, ipishe yende upande, Baada ya kusaburi, ikikujia jilinde, Jilinde kwa ujasiri, pigana hata ushinde. Heri acha kupenda, ukipenda ufulize, Fuliza kuyatenda, mapenzi uyatimize, Mapenzi anayepanda, mmea wake atunze, Mapenzi Peponi tunda, duniani siyabeze. Heri nikibishana, mweledi awe mshinde, Nitaelewa maana, wala sitapata shonde,

Nimeapa kubishana, na mjinga nisitende, Faida sitaona, hata nikiwa mshinde. 80

|

MAREHEMU

RAJABU

WA MPWAPWA

AGOSTI kumi na saba, kuandika ni wajibu, Ukurasa uliziba, wa maisha ya Rajabu, Mtu huyu alishiba, elimu na adabu, Twamwombea thawabu, katika wetu msiba,

Mwaka wa hii huzuni, elfu na tisa mia, Nne na arobaini, mwezi nimewatajia, Ndipo huu ugeni, wa faradhi ya dunia,

Hapa ulipoondoa, mtu mwenye thamani.

Huyu ni mwanachuoni, ambaye tutakumbuka, Kwa matendo na kanuni, na sheria kushika, Hakufanya mtu duni, kwa wote alipendeka, Mauti yake hakika, yametwachia huzuni.

Na zaidi ya elimu, alipata tuzo bora, Tabia ya kukirimu, maskini kila mara, Haba kwake karamu, na dhaifu kwake bora, Kadiri hii imara, Mungu alimkirimu.

Alikuwa mbashasha, mpole tena baridi, Na watu kuelimisha, sana alijitahidi, Hakutenda la kuwasha, neno wala ukaidi,

Nia yake na muradi, ilikuwa kufundisha.

Alikuwa na furaha, juu ya kila kitu, Hakutia jeraha, katika moyo wa mtu, Kwa kicheko na mzaha, aliongea na watu, Hakufanya utukutu, katika yake maisha. Hakutafuta malipo, kwa kueneza elimu, Hakutamka kiapo, ahadi isiyotimu, Sasa Mungu mpe Pepo, awe katika kaumu, Ya roho zilizopo, mbali ya Jahanamu.

81

Basi twashukuru Mungu, mauti tumeumbiwa, Kiumbe hana mzungu, wa kuepa hii njia, Na baada ya machungu, mwilini kutuishia, Pepo katuandalia, tayari Bwana Mungu.

MALI MALI kama mshipa, wa damu katika mwili, Mali kama mfupa, jengo la kiwiliwili, Huweza kuleta hapa, kitu kutoka mbali, Kujaa na kupwa, ndiyo mwendo wake mali. Mali haina Komeo au Kufunguka Tajiri hawi

mlango, ambao una kufuli, kifungo, ambacho hakikubali, kwa ngo ngo ngo, ibishapo hodi mali, mwongo, kila asemalo kweli.

Mifuko yetu pakacha, kuvuja yake shughuli, Pato la kutwa na kucha, kudumu halikubali, Na tupatacho machicha, uto hayana asili, Akiba tunayoficha, huvunda siku ya pili. Nataka nisithubutu, kubeua jambo hili, Waliojaliwa watu, ili watengeze hali, Ila haja yangu tu, ni kuonyesha dalili, Ya manufaa ya watu, juu ya jambo hili. Mahali ilipo fedha, dhahabu na mithkali, Fahamu hapana adha, wala hapana zohali, Mambo kadha wa kadha, hufanyika tasihili, Nasi twaomba karadha, kidogo ya jambo hili. Twaomba tuhifadhike, tusahau dhiki kali, Fukara tuna makeke, mazito yanatudhili, Zaidi tusihizike, Muumba yote badili, Badili tuneemeke, tena tuwe na akili.

82

Tutie katika moyo, jitihadi na amali, Tuwe na mafanikio, ya jasho letu la mwili, Tena tuvune mazao, katika konde hili,

Ambalo ndiyo makao, ya viumbe awali. Tunu nyingi hutaka, roho Tutanulie baraka, ya kila Dhiki zinatuwaka, zizime Tupate kuburudika, tuwe

katika mwili, kitu halali, katika mwili, ndani ya kivuli.

Maisha kama lema, wazi kila mabali, Na mfano wa uzima, tulio nao dhalili, Lakini tunapohema, kwa wastani wa hali, Twapenda yanayouma, kidogo yakae mbali.

Dua tumekwisha taka, sasa twangoja kabuli, Machungu tunayoshika, geuza yawe asali, Istawi Tanganyika, wote tuwe na shughuli, Twendelee kila mwaka, kwa jambo lile na hili. Hapa natia nanga, mbele upepo mkali, Chombo changu nakinga, dhoruba hakihimili, Itapasua tanga, wala sina la pili, Shaaban ni malenga, mtunga shairi hili.

MASKINI MASKINI haokoti, aokotapo kaiba, Akijaliwa bahati, hudhaniwa kala riba, Hili si madhubuti, kusudi lake kuziba, Watu katika umati, wasipate cha kushiba.

Maskini si mufti, watu wengi hutamka, Hili nalo si thabiti, hafai mtu kushika, Nusu ya matafiti, ambayo yamezuka, Na kufaa umati, kwa maskini hutoka.

83

Maskini si msemi, asemalo Akijaliwa ulimi, nahau na Duniani havumi, avumapo Kizuri kutiwa lami, busara

si furaha, ufasaha, ni mzaha, au ujuha?

ni, Maskini hana kimo, anapokuwa kundi oni, mach yupo wa inga Huhesabiwa hayumo, ni, thama wana ine weng o, Maskini wangawam ini. umask kwa siyo o, vipim Wangepimwa kwa Maskini si shujaa, kweli au utani? Usione hakuvaa, kifuani manishani,

Maskini mkichaa, usitie akilini, Umaskini si doa, kwa watu duniani.

Maskini si mwalimu, uongo neno hili, Wengi wamehitimu, zaidi ya wenye mali, Maskini hakutimu, pia hili ni batili, Mwenye yote sifahamu, ila Mungu ni kweli. Umaskini watisha, tangu utoto najua, Zamani nikinyonyeshwa, baba alinipotea, Dhiki zikanitingisha, lakini sikulegea, Ikawa kujibidiisha, kusimama nami sawa.

Nilifanya ni pilau, wishwa nikasetirika,

Wala sikuwa bahau, kudhani nimelanika,

Mungu hakunisahau, kuacha nikahizika,

Kwa mkono wa nafuu, akazidi kunishika.

Japo tajiri siwi, lakini sijidunishi, Nikiwa bado ni hai, kujaribu hakunishi, Hainishi bidii, na chini sijiangushi, Kibaba nitakinai, kama nikikosa pishi. 84

TAFSIRI YA SHAIRI LA MSIBA WA LISBON au MAANGALIZI

KATIKA

“YOTE MEMA'

(VOLTAIRE) VIUMBE si wakunjufu, dunia ina huzuni, Watu wote wana hofu, waliomo duniani, Kwa usiri mrefu, wa maumivu ya ndani, Enyi mnaoarifu, 'yote mema” njooni, Mashekhe msarifu, madhara ya dunia.

Matambaa tazama, na majivu ya jamaa, Huyu mtoto na mama, chini wamefusiwa, Viungo vimeachama, mashimoni vimejaa, Jumla laki nzima, watu wamefukiwa, Pumzi bado wahema, mwili umeraruliwa. Makao yao mazuri, chini yamewafukia, Kwa shida bila kadiri, maisha yameweshia, Mauti yakidhihiri, na miguno kutokea, Inayotisha dhahiri, kwa msiba mbaya, Jawabu mtahubiri, mfananishe ya kuwa. “Ni sheria halisi, zake Mungu madhubuti, Na maneno mwaandasi, juu ya hii kahati, Mungu kalipa kisasi, pato la dhambi mauti, Dhambi gani mwakisi, hawa imewasaliti, Kuraruliwa kwa kasi, bado wanajinyonyea? Tuseme Lisbon, kwa maasi imezidi, Kushinda hata London, Paris na Madrid? Huko wamo furahani, Lisbon haizidi, Watu wamo msibani, na shimo kuwahasidi,

Wametenda ovu gani, kustahilisha haya? 85

Kwa raha watazamao, msiba wa ndugu zao, Wasiostuka moyo, kwa mauti yachezayo, Kimya watafutao, kisa cha tufani hiyo, Acha wafunge komeo, salama mliyo nayo, Gharika na machozi yatokayo, yatajiunga bia. Ardhi ikifunua, tai zake kwa hamaki, Ombolezo langu sawa, yowe langu lina haki, Makali kuzungushiwa, ya ajali na dhiki, Kwa ghadhabu na ubaya, mitego ya kufariki, Mbele ya ukali kuwa, wa mambo ya dunia. Shariki zetu shari, fariji changu kilio, Mwanena “Ni kiburi, cha uasi wa moyo, Kudhani kupata heri, kuliko tuliyo nayo, Kawape Tagu habari, pwani ibomokayo, Pekua katika shari, ya shindo lile baya. Uliza watu wafao, nyumba ile ya msiba, Ni kiburi ama siyo, kinacholeta toba, Na huruma kama ndiyo, katika mateso tiba, Yote mema msemayo, tena yote ni haiba, Fikira mliyo nayo, hii dunia ni mbaya? Bila shimo la nakama, Portugal kutokea, Kweli mwaelewa kama, Muumba hii dunia, Mjua yote hekima, na kila tusilojua,

Hakuweza tupa pema, sisi pa kujikalia, Ila ya moto milima, chini kutuchemkia? Upeo huu dhania, kuwa uwezo wa ungu, Huwezaje kuzuia, kuwafaa walimwengu, Fundi huyu zake njia, jinsi zilivyo chungu, Huwaje kutotumia, kufanya yake mizungu, Sithubutu Mungu kutoa, ujuvi ila kuomba dua.

86

1

Shimo la moto hili, napenda lingefurika, Gharika yake kali, katika jangwa na nyika, Mungu naheshimu kweli, bali dunia nataka, Wala hii si fedhuli, ila mapenzi hakika, Kwa pigo kama hili, mtu mayowe kutoa.

Kwa watu wenye huzuni, hili lisingefariji, Pwani kule motoni, kusiko na mkaaji, Kuwambia kwa amani, maisha wayahariji, Kwa sadaka duniani, makao wasihitaji, Nyumba zao gharikani, wengine watazindua. Wetu wengine kama, watajenga nyumba zenu, Kasikazini huchuma, kwa hasara mbaya kwenu,

Kwa sheria daima, ni kifungo shari yenu, Nyinyi kwa Mungu kama, mafunza mfano wenu, Makaburini daima, ambayo huwangojea. Kwa maskini hao, hii si faraja nzuri, Katika machungu yao, siongeze taksiri, Wa fadhaa wangu moyo, usiuzidishe hari, Sheria namna hiyo, kutanguka isokiri, Mnyororo huwa kwao, wa akili na tamaa. Kwa wasiodhurika, hudhani hivi hakika, Mnyororo ameshika, Mungu shida kufungika,

Kila analotaka, kwa upendo hutendeka, Wala hana mashaka, huri ametakasika, Mbona basi twateseka, chini ya mwenye haya? Fundo limekingama, la weledi kufungua, Watudhaniao mema, wasikanushe haya, Watu wote hutetema, mkononi mwake Allah, Mwanzo hutazama, wa uovu wa dunia, Kwa sheria ya daima, vyote vinavyojendea.

87

-

AA

Mwamba hutikisika, kwa dhoruba ya upepo, Na msaji hupasuka, kwa radi ipigapo, Wazo hawana hakika, la mapigo yavumapo, Uchungu na mashaka, moyo wangu uonapo, Msaada hutaka, kwa mwenye kuuandaa. Watoto wa Uwezo, huo wa Mwenyezi, Twaomba kitulizo, kwako baba wa vizazi, Chombo hakina uwezo, wa kusema waziwazi, “Kwa nini nina mzo, wa ubaya na ushenzi?' Maneno wala mawazo, chombo hakikupewa.

Chombo kikiponyoka, mkono wa mfinyanzi, Chini kikipasuka, furaha hakiwezi, Moyo wake kutunuka, wala kuhofu majonzi, Mwasema haya mashaka, kwa wengine ni azizi, Ukioza kwa hakika, mwili wangu huzaliwa.

Mafunza kama elfu, mwisho wa machungu yangu, Faraja gani tukufu, katika msiba wangu, Mtazamao kwa hofu, misiba ya walimwengu, Ziada na upungufu, sitaki katika msiba wangu, Naona wenu wangafu, wa fahari is'okuwa.

Ifichayo mabaya, kwa kudai kuridhika, Na mimi niliyevia, katika ushirika, Naam wanyama hawa, kuishi wal'ohusika, Vitu vionavyo pia, vizawavyo kwa mashaka, Kama mimi hufikiwa, na dhiki na kujifia. Kozi hukimbilia, mawindo yaogopayo, Kwa mdomo hudonoa, mwili utetemao, Haya kwa kozi huwa, 'yote mema' yasemwayo, Na tai humrarua, ghafla kozi vizio, Kwa mshale hutokea, tai kufumwa pia.

88

Mtu katika vita, pia huanguka fuli, Damuye ikajiseta, na ya wafu wa awali, Baadaye hupata, chakula ndege wakali, Viumbe wote hujuta, juu ya hii asili, Ya mateso kupata, na kifo wakizaliwa. Tena juu ya huzuni, kama hii mwasema, Kila maovu yakini, ya mtu kwa wote mema, Je baraka gani! kwa sauti kutetema,

Ya mauti na huzuni, mnenapo “yote mema,” Mwaingia ujingani, msemapo kama haya. Moyo wenu haukiri, wazo lenu mara mia, Kufungwa katika shari, wafu na wazima pia, Uovu heri mkiri, wanyemelea dunia, Asili yake ya siri, sisi bado kuelewa, Kwa Muumba mema fikiri, hutokeaje mabaya?

Twapatilizwa kulia, kwa sheria ya dhalimu, Ya waovu na wabaya, Typhon na Ahrim? Wakorofi kama hawa, ambao ililazimu, Kwa tetemo dunia, kuwafanya mizimu, Moyo wangu kuridhia, hili naona haramu. Hufikirije lakini, Mungu mwema mno huyo, Aenezaye hisani, kwa wana awapendao, Huletaje duniani, uovu kama huo? Liwezalo jicho gani, kupenya ayafanyayo? Kwa Mkamilifu shani, kutoka haya mabaya.

Kwa mwingine kutokea, asingekubali Bwana, Bali uovu hujaa, loo sheria kali sana! Loo fadhaa zatia, tofauti hizi tena! Alishuka kuinua, taifa letu Bwana, Alizuruje dunia, bila kugeuza haya?

89



Mnafiki husema, kugeuza hakuweza, Na wa pili asema, angetaka aliweza, Atabadili lazima, vile wakizungumza, Radi chini za kuchoma, ghafla zikatokeza, Zikapanua nakama, ya miji kuangamia.

Uso wa kufurahia, Portugal katikati, Mungu hurudi hatia, siri katika umati, Mwamuzi huamua, wa nafasi na wakati, Bila kuhurumia, wala hasira hapati, Mradi hushikilia, wake alionuia. Au pengine asili, yake isiyo mfano, Kwa ndani hustahimili, makosa mabaya mno, Au pengine Jalali, amefanya mlingano, Mauti kutukabili, tunapoteseka mno, Si kitu ila dalili, njia ya kuokolewa. Lakini hii njia, itishayo ikipitwa, Nam atahitajia, kubisha taji kupata? Upande tukichagua, wo wote tutateta, Hapana tunalojua, na vitu hofu hupata, Maumbile bubu haya, bure kuyategemea. Taifa la wanadamu,

hutaka neno la Mungu,

Peke yake fahamu, ndiye mwonya mizungu, Huangaza watalamu, hutuza wenye machungu, Bila Yeye binadamu, kosa ndiyo lake fungu, Kuliona ni vigumu, jani la kutegemea. Liebnitz hatufunzwi, kwa yasiyoonekana, Dunia hii azizi, bora kwa kujulikana, Machafuko na majonzi, mashaka kila aina, Furaha yetu haituzi, kukutana daima na, Maumivu na simanzi, na wingi wa ghasia.

90

1 Wema hapana mafafanuzi, kuteseka yake maana, Kama wenye machukizi, yaliyo makubwa sana, Katika maongezi, mzaha mimi naona, Juu ya ishara hizi, yote mema mkinena, Kama watalamizi, mashekhe hapana ninalojua. Plato ametwambia,

tulikuwa na mabawa,

Mwili imara pia, mbele ya wote ubaya, Dhiki na mauti haya, mageni yalikuwa, Tumekuwaje wakiwa, hali bora kupotea! Leo mtu hutambaa, vyote vinavyozaliwa hufariki dunia.

Ni ufalme dunia, wa uharibifu basi, Undo hili elewa, la mishipa na mifupa myepesi, Haliwezi vumilia, dunia shindo lake la kasi, Damu na vumbi pia, ni mchanganyo halisi, Pamoja uliotiwa, mwisho kujiyeyukia. Mishipa ya welekevu, iliyo wazi thabiti, Imewekewa maumivu, mjumbe wa mauti, Umbile wake werevu, ndivyo ninavyodhibiti, Plato nafanya ukatavu, na Epicurus si mutti, Kwa welekevu, nafuata Bayle anayejua.

Hata Bayle mweledi, mashakani hunitia, Huyu stadi zaidi, dini aliyekataa, Mwenyewe kajikaidi, kavunja zote sheria, Kama pofu mshindi, wa Philistine kaingia, Katika uhasidi, ambao aliandaa.

Jibu wapi liliko, la wingi wa Sababu kwetu hakiko, kitabu Matafitini aliko, mtu ni mgeni Hajui atokako, wala endako Ndani ya mzunguko, twaishi

91

akili? cha ajali, kweli, mahali, na kupotea.

aa WA ——

Chembe za kuadhibiwa, chini katika mchanga, Mauti huzinyafua, umbile la kusimanga, Chembe hizi kwa kuwa, huona mbali hutunga, Kwa fikira huelewa, kupima nyota za anga, Machanganyiko zajua, yetu ya milele pia.

Sisi hatuoni, ama kupata kujua, Dunia hii ya shani, ya furaha na hatia, Wajinga wagonjwa ndani, furaha hujidaia, Kwa vilio na huzuni, uchunguzi huwania, Kufa bila kutamani, ama tena kuzaliwa. Katika yetu matata, ziko nyakati hususa, Furaha inapofuta, machozi yetu kabisa, Bali furaha hupita, kama kivuli hasa, Urithi wake twapata, maumivu ya kutesa, Wakati uliopita, sikitiko kwetu huwa. Wakati watisha sasa, ujao usipotakasa kitu, Kama fikira hasa, zesha kaburini tu, Yote mema hususa, ilivyo tamaa yetu, Yote mema kuwa sasa, si kitu ni ndoto tu, Wenye busara hufyosa, ila Mungu hana doa. Kidogo kwa mauguzi, katika mashaka yangu, Sijitupi kwa chukizi, mbele ya Bwana Mungu, Japo nimeimba hizi, kwa huzuni beti zangu, Njia za furaha wazi, hutawala ulimwengu,

Nyakati za mageuzi, maisha kufanza haya. Na ushirika sikiliza, wa udhaifu wa bia, Hutafuta mwangaza, kati ya giza ghaya, Kuteseka naweza, wala sitajijutia, Khalifa alitangaza, kifo kilipomkaribia, Kwa yote Anayeweza, akaomba hii dua.

92

“Mungu mwenye mamlaka, na nguvu bila kiasi, Mzigo nimejitwika, kwako si tunu halisi, Wa uovu na mashaka, ujinga na uasi, Angezidi kutamka, kama hivi iwe basi, Tumaini nimeweka, kuwa nitaokolewa.

Published by Ozford University Press, P.O. Bor 12532, Nairobi and printed by Kenya Litho Ltd., P.O. Bor 773, Nairobi

93

.

aa



ui

PLATE

zai

aa

——

Kitabu chengine cha mashairi ya marehemu Shaaban Robert. Mashairi yaliyomo humu si mfano mwema tu wa utunzi bali ni vielezo vizuri vya mambo yaliyokuwa yakitendeka katika jumuia ya marehemu Shaaban na ambayo, baadhi yake mpaka sasa, yangali yakitendeka katika sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki. Lugha iliyotumiwa ni nyepesi na kunjufu. Kila shairi limejaa maana, na ni ushahidi tosha wa ubingwa wa marehemu Shaaban Robert.

Eastern

Africa

DO wa

OKFORD

UNIVERSITY

PRESS